Mkapa anakana vipi matokeo ya Sera yake iliyoshindwa?


Chuo Kikuu cha Dodoma ni Mkapa's brainchild, Kikwete amekuja kuhimiza tu mifuko ya pensheni itumbukize fedha zake pale na kujenga chuo ambacho majengo yake ingawa ni ya gharama kubwa lakini ni ya kiwango cha chini na sidhani yatadumu hata muongo mmoja na nusu!! Tunazalisha wahitimu kila mwaka lakini hakuna ajira wala mitaji ya kuwawezesha kujiajili they end up joining the army of the unemployed!
 
Ni ujinga usio kifani kwa nchi kubinafsisha reli na bandali yake kwani hizi ni strategic infrastructure assets kwa nchi!! Reli yetu tungeweza kuikarabati kwa kutumia resources zetu wenyewe kama tungetumia akili katika mikataba tulioingia kijinga kwenye kuchimba madini na sasa tunafanya makosa yale yaale kwenye uchimbaji wa gesi! Ufisadi wa viongozi wetu kwa kuwakumbatia wafanyabiashara wa trucking industry[ ambako nao ni wabia] ndio kumeifanya serikali isiwe na moyo wa dhati wa kuikarabati reli ya kati kwani ingeuwa kabisa biashara yao ya malori lakini nchi ingefaidika kwa kupunguza mfumukoa wa bei kutokana na lower transport costs!! Kuna mtu ameuliza nadhani Waberoya kuwa nani aliwapa wahindi TRC jibu ni Mkapa kwa kupitia kwa Any chande na ukitaka kujua uhusiano wao soma kitabu cha Chande" A knight from Bukene"
 
nimekuwa nikiikwepa hii thread sababu ni kuogopa ban! I hate hili liuaji.
 
Ni ujinga usio kifani kwa nchi kubinafsisha reli na bandali yake kwani hizi ni strategic infrastrure assets kwa nchi!! Reli yetu tungeweza kuikarabati kwa kutumia resources zetu wenyewe kama tungetumia akili katika mikataba tulioingia kijinga kwenye kuchimba madini na sasa tunafanya makosa yale yaale kwenye gesi! Ufisadi wa viongozi wetu kwa kuwakumbatia wafanyabiashara wa trucking industry[ ambako nao ni wabia] ndio kumeifanya serikali isiwe na moyo wa dhati wa kuikarabati reli ya kati kwani ingeuwa kabisa biashara yao ya malori lakini nchi ingefaidika kwa kupungua mfumukoa wa bei!! Kuna mtu ameuliza kuwa nani aliwapa wahindi TRC jibu ni Mkapa kwa kupita kwa Any chande na ukitaka kujua uhusiano wao soma kitabu cha Chande" A knight from Bukene"
 
Mnajua ndiyo maana viongozi wa Tanzania hudhania watu hawana kumbukumbu vichwani mwao.
Yaani baada ya kuuza kila kitu anarudi na kukana hadharani.
Swali langu ni kuwa kama hakuwa yeye je ni nani aliyekuwa anafanya kazi yake?
 
Mkuu Waberoya
Lazima tu nikiri wazi kwamba nimeshindwa kuunganisha dots kati ya excerpt uliyoitoa na conclusion yako (in red)!! Je, unataka kuniambia hiyo excerpt inaonesha matunda ya ubinafsishaji au sekta zinazochangia uchumi wetu?! Binafsi, ninachokiona hapa ni kushindwa vibaya kwa sera za ubinafsishaji nchini na matokeo yake kilimo kinaonekana bado ndio shughuli kuu ya kiuchumi na mamilioni ya Watanzania. Pamoja na mambo mengine, lengo kuu la ubinafsishaji na kuongeza tija ambayo in turn itakuwa source of employement! Badala yake, kilimo kinaonekana bado ndio source kubwa ya ajira kwavile ubinafsishaji ambao ungeweza kutoa ajira umeshindwa. Sana sana hapo ninachokiona ni kwamba unataka kuchanganya kati ya ubinafsishaji na ukuaji wa sekta binafsi! Ni ukweli usiopingika kwamba, sekta binafsi imekua nchini lakini ni asilimia ndogo sana ya ukuaji huo ambao umetokana na ubinafsishaji. Leo hii pangekuwa na contribution kubwa kwenye textile industry, basi sina shaka yoyote kwamba matunda hayo yangetokana na ubinafsishaji! Endapo contribution kubwa kwenye national economy ingekuwa ni viwanda, basi sina shaka yoyote kwamba hiyo ingekuwa ni result ya ubinafsishaji. Kwa bahati mbaya, labda tuiangalie hii kwa makini: "Livestock population in Tanzania is great, but due to lack of packaging and preserving industries, export of eanimal products has become difficult in the country." Sentensi hiyo fupi ndani ya andiko kuu, inadhihirisha namna gani ubinafshaji umeshindwa kwani pamoja na kwamba Ranch za Taifa zilibinafsishwa, lakini bado zoezi hilo limeshindwa kutatua tatizo la msingi ambalo suluhisho lake lingekuwa ni kuwapo kwa viwanda vya usindikaji wa nyama na hivyo kuwezesha export.

