Mkasa ulionikuta COCO beach usiku

Mkasa ulionikuta COCO beach usiku

Habari zenu wakuu, Natumai mnaendelea vizuri na shughuli za kila siku kwa maendeleo ya taifa letu la Tanganyika.
Ilikua siku ya jumamosi tarehe 12/07/2014.

Mida kati ya saa mbili na saa tatu usiku, baada ya kupata chakula nikaamua mimi na mwenzangu(rafiki wa kike) twende fukwe za coco kupunga upepo na kubadilisha mazingira, Tulipofika(upande wa sinema) hatukutaka kushuka kwenye gari bali tulibaki ndani ya gari huku tulibadilishana mawazo na pia kupiga picha kwa kutumia simu zetu, kuna wakati ilibidi tutoke nje ili kupata madhali nzuri ya kupigia picha, Tulikaa kwa muda wa kama dakika 40 kisha tukaamua kuondoka.

KASHESHE LAANZA.
Nilipowasha tu injini ya gari yangu kuna bwana aliekua amevalia mavazi meusi na koti refu jeusi alikuja kwa mwendo wa haraka kuelekea upande wangu(dereva) akitokea upande wa sinema(big screen) ile ambayo hupenda kutumia kuoneshea mpira, alipofika kwangu jambo la kwanza alinisalimia, nilipomjibu alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa polisi, Nikamjibu "Nashukuru kukufahamu"(huku nikimtazama machoni).

Baada ya kumjibu vile kwa namna fulani nahisi nilimpunguza kasi, Akakosa maneno ya kuongea, Akaanza kuulizia leseni yangu, nikamtolea leseni orijino lakini zilikua mbili(moja iliyoisha muda wake na mpya) hapo ndio vuguvugu likaanza.

VUGUVUGU;
Aliniuliza kwa nini namiliki leseni mbili kwa jina moja nikamjibu kuwa moja imeisha muda wake, akataka azishike zote nikamgomea, ila nikamuonesha nikiwa nimezishika na hapo tukapishana, akanitukana tusi moja kubwa sana tena nikiwa na rafiki yangu wa kike, hapo hasira zikanipanda nikamuambia mimi siwezi kukupa chochote, Akanijibu ni lazima nimpe, akapiga hatua moja nyuma akatoa bastola(ra) kiunoni akabadilisha kidude cha kuwekea risasi akaweka kingine,akaikoki akaniwekea kichwani kisha akaniambia nimpe leseni, kwa ubishi wangu nikagoma, akahesabu mpaka tatu kisha akavuta lakini sikusikia paaaah! Wala nini japo mwili mzima ulishalowa jasho, nikapata kiburi huku nikitetemeka nikaendelea kubisha kwa nguvu zote, naye akanisogelea kwa ukaribu zaidi na kisha akashika bastola vizuri tena, kwa mara ya pili nikapatwa na uoga nikamkabidhi leseni zote, akaziangalia kisha akanirudishia na kuondoka zake, na mimi kwa kiburi huku nikitetemeka nilimjibu hovyo huku nikiondoka.

Mpaka sasa siamini kama yule alikua ni askari ama ni tapeli.

ANGALIZO;
Tuwe makini sana tunapotembelea maeneo yale.
Jeshi la polisi inabidi waangaze pale kwani matapeli pia wapo na kama yule jamaa alikua ni askari, ni kwa nini aliamua kutumia nguvu na lugha ya matusi katika mazingira rahisi kiasi kile??

MCHANA MWEMA.
Aisee unauliza jibu?huyo alikuwa jambazi!...motor vehicle inspector ndo mwenya haki ya kukagua leseni yako!..kama kweli alikuwa askari angekuambia umpe kadi ya gari na kitambulisho chako aangalie majina ili kujiridhisha hilo gari hujaliiba hapo coco, alafu cha kushangaza hao askari wanakaa na wateja maeneo ya hapo coco wakati pembeni tu hapo kwa pinda watu wanakabwa saa moja usiku,aisee mungu wako mkubwa!
 
hivi kila mwenye gari ana bastola??!! coco beach kuna kitisho gani cha kusema huwezi kwenda huko na gari bila bastola??!!

Wewe saa mbili kwa sehemu za dar ni hatari, tena kwenye sehemu za starehe? wewe utakubali vipi mwanaume mwenzako anakuwekea bastola kichwani?
 
Jeshi lenu kwani wewe ni mwanamgambo wa Al-Shabab au Hamas?

Tanzania kuna majeshi yafuatayo na yote ni mali ya umma:
Jeshi la Polisi
Jeshi la Kujenga Taifa
Jeshi la Wananchi
Jeshi la Zimamoto
Jeshi la Uhamiaji

Enewei inawezekana wewe ni Mkurya...

J.W.T.Z= Jeshi la Wakurya Tangu Zamani.
 
Sehemu yangu ya sita ya ufahamu inanipa alert km hii ni habari ya kutunga au ilioongezwa chumvi isiyotumia upeo wa akili na iliyolenga kutuhabarishanulivyo kidume wa ovyo. Hakuna polisi wala jambazi anayeweza kuigiza kufikia kiwango hiki. Sare za polisi zinajulikana na wakati wa usiku huwa ni wengi. Jambazi anajua wenye gari huwa wamebeba pistol hivyo sidhani km wanaweza kufanya huo mchezo.

Kama majambazi wangekuwa wanajua hivyo wasingekuwa wanavamia watu.
 
coco huwa pamekaa kiizi izi nakumbuka nilinusurikaga hapo na janga flani hivi

panahitaji ukakamavu japo pan shangwe sana hapo aisee
 
Habari zenu wakuu, Natumai mnaendelea vizuri na shughuli za kila siku kwa maendeleo ya taifa letu la Tanganyika.
Ilikua siku ya jumamosi tarehe 12/07/2014.

Mida kati ya saa mbili na saa tatu usiku, baada ya kupata chakula nikaamua mimi na mwenzangu(rafiki wa kike) twende fukwe za coco kupunga upepo na kubadilisha mazingira, Tulipofika(upande wa sinema) hatukutaka kushuka kwenye gari bali tulibaki ndani ya gari huku tulibadilishana mawazo na pia kupiga picha kwa kutumia simu zetu, kuna wakati ilibidi tutoke nje ili kupata madhali nzuri ya kupigia picha, Tulikaa kwa muda wa kama dakika 40 kisha tukaamua kuondoka.

KASHESHE LAANZA.
Nilipowasha tu injini ya gari yangu kuna bwana aliekua amevalia mavazi meusi na koti refu jeusi alikuja kwa mwendo wa haraka kuelekea upande wangu(dereva) akitokea upande wa sinema(big screen) ile ambayo hupenda kutumia kuoneshea mpira, alipofika kwangu jambo la kwanza alinisalimia, nilipomjibu alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa polisi, Nikamjibu "Nashukuru kukufahamu"(huku nikimtazama machoni).

Baada ya kumjibu vile kwa namna fulani nahisi nilimpunguza kasi, Akakosa maneno ya kuongea, Akaanza kuulizia leseni yangu, nikamtolea leseni orijino lakini zilikua mbili(moja iliyoisha muda wake na mpya) hapo ndio vuguvugu likaanza.

