Mkapa anakana vipi matokeo ya Sera yake iliyoshindwa?

matatizo gani ya leo yametokana na mkapa?

ebu eleza kuhusu reli ya kati...wahindi wako wapi?

tulikuwa na uwezo wa kutafuta mwekezaji mzuri na reli ingekuwa ina operate vizuri tu, wakaleta wahuni wahuni fulani hivi ambao waliingia ubia na watanzania ambao ni viongozi. leo wamefilisika

njoo ATCL

sababu ya mkapa na ambayo itabaki kuwa kweli ni kuwa

1. hatuna mitaji!!! fedha hamna ......somebondy prove Mkapa is wrong , sio kwa sababu kasema shivji basi ni sawa

2. Pili watanzania hawa ni wezi, waongo, wabinafsi,mafisadi, wankula mali za umma, nenda JKN aiport wafanyakazi karibu wote wana magari na wanapaki...huku shirika la nedege halina ndege hata moja!!! wanapata wapi mishahara??

hivi solution ya haya mashirika sio ubinafsishaji kweli??

kama ndivyo mtu aseme nini kifanyike

sera za ubainsafsishaji ni nzuri tena sana kwa nature yetu tulivyo...sasa kama kuna kasoro is something else kujadili hizo kasoro

HUWEZI UKASEMA DHANA NZIMA YA UBINAFSISHAJI NI FAILURE..huku hatuna alternative solutions

nchi hii leo hii inaendeshwa na yale yale aliyoyaacha mkapa, sasa for nearly 10 yrs anasema hakuna kiwanda kipya cha serikali, au ndio ATCL na TRC tunahesbabia, where is TTCL? si tulisema tunaweza kuendeleza? japo management yake ni wazungu leo hii haina mtaji wa kutodha kushindana

Tujiulize viwanda vilikufa kipindi gani? leo hii tukisema mashirika yarudishwe serikalini tunaweza kuyaendesha?? what a joke! tusijifanye kama hatuwajui watanzania...Mkapa alitujua vyema
siku zote adui namba moja wa maendeleo ya mtanzania atabaki kuwa ni mtanzania.....hili halina mjadala.....watanzania ndio walioifikisha TZ hapa ilipo.....ubinafsi,ulafi,uvivu, kujuana, na wizi wa mtanzania ndio umetufikisha hapa tulipo......Ubinafsishaji per se wala si shida......shida ni watu gani watanzania waliokuwa wanapewa hivyo viwanda/mashirika???........wengi walipewa kwa kujuana/kishkaji/kusaidiana.....na wengi wao pia hawakuwa na capacity ya ku manage walichobinafsishwa.....matokeo yake ndipo tulipo leo......Pia mikataba ya ubinafsishaji iliandaliwa na hawa hawa watanzania...na loopholes zooote za kifisadi zilifanywa na hawahawa watanzania.......itabaki kuwa pale pale kuwa anaeifilisi TZ ni mtanzania mwenyewe...period.....Hata mikataba feki wanayopewa wageni inaandaliwa na hawahawa watanzania.......wakulaumiwa kwenye kuiua TZ ni watanzania wenyewe...tena wasomi....very very sad indeed.......
 
Mkuu Wabes nimekusoma sana nadhani....

Ni kweli imeaminishwa hvyo kuwa Watanzania wavivu, wazembe, wabinafsi, wezi nk nk nk
na ni kweli katika maisha tunayoishi hlo si kazi sana kuliona!

Labda unisaidie kidogo, ni nini nafasi ya uongozi katika ku-shape watu wake?
Je watz hawa wa leo ndio wale wa zama zile za enzi viwanda hvyo vinaanzishwa?
Sababu sio haki tu kusema tupime eti sijui kwanini viwanda vilikufa na kwanini tunadhani tunaweza saiv!
Mi naomba nikuongezee swali lingine, Watanzania gani walioanzisha hvyo viwanda??
Hapo kuna hoja ipo, kwamba kama watz hawa walianzisha viwanda na kuviendesha kwa mda flani basi kuna kitu chanya kipo ndani yao zaidi ya hizo hasi nimeziorodhesha hapo juu!!

Tunapowatupia lawama watz pia ni lazima tuhoji ni kwa kiasi gani uongozi kwa dhana kamili ya uongozi umehusika kwenye kujenga watu wenye tamaduni ya aina fulani ambayo itakuwa rahisi kwa watu hao kuitikia ndoto na maono toka kwenye uongozi huo!
Hili Mkapa amelifanya kwa kiasi gani? Au alimuachia Mungu (kama kawaida yetu?)

Lakini Wabes we hauoni kuwa tabia za watoto zinaakisi mienendo ya wazazi wao?
Hicho ndio kilichotokea Tanzania, wananchi wa hovyo sababu serikali na utawala wa hovyohovyo tu.

Mi nadhani mara zote tutaendelea kujikwaa sababu tunakurupukia vitu bila kuvipima vitaendana kwa kiasia gani na utanzania wetu,
sera za kubinafsisha sawa ila je ni kwa kiasi gani serikali ilijenga uwezo wa kijasiliamali na kibiashara kwa watu wake?
Hata kwasasa bado watz wametelekezwa na hawajaandaliwa kupambana kisoko, huku mtaani kwetu shughuli kuu ni bidhaa za mbao na mbao zenyewe, ukiangalia mazingira ya utendaji wao na uzalishaji hawa watu na bidhaa inayokuja kukamilika ni wazi hawawezi kushindana na bidhaa za mchina zinazotokana na malighafi dhaifu ila ikipita kwenye teknolojia kubwa na ya juu....
Hatuwezi kutoka kwenye mfumo tuliokuwa enzi za awamu ya kwanza (ujamaa??) na kuja kwenye mfumo mpya wa wakina Mwinyi, Mkapa na Kikwete bila maandalizi mapya ya kifikra na kitamaduni.
Inawezekana Kikwete hajafanya kitu ila hyo haizuii baadhi yetu kupata harufu kali ya uvundo aliouacha Ben.
Inapokuja kwenye kushauri njia mbadala jibu ni moja tu TUNATAKA UONGOZI kwa dhana ile ile ya KUONGOZA!
Ni mda mrefu sana toka taifa hili mara ya mwisho liwe na KIONGOZI.
 
Wazee hivi mtu kama Rostam Aziz mtamuita mzawa? watu kama hawa ndo walouziwa haya makampuni na viwanda Rostam aliuziwa Kiwanda cha ngozi Mwanza (Tannaries) lakin alichukua mashine zote na kuuza vyuma chakavu na sasa ni ghala la kutunzia magreda yake ya kampuni ya Caspian, Mkapa asitudanganye. Kumbukeni sakata la Mount Meru Hotel Arusha ambalo mengi alipigwa zengwe na kuuziwa watu wengine toka cjui nje au viongozi wenyewe: au mgodi wa Kiwira waliojiuzia wenyewe akina Mkapa.

My take: Asikwepe damu ya umasikini wetu na watoto iko juu yake.
 
heshima yake inashuka kwako mkuu, kwa wengine anaheshimiwa..dont generalise

huyu mzee mlisema sana na kumtukana kila siku kipindi kile Kikwete is a 'saint' na rescue man

Kikwete mmeona ame adopt mbinu zile zile mmeanza kurudi kwa mkapa!! Ili hali hatujaona any remarkable change kutoka 2005 mpaka leo,

Mkapa anasema hivi ''Mkapa alitoa wito kwa watanzania kujituma kwa bidii kutafuata maendelea badala ya kuendelea kujadili masuala yasiyo na tija kwa maendeleo ya taifa''

Nadhani kama tungekuwa tunaipenda nchi yetu, tungejadili sana report ya CAG kuhusu matatizo ya ubinafsishaji na sio kufanya this issue as was a 'one man show'

Mkuu kufanya this issue 'one man show' haikwepeki kwa namna nchi yetu inavyoendeshwa na sheria zetu zinazofanya mkuu wa nchi kuwa 'one man show' lazima kwa nafasi yake awajibike kama mfano.amelalamikia uongozi uliokuwa ukisimamia ubinafsishaji utafikiri yeye aliyewateua hatakiwi kukiri uzembe wake yeye binafsi.

Sera ya ubinafsishaji si mbaya kama tungeweka sawa kwanza sheria zetu na kujua kiundani namna tutavyo faidika kama nchi.mfano mpaka leo benki ya NBC hawatengenezi faida na moja ya sababu ninayoiamini ni kitu kinachoitwa management fees! unakuta management fees pekee inakula billions of money mpaka inaumiza kichwa kwa mzalendo yeyote.

Mkapa tutamlaumu kwa kuuza tu mashirika bila kujua hao wageni watakuja kuokoa nini! Investor kuwa na mtaji haitoshi kumpa shirika,lazima tuwe na malengo na haya mashirika na mwekezaji lazima ajue tunataka kuelekea wapi.Swala la mwekezaji kutengeneza faida halina mjadala lakini lazima tuwe na sheria zinazoziba mianya ya wizi kimahesabu.Tatizo tunawapa tu wageni mashirika kama vile hatuyataki tena!

Swala la Watanzania kushindwa kuendesha mashirika waliyopewa nayo inatokana na system mbovu tu! Hata kama ingekuwa USA kwa loop hole zilizopo yangekuwa yale yale.Maendeleo ya shirika lolote ni uongozi bora unaotokana muongozo bora na usimamizi makini wa share holders.

Nature ya maendeleo yetu bado inategemea sana Rais aliyepo madarakani ndio maana tunaomba Katiba mpya ipunguze madaraka ya Rais ili kila mhimili wa dola ujisimamie na watawala watofautishe siasa na utendaji wa dola.
 
Mkapa, wacha kuimba nyimbo za wachawi zisizo na tija, kwani Nyerere alipata wapi mitaji ya kuanzisha viwanda ambavyo wewe na mafisadi wenzako mliuza na kugawana?Wewe na mtangulizi wako mlipo amua kuliua Azimio la Arusha na misingi ya kujitegemea na kuanza kutembeza bakuli kisha kukumbatia rushwa na ufisadi ndani ya lichama lenu CCM ndipo Tanganyika yetu ilipolaaniwa. Ulipokwenda Arumeru kueleza upumbavu wako wameru walikuonesha kwa vitendo kuwa hawapo tayari kuupokea ufisadi wako.
 
Mkapa alijitekenya, Akajichekesha Sasa analia , Mkapa bado unasema wapinzani nikokoto,sasa angalia uliwachokonoa wakakuchanavilvyo. Rudisha viwanda vyetu tupate ajira tuwe wasomi sio wabongo fleva!!
 
alivyoambiwa sera ya ubinafsishaji ime-prove failure amejibu eti asilimia kubwa ya viwanda na makampuni yalibinafishwa kwa wazawa ivyo yeye sio wa kulaumiwa.
Hivi mkapa anaakili kweli? kwani hata kama ni wazawa wameua viwanda je aliyewapa hivyo viwanda kwa sera ya ubinafsishaji ni nani kama sio yeye??

Ni matokeo ya ufisadi ambayo kiharakaharaka yeye BM ni miongoni wa waasisi wakuu

Kashifa kubwa zote dep gree, rada, ndege mbovu ya rais kwa bei kubwa ya hovyo, mgodi wa makaa kiwira, kagoda, Epa, uuzwaji wa nyumba za serkali (ni yeye Bm akishilikiana na akina yona, mramba, Balali na nk) uuzwaji wa mashirika ya umma kwa bei powa na ya kutupwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Aliyevaa viatu vyake na anapita humohumo. Hakika siku zinzkuja wote watalia na kusaga meno.
 
Wakatimwingine mambo mengine yanaudhi:



Mzee Mwanakijiji. You have been in US for too long. unatakiwa uje uangalie jinsi mambo yanavyokwenda huku Tanzania, kuna wakati naona mambo yalikuwa mazuri wakati wa mkoloni kuliko sasa. Watu wanaosema sera ya ubinafsishaji imeshindwa hawasemi ile iliyokuwepo iliweza nini. Na hawataki kusema uzembe, ujinga, ufujaji na uchafu mwingine uliokuwa unafanywa na wanaoongoza makampuni yaliyofilisika kwa kutumia fedha za umma. Kama kweli kiongozi unaakili timamu huwezi kuendesha kampuni kwa kusubsdize kila siku, kuna wakati ni lazima uangalie kama kampuni inaleta faida au haileti faida, then ufanye uamuzi unaweza kubadilisha hali.

Nakumbuka jamaa wa PSRC walikuwa wanaeleza vizuri sana na walikuwa wanatoa evidence nyingi sana kuhusu upuuzi uliokuwa unaendelea kwenye mashirika yaliyobinafsishwa.

