Mkasa huu nimesimuliwa na rafiki yangu

Mkasa huu nimesimuliwa na rafiki yangu

TANZANNIA

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2015
Posts
1,047
Reaction score
385
Baada ya kumaliza chuo, akaajiriwa kwenye shirika moja la umma miaka kadhaa iliyipota na hajaoa. Siku moja alipokuwa akitoka kazini akaona foleni imezidi barabarani hivyo akaamua kupumzika kwenye mgahawa moja maarufu katikati ya jiji ili kupitisha muda, akiwa pale mgahawani alikaa jirani na mrembo mmoja mwenye sura ya upole fulani hivi...!

Baada ya kujuliana hali na maneno ya hapa na pale wakajikuta wanazoeana kwa muda mfupi kiasi cha kubadilishana mawasiliano. Uhusiano ukazidi kukua ndipo siku moja akamkaribisha binti nyumbani.

Bila hiyana alikaribia, baada ya mlo na vinywaji wakajitupa uwanjani, pre-match rom zikafanyika, ilipofika wakati sasa jamaa ameshapagawa, yule binti akasitisha ushirikiano ghafla na kujiinamia huku akilia. Ikumbukwe kuwa wakati huo jamaa akili zimeshahama, akaanza kumhoji na kumbembeleza kulikoni, lakini yule dada alikataa katakata kuendelea na mechi bila kusema kinachomsibu.

Baada ya jamaa kung'ang'ania ikabidi aseme ukweli,k wamba yeye aliolewa na mumewe ameshafariki kwa haka kagonjwa ketu hivi karibuni,n aye amethibitika kuwa ni mwathirika, hivyo hapendi kumwangamiza kijana mdogo kama huyo best yangu.

Sasa sielewi rafiki yangu alikumbwa na pepo au nini, pamoja na kuambiwa ukweli akaona kama anadanganywa na wakati huo muda ulishaenda na maduka yamefungwa na hakukuwa na akiba ya kondom, matokeo yake akajipa moyo na kuzama kavukavu pamoja na jitihada kubwa za binti kumkatalia.

Ni muda sasa umepita, jamaa yangu baada ya kupima nae ameonekana ni hiv+. Hajui amlaumu yule dada au ajilaumu yeye mwenyewe. Yupo hata ukitaka nitakuonyesha.
 
Yani mtu akwambie ameathirika then uendelee kupiga?? It doesn't make sense,i think that's why umejihami hapo chini kwamba tukitaka utatuonesha.

Anyway mayb alikuwa na nyota ya HIV.
 
Yani mtu akwambie ameathirika then uendelee kupiga?? It doesn't make sense,i think that's why umejihami hapo chini kwamba tukitaka utatuonesha.

Anyway mayb alikuwa na nyota ya HIV.
huajawahi kupagawa wewe eh?chezea pale mahala wewe?afu kitu chenyewe kiwe up dated!
 
Yani mtu akwambie ameathirika then uendelee kupiga?? It doesn't make sense,i think that's why umejihami hapo chini kwamba tukitaka utatuonesha.

Anyway mayb alikuwa na nyota ya HIV.
Usishangae ndugu. Kuna ile hali ya mtu kuhisi unadanganywa ila kama ni mimi nisingepiga yango na yango kwa kuwa nimeshatahadharishwa.
 
Dem akwambie anao afu umkule hvyo c vitu vy maskhara ht kdg lbd angesingizia ht kitu ingne sio
 
Ajilaumu mwenyewe kwa kuwa huyo dada alifika mahali akaona amwokoe ili jamaa angalao avae ndom, ndo hivyo tena kichwa cha chini kikakishinda cha juu!!!

Mwingine angeambiwa hiyo ishu ya h.i.v mjegeja ungenywea hapohapo.
 
mmmmmm huyo sio mwanamme wa Dar atakua...mwanmme wa DAR angetoka mbio hata viatu angesamehe..
 
Ukivuta Kaya huwezi Fanya haya.. Ila ukinywa "Kinywaji" lazima ufanye..

Legalize marijuana.
 
Ha ha ha kumbe inawezekana kufanya siku moja na siku hiyo hiyo mkaabukizana??? niliwahi kuulizwa hili swali hapa hapa jf na mie leo nauliza ha ha ha ha ha ha ha
 
Vile watu tunaogopa ukimwi mtu akikuambia ameathirika hata hamu kama ilikua imefikia juu zaidi ya kilele cha mlima Kilimanjaro lazima ikate
 
Back
Top Bottom