Mkuu FMES,
Habari za Nyerere kumalizwa na Mkapa tulishasikia miaka mingi iliyopita Vicent karudia tena vyombo vya habari vimeamua kuipatia umuhimu kwasababu aliyesema ni mwanaukoo wa Nyerere.Mkuu FMES hakuna siri nyingine zaidi ya hii kwamba Nyerere alitangulizwa kabla ya siku zake ili wauze benk yetu ya NBC kwa bei poa,waingie mikataba mibovu ya uchimbaji wa madini,wanunue ndege ya rais ikibidi tule majani,wanunue rada kwa bei kubwa kupita kiasi na wauze viwanda vyetu kwa marafiki zao kwa bei poa.
Yote haya yasingefanyika kama Nyerere asingetangulizwa mapema,bahati mbaya Nyerere hakumjua Mkapa hadi aliposhiriki kumuingiza magogoni kwa gharama kubwa sana ikiwemo kuwapakazia na kuwachafua washindani wake ndani ya CCM na nje ya CCM.