Mkao huu umenikumbusha mbali; | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkao huu umenikumbusha mbali;

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jun 30, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,279
  Likes Received: 5,638
  Trophy Points: 280
  [h=3]NIMEUKUMBUKA MKAO HUU:- KUKAA PAMOJA FAMILIA NZIMA KWA KUJUMUIKA KULA!![/h]

  [​IMG]Picha hii imenikumbusha enzi zile miaka arobaini na saba familia nzima inajumuika pamoja na kushika chakula iwe cha asubuhi, mchana au jioni. Hakika hii ilikuwa safi sana. Ila hapa naona watatu wanatumia vijiko na mmoja anatumia mkono... Halafu unajua kitu kimoja ukishazoea kula chakula mkiwa wengi huwa kinanoga sana kuliko kula peke yako...je wewe nawe umekumbuka nin? IJUMAA
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,279
  Likes Received: 5,638
  Trophy Points: 280
  [h=3]NDOA YA MALAIKA HAIJAWAHI KUWEPO DUNIANI!!![/h]

  Kama kawaida leo ni jumatano ambayo ni siku ya kile KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO haya karibuni tujumuike nami!!!!!


  [​IMG]  Wakati mwingine misukosuko ya ndoa huwaliza wanawake,


  lakini hizo zote ni changamoto !​


  Kuna kudanganyana kwingi kuhusu ndoa pale mtu anaposhindwa kuwa mwangalifu sana kwa kauli za wengine walio kwenye ndoa. Hii hutokana na ukweli kwamba kuna kujumuisha kwingi sana. Kuna wakati huwa tunasikia au kuambiwa kwamba ndoa ni sawa na jehenamu. Baadhi ya watu walio kwenye ndoa kuna wakati huzungumza kwa njia ambayo hutufanya tuamini kwamba kuoa au kuolewa ni jinai.

  Ndoa ni ujinga mtupu haina maana, mtu anaweza kusema. Wasemaji hawa wanaweza kuwa ni watu tunaowaamini sana kama wazazi wetu na wengine wa aina hiyo.

  Baadhi ya watu badala ya kuponda na kubeza kuizungumzia kama kitu kizuri sana kisicho na doa wala chembe ya usumbufu. Inawezekena kabisa nasi tukawaamini wazungumzaji hao, hivyo kuamini kwamba, ndoa hazina usumbufu.

  Inawezekana dhana hii ikaingizwa vichwani mwetu wakati tukiwa wadogo au hata tukiwa watu wazima. Hebu fikiria juu ya mtu ambaye anajisifu kwamba ndoa yake haina hata chembe ya mkwaruzo. Ambaye anaieleza ndoa yake kwa njia yenye kushawishi kuwa, kumbe ndoa zenye matatizo siyo ndoa bali kisirani kitupu.

  Kama nawe uko kwenye ndoa na ndoa hiyo ina matatizo hata madogo unaweza kudhani kwamba ulikosa kuoana na huyo mwenzako. Dhana hiyoinaweza kuchipuka kutokana na kauli kama hiyo inayoelezea ndoa kama kitu kisicho na mikwaruzo hata kidogo.

  Kama usipokuwa mwangalifu unaweza kuacha kuchukua hatua za kujaribu kuondoa tofauti zilizo kwenye ndoa yenu. Utaacha kufanya hivyo kwa sababu mtu fulani atakuwa tayari ameingiza kichwani mwako uongo kwamba ndoa ni "asali" na "maziwa" matupu. Ni uongo kwa sababu hakuna ndoa isiyo na mikwaruzo.

  Tunatakiwa kujua kwamba lengo la ndoa siyo kuepuka kukorofishana , hapana . Ukweli ni kwamba kukorofishana kunapotumiwa vema huweza kujenga uhusiano mzuri na imara sana. Kwa sababu kukorofishana hakuwezi kuepukika kwenye ndoa kunatakiwa kutumika kama shule na dawa ya kuimarisha ndoa.

  Bila kukwaruzana kwenye ndoa zetu inaweza ikawa vigumu sana kwetu kubandua tabaka la uongo lililotufunika ambalo humfanya kila mmoja kati yetu kushindwa kuona na kumfahamu mwenzake katika tabia yake halisi.

  Bila kukwaruzana, kila mmoja wetu atajidanganya kwamba anamfahamu mwenzake kama alivyo wakati siyo kweli. Tunapokwaruzana tunapata nafasi ya kufahamiana vizuri katika hali halisi.

  Mwanamke mmoja maarufu aliwahi kuulizwa kama huwa anakwaruzana na mumewe. Alikiri kwamba huwa wanakwaruzana kwa kusema , "ndiyo tunakwaruzana, vinginevyo tungekuwa hatuna tofauti, na hapo bila shaka ndoa na maisha vingekuwa vimepooza sana". Huo ndiyo ukweli wenyewe, kwamba bila kukwaruzana hatuwezi kufahamiana vema na kujua kwa undani tofauti kati yetu na wenzetu.

  Inabidi tujue kwamba hakuna binadamu aliyekamili, yaani asiyekosea, kama ilivyo dunia yenyewe. Kwa hali hiyo hakuna ndoa ambayo haina makosa, kwa sababu ndoa ni binadamu hao ambao siyo kamili. Kwa hiyo, mtu anapotarajia kuwa au kuishi kwenye ndoa isiyo na kukwaruzana, ni sawa na mtu huyo kutarajia kukutana na binadamu ambaye ni kamili, yaani asiyekosea.

  Kutarajia kuwa na ndoa ambayo haina kukwaruzana kunaelezwa kuwa ni chanzo kizuri sana kwa ndoa nyingi kulegelege au kuanguka kabisa. Mtu anapoingia kwenye ndoa akitarajia kwamba huko hatapambana na maudhi au kero za aina fulani, ni lazima ajue kwamba, hatadumu kwenye ndoa yake kwa sababu ndoa hiyo anayoitarajia haipo.

  Mtu ambaye hakubali au angalau hataki kuelewa kwamba, ndoa ni lazima iwe na mikwaruzo anaweza kukabiliwa na tatizo lingine baya zaidi kwenye ndoa yake. Kwa kutokujua au kuepuka kukwaruzana, hawezi kuwa tayari kukubali kujadili migogoro ya kindoa ili kupata ufumbuzi. Hawezi kulikubali hilo kwa sababu haamini kwamba ndoa yenye kukwaruzana ni ndoa.

  Wakati mwingine rafiki, ndugu au jamaa zetu hutusimulia jinsi ndoa zao zisivyo na kukwaruzana kama kwamba ni za malaika watupu. Bila kujua, huwa tunajikuta tumewaamini. Tunapowaamini huwa tunachukulia kukwaruzana kuliko kwenye ndoa zetu kama jambo au kitu ambacho hakikutakiwa kuwepo. Hapo hujikuta tukitamani kuondoka kwenye ndoa hizo kwa matarajio kwamba tunaweza kukutana na "malaika" ambao tutajenga nao ndoa zisizo na doa.

  Hata pale ambapo tunasema wanandoa wanapendana sana, bado ndoa yao ni lazima itakuwa na kukwaruzana. Lakini wanachofanya hawa na ambacho huenda wengine hawafanyi ni kujadili tofauti hizo sawia na kuamua kuzisahau na hapo wote kukubali kujifunza kutokana na tofauti hizo.
  Wale walio tayari kujadili tofauti zao sawia ndiyo ambao ndoa zao huwa na afya sana hadi wengine kushangaa kama siyo pamoja na kuona wivu.

  Wale wanaodhani ndoa ni mahali pa kila jambo kwenda kama mtu atakavyo, ndoa zao hupogoka vibaya na kufa kwa kishindo........
   
 3. m

  mzighani Senior Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  siku hizi dunia imevaa kaptula, wana familia hawaelewani
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,279
  Likes Received: 5,638
  Trophy Points: 280
  Yaani umejuaje best kwanza kukutana hivyo mpaka msibani
   
 5. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Duh! Mkuu umenikumbusha paleeeee Ilala flats, miaka ya 70!!! Ilikuwa raha sana, asubuhi chai na mkate wa boflo (au gloria!!), mchana ugali wa Yanga (wa njano), jioni ni wali maharagwe kwa kwenda mbele!
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,279
  Likes Received: 5,638
  Trophy Points: 280
  Mkuu kumbe ulipanga folen yaushirika eeh
   
 7. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  we acha tu!
   
 8. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Saa 12 unaamshwa ukaweke kijiwe kwenye foleni..........ukifika unakuta foleni imeshakwenda kama km 1,sijui walikuwa wanalala hapo?
  Ukinunua sukari,unga wa muhogo ni mandatory!
   
 9. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hivi si ndio enzi zile viliingia viatu vinaitwa "robot shoes",vilikuwa vyeusi vya mpira,ukivaa mchana lazima ukitembea umbali fulani uvimwagie maji ndani kupunguza maumivu ya kuungua.(Nakumbuka dada yangu alipiga kampeni mpaka mama akatununulia sare sare mi na yeye)wanaume walikuwa na vyao vinaitwa "chachacha"
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,279
  Likes Received: 5,638
  Trophy Points: 280
  Na mashati ya juliana unakumbuka best ,,mi sitoka nishau mama yangu alikuja siku moja analia nikamuuliza nini
  akawa amefungua mfuko akijua amenunua juliana mbili nakaka yangu kufika kufungua akakuta yale matambara ya
  wanayotupa baada yakushona ..sijuini laana baada ya wiki nikaenda kariakoo nikanunua viatu naviona kabisa
  nilipofika nyumban nikakuta size ya tofali iemchongwa kama kiatu vyakulia na kushoto sina hamu nikikumbuka
  those days watanzania tulikuwa na akili sana sana
   
 11. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mama yangu alivuliwa kitambaa cha kichwa pale magomeni kwenye saa 11 za asubuhi. Tulikuwa tgunashuka kwenye basi palke, wakati ule mabasi yalikuwa yanasimama mnazi mmoja!
   
 12. m

  mnero Member

  #12
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu una vituko
   
 13. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Wali ilikuwa sikukuu tu. hatumwi mtu hapo.
   
 14. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tulipaka mafuta fulani ya mgando sijui ndio rays????ukipaka mwili wote unabaki na vitu vinameremeta!teh teh teh...........Kupiga picha mpaka uende studio tena za kutafuta!
   
 15. s

  shosti JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  tulikuwa tunalala vibarazani mitaa ya kkoo gerezani japo kulikuwa kunasifika kwa uhuni...jaribu sasa kama hujaumia
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,279
  Likes Received: 5,638
  Trophy Points: 280
  shosti unaogopa kuvunjiwa yai siku izi wanakuja wenyewe awavunji yai washenzi hawa
   
 17. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Siku ya hitima ya nani huyo mkubwa? teh! Mlitoka poa sana na ubwabwa wenu!
   
 18. s

  shosti JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  hahahahahhha washenzi kwelikweli,ila dunia imebadilika kwa kweli!
   
 19. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280

  umenikumbusha mbali sana...zamani umoja ulikuwe lakini siku hizi ubinafsi unaanzia kwenye familia.....kila mtu na sahani yake ..huyu anakata kidogo ...yule anakata kikuuubwaa
   
 20. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Pdidy huyo ni wewe??
   
Loading...