Mkapa was not 100% correct, but for sure he was not wrong. Ningekuwa rais katika wakati wake ningefanya hivyo, mimi nadhani hata ikulu tunatakiwa kuibinafsisha as long as kuwe na njia nzuri ya kuwafanya wanaokuwa pale wanafanya tunachotaka wafanye

Naomba siku uje Tanzania, uliza utendaji wa kawaida wa kazi kwenye serikali, mashirika na idara mbalimbali. Huwezi kuona substantial amount of work zaidi ya kusikia ufisadi, ufuska, vitisho, ushirikina, majungu, siasa. Kazi hakuna kabisa, kama kweli una akili timamu nadhani mazingira hayo yanakufanya uchukue uamuzi, ukikaa kimya unakuwa mpumbavu zaidi kuliko kuchukua uamuzi mzuri wenye dosari.

If i was president i would do the same. Namlaani Mkapa kwa kuitelekeza nchi alipoona kipindi chake kinaisha, akabariki EPA na wizi mwingi wa fedha za umma. Alitudanganya kuwa atapinga rushwa, taendesha utawala kwa uwazi, lakini alifanya kinyume.

Kuna mengi machafu alimfanyia Jenerali, i wish wanaojua wanweza kuyasema zaidi. nadhani alidhani kuwa he would be president forever.

JK alichukua nchi ambayo uchumi wake ni stable na promising, thanks to utendaji mzuri wa serikali ya Ben. Angalia kazi ya serikali ya sasa kama sio malalamiko zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Ni matokeo ya ufisadi ambayo kiharakaharaka yeye BM ni miongoni wa waasisi wakuu

Kashifa kubwa zote dep gree, rada, ndege mbovu ya rais kwa bei kubwa ya hovyo, mgodi wa makaa kiwira, kagoda, Epa, uuzwaji wa nyumba za serkali (ni yeye Bm akishilikiana na akina yona, mramba, Balali na nk) uuzwaji wa mashirika ya umma kwa bei powa na ya kutupwa kwa ndugu, jamaa na marafiki.

Aliyevaa viatu vyake na anapita humohumo. Hakika siku zinzkuja wote watalia na kusaga meno.


Yoooooooooooooooooooote tisa lakini kwa hili la kuuza nyumba za serikali basi hapo hatutasamehe na naaamini kuna siku nyumba zote hizo zitarudi mikononi mwa wanainchi ndani ya serikali inayowajibika kwao wanainchi, Naamini historia kamwe haifutiki na pia hujirudia kwa namna nyingine, Watanzania tuombeane uhai tu.
 
Bht Hakika! na hii ni nje ya ushabiki kabisa ... maana mimi niliangalia hata body language response yake baada ya "kuguswa" na watu wakawa kama wamemcheka kidigo ... Loo alionekana kama kituko kidogo aliruka juu na kama kiti nicha moto alafu akakaa chini... ...!! sidhani kweli yuko totally ok!! Lakini ndio hivyo bahati mbaya ..Mwenzio ana kinga ya kurushwa mahakamani!!

Hakika kwa mtu ambae alipata kuwa Rais mwenye aina ya ubabe wake hakika syle ile ya kuchekwa na yeye kudhili kuwa kachekwa kiasi cha kutengeneza self defense mechanism mpaka kwenye lugha ya mwili.Ni as if isingekuwa Public basi angesimama kukoloma mbele.Ingekuwa ni mkutano ndani ya boardroom hakika angekoloma kwa jambo ambalo tayari limeshabomoka.

Ishara yake ya mwili pia kwa watu makini ni ishara ya kuwa mambo si shwari,watu makini mmoja akikutalia jambo ina maana sana kuliko watu wa kawaida mia kukubalia jambo hilo hilo.Hivyo katika mkusanyiko huo wa kigoda cha Mwalimu imekua ishara ya kuwa watu makini baadhi wamemwabia HAPANA ULISHINDWA.Aijalishi watanzania mamilioni wa kawaida baadhi kusema alifanikiwa katika kuinua uchumi bali watu makini wamempa za USO kuwa ALISHINDWA na chanzo cha TAIFA kuwa hapa lilipo ni bidii zake YEYE.Na pro Shivji kitaaluma nae akapigilia msumali kuwa KUFUNGUA MILANGO PASIPO MASHARTI NDIO CHANZO CHA KUSHINDWA.Pro Shivji anaonekana anamkubali ilikuwa sawa iyo option ya kuibinafsisha na uwekezaji lakini pasipo masharti na miiko, basi ndio matokeo yake haya leo.
 
Mambo yameenda mrama lazima awe mkali. Isipokuwa anajua kwanini watu wanamlaumu kwa sera zake za ubinafsishaji. Mkapa alichemka. Viwanda karibu vyote vimekufa na wahindi waliovinunua wamegeuza ni magodown.
 
Mkapa kajenga barabara,kadhibiti mfumuko wa bei,karudisha nidhamu ya matumizi ya fedha,huyu dugu yetu j.k. Kafanya nini?
 
Labda mkuu bado hujaelewa maana ya kubinafsisha.
Kubinafsisha inamaanisha serikali siyo majority owner!
Serikali ikiwa na 51%, ujue hilo ni shirika la umma. Tatizo ni kuwa, WB na IMF ndiyo waliotupa masharti ili tupate mikopo na kufutiwa mikopo ya zamani.
Kwa ujinga wetu, tukakubali, as if that will make us rich.
Sasa niambie, unaionaje balance of payments?..
Tunadaiwa dola bilioni 10 i.e 50% of all the money and properties we own is not ours!! na inazidi kuongezeka.
Tuna fedha chache zaidi ya tulizokuwa nazo 1991.
Kisa, ubinafsishaji.. yes, I said it ubinafsishaji.
Unajua mkuu, kutafuta Capital kwa kuwashirikisha watu binafsi ni kitu cha kawaida sana!! as long as we have the majority ownership (i.e we can decide to go on by ourselves once things get better).

Mpendwa Kobello, do you real know your country?

Kindly read this excerpt below and point out where does your claims fit



"Agriculture is the primary
economic activity of Tanzania, which provides employment to 80 percent people in the country. Sixty percent GDP is contributed through agriculture in Tanzania economy. Three fourths of foreign exchange in is earned through agricultural activities. The country grows both food crops as well as cash crops. Food crops in Tanzania include rice, wheat, potatoes, sorghum, maize, beans and cassava. Among the vital cash crops of Tanzania are coffee, tea, tobacco, cashew nuts, cloves, sisal, groundnuts, cardamoms, palm oil seeds and many more.

Fishing is also an important economic activity of Tanzania. Both marine as well as fresh water fish are available in plenty in the various islands and lakes of Tanzania. As fish is a perishable commodity, it is exported to the nearby areas and countries. Livestock population in Tanzania is great, but due to lack of packaging and preserving industries, export of animal products has become difficult in the country. Mining has become a popular and profitable industry in Tanzania earning huge foreign exchange.

Last but not the least, tourism, transport and communication and several small scale industries are playing an important part in boosting the economy of Tanzania"

source: Tanzania Economy


Your claims are nullified by that excerpt above...it is not privatisation that have caused our economy to be as it is today!! if you have that thought please make u-turn to face reality!

do I need to say more??
 
Mkapa defends privatisation, blames bad management
Saturday, 14 April 2012 10:35



By Frank Kimboy

The Citizen Reporter

Dar es Salaam. Former President Benjamin Mkapa put up a spirited defence for the decision of his third phase administration to privatise state firms, at a public forum held in Dar es Salaam yesterday.

He told participants at the fourth Mwalimu Nyerere Professorial chair that the poor performance of the firms was due to bad management, in reaction to accusations directed at him personally from some participants.Mr Mkapa said during his time in office when he decided to adopt the privatisation, some 386 state owned industries were privatised, 180 of which were sold to locals.

According to Mr Mkapa, all the 386 companies have since collapsed due to what he termed as bad management.

"For one to invest, one needs to have three components, namely: capital, market and management and all of them work hand in hand…but sadly most of the privatised firms lacked the third component," said Mr Mkapa.
Mr Mkapa, who was the guest of honour during the closure of the two-day event, said there was enough evidence that the privatisation succeeded in various firms which had good management.

He cited sugar production, which had doubled under the private sector compared to when the state was running the sugar production factories. "You are blaming me for endorsing privatisation but tell me how many industries have been built since 2005?" posed Mr Mkapa.

The former president also said that there is a bright sign that Africa will become a world economic powerhouse. However, Mr Mkapa said there were some conditions for the country to achieve that. He named some of the conditions as proper utilisation of resources and integration.

One of those who faulted the retired president was Dr Ng'wanza Kamata, who said that the western countries had used the policy to exploit Africa's resources for the benefit of their countries while majority of Tanzanians had been living in extreme poverty.

"Due to their problems in Europe, European countries have used the privatisation policy as a loophole to stabilise their countries which have been hit hard by economic crisis," he said.

For his part, Prof Issa Shivji accused the country of ‘not strategically privatising its firms'. For instance, Prof Shivji said the government was wrong to privatise important sectors like banks and the insurance sector.
He said although China and other countries adopted the policy, they did so strategically by ensuring that important sectors remained under state control.

Mr Jenerali Ulimwengu said for Tanzania to succeed economically, the only weapon is for the government to turn back to its people. "You should turn back to wananchi and start a dialogue on how the country's resources could be exploited for the public interest openly and transparently.

Mr Ulimwengu said it is a saddenning reality that most wananchi, notably the youth, have lost faith in the government and even in their own lives.

"I am always asking myself where has people's faith, which I used to experience during the Mwalimu era, gone and I think the government should do the same before people's patience runs out," the distinguished political commentator said.

Source: Citizen Mkapa defends privatisation, blames bad management



There was no 'war' as some of you want us to believe...this is just a normal challenge and as I said out 'he is a man' to attend that conference!


shivji-mkapa.jpg
 
Mkuu kufanya this issue 'one man show' haikwepeki kwa namna nchi yetu inavyoendeshwa na sheria zetu zinazofanya mkuu wa nchi kuwa 'one man show' lazima kwa nafasi yake awajibike kama mfano.amelalamikia uongozi uliokuwa ukisimamia ubinafsishaji utafikiri yeye aliyewateua hatakiwi kukiri uzembe wake yeye binafsi.

Sera ya ubinafsishaji si mbaya kama tungeweka sawa kwanza sheria zetu na kujua kiundani namna tutavyo faidika kama nchi.mfano mpaka leo benki ya NBC hawatengenezi faida na moja ya sababu ninayoiamini ni kitu kinachoitwa management fees! unakuta management fees pekee inakula billions of money mpaka inaumiza kichwa kwa mzalendo yeyote.

Mkapa tutamlaumu kwa kuuza tu mashirika bila kujua hao wageni watakuja kuokoa nini! Investor kuwa na mtaji haitoshi kumpa shirika,lazima tuwe na malengo na haya mashirika na mwekezaji lazima ajue tunataka kuelekea wapi.Swala la mwekezaji kutengeneza faida halina mjadala lakini lazima tuwe na sheria zinazoziba mianya ya wizi kimahesabu.Tatizo tunawapa tu wageni mashirika kama vile hatuyataki tena!

Swala la Watanzania kushindwa kuendesha mashirika waliyopewa nayo inatokana na system mbovu tu! Hata kama ingekuwa USA kwa loop hole zilizopo yangekuwa yale yale.Maendeleo ya shirika lolote ni uongozi bora unaotokana muongozo bora na usimamizi makini wa share holders.

Nature ya maendeleo yetu bado inategemea sana Rais aliyepo madarakani ndio maana tunaomba Katiba mpya ipunguze madaraka ya Rais ili kila mhimili wa dola ujisimamie na watawala watofautishe siasa na utendaji wa dola.

Mkuu naona umeeleza vizuri. Tanzania ikiwa na rais mzuri nchi inaenda vizuri ikiwa na rais ovyo nchi inaenda ovyo. Hili ni moja ya matatizo makubwa yanayoikumba Tanzania, sheria na taratbu hazipo, kilichopo ni utashi wa aliye madarakani. same applies kwenye ubunge, uwaziri, ukatibu mkuu etc etc

Issue ya ubinafsishaji inatakiwa kuangaliwa kwa akili zaidi, na sio kisiasa na kiushabiki. Kwa mzaingirayaliyopo Tanzania i still believe that is the way, lakini bado hatujaweka sera na sheria nzuri za nchi kunufaika kutokana na ubinafsishaji ule. for sure kwa sasa tuna revenue nyingi kiasi kutoka sekta binafsi, kama kila kitu kingeendelea kuwa state owned hayo yasingekuwepo.

Nawaomba wanaJF tuwe wakweli na hali ilivyo kwenye serikali yetu, tuseme kama kweli kazi inafanyika au kama ni porojo tu na uswahili, kwenye mashirka ilikuwa worse. wafanaykazi walikuwa wajomba, shangazi, watoto wa nje etc etc, director babu, what do you expect.

Kuna siku nilisikitika sana jamaa mmoja mkurugenzi alitembea na wanawake karibu wote kwenye kampuni, na alikuwa anajidai, kila ki-opportunity cha vijisenti kikija basi anakitumia hicho hicho, hakuna lolote la maana alilokuwa anafikiri zaidi ya hayo, pesa za shirika yeye ndio mhasibu, yeye mwenyewe ndio chief administrator, kila kitu yeye. Angekuwa mwenye vision na akili shirika lingekuwa mbali sana, lakini matokeo yake shirika likapiga magoti. Mashirika kama haya ni bora kuyabinafsisha tu kuliko kuteketeza pesa za walipa kodi. Mkapa was damn right.
 
wanaJF ktk kosa kubwa alilolifanya Mkapa ni hilo la ubinafsishaji

ni kwamba hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na viwanda vyake hiyo haipo,serikali ilitakiwa imiliki viuwanda hivyo hata ingekuwa kwa kushare hisa na wawekezaji,kuliko kuviuza

nawaambieni kuwa hata china sera hiyo ilifika,lakini wenzetu walikuwa ni waelewa walichokifanya ni kutenga maeneo ya uwekezaji na si kuuza viwanda kama alivyofanya mkapa,china ilishirikiana na wawekezaji,serikali ikamiliki share na ikawa ndio inasimamia kila kitu,lakini Mkapa alichokifanya ni kuuza viwanda pasi hata serikali kumiliki share,tena aliviuza kwa bei chee sana na wawekezaji waliowengi walikuwa wanahitaji ardhi tu,walichokifanya ni kufuga nguruwe na mbuzi ktk maghala ya viwanda hivyo

Jamani,
viongozi wa china walichokifanya ni ku identify maeneo ya uwekezaji,wakajenga viwanda GUADONG wakawaita wawekezaji,wakawapa mashariti yao na nini wanataka,mwisho wa siku serikali ikajihusisha ktk umilikaji wa viawanda hivyo kwa kuchukua share kwa sasa viwanda vote vimafanya kazi na nchi hiyoo inapaa kiuchumi


mkapa alichemka tena sana,KUUZA VIWANDA
hata hicho anacho kisema cha kilombero ni kwakuwa kuna wakuu wanamiliki baadhi ya hisa,hawakutaka kukimaliza
 
Wakatimwingine mambo mengine yanaudhi:



Inawezekanaje Mkapa anasema "..... Kama waliobinafsishiwa nao waliendelea kufanya utumbo ule ule, hilo halinihusu." Natamani mtu amwambie usoni kuwa huo utumbo ulioendelezwa ndio haswa tunataka awajibike kwao. Haiwezekani Mkapa aliyeuza mashirika yote, na sasa yamegeuzwa maghala ya kuuzia bidhaa za wachina na wahindi aendelee kutuhadaa na kujisafisha bila kuwajibika. Tanzania ina utajiri mkubwa wa rasilimali, alifanya nini kuinua uchumi wa nchi zaidi ya kuuza rasilimali zetu kwa bei ya kutupa na kununua cheni na vito vya thamani kama shalobalo!?????

Shame on him.
 
Last edited by a moderator:
Mkapa kajenga barabara,kadhibiti mfumuko wa bei,karudisha nidhamu ya matumizi ya fedha,huyu dugu yetu j.k. Kafanya nini?

Jk hanalolote zaidi ya ngojera na ahadi nyingi zisizotekelezeka
-Atajenga reli kutoka dar hadi mwanza
-Maisha bora kwa kila mtz- ndo ugumu wa maisha unaongezeka geometrically (Ugumu to power miaka)
-Ataboresha afya ndo ovyo kabisa
-Atasimamia uchumi kwa maslahi ya watz- yeye anasimamia uchumi bora kwa mafisadi na kaka Riz
-Ataongeza ajira kwa wazalendo - yeye anongeza kwa warembo kama vile benki kuu akina vick kamata
-Atasimamia elimu bora- sasa imekuwa bora elimu watoto wanafauru hawajui kusoma wala kuandika sijui wanafauru vipi?
-Atanunua meli kubwa za kisasa kwa ziwa victoria, ziwa nyasa na ziwa Tanganyika-Usanii maana serikali kwa sasa hohehahe (haina fedha hata mishahara inakopa)

Kwa hakika katika marais wangu wote wa awamu zote huyu hatuna la kujivunia, watawala wamegeuza shamba la bibi kodi zetu, wanyama wetu, ardhi yetu, madini yetu nk kila kitu wanagawana na Jakaya mrisho Kikwete yupo anatazama.
 
Back
Top Bottom