Mkasa wangu mwingine wa Bolt

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
214
291
Nilipanda bolt, akaniomba sana akate request nusu ya safari. Nilimdanganya kuwa nahitaji risiti kwa ajiri ya ofisi kisha nika muuliza kwanini anataka tucancel request hio.

Dereva huyo alilalamika sana kwa kusema kuwa serikali ilawaagiza Bolt kufanya makato asimilia 15% lakini wao wanakatwa mpaka asilimia 24% kwa 25% hivyo kuwalazimu kuingia makubaliano na abiria ili waweze kuingiza kipato bila kukatwa sana nakuwa na faida finyu.

Pia kwa sababu hizo dereva huyo aliongelea kuwa inasabibsha madereva wengi wa bolt kuwa na dharau, kiburi pia nasababisha kuwa na hasira hivyo kugombana sana na abiria, japo alisema ugomvi hautaki kuwa kati ya dereva na abiria.

Alinifikisha salama, japo wakati wa kurudi na Bolt wa pili alinikasirikia sana kwa kuchagua barabara ya kupita na kwa kuwa nilikataa asicancel request alikuwa akinisema sana. bali na hayo support system ya Bolt ambayo ipo kwenye application inachukua muda mrefu ku tatua complains za watu na madereva wao pia.
 
SAFI
Psalm%2023_1%20Christian%20Wallpaper%20iPhone.jpg
 
Back
Top Bottom