Madereva Tax wa Airport Dodoma wanazuia Bolt kubeba abiria airport hapo

Mugabe wa Bongo

Senior Member
Apr 14, 2012
145
72
Madereva wa Tax wanaofanyia kazi Airport ya Dodoma wameanzisha fitna ya kuwazuia madereva wanaofanya Bolt kuingia kubeba abiria kwenye uwanja huo wa ndege.

Wanafanya fitina wao lakini pia wanashirikiana na baadhi ya watu wa TRA ambapo bolt akiingia wanamkamata na kuamuru kwenda ofisini kukagua kama huna deni lolote TRA, sasa hata abiria wengi wanapata usumbufu na kushuka kuanza kutafuta usafiri mwingine.

Abiria wengi wanaamua kutumia bolt kwa ajili ya usalama na faragha pia ndo maana hawapendi kutumia tax za airport lakini hilo kwa hawa madereva wa airport wao hawataki kukubali na wanataka kila abiria ashukaye atumie tax zao.

Shida nyingine ni kila gari dogo likiingia kubeba ndugu au jamaa hawa madereva wa tax wa airport wanapakazia ka maofisa hao wa tra waikamate na kuikagua kama ni tax mtandao (bolt) ama sio. Sasa jambo hili ni kero sana kwa abiria na hata kwa madereva wa magari.
 
Hii shida nayo ipo sana, unaweza zako kuingia na kababy walker kako ukavamiwa na hao madereva.
 
Nadhani ni swala la uwelewa tu mbn huku mjin hakuna mambo ya kiswahili kama hayo?!!!!Alipo dereva tax na bolt yupo hivyo hivyo kwa bajaji
 
Back
Top Bottom