Mkasa gani uliowahi kukuta na ukaona akili imefika mwisho bila kutarajia ukapata njia

Captain mopao

Senior Member
Feb 25, 2021
133
379
Habar zenu bandugu,

Mwaka 2014 nilipata mkasa mmoja baina yangu na ndugu yangu mmoja, ukanipeleka jela tulizinguana nikadhani yameisha nikawa nime relax tu mtaani mara gafla defender hio nikapigwa pingu mbele ya raia na mtaani kote hii ilikua siku ambayo sitakuja kuisahau wandugu maana nilidhalilka siku hio walipaki mbali defender wakaja kwa mguu sasa walinitembeza mtaani mpka kufika walipo paki gari ikawa ni gazeti mtaa mzima, baada ya kufika kule bn nilikaa km week moja.

Mama akawa anafatilia dhamana askari aliekua anafatilia ile kesi akamwambia maza hawezi kupata dhamana hapa kituoni maana kagerekezewa makosa mengi subiri akienda mahakaman ukaombe dhamana huko.

Utata ukawa mahakaman sipelekwi nipo tu mule sasa mama akachonga nae askari vipi mbona hamumpeleki mahakaman akasema kesho ntaliiweka jalada lake kwenye losta ya kesi zitakazoenda mahakamani.

Lahaula la kwata yule askar jioni hiyo nae kaingizwa ndani nipo nae nje hakuna msaada tena kipindi kile nilikua nashangaa et askari wakizingua wanawekwa rumande wanalala na vibaka.

Sasa nasikia yeye bosi wake alitokea akaamulu awekwe ndani sikumbuki lilikua kosa gani. Kesho wakamtoa bn na nikafanikiwa kwenda mahakamani, nikapata mdhamana huko kwa muda niliokua nimekaa mule akili ikawa ime luuz balaa kesi ikaanza ikawa kila tarehe inatajwa lakin uhakika wa kutoboa ukawa mdogo nikawa nawaza nikimbie lakin mama nitamuachia msala baada ya kesi kuitwa mara kadhaa nikaja kuona mambo magum nikamtafuta wakili anisimamie kipindi kile kisheria wakili alikua haruhusiwi kusimamia kesi mahakama ya mwanzo ilikua wakili wakili anaruhusiwa kuanzia mahakama ya wilaya kendelea.

Sasa wakili nikamlipa pesa akaanza mchakato wa kuihamishia mahakama kuu ili asimamie tarehe ilipofika nikaenda mahakama kuu, taarifa ikaja kuwa wamechelewa kulifata file langu mahakama ya mwanzo kwa hio yanipasa niludi nikasikilize kesi kule tarehe inayofuata file litakua tayari mahakama kuu wakili aanze majukumu.

Nikarudi mahakaman ya mwanzo kesi ikaitwa awam hii nilimkuta hakimu mwingine yule wa kila siku akawa amepata emergency
Tumesimama pale mbele hakimu anatuuliza mshtaki na mshtakiwa mbona kesi yenu haina mbele wala nyuma? Haya maswala mmeshindwa kuyamaliza huko nyumbani au kwa mtendaji hakimu anazidi kufoka anasema tuna kesi za mauaji zinatuumiza akili hizi kesi za sijui nimetishiwa sijui kaharibu mali ni kesi za kipuuzi zimalizwe kwenye ngazi ya kata huko halafu nyie ndugu hamjui mnatia aibu aka conclude kuwa anafuta kesi tuende tukaelewane nyumbani.

Ilikua ni unexpected day kwangu niliona ni kama yesu ndo kavaa uhakimu mahali pale maana ilikua ni pagumu sana halaf hakimu kamaliza kirahisi ivo hio siku ndo nilijua Mungu yupo kbsaaa jamaa akasaini form kuwa amekubali yaishe na mimi nikasaini nikawa huru, nilivotoka hapo nikahama na mtaa, tukio gani uliwahi kupitia ukavuka ki miujiza?
 
Back
Top Bottom