Mkoa wa Mara naufahamu vizuri sana; una makabila zaidi ya 12. Waryoba ni Muikizu wa Nyamuswa, Msuguri ni Mzananki kama Nyerere mwenyewe kwao ni Butiama, Wassira ni Mshashi (au Msizaki) wa Ushashi ingawa sasa hivi anakaa Bunda, Marehemu Nyirabu alikuwa Mkuria wa Tarime. Ukiachia Msuguri, wote hao unaowasema hawana undugu na Nyerere, ingawa wakati fulani Wassira aliwahi kumwoa binti wa Chifu Wanzagi kwa muda mfupi wakati akiwa akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
- Sidhani kuwa teuzi za Wassira zilitegemea ndoa hiyo ya binti Wanzagi kwa vile tayari alikuwa keshateuliwa mara mbili kabla ya ndoa hiyo na hata baada ya kuachana na huyu binti wa Wanzangi bado Wassira aliteuliwa mara nyingi hasa wakati wa Mwinyi hadi pale alipopigwa stop na Waryoba kufuatia kinyanganyiro cha ubunge; nina imani kuwa unajua kuwa hata JK amemteua tena.
- Nina imani kuwa Waryoba aliteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa qualifications zake; sijui kama unasema kuwa hakuwa na qualifications au vipi, ila ninajuwa alikuwa kati ya wanasheria wa kwanza kwanza nchini hapa. Na alianzia chini akapanda pole pole mpaka hapo. Uteuzi wake kuwa Waziri Mkuu ulifanyika wakati wa Mwyinyi kwa hiyo siwezi kuita wa Nyerere.
- Kuhusu mkuu wa majeshi inawezekana kuwa ni kweli alimteua ndugu yake Musuguri, hata hivyo angalia kuwa population kubwa ya jeshi inatoka mkoa wa mara, na hiyo imejionyesha kwa kuwa na wakuu watatu wa majeshi kutokea mkoa huu. Nyerere aliteua mmoja tu kati ya hao watatu, wengine wameteuliwa na Mwinyi (General Kiaro) na Mkapa (General Waitara).
- Ninavyofahamau, Nyirabu aliteuliwa kuwa gavana wa benki kuu kwa vile ndiye aliyekuwa second to Mtei wakati huo. Mtei alikuwa gavana wa kwanza na alipopata promotion nafasi hiyo ikaenda kwa mtu aliyekuwa wa pili yake; sidhani kama huo ulikuwa ni ukabila. Mtu closest kwenye position hiyo angekuwa Bob Makani ambaye kwa bahati mbaya hakuwa mchumi.
Kichuguu.
Bob Makani unasema hakupewa kwa vile hakuwa na digrii ya uchumi. mbona Mtei alipewa akiwa na Literature? wakati Makani ana sheria ambayo kidogo inafanana.
Baada ya Nyirabu alikuja Rutihinda kuwa gavana, huyo alikuwa na Political Science na International Relations.
Nadhani Makani hakupewa kwa dini yake lazima tukubali Mwalimu alivyokuwa Mdini.
Back 2 Warioba kuwa alikuwa na Qualification ndio akapewa uwaziri mkuu,na Jaji Chande ana Qualification zaidi ya Warioba au Augustino Ramadhani.sasa unataka tuamini kuwa Qualification ni kigezo, wakati jana ulisema kuwa SENIORITY ndio kigezo. mkuu sikuelewi kabisa!Chande ana exposure kubwa sana ambayo hana Warioba wala Jaji mkuu mpya.
Nakurudisha UDSM nyumbani kwako. wakati anatafutwa Dean wa Faculty ya Commerce and Management- Assad Mussa akamshinda vibaya Chijoriga kwa qualification na Seniority, akapita kwenye interviews zote. lilipofika File kwa Luhanga-VC wenu akampa bibi Chijoriga kwa madai ya Gender. hili limelieleza sana kwenye Mada ya Mzumbe VS UDSM nenda kwenye elimu utaona.
U-TURN ya Luhanga kuwa ni Gender imetoka wapi? mtu akija na Qualfication kama Chande unasema unataka Seniority. ikija Seniority kama DR.Assad unasema GENDER ISSUE and Globalization.
Warioba alipewa uwaziri mkuu kwa upendeleo kigezo cha elimu hakihusu kwa cheo cha uwaziri mkuu. ndio maana unaona Sumaye alipewa madaraka hayo huku akiwa hana elimu. baada ya kumaliza Uwaziri mkuu ndio amekwenda kusomea Management skills, wakati alitakiwa awe na Knowledge hiyo kabla ili apply kwenye uwaziri mkuu wake.
Na kwa taarifa yenu Course work na Dissertation amefanyiwa na vijana wa kikenya.
Nawaomba WaTanzania tusibaguane wote wapewe vyeo. kama balance ya Muungano inatazamwa why not ya Dini?