Inaonekana kuna watu wanataka kumpaka raisi wetu mkapa matope bure kwa sababu za kisiasa. Mkapa kaifanyia mengi Tanzania, kainua uchumi wa Tanzania, kajenga barabara na mengine mengi.
Watu wasiompenda hasahasa wapinzani ndio wanampaka matope tu bila sababu yoyote. Kiwira sio ya Mkapa, wenye uthibitisho walete na sio kupakana matope tu bila sababu.
Wanaccm acheni Mkapa ajitetee mwenyewe, yeye ni fisadi tu pamoja na hayo unayosema ya kuinua uchumi hayana ushahidi. Kama unao uweke hapa.
Wanaccm acheni Mkapa ajitetee mwenyewe, yeye ni fisadi tu pamoja na hayo unayosema ya kuinua uchumi hayana ushahidi. Kama unao uweke hapa.
tatizo lako ni kwamba mtu hawezi kutoa hoja hadi awe ccm ! wewe kama mgaya una ushahidi gani kwamba mkapa kafanya ufisadi ? ulikuwa nae ? au ndio unafuata mkumbo ??
mwambie huyo, haya yote wanayoweka hapa ni ya uongo. hakuna kilichofanyika ila wivu wa wapinzani tu wanawaonea viongozi wa ccm.
yaani wapinzani kusema mabaya ya Mkapa ni wivu? kweli fisadi hana aibu
wivu tu na hakuna ushahidi wowote mlio nao hapa.
Inaonekana kuna watu wanataka kumpaka raisi wetu mkapa matope bure kwa sababu za kisiasa. Mkapa kaifanyia mengi Tanzania, kainua uchumi wa Tanzania, kajenga barabara na mengine mengi.
Watu wasiompenda hasahasa wapinzani ndio wanampaka matope tu bila sababu yoyote. Kiwira sio ya Mkapa, wenye uthibitisho walete na sio kupakana matope tu bila sababu.
Kwahiyo licha ya hao waendeshaji wa Kiwira kusema Mkapa aliziuza hisa zake bado huamini alikuwa anafanya biashara akiwa Ikulu?
Mkapa alifanya biashara kama mjasiriamali yoyote yule, hakuna tatizo na hilo jamani.
--------------------------------------------------------------------------------------
Najua watu mpaka waone neno Mkapa ndiyo wanachangia, tukihoji sera wanaingia mitini. Inaweza kuwa sababu siyo ya msingi kwako ila kwangu ni ya msingi.naona sana mmeanza kujaza forum kwa threads zisizo na msingi. Naona mmepania leo.
Najua watu mpaka waone neno Mkapa ndiyo wanachangia, tukihoji sera wanaingia mitini. Inaweza kuwa sababu siyo ya msingi kwako ila kwangu ni ya msingi.
mjasiriamali gani bwana wewe!!!! Huo mshahara mnono na marupurupu manono aliyokuwa analipwa na Watanzania havikumtosha mpaka awafisadi wale waliomchagua? Huko Ikulu alikuwa anafanya biashara gani? Ndani, nje ya nchi au vyote? Mafisadi na wale waliofaidika na ufisadi sasa wanagwaya kijasho chembamba kinawatoka!!!
wape wape vidonge vyao, watakimbia forum hao, na muda si mrefu nitaleta thread zaidi za ccm.
Its pay back time.
haya bwana naona mmejaa hapa na nimeelemewa. Hata kama mnalipwa pesa bado tutambana nanyi tu. Mmeshinda kwa leo.