Mkapa anakana vipi matokeo ya Sera yake iliyoshindwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa anakana vipi matokeo ya Sera yake iliyoshindwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 13, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wakatimwingine mambo mengine yanaudhi:

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kabla ya kadhia ya Arumeru watu wangemsikiliza bila kuguna, lakini Arumeru imemuondelea Mkapa heshma, he will never be the same!
   
 3. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,800
  Likes Received: 17,885
  Trophy Points: 280
  M.M.M ni mtu wa data nzito nzito, sasa ukiona kashindwa kuongea badala yake kaweka picha ujue anayehusika ni kama kajipaka mavi
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Hivi Mwanakijiji bado unadhani Mkapa kuna akili iliyosalia kichwani mwake? watu wengi wanashindwa kuelewa ni kwa nini Mkapa alikwenda Arumeru, wengi wanadhani alikwenda kumfanyia kampeni Sioyi lakini si kweli, ukweli Mkapa alitaka kulitumia jukwaa la Arumeru kujisafisha na tuhuma nyingi anazotuhumiwa nazo lakini bahati mbaya akaharibu hata kabla hajaanza alilokusudia. na bado mtasikia upuuzi mwingi tu kutoka kwa huyu Muuwaji, damu ya Baba wa Taifa haitamuwacha salama.
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ulikuwa wakati muafaka kuwepo pale ili ajimalize nakujifungasha .... !! Honestly if he was that smart asingehudhuria lile Kongamano! Ni aibu tupu!!! ...Sasa what is he talking!!!?
   
 6. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Tangu nilipojua kuwa alitumia madaraka yake kujunifahisha yeye na familia yake (ANBEM) na kutumia ofisi ya umma kwa biashara zake binafsi bila kulipa kodi ya pango, imani yangu kwake iliisha kabisa.
   
 7. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Akamatwe mara mojaa
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,892
  Trophy Points: 280
  alivyoambiwa sera ya ubinafsishaji ime-prove failure amejibu eti asilimia kubwa ya viwanda na makampuni yalibinafishwa kwa wazawa ivyo yeye sio wa kulaumiwa.
  Hivi mkapa anaakili kweli? kwani hata kama ni wazawa wameua viwanda je aliyewapa hivyo viwanda kwa sera ya ubinafsishaji ni nani kama sio yeye??
   
 9. M

  Mlyafinono Senior Member

  #9
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eti ansema alianzisha sera ya ubinafsishaji wa viwanda kwasababu tatizo lilikuwa usimamizi mbovu (poor management) hasa kama tatizo ni hilo mbona yeye pia alishindwa kusimamia sera ya ubinafsishaji aliyoanzisha.ni upuuzi mtupu
   
 10. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Na ninafikiri waandaji wa Kongamano they had that in mind ...!! Sasa walitaka aje na hoja ipandishwe mezani wamsikilize akibwabwaji!! Na ...ndicho anachokifanya!!
   
 11. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kimsingi nchi hii inekuwa fukara kutokana na sera ya ubinafsishaji iliyosimamiwa na huyu mzee!
   
 12. dallazz

  dallazz Senior Member

  #12
  Apr 13, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mkapa ni janga kuwahi kutokea ktk taifa hili
   
 13. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Na hakikia analakujibu juu ya yote hayo!!! ILA anakinga ya kutinga mahakamani???!! So sad!!!
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mkapa awa mbogo [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 13 April 2012 21:40 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa

  NI BAADA YA WASOMI KUMKOSOA KWA SERA ZAKE ZA UBINAFSISHAJI, AWAJIA JUU, AHOJI TANGU 2005 KUNA KIWANDA KIPYA?
  Waandishi Wetu
  RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kubanwa na wasomi waliokosoa hadharani sera zake za ubinafsishaji kwa maelezo kwamba hazijaonesha mafanikio, badala yake zimechangia kudorora kwa uchumi wa nchi.Sakata la Mkapa na wasomi hao lilibuka jana katika Kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuibua msisimko wa aina yake kwa watu waliohudhuria.

  Katika mjadala huo uliochukua takribani saa mbili, washiriki hao wengi wao wakiwa wasomi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), walihoji sababu za Rais huyo mstaafu kupigia debe sera zake za uwekezaji kwamba zingekuwa suluhisho lakini hadi sasa hali ya uchumi wan chi imezidi kudorora.

  Hata hivyo, Mkapa alipinga vikali hoja za wasomi hao na kuwahoji akitaka wamtajie, tangu mwaka 2005 alipoondoka madarakani, ni viwanda vingapi vipya vimejengwa?
  'Mnanilaumu kwa sera ya ubinafsishaji lakini niambieni viwanda vingapi vipya vimejengwa tangu mwaka 2005?" Alihoji Mkapa ambaye aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

  Mkapa alitetea sera za ubinafsishaji na kueleza kwamba kimsingi hazikushindwa lakini zimeonekana kuwa na kasoro kwenye utekelezaji wake kutokana na matatizo ya uongozi na kwamba aliamua kubinafsisha baadhi ya vitega uchumi kwani vilifilisika.
  "Ili uendesha kiwanda unahitaji mitaji, uongozi bora na soko pamoja na ujuzi, sisi tulibinafisha baada ya kukosa mitaji na uwezo wa kuviendesha, tulishindwa kuviendesha, tulikuwa na viwanda vitano vya nguo… vyote vilikwenda hovyo hovyo,"alisema Mkapa.
  Aliilaumu mamlaka iliyohusika na uwekezaji wakati wa utawala wake, kwa kile alichodai, kushindwa kuueleza umma ukweli uliosababisha Serikali yake kuchukua uamuzi wa kubinafisha mashirika na viwanda mbalimbali.

  "Tulibinafsisha mashirika na viwanda 330, kati yake 180 walikabidhiwa Watanzania na 23 wageni, vilivyobaki vilimilikiwa kwa ubia kati ya Watanzania na wageni, kwanini watu hawahoji sababu za hata wenyeji kushindwa kuviendeleza? Twende tufanye utafiti tupate sababu za kushindwa,"alisizitiza Mkapa.

  Aliongeza kuwa mbali ya kuwapo matatizo katika sekta ya uchumi wa nchi, baadhi ya viwanda vilivyobinafisishwa vinafanya vizuri huku akitolea mfano kile cha Sukari cha Kilombero mkoani Morogoro.

  Mkapa alitoa wito kwa watanzania kujituma kwa bidii kutafuata maendelea badala ya kuendelea kujadili masuala yasiyo na tija kwa maendeleo ya taifa.
  Akizungumza kwenye mjadala huo, Profesa Issa Shivji, alisema ubinafsishaji uliofanywa nchini uliuza njia kuu za uchumi zikiwemo benki na Shirika la Bima na kuifanya Serikali kushindwa kusimamia na kulinda uchumi wa nchi.

  Shivji alitofautiana na mtazamo wa Mkapa aliyedai kuwa ubinafishaji ulifanywa kwenye viwanda vilivyoshindwa kujiendesha kwa kukosa mitaji akisema:

  "Viwanda tulivyobinafisha ni vile vilivyokuwa vinatoa faida, tatizo tulilofanya tulibinafisha njia kuu zote za uchumi hali iliyosababisha Serikali kushindwa kusimamia uchumi wa nchi."

  Msomi huyo alibainisha kuwa hata nchi zilizoendelea, ikiwamo China, ziko kwenye ubinafishaji lakini zinatenga maeneo ya kubinafisha.
  Kwa upande wake Dk Ng'wanza Kamata ambaye ndiye aliyechokoza mada katika mdahalo huo, alihoji kama Afrika inaweza kutimiza ndoto ya kuwa kitovu cha uchumi duniani kwa kutumia sera na mfumo uliopo ambao unatoka mataifa ya Ulaya.

  "Katika hotuba yako uliyoitoa Afrika ya Kusini umesema Afrika inaweza kuwa kitovu cha uchumi wa dunia kutokana na wingi wa raslimali zilipo, je ni kweli tunaweza kufika huko kwa kutumia mifumo na sera zilizopo? Alihoji Dk Kamata na kuongeza:

  "Wazungu wanajua kuwa Afrika ina utajiri wa rasilimali tangu mkutano wa Berlin".
  Dk Kamata alisema mfumo wa utandawazi unaonekana kama umejileta wenyewe ambao ndani yake watu wa Ulaya wanatafuta mahali pa kupeleka mitaji yao ili waweze kupata faida.

  "Zipo kampuni 600 zinazoshika uchumi wa dunia, lengo lao siyo kusadia wananchi katika nchi husika bali kutengeneza faida kwa maslahi yao,"alisema.

  Kuhusu udhaifu wa Serikali wadau hao walisema mikakati mingi ya maendeleo inashindwa kutekelezeka kutokana na tatizo la viongozi kutowashirikisha wananchi katika kuandaa miradi ya maendeleo.

  "Kama viongozi serikalini wangewashirikisha wananchi katika kujadili miradi ya maendeleo mikakati mingi ingefanikiwa,"alisema Maselina Charles kutoka Morogoro.

  Historia ya ubinafsishaji
  Ubinafsishaji wa Mashirika ya umma hapa nchini ulianza tangu mwaka 1993 na ulikuwa unaratibiwa na Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) iliyopewa mamlaka ya kusimamia
  na kuongoza shughuli zote za ubinafsishaji.

  Hata hivyo shughuli za tume hiyo zilisitishwa Desemba 2007 baada ya kukamilisha ubinafsishaji wa mashirika mengi ambayo yalikuwa yametengwa.

  Mashirika ya Umma 34 ambayo yalikuwa kwenye hatua za ubinafsishwaji yalihamishiwa katika Shirika Hodhi la Mali za Makampuni yaliyobinafsishwa kutoka PSRC kuanzia kuanzia Januari 2008.

  Januari 2008 Shirika Hodhi la Mali za
  Makampuni Yaliyobinafsishwa lilipewa majukumu ya kuendesha shughuli za kampuni zilizokuwa kwenye makakati wa kubinafsishwa.

  Matatizo kwenye Ubinafsishaji
  Kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (SAG)mashirika yaliyotengwa kawa ajili ya kubinafsishwa, yalikuwa yamezuiwa kupanuka zaidi kwa sababu hayawezi kuandaa na kutekeleza mipango mikakati au kuwekeza.

  Pia wafanyakazi wa mashirika hayo wanakuwa hawana morali wa kufanya kazi au kutimiza wajibu wao kwa sababu ya kutokujua hatima ya ajira yao na ya mwajiri wao.

  Uchakavu wa mali na raslimali za mashirika yaliyotengwa unakuwa ni wa kiasi cha juu kutokana na kukosa fedha kwa ajili ya ukarabati au urudishwaji wa mali zilizoharibika unakuwa mgumu.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 15. bht

  bht JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  AJ mie nilishtuka kumuona na nikafikiria hivyo hivyo kuwa nini kimempa ujasiri kwenda na kuzungumza upuuzi qake tena pale?

  Wakati mwingine nashawishika kuamini Mkapa kuna kitu hakiko sawa kumkichwa!
   
 16. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Bht Hakika! na hii ni nje ya ushabiki kabisa ... maana mimi niliangalia hata body language response yake baada ya "kuguswa" na watu wakawa kama wamemcheka kidigo ... Loo alionekana kama kituko kidogo aliruka juu na kama kiti nicha moto alafu akakaa chini... ...!! sidhani kweli yuko totally ok!! Lakini ndio hivyo bahati mbaya ..Mwenzio ana kinga ya kurushwa mahakamani!!
   
 17. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimesikitika sana kauli ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa......Tatizo anaogopa kula matapishi yake lakini ukweli uko wazi. Nchi hii umasikini uko siku nyingi. Ila matatizo haya leo kuhusu ubinafsishaji yametokana na kipindi cha Urais wa Mkapa hilo hawezi kataa ukweli ndio huo. Rada, Ndege ya Rais, Uuzwaji NBC na mambo mengine mengi hata ubinafsishaji migodi.

  Napenda kumueleza Mkapa Tanzania ya leo si ya miaka 10 iliyopita HAPA NI UKWELI NA UWAZI tatizo lake ubabe ulizidi sana kipindi hicho sasa yana mrudia mwenyewe.
   
 18. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Sera ya ubinafsishaji haikutokana na akili na mipango ya Mkapa na CCM yake, bali ujinga, umaskini na maradhi yaliyokuwa yametamalaki ndani ya watunga sera na wataalamu walioshindwa wakitanzania ambao kama choo cha shimo walipokea kila kitu kutoka kwa world bank, IMF, EU na wanaojiita wawekezaji. Nawashangaa sana wasomi uchwara waliokuwa wanamshauri ati leo wanamruka! hata akina S.Sita na Abdala Kigoda wapo kimya!
   
 19. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Kumbe hakukuwa na jasiri wa kumwambia toka Mwanzo ila Vincent alimchana Live angalau na sie tunapandia hapa hapa CDM kiboko yao
   
 20. Machiavelli

  Machiavelli Member

  #20
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kweli wadanganyika ni wavivu wa kufikiri. Hivi tijiulize mashirika mangapi ya umma yame kuwa privatised to foreigners? 80-90% wamepewa wazalendo who had selfish motives. THEY WANTED THE REAL ESTATE NOTHING ELSE. Sasa kama we have to personalize the issue lets bring the facts to the table and do the analysis. No research no right to speak should apply to this subject. Ndio maana TZ hatuendelei we cling to the past. We are a nation of WHINERS WITH NO ONE READY TO STEP UP.
   
Loading...