Mkapa angewafaa zaidi Waislam Kuliko Kikwete

Status
Not open for further replies.
No way. Far from it by any imagination. Religious zealots the world over would want us believe that the end of the world is here already!

Watanzania wote, bila kujali dini zao (ukiacha hawa zealots, especially these Islamic extremists) hawawezi kukubali kuharibiwa amani yao na vikundi hivi, ambavyo kila kukicha vina kila aina ya madai. Hakuna linaloweza kufanyika kuwaridhisha kabisa na mlengo wao wa siasa. Ni lazima litaibuliwa tu jambo jingine jipya. Hata kama ungewapeleka nchi ambayo watu wote ni dini hiyo hiyo moja, bado watakuwa na madai. Hata kama ni kudai pawepo na polisi wa kidini ili kuenforce sheria za dini yao.

Biafra haiwezi kuwepo Tanzania kama haki ya kila raia mTanzania, bila kujali udini wake itadumishwa. Adui mkubwa ni upendeleo wa aina yoyote ile. Kwa hiyo dawa ya tatizo ni Haki kwa kila raia wetu, mradi awe na sifa zinazotakiwa.

This nonsense of Mkapa's leg is simply bizarre. It is amazing to find seemingly educated and perfectly intelligent people propagating such crap in this day and age!

If there were to be a Biafra in Tanzania, how different would the outcome from the actual Biafra be! Those who advocate or threaten us with their make believe imaginations need think very carefully on this this.
 
Mkuu Kichuguu.

CV ya Jaji Chande inaonekana ametumikia Red Cross na UN kote ameshika nafasi nzito. Umesema amefanya kazi UN tu,kama Chief Marreale lakini Chande kafanya na RED CROSS-Uswisi jee unasemaje
Swali Augustino Ramadhan aliwahi hufanya kazi yeyote ya kimataifa zaidi ya kuwasuluhisha MP (military police) jeshini?

Mzee Kifimbo.

Link yako imemnukuu Mwalimu Nyerere kuwa hakuwa mdini wala mkabila mie nakataa-Nyerere alimpa uwaziri mkuu binamu yake Joseph Warioba,wengine ni Wassira na gavana Nyirabu achilia mbali mkuu wa majeshi Musuguri- wote walitoka mkoa wake na dini yake. usawa upi aliouleta Nyerere?

Njia aliyopendekeza Kichuguu ya wateule wa Rais kuwa 'confirmed' na bunge ni njia nzuri ya kutupatia watu wenye sifa zinazokubalika.
 
Nungwi,
Ustadhi kidogo punguza Utaliban (mwanazuoni), hiyo Phd ya Nchimbi ni rangi gani? yaani dini, kabila ama jinsia gani?
hapana ndugu yangu vita ya Biafra imeanzishwa na watu wenye mtazamo kama wako na pili wenzetu wameishi kwa mipaka ya dini na Ukabila toka wapate Uhuru. Kwa hiyo walikuwa na kila sababu ya kutazama kundi lao kwani hawa watu walikuwa na states zilizoundwa kwa mipaka ya makabila.
Udini umekuja Tanzania kwa sababu ya watu wenye kutazama rangi za kila mteuliwa. Na sijui nani amesimama kwa ajili ya wanawake maanake tukizungumzia Udini Tanzania sijui Wanawake tumewaacha wapi!... nimeona kwa macho yangu jinsi mnavyo watreat wanawake ni kama vile watumwa na nadhani kuna kila haja ya kulitazama hili kabla ya hata Udini maanake hata wahindi siku hizi wanatoa ajira kwa mabinti zetu wakiitwa TX baada ya kukubali kulala na mwajiri..
Kama kweli wewe salhina na inakuuma sana nadhani ungeanzisha mada inayohusu dada zetu kuwa watumwa ktk majumba ya watu wakipewa mishara duni chini ya kiwango na wengine wanapewa chakula na malazi tu ati kwa madai kuwa -Tunaishi naye (huyo dada yetu) kama ndugu yetu!
Wee uliona wapi ndugu yako akifanya kazi zote za ndani?.. Anzia hapo nitakusikiliza.
 
Kalamu.

Dawa si kukasirika Kaka. ni kujadili njia muafaka na hapa tunatoa darasa juu ya kuiinua jamii moja iliyoachwa nyuma na zikija hoja za kuleta suluhu tunapewa majina kuwa ni wachochezi.

Kalamu vipi watu wanaoleta maneno ya chokochoko dhidi ya serikali yao? mtu kama Mwanakijiji anayejaribu kuweka wazi mambo mbalimbali dhidi ya serikali jee naye anatupeleka kwenye Biafra?
 
Kalamu.

Wasio na shukurani ni waislam? unasema kila wakipewa hawaridhiki wamepewa nini hawajaridhika? jee ni vibaya kutaka haki zao au usawa?

MKANDARA.

Umefika mbali kumuita mkuu Nungwi Talaban. Binafsi naona Nungwi ni mtu aliye fair. kule Mzumbe university amewatetea wahadhiri sita wa Mzumbe wenye vyeti vyenye mashaka pamoja na Waziri Kamala, Nchimbi na VC warioba kwa bahati mbaya wote hao ni wakristu jee ulimwita Nungwi ni askofu?

Jamani tuwe wakweli kujadili hisia zetu sio kufunika funika mada.
 
Mtaliii,
Hapana ndugu yangu Nungwi anaifahamu maana halisi ya neno hilo.... usitake kusikia tafsiri za magharibi hawana haya wadudu hawa walofikia kuita Kuran aya za shetani!
Sidhani kama tunamzungumzia Nchimbi kwa sababu ni mngoni ama Warioba kwa sababu ni Mjita sijui Mruli bali ni cheti kinachozungumziwa sio mtu!
 
Kalamu.

Wasio na shukurani ni waislam? unasema kila wakipewa hawaridhiki wamepewa nini hawajaridhika? jee ni vibaya kutaka haki zao au usawa?

MKANDARA.

Umefika mbali kumuita mkuu Nungwi Talaban. Binafsi naona Nungwi ni mtu aliye fair. kule Mzumbe university amewatetea wahadhiri sita wa Mzumbe wenye vyeti vyenye mashaka pamoja na Waziri Kamala, Nchimbi na VC warioba kwa bahati mbaya wote hao ni wakristu jee ulimwita Nungwi ni askofu?

Jamani tuwe wakweli kujadili hisia zetu sio kufunika funika mada.

Sijui kama unazo sifa za kuwasemea 'waislam' wengi ambao ni waTanzania kwanza, kama walivyo waTanzania wengineo wote, kabla ya kuweka dini zao mbele kama mabango ya utambulisho.
 
Sijui kama unazo sifa za kuwasemea 'waislam' wengi ambao ni waTanzania kwanza, kama walivyo waTanzania wengineo wote, kabla ya kuweka dini zao mbele kama mabango ya utambulisho.

Kalamu,

Ni sifa zipi hizo ambazo mtu anatakiwa awe nazo ili aweze kuwasemea waislamu?
 
Mtalii,

Naona swala la uteuzi huu unalingalia ukiwa biased kiudini sana sana kiasi kuwa unashindwa kukubali ukweli kuwa Jaji Augustino ni senior kwa Jaji Chande.

(1) Kwanza ondoa kabisa hiyo imani ya kuwa mtu akifanya mashirika ya nje tu basi ndiye anayefaaa kuwaongoza ambao hawakufanya mashirika ya nje. Halafu angalia seniority niliyoongelea kuwa ni kwenye judiciary system yetu anayotakiwa kuongoza. Jaji Augustine amekuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar mara mbili, na Jaji wa mahakama ya rufaa zaidi ya miaka ishirini kabla ya Jaji Chande. Kwenye mahaka ya rufaa tu amekuwapo miaka 14 kabla ya jaji Chande, hiyo ndiyo seniority inayoongelewa. Swali ambalo ungeuliza labda ni kwa nini Jaji Augustino aliteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na baadye kuteuliwa kwenye mahakama ya rufaa kabla ya Jaji Chande.

(2) Fairness ya Nungwi siwezi kuijadili; ninachojua kuhusu Nungwi ni kwamba yeye ama ni graduate wa Mzumbe au ana interest fulani Mzumbe na ana chuki fulani na UDSM, kila mara haishi kulinganisha Mzumbe na UDSM. Utetezi wake wa Ph.D za watu ambao wana uhusiano na Mzumbe unatokana na sababu hiyo na wala hakuna udini wowote. Hebu soma hapa
Mficha ugonjwa kilio kiwamuweka wazi.

Naona mmekuja juu sana na nyie mnasema kila kitu kinajadilika hapa JF. mnajadili Phd za kina Nchimbi hakuna anayelaumu, kwanini tusijadili issue za udini?........

Nchimbi ni mmoja wa wenye Ph.D. fake na ni graduate wa Mzumbe.
 
Sijui kama unazo sifa za kuwasemea 'waislam' wengi ambao ni waTanzania kwanza, kama walivyo waTanzania wengineo wote, kabla ya kuweka dini zao mbele kama mabango ya utambulisho.

Mimi nawasemea waislam wewe unawasemea watu gani? kuna ubaya kuwakilisha kilio au manunguniko ya jamii kwenye nchi yangu? ulitaka nitazame yangu tu na shida za wenzangu nisitizame? wewe unalalamika viongozi hawawajali wananchi ni utaratibu wako wa kujipendelea na kusahau shida za wengine.

Kalamu nini kazi za wabunge?
Acha hizo tunajadili Cv ya Jaji Chande. kama huna kitu nyamaza.
 
Chuma Hata Mtoto Wa Kidoga Anayeitwa Jabir Kigoda Yuko Pale Banki Kuu Nae Ameishia Form 4 Lakini Ako Banki Kuu Nasikia Anaongezea Elimu Yake Online

Mbona naambiwa BOT siwezi kupata kazi bila kuwa na Masters, Kulikoni?
Naambiwa kwa siku hizi hata secretary lazima apandishe kitabu.
labda yule aliye kuwa ameajiriwa enzi hizo.
Au an long time experience
 
Jamani Chande itafika wakati atapewa, Maana kama tulivyo ona Umri wa Augustino ni ndio hivyo tena unaelekea ukingoni, so Let Chande tumuande kuchukua huo wadhifa , tumeanza kumuweka Mahakama kuu, baadea tutampa Ujaji Kiongozi au Mahaka ya Rufaa then U chief Justice.
Tukizungumzia experience na exposure aliyo pata Basi tutasema Sali Ahmed salim anafaa kushika Madaraka Fulani badala ya fulani, au Mahiga anafaaa cheo fulani because he had work in the UN, Kuna akina Sekule former DPP , kuna wakati alikuwa Rwanda Tribunal , Kuna Akina Lubuva hapo Mahakama ya Rufaa.
Na kwa mantiki hiyo hiyo huko Zanzibar Kuna akina Gharib Bilal ni Phd yake lakini kila akitaka kugombea kitu huko Zanzibar anazidiwa Nguvu au hajapata Uteuzi wowote Mbona Hatumtetei na Kusema anasifa zaidi ya Nahodha au Dk Hussein Mwinyi etc etc.
 
Mkuu Kichuguu.

.......Link yako imemnukuu Mwalimu Nyerere kuwa hakuwa mdini wala mkabila mie nakataa-Nyerere alimpa uwaziri mkuu binamu yake Joseph Warioba,wengine ni Wassira na gavana Nyirabu achilia mbali mkuu wa majeshi Musuguri- wote walitoka mkoa wake na dini yake. usawa upi aliouleta Nyerere?
.....

