Mkapa: Wapinzani ni wajinga na hawana adabu

Jana nimebahatika kusikiliza sehemu ya Hotuba ya Mheshimiwa Benjamin Mkapa Katika Uzinduzi wa Kampeni za CCM arumeru.

Moja ya mambo aliyofafanua ni habari za yeye kutoa masharti kabla ya kuzindua kampeni hizo na habari za yeye kuhusishwa na ufisadi wa Ardhi Arumeru.

Kwa mujibu wa bwana mkapa hizi habari ziliandikwa na wapinzani kwenye mitandao yao.

Wanajamvi mnaweza kunisaidia link ya huu mtandao wa wapinzani? Mimi ni mpinzani damu damu lakini nasikitika sijawahi kupata bahati ya ku access huo mtandao wa wapinzani.

Natanguliza shukrani.

Vivy.
 
Mbona hawaanzishi yao ili iwe leading,naona wameliteka vilivyo gazeti la mwananchi,nimeacha kulinunua rasmi
 
Jana nimebahatika kusikiliza sehemu ya Hotuba ya Mheshimiwa Benjamin Mkapa Katika Uzinduzi wa Kampeni za CCM arumeru.

Moja ya mambo aliyofafanua ni habari za yeye kutoa masharti kabla ya kuzindua kampeni hizo na habari za yeye kuhusishwa na ufisadi wa Ardhi Arumeru.

Kwa mujibu wa bwana mkapa hizi habari ziliandikwa na wapinzani kwenye mitandao yao.

Wanajamvi mnaweza kunisaidia link ya huu mtandao wa wapinzani? Mimi ni mpinzani damu damu lakini nasikitika sijawahi kupata bahati ya ku access huo mtandao wa wapinzani.

Natanguliza shukrani.

Vivy.

acha uchokozi wewe...unathani huyo Che Nkapa amependa kwenda pale wamemshurutisha mpaka akaamua yaishe maana kumbuka wana mafaili yake yake ya ANBEN na Kiwira! Kwa hiyo ni mwendo wa kukaa chonjo jambajamba kwenda mbele!
 
Unajua Benjamini Mkapa anachekesha kweli sasa yeye ndiye mgombea wa Arumeru au ni SIYOI kwasababu yeye anaongelea kuhusu wizi wake wa ardhi tu mimi simuelewi
 
TBC TAIFA asubuhi hii wametoja dakika 4 kwa tukio la jana la uzinduzi.ivi tunapelekwa wapi na kodi zetu? Mbona cdm hawapewi muda ivyo,hili bomu kuna siku litalipuka tu.
 
Kutokana na Kuongoza Kampeni Arumeru Mzee Mkapa ameonesha kuchanganyikiwa kwa kutumia muda wake Mwingi kujibu Makombora yanayorushwa kutoka CHADEMA ametumia muda wake Mwingi sana kujitetea katika tuhuma za Ufisadi na kuasisi Ufisadi Papa ikiwemo tuhuma za Uporaji Ardhi,Akihutubia katika viwanja vya Patandi Arumeru Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Msigwa ameendelea kurusha Makombora kwa Serikali ya CCM kuwa ndio chanzo cha maisha Magumu kwa Watanzania hasa wanapopandisha Bei ya Bidhaa ili kuhudumia Marais wastaafu kama Mkapa waliofikisha Nchi hapa ilipo.
Nikiripoti kutoka Tengeru ni mimi Mgosi Mgeni wenu wa jamii forums
 
TBC TAIFA asubuhi hii wametoja dakika 4 kwa tukio la jana la uzinduzi.ivi tunapelekwa wapi na kodi zetu? Mbona cdm hawapewi muda ivyo,hili bomu kuna siku litalipuka tu.
Mkuu wala usihofu.
Yote yatakwisha na ukweli utahulikana
 
Huyu babu anazeeka vibaya.

Hapana; hazeeki vibaya ndivyo alivyo siku zote hata alikpokuwa Mkulu wetu alikuwa hivyo hivyo: tukaingia mkenge. Wakati wa Nyerere alikuwa akijua namna ya kuficha upu-vu wake kwa hiyo watu hawakujua kuwa hivyo ndivyo alivyo. Kuna rafiki yake mmoja aliyekuwa naye hapo DC wakati Mkapa akiwa balozi wetu Marekani, alitushangaa sana kusikia kuwa eti Mkapa ndiye Rais wetu.
 
ukweli utajulikana kwani watanzania wa sasa siyo wa mwaka 47. Hawa ni watanzania siyo wadangatika wa enzi hizo na bahati nzuri vijana wamehamasika vya kutosha siyo kama zamani walidhani kwamba kumkataa mgombea ni kukaa nyumbani wakati wa uchaguzi bali kupiga kura ili kumwongezea ushindi yule wanayemtaka . nawasilisha.
 
Katika namna iliyowashangaza wengi akizindua kampeni za CCM jana huko Arumeru Mashariki, Rais mstaafu Benjamin Mkapa alidai kuwa meneja wa kampeni za CHADEMA, Vincent Nyerere, sio mmoja wa wanafamilia wa Mwalimu Julius Nyerere akidai kipindi chote alichofanya kazi na mwasisi huyo wa Taifa hakuwahi kutambulishwa mtoto yeyote mwenye jina hilo katika familia hiyo.

Mkutano huo wa CCM umeshindwa kuvunja rekodi ya umati wa watu waliofurika juzi wakati CHADEMA ilipozindua kampeni zake, ambapo licha ya kuwa na vikundi vingi vya burudani, idadi ya watu haikulingana na ile ya wapinzani wao.

Source:Tanzania Daima.
 
Unajua Benjamini Mkapa anachekesha kweli sasa yeye ndiye mgombea wa Arumeru au ni SIYOI kwasababu yeye anaongelea kuhusu wizi wake wa ardhi tu mimi simuelewi

Ametuibia sana na bado hana aibu anasimama mbele ya watu aliowaibia na wanampigia makofi. Watanzania majuha kweli!!!

 
uzuri wa maneno kama haya hu-backfire at times we ngoja kamati ya ushindi CHADEMA ije na ushaidi kwamba hata pamoja ya kuwa si mtoto wa kuzaa basi ni mpwa then unaleta picha ya Mwl Nyerere na Young Vincent kwishnei unakuwa ushawasadikisha Wameru! Tena kama inatokea labda Mwl ashawahi shiriki shuguli za Vincent then unaweka picha!

Siasa mchezo mtamu...btw kwani Mkapa ni nani kwa Mwl zaidi ya ukaribu wa kikazi kama mwandishi wa Rais kipindi kile? Mbona yeye hakuwahi kututambulisha sisi baadhi ya watoto aliolea walikuwa wa Mramba na mama Mkapa na si wake wa kuzaa na ukizingatia alikuwa Rais wa JMT kwa miaka 10!? Hizi hekima huenda wap jamani?

Hizi siasa za kuvuana chupi zisije kumwacha uchi mzee wa watu, ohooo!
 
Mkapa alishajichafua sana wakati akiwa madarakani nashangaa analisahau hilo na anakubali kuendelea kutumika kuwasafisha wenzake ilhal yu bado mchafu! Inakuwaje leo anawadanganya wananchi kuwa atamshauri rais afute hati miliki za wawekezaji waliopora ardhi ya wananchi wakati yeye mwenyewe alishiriki ama alibariki uporaji huo na alifikia mahali akasema wazi kuwa watanzania wana wivu na wawekezaji aliowapa ardhi hiyo?
 
Mimi nimefurahishwa tu na maelezo kwamba pamoja na kubeba watu kwenye malori na vikundi vya burudani lakini hawajavunja rekodi ya CDM.
 
Wamlaumu kwanza Yule sharobaro wao Mbowe manake yeye huwa anafikiri kila wakati yuko BILCANAS na kuanza kuporomosha matusi, hawakumbuki aliyoyasema arumeru wanasema ya Mzee Mkapa

mbowe aliporomosha matusi yapi? fanya kama mtoa mada ametaja matusi ya mmiliki wa mgodi wa kiwira,na wewe tueleze mbowe alitoa matusi yapi?
 
Au ni wale wa mdogo wake, shangazi yake wana udgu na mama mdogo, na shemeji kaolewa na kakake mkubwa ndio hapo nikalipata jina la ukoo?
 
Back
Top Bottom