Mkasa ulionikuta COCO beach usiku

Mkasa ulionikuta COCO beach usiku

Talking nonsense solves no problems, as everyone knows,so why is it unjust to deprive you of the right to speak?

Mkuu unadhani ukiandika kithungu ndo utapata pointi ? Usitetee uovu ...penye ukweli paachwe pawe ivo...cocobeach askari wamepaharibu sio sehemu tena ya kwenda na kuwa na amani..vitisho vingi..
 
Nilipokuwa nasoma nilikuwa natetemeka sana sijui hasira!!! daah aisee pole sana, nadhani hukulala siku hiyo mkuu kwa hasira.Ila ulimvimbia kinoma,alikoenda alijua amekutana na kidume.Wajinga sana hawa jamaa.

Tuna hasira wengi sana
 
Pole kwanza kwa mkasa ila pili sishangai sana kwa kilichokupata hua inatokea mda mwengine anakua na wenzake wanaangalia kwa mbali.

Nakusifu hukuchukua uamuzi wa kuondoa gari lako kwani ungempa mwanya wa kufyatua kama alivyodhamiria. Ushauri wangu ukikutana na askari mwenye silaha usioneshe kua juu au jeuri zaidi yake utajikuta matatizoni kwa kujeruhiwa bila sababu ya msingi.

Nakumbuka niliwahi kimbizwa na wale antirobery kama jambazi usiku wa manane wakaniblock kwa makeke yote wametoa mitutu na amri juu ya kuzima taa na gari nikatii ila waliponikaribia wakaniomba masamaha na kusema wamekosea sio mimi, hapo mwili wote wa baridi najua napigwa risasi leo.
 
Habari zenu wakuu, Natumai mnaendelea vizuri na shughuli za kila siku kwa maendeleo ya taifa letu la Tanganyika.
Ilikua siku ya jumamosi tarehe 12/07/2014.

Mida kati ya saa mbili na saa tatu usiku, baada ya kupata chakula nikaamua mimi na mwenzangu(rafiki wa kike) twende fukwe za coco kupunga upepo na kubadilisha mazingira, Tulipofika(upande wa sinema) hatukutaka kushuka kwenye gari bali tulibaki ndani ya gari huku tulibadilishana mawazo na pia kupiga picha kwa kutumia simu zetu, kuna wakati ilibidi tutoke nje ili kupata madhali nzuri ya kupigia picha, Tulikaa kwa muda wa kama dakika 40 kisha tukaamua kuondoka.

KASHESHE LAANZA.
Nilipowasha tu injini ya gari yangu kuna bwana aliekua amevalia mavazi meusi na koti refu jeusi alikuja kwa mwendo wa haraka kuelekea upande wangu(dereva) akitokea upande wa sinema(big screen) ile ambayo hupenda kutumia kuoneshea mpira, alipofika kwangu jambo la kwanza alinisalimia, nilipomjibu alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa polisi, Nikamjibu "Nashukuru kukufahamu"(huku nikimtazama machoni).

Baada ya kumjibu vile kwa namna fulani nahisi nilimpunguza kasi, Akakosa maneno ya kuongea, Akaanza kuulizia leseni yangu, nikamtolea leseni orijino lakini zilikua mbili(moja iliyoisha muda wake na mpya) hapo ndio vuguvugu likaanza.

VUGUVUGU;
Aliniuliza kwa nini namiliki leseni mbili kwa jina moja nikamjibu kuwa moja imeisha muda wake, akataka azishike zote nikamgomea, ila nikamuonesha nikiwa nimezishika na hapo tukapishana, akanitukana tusi moja kubwa sana tena nikiwa na rafiki yangu wa kike, hapo hasira zikanipanda nikamuambia mimi siwezi kukupa chochote, Akanijibu ni lazima nimpe, akapiga hatua moja nyuma akatoa bastola(ra) kiunoni akabadilisha kidude cha kuwekea risasi akaweka kingine,akaikoki akaniwekea kichwani kisha akaniambia nimpe leseni, kwa ubishi wangu nikagoma, akahesabu mpaka tatu kisha akavuta lakini sikusikia paaaah! Wala nini japo mwili mzima ulishalowa jasho, nikapata kiburi huku nikitetemeka nikaendelea kubisha kwa nguvu zote, naye akanisogelea kwa ukaribu zaidi na kisha akashika bastola vizuri tena, kwa mara ya pili nikapatwa na uoga nikamkabidhi leseni zote, akaziangalia kisha akanirudishia na kuondoka zake, na mimi kwa kiburi huku nikitetemeka nilimjibu hovyo huku nikiondoka.

Mpaka sasa siamini kama yule alikua ni askari ama ni tapeli.

ANGALIZO;
Tuwe makini sana tunapotembelea maeneo yale.
Jeshi la polisi inabidi waangaze pale kwani matapeli pia wapo na kama yule jamaa alikua ni askari, ni kwa nini aliamua kutumia nguvu na lugha ya matusi katika mazingira rahisi kiasi kile??

