Mkapa angewafaa zaidi Waislam Kuliko Kikwete

Status
Not open for further replies.
Professor Mtulia kuwa waziri ni sawa.DR.Kawambwa hazuii kwa vile wanatoa mkoa wa Pwani. mbona kuna wilaya ina mawaziri wawili, nayo ni RUNGWE -Mbeya.wilaya hii imetoa waziri Mwakyusa na Mwakyembe kama ajabu ianzie huko.

Kwanza Mwakyembe si Naibu Waziri

Lakini pamoja na kuwapo na hizo hisia za udini kutoka pande zote, bado JF tuna mambo mengi na muhimu ya kujadili kwa maslahi ya taifa na tusianze kuumiza vichwa kwa sababu ya uteuzi wa JK ama Mkapa.. Hapa JF mjadala huu hautatusaidia.. Tuendelee kuwasaidia hawa viongozi wetu kwa kuwakosa kwa nguvu zetu zote, wawe Waislamu ama Wakristu ama Wapagani kama Kingunge

Kuna Musialamu mmoja aliniambia, "Unajua Mkapa alipougua na kulazwa Uswisi watu walimwambia kwamba hiyo ni laana ya damu iliyomwagika Pemba mwaka 2001. Alidhani watoto wa wenzake wanatembea na vilema huku yeye anatesa, ngoja na yeye atembee na fimbo.." mtu huyo huyo akaja kuniambia tena, "unaona Mkapa kagundua laana sasa anaombewa dua na Waislamu na wamemwambia ni lazima atoe sadaka kusafisha aliyowafanyia Waislamu maana aliwaua Mwembechai na baadaye Pemba japo nafasi yake ilikua ikikaimiwa na marehemu Dr Omar, ambaye ni Mpemba lakini alitoa maelekezo huko huko alipokua na ndio maana ameamua kuwasaidia Waislamu kwa kuwapa Chuo Kikuu cha Morogoro.."

M
 
Halisi.

Hii ya Mkapa ni halisi au nyepesi nyepesi?

kama kweli uongozi ni kazi nzito. Mjadala huu naona una manufaa kwa jamii kwanini tufiche ukweli? kama tunaamini wanawake wako nyuma why not tusijadili waislam?

Hivi hatuwezi kuwajadili wamang'ati kuwa wako nyuma na hatua za kuwasaidia? tusiwe na roho za kihindi ambapo ukiwa tajiri unafunga vioo na hutaki kujua jirani zako wanavyohangaika na dhiki mbali mbali, matokeo yake ukifika India unakutana na mhindi tajiri sana jirani yake analala na njaa na yeye hakosi usingizi kwa njaa ya jirani yake.
 
mtalii said:
Kichuguu.

Udini umejadiliwa sana humu. fuatilia thread ya mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa ipo hapa hapo utaona joto la udini lilivyo. mtu kama Nungwi naona ameamua kuwa mkweli sasa anapachikwa majina kama haya kuwa ni Osama au Al-qaida. huyu Nungwi ni wakili wa professor Warioba vc wa Mzumbe ambaye si muislam. au wale malecturers watano wa Mzumbe wenye phd feki toka PWU ambao wote si waislam. pia mawaziri wenye phd feki kuanzia Nchimbi, Kamalla, Nagu, Mahanga, wote ni wakristu na wanatetewa na Nungwi.

Kichuguu fuatilia uteuzi wa mabalozi watano kundi la Adadi watu walikuja juu sana humu hadi Mwanakijiji kuwa JK ni mdini. lakini hakutokea Eric wala Joka kuu na kusema hoja hiyo ya udini ni hoja lemavu. kama tunaamini kuwa ukabila kwanini tusiamini kuna udini?

Sijui ndugu yangu hapa unaniambia kitu gani binafsi, mimi sijakataa kuwapo kwa mijadala ya udini kwani JF ina kila kitu, nilijibu swalia la kifimbo cheza kuwa kuwa huenda sikuisoma na huenda sikuwa na muda wa kujibu. Kuna thread ambazo sijazisoma siku nyingi mojawapo ikiwa ni Ukabila Ikulu, na kuna thread ambazo sikuzifunua kabisa hata zile ambazo nilizianzisha mimi mwenyewe kwa kukakosa muda. Kuanzia May hadi July hii nilikuwa na nafasi kidogo na nimekuwa active sana, lakini usishangae kuona kuanzia August presense yangu ikapungua tena, ndiyo maisha yalivyo.