Sasa, turudi kwenye hoja ya msingi, UBINAFSISHAJI!
Kimsingi, UBINAFSISHAJI ni sera muhimu lakini sina shaka yoyote kwamba nchi yetu ilikuwa haijajiandaa kwa sera hiyo!! Katika hili, naomba chochote kinachobinafsishwa nikiite "kampuni" ili kurahisisha majadiliano! Hivyo basi, binafsi, ninapoangalia ubinafsishaji huwa siangalii ni nani ananunua kiwanda husika bali naangalia economic impact after privatisation. Kama patakuwa na positive impact, then i don' care kama kampuni husika itakuwa imenunuliwa na Mzawa au Mgeni kwa 100%!!

Let's go step by step! Assume we've TWO companies; X and Y, where company X is fully owned by a Tanzanian Investor and Company Y is fully owned by a Foreign Investor. Pamoja na yote hayo, Company X inategemea majority ya inputs kutoka nje kiasi kwamba inatumia as much as 80% ya mapato yake kwenda nje kwa ajili ya vipuri, malighafi, na mengineyo! Kwa maana nyingine, only 20% of company revenues circulates in country economy and the remainder circulates in foreign economies! Kwa upande mwingine, Company Y inatumia as much as 80% ya mapato yake ndani ya nchi kwa ajili ya gharama za malighafi, vipuri, manpower, etc. Kwa maana nyingine, as much as 80% of company Y's revenues circulates in country economy and only 20% circulates in foreign economies! Kwangu mimi, hata kama Company Y inamilikiwa na mgeni kwa 100% then ubinafsishaji wake una tija maradufu kwa nchi kuliko ubinafsishaji wa Company X aliyouziwa Mzawa! G

enerally speaking, over 95% ya ubinafsishaji uliofanyika nchini ni sawa na ubinafsishaji wa Company X ambao katu hauwezi kuwa na tija hata kidogo hata kama tutaona kampuni fulani inafanya vizuri. Take a good example of TBL ambayo mara kwa mara inapigiwa mfano na serikali…..ni kweli inafanya vizuri sana na ni kampuni ambayo inalipa kodi kwa kiasi kikubwa sana nchini! Hakuna ubishi katika hilo! The question is, ni % ngapi ya TBL revenue ina-circulate kwenye national economy? Tuangalie hilo huku tukizingatia kwamba, hata chupa nasikia wanaagiza kutoka nje! Je, ni ngano ya Kitanzania kiasi gani inatumiwa na TBL?!

NINI KINGEPASWA KUFANYIKA?!
Hilo ndio swali ulilohoji kwenye posts zako! Kama alivyoshauri mdau mmoja…..suluhisho hapo ilikuwa ni kufanya ubia kati ya serikali na wawekezaji ili kupunguza kile kiasi ambacho kinaenda ku-circulate nje ya nchi. Ikumbukwe kwamba, NET profit ya kampuni ambayo ni fully owned by Foreign Investor itaenda nje ya unless afanye re-investment ambayo nayo NET profit yake pia itaenda nje. BUT, endapo pangekuwa na ubia kati ya serikali na foreign investors, part of NET PROFIT inge-circulate nchini.