MCHANA MWEMA.
Je ulimuuliza kama anakitambulisho cha upolisi?
 
Pole Mkuu!

Ila kama nimekupata vizuri ,inawezekana huyo askari feki,alikuwa na bastola feki,au kama ilikuwa bastola halisi haikuwa na risasi.

Mtu anapojaribu mara mbili kukupiga risasi bila mafanikio-kwa upande wangu ama zake ama zangu;kwanza kosa lenyewe si la kutishiana kifo namna hiyo,ungeamua kumkuja kisawasawa,ungekuwa na utetezi mzuri wa self defence.

Pili,mtu kama huyo hukupaswa kumwacha,ungeenda polisi ukaripoti ili kama ni askari kweli anapata wapi kiburi cha kutishia watu maisha.Lakini pia,si kawaida askari akukute kwenye parking aanze kukuomba leseni-huyo ni muhuni.
 
Kama unaona hakuna haja ya kubeba bastola poa, ukichezewa makalio uwe mtulivu.

aah kumbe wewe unabeba bastola ili usichezewe makalio??!! wenzio wanazo hizo wanaziweka pembeni na watu wanawachezea makali.....wakuchezewa ni wakuchezewa tu hata uwe na AK47.
 
Pole mkuu...kama wewe ulikuwa unatokwa jasho nahisi huyo wa pembeni yako alikuwa amezimia kabisa


kwikwiwkwiwkwiiiiiii wewe tabia yako mbaya sasa kwa nini mwenzake azimie ila atakuwa alilowa chapachapa.
 
duh pole mkuu.
ila tumefika huko kwa askari kuuliza leseni na ukigoma unatolewa bastola ama kutishiwa maisha?
bado naendelea kuitafakari kama alikuwa jambazi angemalizia dhamira yake,

kama ni tapeli tu wa kawaida tapeli hutumia maneno mengi sana na si silaha

kama alikuwa tapeli anayetumia silaha feki basi kazi ipo ila alikuwa anataka utoe pesa au akuibie nini kingine zaidi ya pesa mbona hakufanya hivyo sasa na mwisho umesema wewe mwenyewe ulitoa leseni zote hivyo ulitii na kwa vile ulishaonesha kushindwa chochote kingine angeweza kufanya
alikuwa nani huyo kwa nini alifanya hivyo.
poleni sana.

lakini siku nyingine na wewe mkuu usiende sehemu hatarishi kama hizo ufukweni usiku wa saa mbili? unaweza hata kukumbwa na jini jamani , zipo sehemu nyingi ambazo unaweza kwenda na baby wako kwa raha zenu na faragha bila mahoteli makubwa, malls, etc
haya ni mawazo yangu
 
Pole Mkuu!

Ila kama nimekupata vizuri ,inawezekana huyo askari feki,alikuwa na bastola feki,au kama ilikuwa bastola halisi haikuwa na risasi.Mtu anapojaribu mara mbili kukupiga risasi bila mafanikio-kwa upande wangu ama zake ama zangu;kwanza kosa lenyewe si la kutishiana kifo namna hiyo,ungeamua kumkuja kisawasawa,ungekuwa na utetezi mzuri wa self defence.Pili,mtu kama huyo hukupaswa kumwacha,ungeenda polisi ukaripoti ili kama ni askari kweli anapata wapi kiburi cha kutishia watu maisha.Lakini pia,si kawaida askari akukute kwenye parking aanze kukuomba leseni-huyo ni muhuni.
umeona ehee maeneo hayo labda angemuomba kitambulisho cha kazi au cha taifa nk
yani sijaisoma hali kabisa
 
Mod post kama hivi za zakutunga na kuchafua jeshi letu.It's the usual complaint system does good, system is abused.

i thought it is an alert to the rest, yet you noticed fabrications!!!!!!!!! how will the real incident be?

Aisee mie nachukua hiyo tahadhali na kumshukuru mtoa mada kwa hilo ambalo hata maaskari wetu watalifanyia kazi kubaini wanaojihusisha matukio kama haya.
 
Mkuu huyu jamaa nafikiri ni mmoja wao. Ni mara nyingi post zinazoonesha uovu wa jeshi letu la polisi huwa anazipinga tena kwa jazba na hata kutumia lugha chafu hapa. Ukweli utabaki kuwa jeshi letu limekuwa so corrupted in a way that we can never trust it again labda libadilike. Kwa sasa hivi no trust! I mean zero!

Until they can be proved,allegations remain merely assertions
 
Mkuu unadhani ukiandika kithungu ndo utapata pointi ? Usitetee uovu ...penye ukweli paachwe pawe ivo...cocobeach askari wamepaharibu sio sehemu tena ya kwenda na kuwa na amani..vitisho vingi..

What should you do once an allegation has been made?
 
Back
Top Bottom