Mkapa angewafaa zaidi Waislam Kuliko Kikwete

Status
Not open for further replies.

Nungwi

Senior Member
Sep 9, 2006
196
12
Rais Mstaafu Mkapa alikuwa na nia madhubuti ya kuwasaidia waislam,kuna mengi amefanya ambayo si dhambi, mfano wa chuo kikuu cha Morogoro cha waislam, zaidi ni pale Waziri mkuu Sumaye alipoteua bodi ya PAROLE ambapo waziri Sumaye aliweka wakristu watupu na mzee Mkapa akakataa kuipa baraka bodi ile kuwa haina usawa.

nimefuatilia chaguzi za Kikwete kwa muda mrefu amekuwa akienda kinyume na Mstaafu Mkapa.juzi kachagua Jaji mkuu ambaye ni MKRISTO.

Chaguzi nyinyi tu toka kwa Waziri Membe kupewa mambo ya nje kulienda sambamba na mawaziri wa nne wote wakristu. hivi karibuni kachaguliwa mkuu wa magereza na makamishina wanne wote wakristu.

Naomba tuwe wa kweli. waislam wako nyuma inabidi kuwepo na juhudi ya maksudi ya kuwasaidia. na sisi humu JF tunaliona hili lakini tunaacha ikifikia hali ya RWANDA au Burundi tutakaa?

Mtu kama Professor Idrisa Mtulia aliyekuwa katibu mkuu wa Afya na daktari wa Rais Mwinyi hajapata hata uwaziri ndani ya kundi la watu sitini jee hana sifa au hakuwa mtandao?.

Mkapa angemchukua huyu Professor, kweli David Mathayo anamzidi Professor Mtulia? au Jaji Chande alifaaa kuwa jaji mkuu amefanya kazi sehemu nyingi ikiwa na UN.

Nataja nafasi chache ambazo hazina uwiano baina ya waislam na wakristu.

SPIKA -mkristu, Jaji mkuu-MKRISTU,mkuu wa uhamiaji-mkristu, mkuu wa magereza-mkristu,DPP-mkristu,mkuu wa majeshi-mkristu. mkuu wa polisi-muislam,mkuu wa usalama-muislam, jaji kiongozi-mkristu, Mwanasheria mkuu-mkristu, DCI-mkristu, Mkuu wa PCB-mkristu, Chief of staff jeshini-mkristu,mwenyekiti tume ya uchaguzi-mkristu, mwenyekiti usajili wa vyama vya siasa-mkristu.
Gavana-mkristu,mhasibu mkuu-mkristu, Auditor General-mkristu,Commissioner wa TRA-mkristu, Katibu wa bunge -mkristu, katibu mkuu ofisi ya rais-Mkristu,mkurugenzi mkuu wa TVT-mkristu huyu bwana ni kidato cha nne-form four leaver angekuwa muislam tungesema hana sifa.

jamani fuatilieni wakuu wa wilaya na maafisa tawala. Najua subject hii itapata upinzani kwa vile watu hatutaki kuwa wakweli. si vizuri nchi kuwainamilikiwa na watu wa upande mmoja.

Kikwete huwatendei haki ndugu zako. mie nakusaidia uwainue waislam ikitokea vita itatuumiza wote.

Professor Mtulia anatatizo gani? hana uzoefu au qualification? DR.Nagu anamshinda Mtulia? au jaji mkuu Augustino CV yake haifanani na ya Jaji Cahnde mtu anayekubalika na UN amekwenda hadi Iraq.

naomba michango yenu yenye nia ya kujenga taifa imara lenye mshikamano wa kweli.

MFICHA MARADHI KIFO KITAMUUMBUA.Mwanakijiji na wote tunaomba michango yenu hapa.
 
Mimi naona Nungwi umekuja na lako jambo! haya maswala ya dini yametoka wapi tena. Mbona hujatwambia nani angewasaidia zaidi kina mama kati ya Mkapa na JK? maanake kati yao hakuna anayeweza kubadilisha jinsia yake.
 
Mkandara.

Juhudi za kuwainua wanawake zipo ndio unaona Rita Mlaki anapata uwaziri ingawa kichwani hakuna kitu na JK ametamka mara nyingi kuwa ana nia ya kuwainua wanawake. lengo ni asilimia zaidi ya 45.
Hilo limejionesha wazi kwenye baraza lake la mawaziri lilivyo balance.
 
Nungwi,
1.Raisi hajateua Gavana wa BOT. Lakini waziri wa fedha na manaibu waziri wote ni waislamu.

2.Raisi ameteua Mhasibu Mkuu Muislamu tena Mwanamke. Naomba umpongeze kwa uteuzi huo.

3.Jaji Kiongozi ni Muislamu, Amiri Manento. Tatizo anatokea Kilimanjaro ambako una matatizo nako.

4.Jaji Mkuu, kwa mara ya kwanza Raisi ameteua Mzanzibari. Hiyo ni katika kudumisha Muungano.

5.Spika wa Bunge hateuliwi na Raisi. Usimbebeshe lawama asizostahili.

6.Usimnyanyase Tido Mhando kwamba ana elimu ndogo. Uzoefu wake Idhaa ya Kiswahili BBC unamuzesha kuongoza chombo chochote cha habari Tanzania.

7.Raisi anapotafuta Jaji Mkuu mara nyingi huangalia kuanzia ngazi ya Jaji Kiongozi, na Majaji wa Mahakama ya Rufaa. Jaji Othman Chande hayuko ktk nafasi hizo.

8.Raisi aliteua Majaji wawili wa Mahakama ya Rufaa. Mmoja alikuwa anatokea Zanzibar na mwingine Bara. Sijui kwanini ile nafasi ya Bara hakumpa Othman Chande. Labda hawaivi, au Jaji Chande ni junior sana ktk Majaji wa Mahakama Kuu.

9.Kuhusu Prof.Idirisa Mtulia, mkoa wa Pwani tayari wamepewa Uwaziri kupitia Dr.Eng.Shukuru Kawambwa. Katika mazingira hayo inabidi umpambanishe Dr.Kawambwa na Dr.Mtulia. Mary Nagu yeye amepewa kwasababu anatokea Manyara, na zaidi ni mwanamama.
 
Mzee Nungwi,

Heshima yako mkuu, mimi nilifikiri the deal ni Kikwete kuwasaidia wanachi wote au taifa letu kwa ujumla kama Tanzania, sasa hayo mambo ya kuwasaidia Waisilamu peke yao, tutafika kweli?

Napinga hoja za Nungwi zilizojikita kwenye udini.
Sielewi kama ana maana ya kwamba waTanzania wasio waislamu sio ndugu zake Kikwete. Na je, hao wasio na dini nao wameonewa au wamependelewa na huyo Kikwete. Je, makabila je? Wakwere wametendewa haki chini ya Kikwete au hapana?

Je, kuwa na jina la kikristo au kiislamu hata kama mhusika hashiriki na dini hizo inatosha kuwa mwakilishi? Au hapo baadae tutaanza kudai kila atakayeteuliwa katika cheo ni lazima awe anahudhuria kanisani au msikitini mara kadhaa kwa siku au wiki?

Prof. Mtulia ni mtaalam wa nini. Paediatrics (watoto)? nadhani. Alipewa ukatibu wa wizara, hakufanya vizuri hata kidogo. Ungependa kumwongelea huyo prof. kwa sifa zake za kiutendaji kazi ingekuwa bora zaidi kuliko kuhusisha dini yake.

Naelewa sio rahisi kwa wengi, lakini ni mhimu sana kwetu kama taifa, sifa ya kwanza kabla ya nyingene nyingi, iwe ni uTanzania wetu sote. Sijui kama kuwa na sifa ya ukristo au uislamu kunaongezea ufanisi katika utendaji wa kazi wa mteuliwa. Na sijui kama dini ya mhusika binafsi ni faida kwa shirika la dini au waumini wa dini hiyo.
 
Kalamu,
1.Prof.Idirisa Mtulia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo.

2.Huyu Nungwi na kikundi chake huwezi kuwaridhisha hata kidogo. Katika huo huo Uislamu kwa mfano wanaona Waislamu wa Kilimanjaro siyo Waislamu kamili. Wanadai Kilimanjaro hawana asili ya Uislamu.
 
Joka kuu.
Nungwi si muislam huyo ni mtu wa Professor Warioba wa Mzumbe University labda Mzumbe kuna kikundi cha mujahidina.
 
Hii analysis iliyoletwa na Nungwi kutoka LSE ina walakini; inahitaji masahihisho makubwa.
 
