Mkapa: Wapinzani ni wajinga na hawana adabu

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
"Wapinzani ni wajinga na hawana Adabu". Hii ni kauli ya Mkapa. Mzee gani huyu? Nitaiga nini kutoka kwake? Mzee mzima ametoka Dar kwenda Arumeru kutoa matusi?

Je, na mimi nikipewa jukwaa pembeni nikaanza kutoa hotuba kuwa Mkapa ni Mjinga na hana adabu, maneno hayo hayo aliyotumia jukwani tutafika? Inaelekea ametoa matusi kibao ila TBC wameona hayo ndo yanafaa kutuletea kwenye Taarifa ya habari ya saa mbili usiku.

Kwa busara hii inayopaswa kutiliwa shaka na kila Mwenye akili, Mkapa ana sifa zote za kuwa "Mzee wa Dar es Salaam".



Katika namna iliyowashangaza wengi akizindua kampeni za CCM jana huko Arumeru Mashariki, Rais mstaafu Benjamin Mkapa alidai kuwa meneja wa kampeni za CHADEMA, Vincent Nyerere, sio mmoja wa wanafamilia wa Mwalimu Julius Nyerere akidai kipindi chote alichofanya kazi na mwasisi huyo wa Taifa hakuwahi kutambulishwa mtoto yeyote mwenye jina hilo katika familia hiyo.

Mkutano huo wa CCM umeshindwa kuvunja rekodi ya umati wa watu waliofurika juzi wakati CHADEMA ilipozindua kampeni zake, ambapo licha ya kuwa na vikundi vingi vya burudani, idadi ya watu haikulingana na ile ya wapinzani wao.

Source: Tanzania Daima.

Jana nimebahatika kusikiliza sehemu ya Hotuba ya Mheshimiwa Benjamin Mkapa Katika Uzinduzi wa Kampeni za CCM arumeru.

Moja ya mambo aliyofafanua ni habari za yeye kutoa masharti kabla ya kuzindua kampeni hizo na habari za yeye kuhusishwa na ufisadi wa Ardhi Arumeru.

Kwa mujibu wa bwana mkapa hizi habari ziliandikwa na wapinzani kwenye mitandao yao.

Wanajamvi mnaweza kunisaidia link ya huu mtandao wa wapinzani? Mimi ni mpinzani damu damu lakini nasikitika sijawahi kupata bahati ya ku access huo mtandao wa wapinzani.

Natanguliza shukrani.

Vivy.
 
Last edited by a moderator:
Aibu kubwa kwake,si busara kwa mtu kama yeye.hata kama ni kampeni lakini amepitiliza sana.wapinzani kwa muda mfupi ukilinganisha na chama tawala wameleta changamoto nyingi nchini.wapinzani wanasaidia chama tawala kutojisahau.
Ngoja arudi mjini atatukanwa na watoto wadogo sijui atawaambia hawana adabu.
 
Aibu kubwa kwake,si busara kwa mtu kama yeye.hata kama ni kampeni lakini amepitiliza sana.wapinzani kwa muda mfupi ukilinganisha na chama tawala wameleta changamoto nyingi nchini.wapinzani wanasaidia chama tawala kutojisahau.
Ngoja arudi mjini atatukanwa na watoto wadogo sijui atawaambia hawana adabu.

yaani kafanya yale yale aliyoyafanya mbowe juzi
 
Ujinga cyo tusi bali kukosa maarifa ya kitu fulani, na kukosa adabu cyo tusi pia bali ni kukosa busara ktk jambo fulani!
Mimi nawashangaa wanaJF Mnavyobadili mana halisi ya maneno yaliyotumika!
 
Ujinga cyo tusi bali kukosa maarifa ya kitu fulani, na kukosa adabu cyo tusi pia bali ni kukosa busara ktk jambo fulani!
Mimi nawashangaa wanaJF Mnavyobadili mana halisi ya maneno yaliyotumika!
Wamlaumu kwanza Yule sharobaro wao Mbowe manake yeye huwa anafikiri kila wakati yuko BILCANAS na kuanza kuporomosha matusi, hawakumbuki aliyoyasema arumeru wanasema ya Mzee Mkapa
 
Mkapa kwanza aturudishie Kiwira yetu aliyotuibia akishirikiana na mkewe kama Marcos na Imelda. Ni mzee wa Aibu aliyepewa bucha achunge yeye akamaliza nyama yote!
 
Sikumsikia Mbowe, sijamsikia Mkapa! Kama wameanza kwa matusi basi mstakabali wa uchaguzi uko kwenye mzani. Niko njiani kwenda Arumeru kujionea.
 
Huyu mzee hana hekima aisee! Ina dr. Slaa, mbowe, lipumba, lisu, lema, myika, mtei, marando, zito, pamoja na vjana woooote nchini hatuna adabu.!. Na hatia yote hiyo hajioni? Masikini anatembea peku kisa hana pesa za viatu, mkapa anatembea peku mda mwingine kisa unene na kuridhika na fedha zetu alafu leo anatu tusi. Ah wee ngoja tu.
 
Mzee Mkapa alikuwa anamjibu yule Kaka yake yule SHOGA wa Marekani, Sharobaro MBOWE anayewatukana watu kuwa ni weupe akimaanisha hawana akili. Hivi kweli huyu Mbowe ni Mwenyekiti wa CHama? Machangudoa wa Bilkanas wamemharibu sana huyu bwana mdogo. Bora hata Mzee Mkapa ameliona hilo

naona upo kwenye practical ya kutukana kwa maandishi..jitahidi ivyo ivyo..utajua tu
 
Yule mzee ana bahati sana kuendelea kuwa uraiani kwa ufisadi aliofanya. Ndio maana anasimamia uovu aliouanzisha katika CCM. Ila akae akijua kuwa wana wa Meru wana other ideas kwa sasa, wanataka Nassary mjengoni na sio mvuta bange Siyoi
 
Mkapa kasema wameandika kwenye mtandao wao kuwa yeye Mkapa amewazulumu wananchi wa Arumeru aridhi kwamba anaubia na mgeni mmoja kutoka nje nawamepora aridhi ya wanaarumeru mashamba makubwa manne na pia Mkapa amekanusha kumiliki aridhi yoyote arumeru na hajapora aridhi yoyote kutoka kwa mwananchi yoyote hapa nchini.Kilichonichosha ni pale TBCkuisoma habari hii ya ndani baada ya habari za kimataifa.
 
Back
Top Bottom