Nungwi nilijibizana naye pale tu alipotetea sana Ph.D feki za Mzumbe na wala sijui unawezaje kusema kuwa nimemwita Osama wa Al-Qaida kama huo siyo uzushi. Sikujua kuwa yeye ni mwislamu na ni wakili wa Waryoba; siku zote amekuwa analeta ushindani wa Mzumbe na UDSM tu hapa. Ph.D zile zilihusishwa zaidi na Mzumbe kwa vile ndipo zilikokuwa nyingi lakini watu kama akina Makongoro Mahanga, Mary Nagu, na Didas Masaburi ambao hawana uhusinao na Mzumbe pia walizungumzwa, mjadala ule haukuwa na udini wowote.

Udini wa mwisho mimi kujadili hapa JF ulihusu kile kitabu kilichotoa historia ya uislamu na mapambano ya uhuru ambao ulikuwapo mwishoni mwa mwaka jana au mwanzoni mwa januari mwaka huu. Upinzani wangu mkubwa pale ulikuwa kwenye madai ya mwandishi kuwa Nyerere aliwa-sideline waislamu kwa kutumia "kura tatu" ili aingize wakatoliki.
 
Kalamu.

Naamini Nungwi alitizama suala la sifa kwa kumtaja Professor Mtulia kuwa ana sifa zote, elimu na uzoefu. au Jaji Chande ambaye amesimamia kesi ya mauaji ya Kigali-Rwanda pale Arusha. Jaji Chande ni muafrika pekeee aliyechaguliwa na Katibu mkuu wa kipindi kilichopita-Kofi Annan. ukiwatizama hawa wawili wote wana elimu na sifa.

Kichuguu.

Udini umejadiliwa sana humu. fuatilia thread ya mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa ipo hapa hapo utaona joto la udini lilivyo. mtu kama Nungwi naona ameamua kuwa mkweli sasa anapachikwa majina kama haya kuwa ni Osama au Al-qaida. huyu Nungwi ni wakili wa professor Warioba vc wa Mzumbe ambaye si muislam. au wale malecturers watano wa Mzumbe wenye phd feki toka PWU ambao wote si waislam. pia mawaziri wenye phd feki kuanzia Nchimbi, Kamalla, Nagu, Mahanga, wote ni wakristu na wanatetewa na Nungwi.

Kichuguu fuatilia uteuzi wa mabalozi watano kundi la Adadi watu walikuja juu sana humu hadi Mwanakijiji kuwa JK ni mdini. lakini hakutokea Eric wala Joka kuu na kusema hoja hiyo ya udini ni hoja lemavu. kama tunaamini kuwa ukabila kwanini tusiamini kuna udini?

nchini Italia inajulikana Kanisa Katoliki lina nguvu kuliko wakristu wengine. UK nako Anglikana wana Nguvu sana bungeni (HOUSE OF LORDS) kuna maBishops 22 wote ni Anglikana.

waziri mkuu wa UK lazima awe Anglikana. Blair alikuwa anataka kuingia Ukatoliki hakuweza kufanya hivyo hadi juzi alipotoka madarakani ndio amejiunga na Ukatoliki.

huko nyuma wakatoliki walipanga kuichoma westminster bunge baada ya kuona hawatendewi haki, 2004 bunge la UK limepitisha Religion discrimination Act ambayo ni sheria kamili, jeee kwanini wenzetu wachukue tahadhari sisi tusifanye? kwanini wenzetu wawe na Equal opportunity policy sisi tusijadili? mie nadhani haya mambo yanajadilika au imekuwa kama tulivyokuwa tunakatazwa kuujadili Muungano tukilazimishwa kuwa Mambo ni shwari.

Mtalii,
Mimi sijui ni kwa nini watz tunaogopa kujadili dini- sio dhambi!
Hapo juu thread kumkaribisha Migiro UN kuna mtu alisema 60% ya kazi mara nyingi hupatikana kwa networks, contacts, 'technical know who' n.k
Since hizo sehemu nyingi kuna Wakristo wengi- basi given equal qualifications- na waislamu- sii wataajiriwa Wakristo? Kama nilivyosema 90% ofsini ni Wakristo- yet waislam walikuwepo wengi tu darasani- na walipasi vizuri- na sii tu kwamba majina walitumia bandia- tulikuwa tunawaona wanenda mskitini kila Ijumaa!
Sasa watu wanogopa tusijadili!
Sielewi tatizo ni nini!
 
Hapa JF kuna unafiki, yaani ikija issue ya Ukiristu kuwa unakandamizwa inakuwa right lakini likija suala la uislamu basi inakuwa udini, ah kazi kweli kweli - hapa JF watu waliwahi kumwita JK kuwa mdini (kwa maana anapendelea waislamu) baada ya kuteua mabalozi 5 waislamu, jamani tuacheni huu udouble standard.

Kama mtu anasifa za kushika nafasi flani basi apewe isijalishe yeye ni dini gani.
 
Kwa Mtazamo wangu naona Rais apunguziwe uwezo wa KUTEUA Viongozi,Viongozi wengi wapatikane kwa Sanduku la kura.Viongozi kama Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanaweza kabisa kupatikana kwa kupigiwa kura(Kama wana ulazima wa kuwepo),kwa sababu tumekuwa na Mlolongo wa Viongozi wengi wasio watendaji!
Katiba yetu imempa Nguvu kubwa ya Uteuzi Mheshimiwa Rais,na sasa leo tunaona teuzi za Ajabu sana!na si kwamba zipo kwa mitazamo ya Dini tu!La hasha!kuna Teuzi za Asante kwa kunifanyia kampeni!,Teuzi za shukran kwa kuwa ulikuwa Bibi yangu!,Teuzi za Shukran kwa kumuajiri mwanangu kwenye Firm yako!,Teuzi za kuombewa na Mama,na Teuzi za Shukran kwa kuniachia jimbo la Uchaguzi!.Bado katiba yetu inampa Umungu mtu Rais,Kila siku kunakuja Rais mpya na mambo mapya,tukiliacha hili liendelee tutampata Rais mwenawazimu atakayetuvua nguo Hadharani.Lazima kuwepo na Utaratibu wa Makusudi wa kupunguzwa nguvu Uwezo wa Rais.
Nimepitia wachangiaji wote hapo Juu,na kwa mtazamo wangu naona imefika wakati sasa tuwe na Utaratibu wa kumchambua Mteuliwa na kuthibitishwa na Chombo kama Bunge!.Kwenye Confirmation Hearing yake,Mteuliwa huyu aulizwe uwezo na Elimu yake na atasaidia vipi kumkomboa Mtanzania wa kawaida kutoka ktk Dimbwi kubwa la Umaskini.Hali ilivyo kwa sasa,Rais anaweza kumteua yeyote bila Uoga kwa sababu haulizwi!!
Suala la Dini kwangu sio kigezo,achaguliwe yeyote ili mradi tu ana sifa zitakazokubalika na watakaomthibitisha!,Tuna Watu wengi wanaonekana kuwa ni Viongozi wazuri ,lakini wametupwa nje kwa kuonekana tu kwamba sio wenzetu!Kwa mtazamo huu hatuwezi kupiga hatua!,Tunahitaji challenge na sio watu wa Ndio Mzee hata kwa masuala ya Upuuzi!
 
kuwasaidia Waislamu kwa kuwapa Chuo Kikuu cha Morogoro.."

Kile chuo hakikutoka kirahisi ndugu zangu. Ingawa Mzee Mkapa alionyesha nia tangia mwanzoni lakini kuna vijogoo ambao wanaamini kuwa hakuna haja ya kuwawezesha waislamu walikuwa wanadindisha sana. Ilibidi Mzee wa kuharibu Kitwana Kondo na Kinana kumuambush Mzee mwenzao akitoka safari kutibiwa na kumpa black and white. Offcourse in the end ilikuwa katika interest ya chama tawala kufanya hilo si unajua masuala ya CUF yalivyokuwa yakiumiza kichwa.

Swala linakuja kitasaidia waislamu kweli? Kivipi? Kwa mtindo wa bora elimu ama elimu bora? Wanasiasa kama kina KK watakubali kukaa pembeni kama walivyoahidi ili vijana kama kina Dr Assad, Dau, Musoke na wengine wanaojitolea kwa hali na mali kufanikisha project hiyo?

Tanzanianjema
 
NIna wazo, ili kuondoa haya malalamishi naona serikali itenge mkoa mmoja ili uwe wa waislamu na waislamu wajiendeshe kwa kufuata sheria za kiislamu n.k wanaweza kuomba Irani au Pakistan kuwasaidia jinsi ya kufanya hivyo. Kwa Tanzania nzima napendekeza kwa kila kitu ambacho serikali inataka kufanya kigawanywe mara mbili, kwa watanzania wengine na kingine kwa waislamu. Hospitali za sisi wengine na hospitali za waislamu n.k n.k Na ili kuondoa matatizo mengine, labda tuwe na serikali mbili, ile ya Watanzania wote na ile ya Waislamu, na hivyo utaona hakutakuwa na haja ya kumkumbuka Mkapa na kumkandia Kikwete, kwani waislamu wanaweza kujichagulia Mkapa kuwa Rais wao (kama sheria yao itawaruhusu)

asanteni.
 
dini wala kabila havina nafasi kabisa katika tanzania ya leo. Mnaoleta mada za dini na kabila mna mapungufu ya fikira. Tuunganishe nguvu kupigania uwajibikaji kwa kazi za kitaifa kwani dini au kabila la mtu havituletei maendeleo bali uwezo nauwajibikaji wake. Rais anajitahidi kutafuta watu wenye sifa, tabu ni uwajibikaji waziri anayefanya kazi kutokana na sheria na katiba huhitaji dini yake au kabila lake, kwani upendeleo ni shurwa ya aina yake. mgawanyiko wa kikabila au dini ni wakupigwa vita sana. ningependa mada ya kumbana raisi kuwadili wazembe na wala rushwa kwenye baraza lake la mawaziri zaidi
 
--------------------------------------------------------------------------------

Yeah hilo ndio suluhisho
 
Nungwi,

6.Usimnyanyase Tido Mhando kwamba ana elimu ndogo. Uzoefu wake Idhaa ya Kiswahili BBC unamuzesha kuongoza chombo chochote cha habari Tanzania.

Kama Tido kapewa kazi kwa sababu ya Uzoefu then swali linakuwa je huyu tido ana uzoefu kuliko SULMA KASSIM?
 
Dr Inaonyesha Unajua Vitu Vingi Sana Au Pengine Uko Karibu Na Watu Wengi Kutokana Na Michango Yako Katika Jukwa La Jambo

Tunaomba Utupe Wasifu Wa Watu Wote Wawili Halafu Tujadili Au Fungua Thread Yao Pekee .

Ahsante
 
SPIKA -mkristu, Jaji mkuu-MKRISTU,mkuu wa uhamiaji-mkristu, mkuu wa magereza-mkristu,DPP-mkristu,mkuu wa majeshi-mkristu. mkuu wa polisi-muislam,mkuu wa usalama-muislam, jaji kiongozi-mkristu, Mwanasheria mkuu-mkristu, DCI-mkristu, Mkuu wa PCB-mkristu, Chief of staff jeshini-mkristu,mwenyekiti tume ya uchaguzi-mkristu, mwenyekiti usajili wa vyama vya siasa-mkristu.
Gavana-mkristu,mhasibu mkuu-mkristu, Auditor General-mkristu,Commissioner wa TRA-mkristu, Katibu wa bunge -mkristu, katibu mkuu ofisi ya rais-Mkristu,mkurugenzi mkuu wa TVT-mkristu huyu bwana ni kidato cha nne-form four leaver angekuwa muislam tungesema hana sifa.

Mhhhhhhii kiboko

wewe muda unao, umeweza vipi kutafiti haya
 
Je ushahidi huu unatosha kumhukumu JK?if that is true, Je nchi inakwenda wapi?
 
Dr Inaonyesha Unajua Vitu Vingi Sana Au Pengine Uko Karibu Na Watu Wengi Kutokana Na Michango Yako Katika Jukwa La Jambo

Tunaomba Utupe Wasifu Wa Watu Wote Wawili Halafu Tujadili Au Fungua Thread Yao Pekee .

Ahsante

ndio maana niliomba tupewe special debate forum then hoja zianze. Lakini nilifikiri kuwa kama watu wanapeana kazi kwa uzoefu basi Suluma Kassim alikuwa na uwezo zaidi ya Tido, the same applies kwa wao kumpa kazi SUSAN MUNGI wakati kuna yule binti mtoto wa KAMBONA ambaye yuko pale ofisi za EU, japo ni mkristo lakini ukiniuliza naweza kusema kuwa ni mzoefu na msomi zaidi kuliko susan Mungi
 
Hii ya Kusema Tido kaishia Form 4 ushahidi upo? inawezekana kaongeza ujuzi ktk course mbalimbali. Unajua tena ulaya, hawaangalii tu Form 4 wanaangalia pia umri na uwezo na uzoefu kazini, vinaweza kukupa nafasi za masomo ya juu, kuliko kwetu home.
 
NUGWI MAMBO ??

NAFIKIRI WEWE TUMEZOZANA MARA NYINGI KATIKA ZNZWEBSITE KUHUSU MADA HII WENGI WAKACHANGIA HUJARIDHIKA UKAAMUA KUILETA HUKU KUVUKA MIPAKA ZAIDI , WACHA NICHANGIE KIDOGO TU KUTOKANA NA UZOEFU WANGU .

MIMI NIMAZALIWA KATIKA FAMILIA YA KIKRISTO , SHULE YA VIDUDU NILIZOMA AGHA KHAN , DARASANI WAHINDI WATUPU WAISILAMU NA WAHINDU , NIKAENDA SHULE YA MSINGI NGUZO , WAHINDI NA WAARABU LAKINI NIKIRUDI NYUMBANI NI MAMBO YA BIBLIA , NIKIRUDI MITAANI RAFIKI ZANGU KINA SAIDI HUKO MOROGORO WAISILAMU .

NIKAENDA KENYA KUSOMA ZAIDI , PALE DARASANI NILISOMA NA WACHINA NA WAPHILIPINO , WENGI NI WABUDHA , MARA KADHAA NILIKUTANA NA SINGA SINGA WOTE HAWA NIMEISHI NA KUKUWA NAO SIKU ZOTE HIZO .

BAADAYE NIKAJA KUKUA ZAIDI NA KUJUANA NA WATU ZAIDI NYUMBANI KWETU WATU WENGI WAKAAMUA KUWA WALOKOLE WAKAACHANA NA ULUTHERI , WENGINE KWA KAKOBE , EFADHA NA PALE KWA MAMA RWAKATARE YOTE HAYA NI MAISHA

KWAHIYO NIMEKULIA KATIKA MISINGI HIYO NA NIMEONA MENGI , SASA UNAPOSEMA TUCHAGUE VIONGOZI KUTOKANA NA DINI AU IMANI NASHINDWA KUKUELEWA , WENGINE HATUJAKULIA KATIKA MAZINGIRA NA WALA HATUNA ASILI YA KUISHI KUTOKANA NA MATABAKA TUMESOMA NA WATU WOTE , NA SASA HIVI TUNAFANYA KAZI NA WATU WOTE .

KUTOKANA NA UZOEFU WANGU NAAMINI KATIKA VITU 3 VIKUU NAVYO NI AMANI YA KWELI , UHURU NA UPENDO WA KWELI , VINGINE VYOTE HUJA NA KWENDA KUTOKANA NA MAZINGIRA , KAMA TUKIISHI KWA AMANI , TUKIWA NA UPENDO BASI NCHI ITAENDESHWA KWA AMANI NA UHURU

NUGWI SIKILIZA NYIMBO MOJA INAITWA MUONGO NA MULOZI BY FRANKO UTAELEWA UJUMBE WANGU
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom