Setuba Noel
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 426
- 210
Mh! Hapa umetuingiza chaka, hili tukio halijapata kutokea katika historia ya Mwalimu. Kansa yake iligunduliwa 1998, mwaka mmoja baada ya ile birthday yake maarufu ya 75 (mwaka 1997) ambako katika hotuba alikuwa amesema "....nitapiga makumi mawili manne, NINA HAKIKA! Nitamwona rais wetu wa nne, NINA HAKIKA" akimaanisha alikuwa na uhakika wa kuishi miaka zaidi ya themanini na kuchagua hadi rais wetu wa nne.Kwa wale tuliokuwa watu wazima 1989 tunakumbuka Jinsi Mwalimu alivyolazwa Uingereza kwa matibabu ya Kansa (Saratani) ya damu ambayo hatimaye ndiyo ilikuja kumuua.
Hizi tabia za kusahau mambo ya msingi ndiyo imetufikisha hapa tulipo. Toka 1989 hadi leo 2012 imepita miaka 23 huyu Vincent alikuwa wapi kutuambia kwamba Mkapa amempa Mwalimu Sumu itakayokuja kumuua? Kama amejua siku za hivi karibuni ni nani aliyemwambia? Hivi mwaka 1989 wakati Mwalimu anafanyiwa Opresheni ya kuzuia kansa kusambaa mwilini mwake Mkapa alihusikaje?
Duh mkuu wangu umerukia treni kwa mbele...Haya cheza James Bond chini kwa chini urudi nyuma utalipata jibu..
- Ninajiuliza swali moja hawa wote ni Familia moja, sasa wanapochafuana huko Arumeru as they have done, linakuja swali moja kubwa je hawa wanafamilia moja wana siri ngapi zingine hawajatuambia wa-Tanzania? Au tusubiri kampeni nyingine ya siasa tuwapange tena tusikie zaidi? Just curious!
- Lakini hawa wana siri nyingi tunahitaji kuzijua Wananchi wa Tanzania!, sasa wapangwe tena another kampeni!, I mean kinachoendelea huko Arumeru ni serious business:
- HOWEVER: hivi kweli CCM haikuwa na mwingine wa kumpeleka Arumeru zaidi ya Mkapa? I mean kweli Viajna wote walioko CCM Why him?
FMEs!
Duh ama kweli wewe mgumu sana kuelewa. Sizungumzii alichoandika FMES isipokuwa ulichoandika wewe dhidi ya maneno ya Mkapa.. Mkapa alisema hivi:-Nimefanya kazi na Mwalimu kwa miaka 25, nikiwa mwandishi wake, Waziri na katika muda huo, nimemzika yeye, kaka yake na mama yake mzazi, sijawahi kusikia jina la mtu kama huyo katika familia hiyo.
Ndipo VN na Madaraka wakaingilia kati na kuweka habari hii sawa. Kwa kauli ya Mkapa alikuwa na maana Ukoo (katumia familia hiyo)maana kamhusisha hadi kaka na mama yake mwalimu ndio maana Madaraka na VN wakamwaga mboga.
..Mkapa alilenga kumdhalilisha Vicent Nyerere. tatizo ni kwamba hawa ndugu zetu wa kutoka Mara dharau ni kitu ambacho hawa-entertain hata siku moja.
..alichotakiwa kufanya Mkapa ni kumdadisi Vicent Nyerere directly, kwa uungwana, au kuwatafuta kina Makongoro,Madaraka,Magige, na kuwauliza habari za Vicent.
NB:
..haiyumkiniki Mkapa akawa hamfahamu Josephat Kiboko Nyerere, baba mzazi wa Vicent Nyerere.
- Wakuu ndio tatizo letu wa-Tanzania, mara ngapi wakati wa kumbu kumbu za Mwalimu tumesikia Familia ya Mwalimu wakisema Mkapa ni mwana-familia yao? Magazeti mengi sana yamewahi kusema haya kwamba Mkapa ni familia ya Mwalimu sasa why leo mnashangaa?
- Hebu atokee mwanafamilia ya Mwalimu aseme bila uoga kwamba hawajawahi kusema Mkapa ni member wa familia yao! Tuwakumbushe siku na tarehe na aliyeyasema na wapi, WA-Tanzania sio mabwege tena siku hizi, hawa ni familia moja bana! sasa watumabie what else they know au wanaficha kuhusu Taifa!
Es!
Ahaaaa kumbeeMkuu FMES,
Habari za Nyerere kumalizwa na Mkapa tulishasikia miaka mingi iliyopita Vicent karudia tena vyombo vya habari vimeamua kuipatia umuhimu kwasababu aliyesema ni mwanaukoo wa Nyerere.Mkuu FMES hakuna siri nyingine zaidi ya hii kwamba Nyerere alitangulizwa kabla ya siku zake ili wauze benk yetu ya NBC kwa bei poa,waingie mikataba mibovu ya uchimbaji wa madini,wanunue ndege ya rais ikibidi tule majani,wanunue rada kwa bei kubwa kupita kiasi na wauze viwanda vyetu kwa marafiki zao kwa bei poa.
Yote haya yasingefanyika kama Nyerere asingetangulizwa mapema,bahati mbaya Nyerere hakumjua Mkapa hadi aliposhiriki kumuingiza magogoni kwa gharama kubwa sana ikiwemo kuwapakazia na kuwachafua washindani wake ndani ya CCM na nje ya CCM.
- Wakuu ndio tatizo letu wa-Tanzania, mara ngapi wakati wa kumbu kumbu za Mwalimu tumesikia Familia ya Mwalimu wakisema Mkapa ni mwana-familia yao? Magazeti mengi sana yamewahi kusema haya kwamba Mkapa ni familia ya Mwalimu sasa why leo mnashangaa?
- Hebu atokee mwanafamilia ya Mwalimu aseme bila uoga kwamba hawajawahi kusema Mkapa ni member wa familia yao! Tuwakumbushe siku na tarehe na aliyeyasema na wapi, WA-Tanzania sio mabwege tena siku hizi, hawa ni familia moja bana! sasa watumabie what else they know au wanaficha kuhusu Taifa!
Es!
Lakini mkuu wangu sii aliyefungua mjadala ni Mkapa mwenyewe..sasa tatizo liko wapi kumjadili mwanafamilia ambaye sisi hatukujua?..wanajf,hakuna jipya wanarudia rudia tu,mod maliza mjadala kama ile ya ubadhilifu ya cdm,mod be fair