Alternatively, pangefanyika Management Contract. Ni ukweli ulio wazi kwamba kulikuwa na poor management kutoka kwa wazawa. Management Contract ingepunguza kwa kiasi kikubwa udhaifu uliokuwa umetokana na poor management. Najisikia ukakasi kidogo kutamka bayana kwamba pamoja na kwamba Watanzania wengi ni wasomi na wenye uwezo wa kuongoza lakini inaelekea hatuna uwezo wa kuongoza vya kwetu wenyewe hususani kama ni vya serikali. Naandika haya huku nikipata taarifa za kupinduliwa kwa bodi ya wakuregenzi wa kampuni ya uwekezaji ya NICOL! Najisikia vibaya zaidi hasa nikikumbuka kwamba, wakati inaanzishwa kampuni ya NICO, niliandika makala ndeeeeefu kwenye gazeti la Rai kuelezea ni namna gani nchi inahitaji makampuni kama NICO! Matokeo yake, kwa mara nyingine NICO ime-prove ni namna gani tusivyoweza kuendesha vitu vyetu wenyewe!
 
Habari hii ni kwa hisani ya gazeti la 'The citizen'

My take: BWM anataka kutuambia kazi yake ilikuwa kutangaza ubinafsishaji na yanayofuata haikuwa kazi yake 'wamerudia utumbo ule ule hilo si tatizo langu'. Kazi yake kama rais ilikuwa kutangaza tu! phew!

Marekani ilipoamua ku-bail out viwanda na mashirika, Obama alikuwa anafuatilia hadi kuhakikisha pesa za wananchi zimerudi na 'proud' ya marekani inabaki pale pale. GM ni namba one tena! Kwanini BWM hakufuatilia kujua kuwa 'tangazo' lake limefanyiwa kazi kama inavyopaswa!

Nani aliteua 'management' za TAZARA, TRC, BANDARI kwa kutaja machache. Je, BWM akiwa kama rais hakujua kuwa mashirika hayo ni 'lifeline ya economy' na alifanya nini kuyanusuru hata kabla hayafikia hatua mbaya.
Ni Raia gani au kiongozi gani aliyekuwa na uwezo wa kuteua watendaji na bodi ya mashirika hayo ambaye tunaweza kumsota kidole kama si BWM.
 
Siku zote nilikuwa nawaambia Mkapa ni kapa watu hawakutaka kuamini. Mkapa ndiye kaifilisi nchi na sasa tumepanga ktk nchi yetu wenyewe...
 
Alipoanza hizo vurugu za ubinafisihsaji,mwalimu alimbana bana kwa hoja, nakumbuka kuanzia ile issue ya NBC, mwalimu alipofariki tu ndo ikawa kama "fungulia mbwa"
 
Bahati mbaya anaposhambuliwa Mkapa kuna watu(misingi ya udini) hufurahi sana,mara nyingine husahau hata busara zao za muda mrefu tu zilizowajengea heshima hapa au hata kwingine ambako hujitokeza kama wachambuzi.Ubinafsishaji is the worst thing,unfortunately ulitokea wakati Ben yupo Magogoni.Lakini siku hizi blander za JK kuna ngonjera inaitwa Mfumo,System,Wasaidizi wake yeye hana Tatizo and the Like.Hivi Ben alikuwa One-Man-Arm?Alikuwa Stand-alone?Kwa hiyo all in all ubinafsishaji ulishindwa OK,what the successor did to revert?Richmond,Kagoda,Dowans,Strikes,corruption in public funds,inflation rate,budget deficity.M.M Mwanakijiji you are right Bro,But in a wide view.CCM-Haikubaliki.Mfumo ulishafeli-Cardiac Attack na London alikoponea Muamba ni 2015.
 
“Tulibinafsisha mashirika na viwanda 330, kati yake 180 walikabidhiwa Watanzania na 23 wageni, vilivyobaki vilimilikiwa kwa ubia kati ya Watanzania na wageni, kwanini watu hawahoji sababu za hata wenyeji kushindwa kuviendeleza? Twende tufanye utafiti tupate sababu za kushindwa,”alisizitiza Mkapa



1) 180 + 30 = 330 NDIO au HAPANA?
2) Hao Watanzania "wenyeji" ni akina nani? Maana kuna Wa-Tz kibao ambao sio wazalendo wala wenyeji wa nchi hii
3) Kwa nini hataka kukubali kuwa yeye, familia yake na jamaa zao ndio tu waliofaidika na huo ubinafsi (ondoa neno "shaji" maana sijui liliwekwaje hapo)?
 
Mkapa anazidi kuchanganyikiwa tena hadharani. Prof. Shivji yuko sahihi kabisa....huwezi kuachia njia kuu za uchumi halafu uweze kuthibiti/kuratibu uchumi wa nchi kwa tija...IMPOSSIBLE!


Akubali akatae, hakuwa makini ktk privatization. Walisukumwa na ubinfsi, tamaa na choyo badala ya upendo, uadilifu na maonno ktk zoezi lile, Na pia wangechagua kwa kupanga maeneo na awamu za hiyo privatization. Sasa hata huduma muhimu kama umeme, maji, mabenk, madini nk. Every dog knows he's wrong, ubishi wa nini!
 

Mkuu sekta kuu ya uchumi nchi hii ni kilimo

ni kichekesho kusema kuwa sisi ni maskini kwa asilimia kubwa kwa sababu ya ubinafsishaji!

yaani isifike wakati tukaona utajiri wetu unatagemea tu ubinafsishaji! wakati kilimo ndio uti wenyewe

Kuwa nini kilitakiwa kifanyike ndio hasa lengo langu na umeeleza vyema, That wehre we were supposed to criticise this man kwa kutumia hizo mistakes

kusema sera ya ubinafishaji imeshindwa ili hali tunashuhudia even developed countries wame adopt si sahihi , sera iko sahihi wala haijashindwa....kosa ni poor contracting, bad management na ufisadi katika kuyauza ,,I cant oppose this fact
 

Yes they did it wrongly!
 

Mkuu Waberoya,
Hakika sitathubutu kudai kwamba umaskini tulionao unatokana na ubinafsishaji! La hasha! Umaskini wa kutupwa tunao kabla ya ubinafsishaji na hata baada ya ubinafsishaji! Na kwa sera zilizopo, sichelei kusema utaendelea kuwapo hata baada ya urasmishaji (formalization)! Pamoja na yote hayo, vilevile siwezi sita kwamba ubinafsishaji umeshindwa vibaya sana kutokana na sababu ambazo tayari zimeshaongelewa. Si kwamba umeshindwa duniani, la hasha bali Tanzania na bila shaka sehemu yoyote duniani ambayo ilifanya ubinafsishaji kama ambavyo sisi tulifanya.
Kwa upande mwingine, ni kweli bado kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hii kwavile ndiyo sekta inayoajiri mamilioni kwa mamilioni ya Watanzania. Hili halijatokea kwa bahati mbaya; bali kutokana na ukweli kwamba mamilioni ya Watanzania bado wanaishi vijijini ambako hakuna njia mbadala za kujikimu! Mbaya zaidi, kilimo chenyewe si chenye tija kutokana na ukweli kwamba sekta ya kilimo haiwezi kusimama pekee yake kisha tukaitarajia itoe tija. Lau kama ubinafsishaji ule ungekuwa umefanyika vizuri, bila shaka kilimo kingekuwa na tija hivi sasa! Tabia moja wapo ya bidhaa za kilimo ambayo ndiyo inasababisha kilimo kisiwe na tija ni perishability ya most of agricultural products. Mwarobaini wa hali hii ni uwepo wa viwanda vya bidhaa za kilimo-agroprocessing industries. Ufanisi wa viwanda hivyo ungekuwa ndo nguzo muhimu ya soko la uhakika la bidhaa za kilimo na hapo bila shaka pangekuwapo na kilimo chenye tija kwa mwananchi. Viwanda hivyo vilikuwepo lakini kwavile ubinafsishaji wenyewe ulikuwa wa hovyo hovyo bado vimeshindwa kutimiza dhima kuu ya ubinafsishaji.

Hakuna ubishi kwamba, tumejikwaa na tumedondoka! Mjinga akidondoka atabaki hapo hapo huku akilia…..labda akisubiri atokee wa kumuhurumia kisha amwinue! Hili ndilo linalotokea na ndio maana hatuachi kumlaumu Mkapa kwa sera yake iliyoshindwa!