Wandugu,
1. Sababu za hii imbalance ni Historical- tangu wakati wa ukoloni. Ni kweli kuwa positions nyingi zipo chini ya Wakristo- na Waislamu nao wanaona! Statistics zinaonyesha popolation Waislam na Wakristo tuko sawa. Sii vibaya kuchukua hatua za makusudi to address such imbalances ktk nafasi za juu! Kwa vile kwa sasa kuna Waislamu wengi wamesoma- kama Wakristo- nao wapewe nafasi na upendeleo wa namna fulani! Na upendeleo huu uangalie pia yale makabila yalioachwa nyuma!
Hii ni kwa new positions! Kukiwa na nafasi mpya za kazi if equally wote wanaqualify then we thrive to balance na kutoa upendeleo! Mbona tuanvyoandress maswala ya kina mama tunasema hao waliachwa nyuma due to social and cultural reasons? Kwa nini dini tunasita? Huu sii ubaguzi? Ukikaa kimya ndo pale unakuta TRA wengi Wachaga! Jeshini- ni Mara! Sijui nchi nyingine wana utaratibu gani- sisi ofsini kwetu 90% ni Wakristo na tulisoma na Waislam wengi tu- na walipasi vizuri!
2. One way to address such imbalances ni kuwa na Quota system kuanza na Wanafunzi wanaoingia Vyuo vikuu vya Uma- kila Wilaya itoe say 100 students- pia tubalance kwa gender na dini! The same applies katika ajira- kama wanaajiriwa walimu Dodoma University 100 na kama both wanqualify- ni vyema kujaribu kubalance- hata kama unawapendelea waislam zaidi- Mbona SUA, UD na Mzumbe more than 70% tayari waalimu ni Wakristo!
Namuunga mkono Nungwi!
 
Kalamu,
1.Prof.Idirisa Mtulia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo.

2.Huyu Nungwi na kikundi chake huwezi kuwaridhisha hata kidogo. Katika huo huo Uislamu kwa mfano wanaona Waislamu wa Kilimanjaro siyo Waislamu kamili. Wanadai Kilimanjaro hawana asili ya Uislamu.

Madai haya ya Kilimanjaro unaweza kuyathibitisha?

Professor Mtulia kuwa waziri ni sawa.DR.Kawambwa hazuii kwa vile wanatoa mkoa wa Pwani. mbona kuna wilaya ina mawaziri wawili, nayo ni RUNGWE -Mbeya.wilaya hii imetoa waziri Mwakyusa na Mwakyembe kama ajabu ianzie huko.

kuna waziri Mwandosya nae anatoka MBEYA.

Naamini Mtulia angefaa afya ni mkali kuliko Mwakyusa.
 
Wandugu,
1. Sababu za hii imbalance ni Historical- tangu wakati wa ukoloni. Ni kweli kuwa positions nyingi zipo chini ya Wakristo- na Waislamu nao wanaona! Statistics zinaonyesha popolation Waislam na Wakristo tuko sawa. Sii vibaya kuchukua hatua za makusudi to address such imbalances ktk nafasi za juu! Kwa vile kwa sasa kuna Waislamu wengi wamesoma- kama Wakristo- nao wapewe nafasi na upendeleo wa namna fulani! Na upendeleo huu uangalie pia yale makabila yalioachwa nyuma!
Hii ni kwa new positions! Kukiwa na nafasi mpya za kazi if equally wote wanaqualify then we thrive to balance na kutoa upendeleo! Mbona tuanvyoandress maswala ya kina mama tunasema hao waliachwa nyuma due to social and cultural reasons? Kwa nini dini tunasita? Huu sii ubaguzi? Ukikaa kimya ndo pale unakuta TRA wengi Wachaga! Jeshini- ni Mara! Sijui nchi nyingine wana utaratibu gani- sisi ofsini kwetu 90% ni Wakristo na tulisoma na Waislam wengi tu- na walipasi vizuri!
2. One way to address such imbalances ni kuwa na Quota system kuanza na Wanafunzi wanaoingia Vyuo vikuu vya Uma- kila Wilaya itoe say 100 students- pia tubalance kwa gender na dini! The same applies katika ajira- kama wanaajiriwa walimu Dodoma University 100 na kama both wanqualify- ni vyema kujaribu kubalance- hata kama unawapendelea waislam zaidi- Mbona SUA, UD na Mzumbe more than 70% tayari waalimu ni Wakristo!
Namuunga mkono Nungwi!

Tukitaka kufanikiwa basi tuwe tunaangalia (a) kabila la mtu (siyo mkoa kwani mipaka ya mikoa ni arbitrary), (b) gender ya mtu, na (c) dini ya mtu.

Nina imani kuwa tukianza kutoa vyeo vya serikali kwa kufuata vigezo hivi, tujue tumegawanya taifa kwenye vipande vidogovidogo sana na tutaanza kuwa tunapoteza utaifa wa nchi hii. Najua mikoa mingine kama Mara ina vikabila vingi sana karibu 13, na nchi hii ina dini nyingi sana. Kwa sasa hivi wengi wanaangalia dini kwa msingi wa ukiristo na uislamu bila kujua ukisha sema dini basi utatakiwa uwape nafasi sawa wasabato, warutheli, wakatoloki, na dini nyingine katika ukristo sawa na wasunni, washiite, waahamdiyya, wasikh na dini nyinge za kiislamu; hiyo ndiyo fairness kwa dini zote kwa vile nyingi zinatofautiana kifilosofi.

Mimi ninadhani kuwa open competition isiyotegemea upendeleo wa Rais pekee ndiyo njia nzuri. Ni lazima tupunguze madaraka ya rais katika uteuzi kiasi kuwa mteuliwa anakuwa ni matokeo ya collective efforts za rais na wabunge wote labda na tume huru ya utumishi serikalini.
 
Rais Mstaafu Mkapa alikuwa na nia madhubuti ya kuwasaidia waislam,kuna mengi amefanya ambayo si dhambi, mfano wa chuo kikuu cha Morogoro cha waislam, zaidi ni pale Waziri mkuu Sumaye alipoteua bodi ya PAROLE ambapo waziri Sumaye aliweka wakristu watupu na mzee Mkapa akakataa kuipa baraka bodi ile kuwa haina usawa.

nimefuatilia chaguzi za Kikwete kwa muda mrefu amekuwa akienda kinyume na Mstaafu Mkapa.juzi kachagua Jaji mkuu ambaye ni MKRISTO.

Chaguzi nyinyi tu toka kwa Waziri Membe kupewa mambo ya nje kulienda sambamba na mawaziri wa nne wote wakristu. hivi karibuni kachaguliwa mkuu wa magereza na makamishina wanne wote wakristu.

Naomba tuwe wa kweli. waislam wako nyuma inabidi kuwepo na juhudi ya maksudi ya kuwasaidia. na sisi humu JF tunaliona hili lakini tunaacha ikifikia hali ya RWANDA au Burundi tutakaa?

Mtu kama Professor Idrisa Mtulia aliyekuwa katibu mkuu wa Afya na daktari wa Rais Mwinyi hajapata hata uwaziri ndani ya kundi la watu sitini jee hana sifa au hakuwa mtandao?.

Mkapa angemchukua huyu Professor, kweli David Mathayo anamzidi Professor Mtulia? au Jaji Chande alifaaa kuwa jaji mkuu amefanya kazi sehemu nyingi ikiwa na UN.

Nataja nafasi chache ambazo hazina uwiano baina ya waislam na wakristu.

SPIKA -mkristu, Jaji mkuu-MKRISTU,mkuu wa uhamiaji-mkristu, mkuu wa magereza-mkristu,DPP-mkristu,mkuu wa majeshi-mkristu. mkuu wa polisi-muislam,mkuu wa usalama-muislam, jaji kiongozi-mkristu, Mwanasheria mkuu-mkristu, DCI-mkristu, Mkuu wa PCB-mkristu, Chief of staff jeshini-mkristu,mwenyekiti tume ya uchaguzi-mkristu, mwenyekiti usajili wa vyama vya siasa-mkristu.
Gavana-mkristu,mhasibu mkuu-mkristu, Auditor General-mkristu,Commissioner wa TRA-mkristu, Katibu wa bunge -mkristu, katibu mkuu ofisi ya rais-Mkristu,mkurugenzi mkuu wa TVT-mkristu huyu bwana ni kidato cha nne-form four leaver angekuwa muislam tungesema hana sifa.

jamani fuatilieni wakuu wa wilaya na maafisa tawala. Najua subject hii itapata upinzani kwa vile watu hatutaki kuwa wakweli. si vizuri nchi kuwainamilikiwa na watu wa upande mmoja.

Kikwete huwatendei haki ndugu zako. mie nakusaidia uwainue waislam ikitokea vita itatuumiza wote.

Professor Mtulia anatatizo gani? hana uzoefu au qualification? DR.Nagu anamshinda Mtulia? au jaji mkuu Augustino CV yake haifanani na ya Jaji Cahnde mtu anayekubalika na UN amekwenda hadi Iraq.

naomba michango yenu yenye nia ya kujenga taifa imara lenye mshikamano wa kweli.

MFICHA MARADHI KIFO KITAMUUMBUA.Mwanakijiji na wote tunaomba michango yenu hapa.

Udini mimi huwa nauogopa sana. Huwa napata mashamsham ya kuingia kwenye mijadala ya udini lakini najua mwisho wake huwa si mzuri. Badala ya kujiona kama sisi wote ni Watanzania tunaanza kujigawa kwa makundi ya udini.

Kumbukeni Rwanda na burundi huko kuna makabila mawili tu Wahutu na Watusi, matokeo ya mifarakano yao wote tunayajua sina haja ya kuyarudia hapa. Hivyo nawaombeni kama mnataka kujadili udini basi muwe wastaarabu kitu ambacho ni kigumu mno, vinginevyo mtaipeleka JF pabaya.
 
Nadhani tumeanza kuchakaa kimtazamo.Baada ya hapo tutasema Kikwete kachagua watu wenye rangi ya maji ya kunde wengi zaidi ya wale weusi kama mimi. Kisha tutasema watu wenye miili minene hawajawakilishwa ipasavyo kwenye baraza la mawaziri.Burudani tupu.

Huu mjadala ni mzaha tupu.Mimi hata akiteua baraza zima mabudha hainiumizi kichwa kama hawa watu wana uwezo na dhamira isiyohojika katika kulikwamua taida dhidi ya umaskini.Serekali itengeneze mazingira watu wakamue kwa uwezo wao na si dini zao.

Watu wanafukarishwa kutokana na uwezo mdogo na ufisadi wa viongozi,nchi inaliwa na sisi tuangalia dini za watu.Hawa viongozi wangekuwa na dini kama tunavyofundishwa makinsani na misikitini mbona taifa lingekuwa mbali sana.

Hivi ni dini gani hiyo ambao inaunga mkono upuuzi kama wa richmond, ni dini gani inayosimamia umalaya na uwizi wa kura.Hawa viongozi dini ni kama NGO yoyote ile na wanazitumia kupandia ngazi na kutwaa madaraka.Kwa kuwa tupo ambao tunashangilia dini basi wao wataendelea kupeta.Mtu Mchamungu asingeweza kufanya kazi ndani ya CCM.Maandiko hayaendani na maamuzi na vitendo vya serekali ya CCM.Ila kama dini ni majina basi tuendelee kujadili
 
Tukitaka kufanikiwa basi tuwe tunaangalia (a) kabila la mtu (siyo mkoa kwani mipaka ya mikoa ni arbitrary), (b) gender ya mtu, na (c) dini ya mtu.

Nina imani kuwa tukianza kutoa vyeo vya serikali kwa kufuata vigezo hivi, tujue tumegawanya taifa kwenye vipande vidogovidogo sana na tgutaanza kuwa tunapoteza utaifa wa nchi hii. Najua mikoa mingine kama Mara ina vikabila vingi sana karibu 13, na nchi hii ina dini nyingi sana. Kwa sasa hivi wengi wanaangalia dini kwa msingi wa ukiristo na uislamu bila kujua ukisha sema dini basi utatakiwa uwape nafasi sawa Wasabato, warutheli, wakatoloki, na dini nyingine katika ukristo sawa na Wasunni, Washiite, Waahamdiyya, wasikh na dini nyinge za kiislamu, hiyo ndiyo fairness kwa vile nyingi zinatofautiana kifilosofi.

Mimi ninadhani kuwa open competition isiyotegemea upendeleo wa Rais pekee ndiyo njia nzuri. Bi lazima tupunguze madaraka ya rais katika uteuzi kiasi kuwa mteuliwa anakuwa ni matokeoa ya collective efforts za rais na wabunge wote labda na tume huru ya utumishi serikalini.
Kichuguu.
Kama unakumbuka huko nyuma, JK alishambuliwa sana kuwa Mdini sasa michango kama hii (yako)haikuonekana. nadhani kuna double standards.
 
Kichuguu.
Kama unakumbuka huko nyuma, JK alishambuliwa sana kuwa Mdini sasa michango kama hii (yako)haikuonekana. nadhani kuna double standards.
Inategemea ilikuwa lini; kuna kipindi huwa sichangii sana kutokana na majukumu mengine. Kuanzia mwezi wa tano nimechangia sana na hakukuwa na mada inayohusu udini katika utoaji vyeo niliyoona labda kama ilichanganywa kwenye mojawapo ya threads ambazo sikusoma.
 
Kikwete amewateua hawa viongozi kwa kuwa ni wakristo, au kwa vile ni waTanzania walio na sifa zinazotakiwa katika nafasi hizo?

Mzalendo Halisi ametoa hoja nzuri zaidi hapo chini, kwamba darasani kwake walikuwepo wanafunzi wengi tu wenye majina ya kiislamu, tena waliokuwa na maendeleo mazuri kabisa katika masomo. Sasa swali mhimu la kujiuliza nadhani ni hili: je waTanzania hawa mbona hawaonekani huko katika teuzi za juu (at least kwa majina yao ya kudini). Hii ni hoja ya msingi sana, kwani inaashiria kuwa kuna upendeleo unaofanywa, unaohusiana na majina ya watu na sio sifa zao za uchapa kazi na hatua ya kisomo chao. Kama hivi ndivyo, basi tuna tatizo linalostahiri kushughulikiwa kwa nguvu zote na kwa haraka sana. Kikwete aanze kazi hiyo haraka.
 
kuna majina mengine mtu akijiita tu huwa linamzuru,kwa hiyo watu wa namna hiyo wanaitaji kupepewa.
 
Kikwete amewateua hawa viongozi kwa kuwa ni wakristo, au kwa vile ni waTanzania walio na sifa zinazotakiwa katika nafasi hizo?

Mzalendo Halisi ametoa hoja nzuri zaidi hapo chini, kwamba darasani kwake walikuwepo wanafunzi wengi tu wenye majina ya kiislamu, tena waliokuwa na maendeleo mazuri kabisa katika masomo. Sasa swali mhimu la kujiuliza nadhani ni hili: je waTanzania hawa mbona hawaonekani huko katika teuzi za juu (at least kwa majina yao ya kudini). Hii ni hoja ya msingi sana, kwani inaashiria kuwa kuna upendeleo unaofanywa, unaohusiana na majina ya watu na sio sifa zao za uchapa kazi na hatua ya kisomo chao. Kama hivi ndivyo, basi tuna tatizo linalostahiri kushughulikiwa kwa nguvu zote na kwa haraka sana. Kikwete aanze kazi hiyo haraka.

Kalamu.

Naamini Nungwi alitizama suala la sifa kwa kumtaja Professor Mtulia kuwa ana sifa zote, elimu na uzoefu. au Jaji Chande ambaye amesimamia kesi ya mauaji ya Kigali-Rwanda pale Arusha. Jaji Chande ni muafrika pekeee aliyechaguliwa na Katibu mkuu wa kipindi kilichopita-Kofi Annan. ukiwatizama hawa wawili wote wana elimu na sifa.

Kichuguu.

Udini umejadiliwa sana humu. fuatilia thread ya mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa ipo hapa hapo utaona joto la udini lilivyo. mtu kama Nungwi naona ameamua kuwa mkweli sasa anapachikwa majina kama haya kuwa ni Osama au Al-qaida. huyu Nungwi ni wakili wa professor Warioba vc wa Mzumbe ambaye si muislam. au wale malecturers watano wa Mzumbe wenye phd feki toka PWU ambao wote si waislam. pia mawaziri wenye phd feki kuanzia Nchimbi, Kamalla, Nagu, Mahanga, wote ni wakristu na wanatetewa na Nungwi.

Kichuguu fuatilia uteuzi wa mabalozi watano kundi la Adadi watu walikuja juu sana humu hadi Mwanakijiji kuwa JK ni mdini. lakini hakutokea Eric wala Joka kuu na kusema hoja hiyo ya udini ni hoja lemavu. kama tunaamini kuwa ukabila kwanini tusiamini kuna udini?

nchini Italia inajulikana Kanisa Katoliki lina nguvu kuliko wakristu wengine. UK nako Anglikana wana Nguvu sana bungeni (HOUSE OF LORDS) kuna maBishops 22 wote ni Anglikana.

waziri mkuu wa UK lazima awe Anglikana. Blair alikuwa anataka kuingia Ukatoliki hakuweza kufanya hivyo hadi juzi alipotoka madarakani ndio amejiunga na Ukatoliki.

huko nyuma wakatoliki walipanga kuichoma westminster bunge baada ya kuona hawatendewi haki, 2004 bunge la UK limepitisha Religion discrimination Act ambayo ni sheria kamili, jeee kwanini wenzetu wachukue tahadhari sisi tusifanye? kwanini wenzetu wawe na Equal opportunity policy sisi tusijadili? mie nadhani haya mambo yanajadilika au imekuwa kama tulivyokuwa tunakatazwa kuujadili Muungano tukilazimishwa kuwa Mambo ni shwari.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom