Je, kisukari hakiwezi kutibika kwa transplant ya kongosho?

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Mar 16, 2019
7,693
17,257
Habari za majukumu wana jukwaa?

Nimekuwa nikijiuliza hili swali. Ikiwa ugonjwa wa kisukari ni matokeo ya organ ya kongosho kushindwa kuzalisha kimeng'enya cha insulin cha kutosha kwenda ku balance kiwango cha sukari kwenye damu.

Je, haiwezekani muathirika wa hili tatizo akafanyiwa upasuaji ikaondolewa hii kongosho iliyoshindwa kazi yake akawekewa nyingine nzima na tatizo likawa limetibika kwa namna hiyo?
 
binadamu ana kongosho moja sio kama kidney tunazo mbili kwahyo mtu anaweza kuwa donor akatoa kidney moja akampa mwenye sida ya kidney na wote wakaishi. Je wewe kongosho limefail nani atoe kongosho lake moja akupe wewe ili uishi na yeye afe kwa kutokua na kongosho.

ni kama ubongo kila mtu anao ubongo mmoja, je mtu akiwa kichaa kwanini asifanyiwe transplant ya ubongo mwingine ebo ?! (Japo sina hakika juu ya uwezekano wa transplant ya ubongo, ila tufikiri inawezekana) Huo ubongo mwingine unautoa wapi ??!
 
Habari za majukumu wana jukwaa?

Nimekuwa nikijiuliza hili swali. Ikiwa ugonjwa wa kisukari ni matokeo ya organ ya kongosho kushindwa kuzalisha kimeng'enya cha insulin cha kutosha kwenda ku balance kiwango cha sukari kwenye damu, je haiwezekani muathirika wa hili tatizo akafanyiwa upasuaji ikaondolewa hii kongosho iliyoshindwa kazi yake akawekewa nyingine nzima na tatizo likawa limetibika kwa namna hiyo?View attachment 2817963
Utafanyia transplant watu wangapi bwashee (ikiwa 20% ya watanzania wana kisukari?). Hayo makongosho 12,000,000 ya kuwafanyia transplant hao wagonjwa 12m utayapata wapi?

Mkiambiwa acheni kula michipsi, miugali na mawali hamtaki. Fanyeni mazoezi hamtaki. Eti mnataka transplant. Pambaneni na hali zenu.
 
binadamu ana kongosho moja sio kama kidney tunazo mbili kwahyo mtu anaweza kuwa donor akatoa kidney moja akampa mwenye sida ya kidney na wote wakaishi. Je wewe kongosho limefail nani atoe kongosho lake moja akupe wewe ili uishi na yeye afe kwa kutokua na kongosho.

ni kama ubongo kila mtu anao ubongo mmoja, je mtu akiwa kichaa kwanini asifanyiwe transplant ya ubongo mwingine ebo ?! (Japo sina hakika juu ya uwezekano wa transplant ya ubongo, ila tufikiri inawezekana) Huo ubongo mwingine unautoa wapi ??!
Nilichotaka kujua ni ìkiwa kisukari kinaweza kutibiwa kwa transplant ya kongosho kuhusu linapatikanaje hiyo ni issue nyingine. Kuna nchi wana form unajaza ikiwa utafariki ghafla wanaruhusiwa kuvuna organ zako za muhimu wanazihifadhi kwa ajili ya kuja kuwapa wahitaji baadae so supply ya organ sio issue sana
 
Mkuu wewe unakula nini? Je kama kongosho likipatikana ukawekewa unaweza kupona kisukari, ndo hoja yangu ilipo.
 
Tutachukua ubongo wa waisrael wanaounana kibwege huko
 
Nilichotaka kujua ni ìkiwa kisukari kinaweza kutibiwa kwa transplant ya kongosho kuhusu linapatikanaje hiyo ni issue nyingine. Kuna nchi wana form unajaza ikiwa utafariki ghafla wanaruhusiwa kuvuna organ zako za muhimu wanazihifadhi kwa ajili ya kuja kuwapa wahitaji baadae so supply ya organ sio issue sana
ok nimekupata mkuu in that case its possible but yote ya nini nadhani ni bob Marley aliwahi kusema "if life has come jo an end, why struggle to extend it, while even if succesful it shall surelly end soon or later...., there is no joy in extending life"

mkuu uko na kisukari ?
 