VUGUVUGU;
Aliniuliza kwa nini namiliki leseni mbili kwa jina moja nikamjibu kuwa moja imeisha muda wake, akataka azishike zote nikamgomea, ila nikamuonesha nikiwa nimezishika na hapo tukapishana, akanitukana tusi moja kubwa sana tena nikiwa na rafiki yangu wa kike, hapo hasira zikanipanda nikamuambia mimi siwezi kukupa chochote, Akanijibu ni lazima nimpe, akapiga hatua moja nyuma akatoa bastola(ra) kiunoni akabadilisha kidude cha kuwekea risasi akaweka kingine,akaikoki akaniwekea kichwani kisha akaniambia nimpe leseni, kwa ubishi wangu nikagoma, akahesabu mpaka tatu kisha akavuta lakini sikusikia paaaah! Wala nini japo mwili mzima ulishalowa jasho, nikapata kiburi huku nikitetemeka nikaendelea kubisha kwa nguvu zote, naye akanisogelea kwa ukaribu zaidi na kisha akashika bastola vizuri tena, kwa mara ya pili nikapatwa na uoga nikamkabidhi leseni zote, akaziangalia kisha akanirudishia na kuondoka zake, na mimi kwa kiburi huku nikitetemeka nilimjibu hovyo huku nikiondoka.

Mpaka sasa siamini kama yule alikua ni askari ama ni tapeli.

ANGALIZO;
Tuwe makini sana tunapotembelea maeneo yale.
Jeshi la polisi inabidi waangaze pale kwani matapeli pia wapo na kama yule jamaa alikua ni askari, ni kwa nini aliamua kutumia nguvu na lugha ya matusi katika mazingira rahisi kiasi kile??

MCHANA MWEMA.

Aseh issue hii ni kubwa zaidi unavyodhani. Hata ungeripoti polisi na wao wengestuka. Kawaida polisi siyo watu kukimbiia kutoa silaha kama wanadhaminia kutingisha mtu kwa ajili ya pesa.
 
ndugu majambazi pia husoma alama za nyakati polisi hawezi uliza leseni usiku wana maswali yao kwa muda huo, hiyo ilikuwa ni mis-target kiukweli alikuwa na nia mbaya ila kuna mazingira yalisitisha azma yake.

Jambazi aulize driving licence ya nini? labda alikuwa ni kichaa aliyetoroka hospitali.
 
mkuu sijasema jambazi nimesema raia mwenye nia mbaya kwani hata watoto, vibaka, vidokozi na wengineo sikuhizi wana bastola kwa akili nyepesi jambazi coco beach afuate nini?

Sasa hao raia wenye nia mbaya wanauliza leseni ya nini?
 
Next tym punguza ubish mkuu, uhai ni bora kuliko hzo lesen na mali zingine!
 
Msioamini ngojeni mpaka yawatokee. Mimi yalishanitokea kule karibu na wanakopakigi Wahindi. Ilikuwa mida ya usiku kama saa mbili nimeenda na baby wangu kupunga upepo. Wacha jamaa wa askari kanzu watokee na kutupa kesi ya ufuska!

Eti tulikuwa tunafanya ufuska ndani ya gari! Walichotaka kufanya ilikuwa kutupeleka polisi na kututoa magazetini. Ili kulinda goodwill yangu na ya yule dada, ili bidi zinitoke pesa nyingi sana.

Mpaka leo Coco sina hamu napo, japo naendelea kwenda but nimekuwa makini sana na mapozi ya hapo.
 
Uache kufanya ngono kwenye gari...nisamehe kama nimetafsiri vibaya hii story yako..siku nyingine wale vijana wa Shigongo watawapiga picha itakuwa aibu!
 
Aaahaaaaahaaaaaaaaa ................
Dah hili ni picha la kihindi tofauti yake staa ajafa ila ma.shu.zi tu kayamwaga
 
Uache kufanya ngono kwenye gari...nisamehe kama nimetafsiri vibaya hii story yako..siku nyingine wale vijana wa Shigongo watawapiga picha itakuwa aibu!

Hii ni kesi ya kubambikwa. Magest yote haya mtu unaanzaje kugegeda ndani ya gari. Tulikuwa tumekaa tunapunga upepo ndio tukapewa kesi!
 
Wewe ulibugi toka mwanzo alipoomba kuona leseni ungemwomba kitambulisho!
 
Back
Top Bottom