Mkasa ulionikuta COCO beach usiku

Mkasa ulionikuta COCO beach usiku

Wewe una gari na unatembea sehemu kama hizo usiku huna bastora!! hata sime?
Mambo ya kutishiana kwangu no. Na nnapiga picha kama ingekuwa ni mimi angekiona cha moto. Huyo alikuwa ni polisi sio jambazi kwani ingekuwa jambazi angekuomba leseni kwa kazi gani? tena anashika na kukurudishia!! hao ni vijana wa mangu hawana kipya.

hivi kila mwenye gari ana bastola??!! coco beach kuna kitisho gani cha kusema huwezi kwenda huko na gari bila bastola??!!
 
Jerrymsigwa avatar yako imeniacha hoi.

avatar89690_4.gif
 
Mod post kama hivi za zakutunga na kuchafua jeshi letu.It's the usual complaint system does good, system is abused.

sasa wapi kachafua, kama ni yakutunga basi inaendana na kweli.
 
utii wa sheria bila shuruti
**Msininyooshee vidole**
 
Mod post kama hivi za zakutunga na kuchafua jeshi letu.It's the usual complaint system does good, system is abused.

Hongera sana mkuu kwa kutambua utunzi wangu, lakini kwa kuwa hukuwepo eneo la tukio nakushauri kukaa kimya ukisubiri yakutokee na wewe ndio uamini.
 
Cooking up a Story vilaza mupo wengi

Yaelekea mkuu wewe ni mpishi mzuri sana, ndio maana hutaki kuamini. Hiyo ishu ni ukweli kwa asilimia mia, na imenitokea mimi mwenyew jumamosi
 
Mod post kama hivi za zakutunga na kuchafua jeshi letu.It's the usual complaint system does good, system is abused.

Jeshi lenu kwani wewe ni mwanamgambo wa Al-Shabab au Hamas?

Tanzania kuna majeshi yafuatayo na yote ni mali ya umma:
Jeshi la Polisi
Jeshi la Kujenga Taifa
Jeshi la Wananchi
Jeshi la Zimamoto
Jeshi la Uhamiaji

Enewei inawezekana wewe ni Mkurya...
 
Polisi wetu na uzembe wetu!

Polisi anapofika hasa mda usio wa kazi na hana uniform ni lazima ajitambulishe na atoe ID ndipo afanye kaZi yake. Hapo kwa vile wengine tuna uoga basi nao wanachukulia huo upenyo na kutubabaisha. Ungemuuliza hizo detail, ndipo afanye yake.

Polisi wanatumia sana ujinga wetu kutunyanyasa 'vile tu ana cheo cha upolisi' wakati ni kazi ka kaZi zingine tu. Pole sana, pia ukute hiyo pisto ilikuwa toy tu, kwa sbabu polisi hawezi fanya huo upuuzi wa kuload ammo kwa ajili ya leseni. Next time jua haki zako kabla ya arrest


Hapo bold ndiyo penye ujumbe mkuu!
 
nakushauri kukaa kimya ukisubiri yakutokee na wewe ndio uamini.

Mkuu achana na huyo kiazi, ujue kuna watu wengine hawajazaliwa bali wamejambwa...

Kwa wanaoijua Coco Beach wanatambua fika usumbufu wa wale askari kanzu wenye kusumbua watu wajifungiao kwa magari yao...

Kuna askari mmoja nilishawahi mtolea uvivu hapo hapo Coco Beach, hivi sasa anajuta maana anapumua hewa ya Kasulu Kigoma huko...
 
Sehemu yangu ya sita ya ufahamu inanipa alert km hii ni habari ya kutunga au ilioongezwa chumvi isiyotumia upeo wa akili na iliyolenga kutuhabarishanulivyo kidume wa ovyo. Hakuna polisi wala jambazi anayeweza kuigiza kufikia kiwango hiki.

Sare za polisi zinajulikana na wakati wa usiku huwa ni wengi. Jambazi anajua wenye gari huwa wamebeba pistol hivyo sidhani km wanaweza kufanya huo mchezo.
 
Sasa hapa ukilaza wangu ni nini? Humu Jf kuna vitu vingi vingine vya kweli ama vya kutunga. Wajibu wa memba ni kufanya uwezalo, ushauri ama kusaidia. Sasa wewe unaposema mimi kilaza kwa kushauri fake story hunitendei haki.

Una support invalid topic mimi na wajua polisi wa coco hakuna mwandawazi hata moja atoe bastola
 
Mod post kama hivi za zakutunga na kuchafua jeshi letu.It's the usual complaint system does good, system is abused.

hapo nitamtetea hii haijatungwa kwa pale coco beach ndiyo sehemu yake mambo kama haya yanatokea sana, mi nilipeleka watoto wangu yalinikuta makubwa sana na mpaka nikaambiwa gari ninayotumia ni ya wizi, wakaniweka kiti cha kushoto wakapanda na wenyewe walikuwa watatu, wakaniambia nitoe hela au wanipeleke kituoni, nikawambia twendeni kituoni, nadhani kiswahili changu kiliwaambia hapawatapata mtaji na mimi nikakomaa twende kituoni, kituoni sifikishwi nazidi kuombwa hela, mwishoe wakashuka eti ooh utakufa unajifanya mjana hapa bongo.

sikujibu kitu nikaondoka. nikapachukia sana coco. hivi huyu jamaa kafanyiwa kweli. polee mkuu
 
Una support invalid topic mimi na wajua polisi wa coco hakuna mwandawazi hata moja atoe bastola

na ndiyo maana amesema inawezekana ni polisi au ni matapeli jamani, kama mimi niliokutana nao hawana uniform wala sijaona vitambulisho na pia nahisi hawakuwa hata na silaha yoyote ila nilikomaa nao. maana wanasema gari ya wizi kwahiyo niwape hela waniachie au wanipeleke kituoni.

niliwaambia nikiwapa hela kesho pia nitakamatwa ni vizuri kwenda kituoni ili nitangazwe na nikamatwe kabisa na kila mtu ajue nina gari ya wizi, wakaniachia na maneno maneo mengi. hivyo kama pale pana polisi waangalie zaidi kuna vijitu vinajifanya wao polisi zaidi
 
hapo nitamtetea hii haijatungwa kwa pale coco beach ndiyo sehemu yake mambo kama haya yanatokea sana, mi nilipeleka watoto wangu yalinikuta makubwa sana na mpaka nikaambiwa gari ninayotumia ni ya wizi, wakaniweka kiti cha kushoto wakapanda na wenyewe walikuwa watatu, wakaniambia nitoe hela au wanipeleke kituoni, nikawambia twendeni kituoni, nadhani kiswahili changu kiliwaambia hapawatapata mtaji na mimi nikakomaa twende kituoni, kituoni sifikishwi nazidi kuombwa hela, mwishoe wakashuka eti ooh utakufa unajifanya mjana hapa bongo. sikujibu kitu nikaondoka. nikapachukia sana coco. hivi huyu jamaa kafanyiwa kweli. polee mkuu

Pole ujumbe utafika
 
Back
Top Bottom