Kabla ya kujibu swali lako naomba tufahamu kidogo aina za kisukari, kuna:
- kisukari cha kupanda: kisukari hiki husababishwa na kongosho kushindwa kutoa hormone ya insulini ambayo husaidia kupunguza sukari kwenye damu. (Mtoa mada unamaanisha kisukari cha aina hii)

- kisukari cha kushuka: hiki husababishwa na upungufu wa ADH (Antiduretic hormone) ambayo huusika na kufanya reabsorption ya sukari na maji katika figo, mgojwa huyu hupata mkojo wa mara kwa mara hivyo kupoteza sukari nyingi kwa njia ya excretion (urination)

Lakini pia tufahamu kuwa kisukari kinaweza kurithiwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine kama magonjwa mengine ya kurithi au ukapata kutokana na sababu zingine za mtindo wa maisha, chakula au umri.

HOJA YA MATIBABU YA KUPANDIKIZWA KONGOSHO.
Matibabu ya upandikizaji wa kongosho yatawezekana pale ambapo "kongosho peke yake" ndio inatatizo la kushindwa kuzalisha hormone ya insulini na si vinginevyo. KWANINI?.

- Ili insulin izalishwe lazima ipate taarifa kutoka kwenye tezi kuu katika ubongo (Hypothalamus). Lakini tezi hii kuu (Hypothalamus) ikishindwa kutoa taarifa hii, Basi hata kongosho ikiwa na hali nzuri kiasi gani haiwezi kuzalisha hormone ya insulini, hvyo hata ukibadilishiwa kongosho mpya, huwezi kupona kusukari.

- Upatikanaji wa Organ kongosho pia ni si rahisi kwa sababu lazima upate mtu ambaye hana uhitaji wa kongosho hio (just like heart transplant).

Wajuzi zaidi wataongezea nyama!!
Ahsante!!!
 
Mkuu wewe unakula nini? Je kama kongosho likipatikana ukawekewa unaweza kupona kisukari, ndo hoja yangu ilipo.
Mimi nakula viazi vitamu, mihogo, ndizi, magimbi, kuku, samaki, mchicha etc
Hakuna haja ya kufanya transplanting ili kutibu kisukari. Kupandikiza kwenye kongosho cells za kutengeneza insulin itakuwa bora zaidi.
 
Kabla ya kujibu swali lako naomba tufahamu kidogo aina za kisukari, kuna:
- kisukari cha kupanda: kisukari hiki husababishwa na kongosho kushindwa kutoa hormone ya insulini ambayo husaidia kupunguza sukari kwenye damu. (Mtoa mada unamaanisha kisukari cha aina hii)

- kisukari cha kushuka: hiki husababishwa na upungufu wa ADH (Antiduretic hormone) ambayo huusika na kufanya reabsorption ya sukari na maji katika figo, mgojwa huyu hupata mkojo wa mara kwa mara hivyo kupoteza sukari nyingi kwa njia ya excretion (urination)

Lakini pia tufahamu kuwa kisukari kinaweza kurithiwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine kama magonjwa mengine ya kurithi au ukapata kutokana na sababu zingine za mtindo wa maisha, chakula au umri.

HOJA YA MATIBABU YA KUPANDIKIZWA KONGOSHO.
Matibabu ya upandikizaji wa kongosho yatawezekana pale ambapo "kongosho peke yake" ndio inatatizo la kushindwa kuzalisha hormone ya insulini na si vinginevyo. KWANINI?.

- Ili insulin izalishwe lazima ipate taarifa kutoka kwenye tezi kuu katika ubongo (Hypothalamus). Lakini tezi hii kuu (Hypothalamus) ikishindwa kutoa taarifa hii, Basi hata kongosho ikiwa na hali nzuri kiasi gani haiwezi kuzalisha hormone ya insulini, hvyo hata ukibadilishiwa kongosho mpya, huwezi kupona kusukari.

- Upatikanaji wa Organ kongosho pia ni si rahisi kwa sababu lazima upate mtu ambaye hana uhitaji wa kongosho hio (just like heart transplant).

Wajuzi zaidi wataongezea nyama!!
Ahsante!!!
Shukrani kwa elimu, umefafanua vizuri sana
 
Habari za majukumu wana jukwaa?

Nimekuwa nikijiuliza hili swali. Ikiwa ugonjwa wa kisukari ni matokeo ya organ ya kongosho kushindwa kuzalisha kimeng'enya cha insulin cha kutosha kwenda ku balance kiwango cha sukari kwenye damu.

Je, haiwezekani muathirika wa hili tatizo akafanyiwa upasuaji ikaondolewa hii kongosho iliyoshindwa kazi yake akawekewa nyingine nzima na tatizo likawa limetibika kwa namna hiyo?
you can reverse or manage diabetes by doing the following ()makali ya kisukari):
  • punguza kula vyakula vyenye asili ya uwanga kwa asilimia kubwa (mchele mweupe, ngano nyeupe, sembe)
  • ondoa kabisa matumizi ya sukari (sugar) kwenye vyakula vyako (maandazi, chapati, keki, visheti, kaimati)
  • ongeza mbogamboga na vyakula vyenye protini (broccoli na cauliflower ni nzuri sana kwa kubalance sukari)
  • usinywe juice, soda zenye masukari mengi, badala yake kula tunda aina moja tu kwa siku tena sio kwa wingi.
  • punguza kula mara kwa mara na hasa usiku maana chakula huwa hakipati nafasi kubwa ya kutumika mwilini.
  • mazoezi hata kama ni walking kwa dakika 15 mpaka 20 kwa siku baada ya mlo wa jioni
 
Theoretically, hiyo itakua applicable for Type 1 Diabetes Mellitus.

Ila kwa Type 2 ambapo kuna insulin resistance, hata uweke kongosho “jipya”, still your cells won’t be able to absorb and use sugar
 
Habari za majukumu wana jukwaa?

Nimekuwa nikijiuliza hili swali. Ikiwa ugonjwa wa kisukari ni matokeo ya organ ya kongosho kushindwa kuzalisha kimeng'enya cha insulin cha kutosha kwenda ku balance kiwango cha sukari kwenye damu.

Je, haiwezekani muathirika wa hili tatizo akafanyiwa upasuaji ikaondolewa hii kongosho iliyoshindwa kazi yake akawekewa nyingine nzima na tatizo likawa limetibika kwa namna hiyo?

Habari!

Kulingana na swali lako, ni kweli kuwa upadikizaji wa kongosho kwa wagonjwa wa kisukari NI SULUHISHO kwa BAADHI ya wagonjwa wa kisukari na matatizo mengine yahusuyo kongosho.

Hii inatokana na aina ya tatizo la msingi kwa wagonjwa husika, kwani kisukari kina aina mbalimbali ambazo ni msingi tofauti wa kasoro na aina ya tiba.

Mfano:

A: Hii inaweza kuwa suluhisho kwa wale ambao kwa njia moja au nyingine:

1: Kongosho halizalishi kabisa insulini.

2: Kongosho linazalisha kiasi kidogo cha insilini kisichotoshereza.

3: Kongosho linazalisha insulini mbovu/yenye ulemavu na isiyoweza kufanya kazi yake.

B: Hii haitakuwa suluhisho kwa watu ambao tatizo la sukari linatokana na:

1: Tatizo la viambata au enzymes baada ya insulini kutolewa.(process zilizopo tangu insulini kutolewa mpaka kufanya kazi yake).

2: Receptors/ sehemu ambayo insulini inaenda kufanya kazi ili sukari iingie kwenye seli ikiwa na shida ya kimapokeo.
(Mfano wa kufuri bovu wakati ufunguo ni mzima).

3: Aina ya kisukari cha kushuka chini, kwani hapa tatizo la msingi siyo insulini au wingi wake au receptors zake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom