MzalendoHalisi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2007
- 4,659
- 1,587
Ipo na inasema wazi kuwa waislamu wamewazidi wakristo kwa asilimia chache. Hata wakuu wa nchi wanakubali hilo lakini sio katika open platforms. Hii ni kwa kuwa wanahitaji kupunguza makali ya kina Ponda na wengine na hata CUF ambayo wanaona kuwa ina strong base katika suala hili.
Suala la Mkapa angeweza kufanya vizuri katika mgao wa madaraka linaweza kuwa kweli kwa kutumia logic kwamba kwake yeye usingekuwa upendeleo bali ni boldness lakini hata hivyo haikuwa rahisi kwake maana wakti tuna kina Sheikh Ponda vilevile tuna kina Mtikila na Pengo kama tulivyo na kina Kilaini na Gorogosi kwa upande mwengine.
hata hivyo muhimu ni capacity building kama vile kuziwezesha shule za waislam haswa zile za bakwata kutoa elimu bora zaidi ya bora elimu. approach nilishapendekeza hapo mwanzoni mwa hoja hii ingawa inaelekea wana jambo si wapenzi wa advise kama zangu. Changamoto ni kwa wale waliopenya ngome kubadili mentality ya baadhi ya watu wanaosumbuliwa na fikira mgando kuwa waislamu aka waswahili hawawezi kuongoza majukumu "nyeti".
Tanzanianjema
TanzaniaNjema,
Hakuna mtu anyekataa- ila nani aziimarishe hizo shule za Waislam kwa kwa mikakati ipi? Serikali? Au Bakwata? Kwani serikali imezuia kuimarika kwa shule hizi? Leo tena Pale Maelezo ktk kuunga Mkono JK Mashehe wameshauri wajengewe vituo vya kupimia VVU karibu na misikiti kwa vile nyingi za hospitali za Wilaya ni za Makanisa- na waislam wanaweza kutokuwa huru kupata huduma kwenye hospitali hizi!
Ni juu ya Bakwata kuchukua changamoto hizi- Waislam wanaweza tu kumanage na kuna shule Nzuri kama El Muntazar etc, ila kweli Bakwata yabidi kujipanga kwanza upya- kwani tayari Wakristo wana institutions nyingi! Wakristo walianza invesment mda mrefu and so strategically- ila ukiondoa seminari za RC -institutins zingine zote hawabagui admission uwe Mkristo au Mwislam! Pia angalia Morogoro Islamic University- wapo pia wanafunzi na waalim Wakristo!
Ni swala ambalo halina majibu rahisi-tuendelee kujadiliana!