Wakati mjinga angebaki alipodondokea huku akilia, mwerevu angefanya jitihada za kuinuka haraka na ikiwezekana pasiwepo wa kugundua kwamba alidondoka! Kwa mwerevu, kudondoka ni aibu….mwerevu hapendi ahurumiwe pasipo na sababu ya msingi ya kuhurumiwa! Mwerevu hapendi kuchekwa….aghalabu, mtu akidondoka huchekwa! Anachekwa kwavile anadhihirisha ama hayupo makini au hayupo fit!

Sera ya ubinasfishaji ikaifanya serikali yetu idondoke! Mbaya zaidi, serikali haikuwa imevaa bukta wala nguo ya ndani.....ilidondoka huku ikiwa imejivika msuli pekee! Serikali ikabaki hapo huku ikiwa haijui cha kufanya! Wananchi wa kawaida wamebaki wakilia lia! Wabunge wamebaki wakilia lia! Eti hata wasomi nao wamebaki wakilia lia! Hakuna anayehangahika kutaka kuinuka ili aibu ya kudondoka isionekana na wata wasio na macho!
Ningekuwa serikali ningefanya jitihada za kuinuka ili nisiendelee kuchekwa! Ningekuwa msomi, ningeionyesha serikali namna ya kuinuka badala ya kulia lia! Hali kadhalika, ingekuwa mbunge au mtu muhimu wa nchi ningejitahidi kumwinua serikali au angalau kuonesha njia za namna gani ingefanya!
Wasomi wetu ni hodari wa kulia lia pasi na kuonesha njia! Mimi, siwezi kujibaraguza kwa kujiita ni miongoni mwa wasomi wa Nchi hii. Hata hivyo, nipo njiani kuonesha njia kwa serikali kupitia andiko langu nililolibatiza TANZANIA'S ECONOMIC DEVELOPMENT BIBLE! Haidhuru hata kama haitafuatwa, lakini angalau nitakuwa nimejiondoa toka kwenye taifa la wenye kulia lia!
 
Mh. Ben kumbe nawe ni member wa jf? Jibu hoja zilizotolewa acha kutupa stori zile zile
 
Yes they did it wrongly!


You might think that they did it wrongly; I think they did it by design so that it would be wrong but they would benefit from it!!Look at the assets that the former chairman of PSRC has accumulated here in Dar and in Mwanza; can John Rubambe account how he lawfully acquired these assets? It is in the same vein that Kiwira coal mine was handed to Mkapa. These guys were nothing but ROBBER barons.
 
Mkuu, nadhani umeenda mbali sana na kuwatuhumu watu kwa chembe za udini.

Kwa taarifa hakuna kiongozi anayeshambuliwa 'one man army' hata pale alipofanya maamuzi mazuri na kuzembewa na watendaji wake kama Nyerere.

Rais Mwinyi naye anashambuliwa kwa kufunguliwa milango kila kitu.
Anatuhumiwa kwa kuacha shilingi ipoteze thamani yake, kuruhusu mijadala ya uundwaji wa Tanganyika, OIC n.k.

Kikwete hadi sasa ana sifa ya kuwa kiongozi dhaifu na anyetumia ujanja kama ghilaba ya utawala hadi kuitwa msanii.
JK amebeba mizigo mizto kama ya Richmond ambayo ina mu-implicate bila kificho.
Nadhani muda wake utakapokwisha atakuwa na historia mbaya kuliko kiongozi mwingine.

Kawawa anatuhumiwa kuendesha zoezi la oporesheni vijiji bila maarifa wala busara.
Sokoine anaonekana mtu aliyeanzisha mambo ya nguvu kazi ambayo tija yake haionekani, kama ambavyo Sumaye anatuhumiwa kuwa PM wa 'ndiyo mzee' huku akijikatia mapande ya ardhi bila woga haya au kificho.
Lowassa ndiye kiongozi aliyechafuka na uchafu wake unajadiliwa hapa bila aibu, kinyongo au woga kila uchao.

Siyo sahihi kusema BWM anashambuliwa kwa dini labda tu kama unataka kumtetea kwa kuchomeka hoja dhaifu kama hiyo. BWM yeye mwenyewe katika hotuba hapo juu amesema 'asilaumiwe kwa utumbo'. Mkapa amekuwa mstari wa mbele kutetea sera za ubinafsishaji. Unakumbuka alivyotetea uuzaji wa bilioni 15 wa NBC. Unakumbuka alivyosimama kidete kuhakikisha mashirika yanakufa. Unakumbuka Nyerere alipofuatwa Butiama ili kununu shea za CRDB alisema nini kuhusu NBC!!

Ni muhimu ukumbuke kuwa Mkapa alikuwa Rais,mwenyekiti wa chama, mwenyekiti kamati kuu na baraza la mawaziri. Maamuzi yote yanayotolewa yeye alikuwa na 'veto' aliyopewa na wananchi kwa njia ya katiba.
Kwahiyo 'the buck stops with him'

Itakuwa ni kituko kama tutaanza kulaumu baraza la mawaziri kwa uuzwaji wa kipuuzi wa mashirika ya umma.
Kumbuka Mkapa ndiye alikuwa na dhamana ya rasilimali za taifa.
Mawaziri ni viongozi wa kupita tu na yeye ndiye anayewateua na wanwajibika kwake.
Kwahiyo hakuna namna tunayoweza kumlaumu mkuu wa mkoa wa Morogoro kwa ujinga wa kuuza Mang'ula au kumlaumu Mkuu wa wilaya ya mwanza kwa ugawaji wa bure wa Mwatex

Unafahamu kuwa Rais ndiye anayeteua viongozi wa mashirika na bodi zao, kwanini leo tuone hahusiki na uzembe wa kuuza mali zetu tena kwa shemeji na wakwe zake. Please!please!

Alipouza Kiwira kwa wakwe zake na mashemeji pesa hazikwenda kanisani, kwahiyo hakuna uhusiano wa imani yake na udalali wa mali zetu. Hatuwezi kumvua imani yake ili tumwambie ukweli. Tutamwambia ukweli kama BWM, aliyekuwa rais wa nchi na mwenyekiti wa chama,period! Hatujui kama ni muumini wa imani gani na wala hakuna sababu ya kujua hivyo.

Kama una hoja juu ya Mkapa na unataka kuitetea basi jibu hoja kwa hoja. Kutafuta kisingizio cha udini bila kujibu hoja ni kufunika uvundo kwa kupulizia manukato.

Nani asiyejua kuwa wizi wa Kagoda ulianzia kwa Mkapa. Nani asiyejua kuwa mikataba ya hovyo iliisainiwa akiwa ofisini katika siku za mwisho. Nani asiyejua siri ya Mkapa na Balali, RA na kundi la wahalifu wengine tunaowajua leo hii.

BWM ni kiongozi aliyeliumuiza taifa hili kwa kutoa sadaka mali na rasilimali za nchi bila aibu, haya au maarifa.
Aliyafanya hayo akiongozwa na kiburi ikiwa ni pamoja na kututukana kuwa na wivu wa kike.
Ndiyo maana leo tunamuuliza ubinafsishaji umeleta tija gani hana la maana ila kusema 'kama wamerudia utumbo si shauri lake'.

Mkapa hajawahi kuhudhuria shughuli zozote za Kigoda au MNF, sina uhakika naye ni mwanaJF maana ilishawahi kuhojiwa kwanini hajitokezi kwenye shughuli za 'mentor' wake. Anyway, sasa hivi amejitokeza kujisafisha akielewa wazi kuwa taifa linaugulia ubabe wake na hasara kutokana na kile kinachojulikana kama 'jeuri'.

Tusimseme kwasababu kufanya hivyo ni kumshambulia kwa imani yake! too low, we can't buy it.
Kuna neno gani mbadala la uzembe! ufisadi, na udalali!

Hajawahi kusimama na kueleza wizi uliofanyika mikononi na machoni mwake, alichokifanya ni kukimbilia makanisani kujisafisha na huo ndio udini aliotaka kuupandikiza. Huwezi kugawa Kiwira kwa wakwe zako, kuruhusu Kagoda halafu uende kujitetea madhabahuni. Huko watu wanakwenda kutubu na si siasa. Hili ameshindwa!
Tumemtoa huko na hatutamwacha hadi pale atakapotueleza ukweli kuhusu mali zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…