Mtalii pokea tano toka kwangu

Ni wengi wanakataa hilo ila ndo ukweli wenyewe, huyu mzee nafasi zote nyeti alikuwa akipasia jamaa wa kulekule kwao, na pia alikuwa mdini nambari moja!.....Huu mjadala leo usingekuwepo kama siyo yeye kuwa ameanzisha mambo ya kulindana na kupasiana post kwa kisigino kisa tu ni wakwao au dhehebu lake!!!! WaTZ narudia tena amkeni na mwangalie pande zote mbili za shilingi!!
 
Wandugu,
Warioba sii ilikuwa wakati wa Mwinyi? Au ilikuwa shinikizo la Mwalimu? Ila hakuna mtu mkamilifu duniani- tunaangalia kiwango cha uadilifu! Mnakunbuka Eyadema wa Togo alipokufa- Majeshi haraka wakampa Faore mtoto uraisi?
Mwalimu alipendelea- ila pia alikuwa mwadilifu- hakuwa mla rushwa!
 
Njia aliyopendekeza Kichuguu ya wateule wa Rais kuwa 'confirmed' na bunge ni njia nzuri ya kutupatia watu wenye sifa zinazokubalika.
Kalamu,
Wabunge wenyewe asilimia 95% wananuka rushwa tupu, watasaidia nini? Si wataishia kuomba chochote kwanza?
 
Kalamu,
Wabunge wenyewe asilimia 95% wananuka rushwa tupu, watasaidia nini? Si wataishia kuomba chochote kwanza?

Huwezi kuhonga wabunge wote 320.

Tatizo la sasa ni kwa sababu bunge liko chini ya Lowasa. Baadhi ya wabunge pia wanajizuia kuikosoa serikali kwa kutegemea kuwa siku moja watateuliwa kushika nyadhifa serikalini kwa hiyo hawataki kujitibulia kwa kuisakama serikali hata kama wanaona uvundo. Tunahitaji marekebisho ya katiba yenye kutenganisha mamlaka ya bunge na ya serikali kabisa, waziri mkuu asiwe na mamlaka bungeni, na rais asiruhusiwe kuteuwa wabunge na kuwapa madaraka zaidi ya ubunge wao. Ukisha tenganisha bunge na serikali kuu, nakuhakikishia rushwa itakwisha kabisa kwa vile ni vigumu kuwahonga wabunge wote, na wabunge watakuwa hawajikombi lolote serikalini.
 
.....

Link yako imemnukuu Mwalimu Nyerere kuwa hakuwa mdini wala mkabila mie nakataa-Nyerere alimpa uwaziri mkuu binamu yake Joseph Warioba,wengine ni Wassira na gavana Nyirabu achilia mbali mkuu wa majeshi Musuguri- wote walitoka mkoa wake na dini yake. usawa upi aliouleta Nyerere?
Mtalii pokea tano toka kwangu

Ni wengi wanakataa hilo ila ndo ukweli wenyewe, huyu mzee nafasi zote nyeti alikuwa akipasia jamaa wa kulekule kwao, na pia alikuwa mdini nambari moja!.....Huu mjadala leo usingekuwepo kama siyo yeye kuwa ameanzisha mambo ya kulindana na kupasiana post kwa kisigino kisa tu ni wakwao au dhehebu lake!!!! WaTZ narudia tena amkeni na mwangalie pande zote mbili za shilingi!!

Mkoa wa Mara naufahamu vizuri sana; una makabila zaidi ya 12. Waryoba ni Muikizu wa Nyamuswa, Msuguri ni Mzananki kama Nyerere mwenyewe kwao ni Butiama, Wassira ni Mshashi (au Msizaki) wa Ushashi ingawa sasa hivi anakaa Bunda, Marehemu Nyirabu alikuwa Mkuria wa Tarime. Ukiachia Msuguri, wote hao unaowasema hawana undugu na Nyerere, ingawa wakati fulani Wassira aliwahi kumwoa binti wa Chifu Wanzagi kwa muda mfupi wakati akiwa akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

  1. Sidhani kuwa teuzi za Wassira zilitegemea ndoa hiyo ya binti Wanzagi kwa vile tayari alikuwa keshateuliwa mara mbili kabla ya ndoa hiyo na hata baada ya kuachana na huyu binti wa Wanzangi bado Wassira aliteuliwa mara nyingi hasa wakati wa Mwinyi hadi pale alipopigwa stop na Waryoba kufuatia kinyanganyiro cha ubunge; nina imani kuwa unajua kuwa hata JK amemteua tena.

  2. Nina imani kuwa Waryoba aliteuliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa qualifications zake; sijui kama unasema kuwa hakuwa na qualifications au vipi, ila ninajuwa alikuwa kati ya wanasheria wa kwanza kwanza nchini hapa. Na alianzia chini akapanda pole pole mpaka hapo. Uteuzi wake kuwa Waziri Mkuu ulifanyika wakati wa Mwyinyi kwa hiyo siwezi kuita wa Nyerere.

  3. Kuhusu mkuu wa majeshi inawezekana kuwa ni kweli alimteua ndugu yake Musuguri, hata hivyo angalia kuwa population kubwa ya jeshi inatoka mkoa wa mara, na hiyo imejionyesha kwa kuwa na wakuu watatu wa majeshi kutokea mkoa huu. Nyerere aliteua mmoja tu kati ya hao watatu, wengine wameteuliwa na Mwinyi (General Kiaro) na Mkapa (General Waitara).

  4. Ninavyofahamau, Nyirabu aliteuliwa kuwa gavana wa benki kuu kwa vile ndiye aliyekuwa second to Mtei wakati huo. Mtei alikuwa gavana wa kwanza na alipopata promotion nafasi hiyo ikaenda kwa mtu aliyekuwa wa pili yake; sidhani kama huo ulikuwa ni ukabila. Mtu closest kwenye position hiyo angekuwa Bob Makani ambaye kwa bahati mbaya hakuwa mchumi.
 
Kichuguu.

Bob Makani unasema hakupewa kwa vile hakuwa na digrii ya uchumi. mbona Mtei alipewa akiwa na Literature? wakati Makani ana sheria ambayo kidogo inafanana.

Baada ya Nyirabu alikuja Rutihinda kuwa gavana, huyo alikuwa na Political Science na International Relations.

Nadhani Makani hakupewa kwa dini yake lazima tukubali Mwalimu alivyokuwa Mdini.

Back 2 Warioba kuwa alikuwa na Qualification ndio akapewa uwaziri mkuu,na Jaji Chande ana Qualification zaidi ya Warioba au Augustino Ramadhani.sasa unataka tuamini kuwa Qualification ni kigezo, wakati jana ulisema kuwa SENIORITY ndio kigezo. mkuu sikuelewi kabisa!Chande ana exposure kubwa sana ambayo hana Warioba wala Jaji mkuu mpya.

Nakurudisha UDSM nyumbani kwako. wakati anatafutwa Dean wa Faculty ya Commerce and Management- Assad Mussa akamshinda vibaya Chijoriga kwa qualification na Seniority, akapita kwenye interviews zote. lilipofika File kwa Luhanga-VC wenu akampa bibi Chijoriga kwa madai ya Gender. hili limelieleza sana kwenye Mada ya Mzumbe VS UDSM nenda kwenye elimu utaona.

U-TURN ya Luhanga kuwa ni Gender imetoka wapi? mtu akija na Qualfication kama Chande unasema unataka Seniority. ikija Seniority kama DR.Assad unasema GENDER ISSUE and Globalization.

Warioba alipewa uwaziri mkuu kwa upendeleo kigezo cha elimu hakihusu kwa cheo cha uwaziri mkuu. ndio maana unaona Sumaye alipewa madaraka hayo huku akiwa hana elimu. baada ya kumaliza Uwaziri mkuu ndio amekwenda kusomea Management skills, wakati alitakiwa awe na Knowledge hiyo kabla ili apply kwenye uwaziri mkuu wake.

Na kwa taarifa yenu Course work na Dissertation amefanyiwa na vijana wa kikenya.

Nawaomba WaTanzania tusibaguane wote wapewe vyeo. kama balance ya Muungano inatazamwa why not ya Dini?
 
Nungwi,
Ustadhi kidogo punguza Utaliban (mwanazuoni), hiyo Phd ya Nchimbi ni rangi gani? yaani dini, kabila ama jinsia gani?
hapana ndugu yangu vita ya Biafra imeanzishwa na watu wenye mtazamo kama wako na pili wenzetu wameishi kwa mipaka ya dini na Ukabila toka wapate Uhuru. Kwa hiyo walikuwa na kila sababu ya kutazama kundi lao kwani hawa watu walikuwa na states zilizoundwa kwa mipaka ya makabila.
Udini umekuja Tanzania kwa sababu ya watu wenye kutazama rangi za kila mteuliwa. Na sijui nani amesimama kwa ajili ya wanawake maanake tukizungumzia Udini Tanzania sijui Wanawake tumewaacha wapi!... nimeona kwa macho yangu jinsi mnavyo watreat wanawake ni kama vile watumwa na nadhani kuna kila haja ya kulitazama hili kabla ya hata Udini maanake hata wahindi siku hizi wanatoa ajira kwa mabinti zetu wakiitwa TX baada ya kukubali kulala na mwajiri..
Kama kweli wewe salhina na inakuuma sana nadhani ungeanzisha mada inayohusu dada zetu kuwa watumwa ktk majumba ya watu wakipewa mishara duni chini ya kiwango na wengine wanapewa chakula na malazi tu ati kwa madai kuwa -Tunaishi naye (huyo dada yetu) kama ndugu yetu!
Wee uliona wapi ndugu yako akifanya kazi zote za ndani?.. Anzia hapo nitakusikiliza.

Mkandara.

Huwezi kuwatetea waislam hadi uwe muislam? kwa hiyo mtazamo wako asiye kuwepo na lake halipo? tuwe tunajadili issue hata kama hatuzipendi ila zina maslahi ya Taifa. nilipopost mada hii niliomba tuchangie kuona weakness zetu. sasa nimebatizwa kuwa ni Talaban.kwa taarifa tu mimi ni Sabato.

Mwanakijiji.

Nimekuomba uje hapa. uliwahi kufanya Interview kuhusu Waislam na serikali kwenye redio yako. naamini una mengi ya kutupatia.

Kalamu.

msemo wako wa "YOU GIVE AN INCH, THEY DEMAND A MILE" naona unawabeza waislamu na kuwaona kama si raia wa nchi hii.

kumbuka wao ni majority kwanini hutaki kujadili mambo ya msingi ya waislam? tukiwapa si ihsani ni haki yao.

wewe unasema maneno hayo kama nani? mbona kwenye harakati za uhuru tuliwatanguliza mbele waislam? dua zote zilisomwa misikiti.

Padri gani aliongoza harakati za uhuru? muulize mama Maria Nyererre nani alikuwa sheikh Ramia na mchango wake kwenye uhuruna maisha ya Mwalimu.

Tizama picha za mwanzoni kwenye harakati za uhuru hadi kura tatu 1958 waliokuwa mbele ni hawa unasema U give an Inch,They demand a Mile.

Fautilia picha za jangwani za Mwalimu Nyerere akiwa amezuungukwa na waislamu enzi za harakati. mtizame bibi Titi Mohammed alivyokuwa mbele jee kulikuwa na Margrett Sitta au Rita Mlaki pale?

Ukisiliza mikutano ya harakati za uhuru. ilikuwa hauanzi mkutano wa Tanu bila Maombi ya waislam.

jamani hawa si MINORITY wametoa jasho lao.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom