Mkakati wa Team Lowassa huu hapa

Mkakati wa Team Lowassa huu hapa

Lowassa kama ilivyoada kwa viongozi wa CCM kijinadi. Lowassa amewabiti wenzake, ndio maana wana jaribu kumchafua.
Hata hao wakina makamba wananunua watu. Ni vitu vya kawaida kwa siasa za Tanzania.
Ile ni kwamba pamoja na matarajio ya wengi kuwa kashfa ya Richmond ingemtoa nishai, imewashangaza ni kwa jinsi anavyoibuka na kuwazidi wao, wanataka kujiaminisha kama watu safi kuliko Lowassa wakati wote wametokea chama kimoja hichohicho. I think mwenye jeuri ya kujiona yuko safi angefaa atoke upinzani na sio CCM. Kwani mwisho wa siku CCM ni walewale na wamoja.
Nakumbuka kuna Waliowahi kuhama wakaenda CCJ, mwisho wa siku wakarudi CCM.
Kuna watu wanalalamika eti lowassa haongei bungeni. Aongee nini wakati yeye ni serikali?
Kawaulizeni watu wake wa monduli
Ndio watatoa jibu la kuhusu mbunge wao lowassa.
Lowassa aliwahi kusema "ukimya wangu umenisaidia sana. .mungu amenipa hekima."

Kumbe ni kweli kimya kingi kinamshindo mkuu.
Mfalme Solomon alikuwa na hekima sana. Na sasa lowasa anayo hiyo hekima.
 
Jadili na mengine haya yanachosha

Wewe ni Mtanzania makini kweli mwenye kuipenda Nchi na kujua yanayoendelea kwenye siasa zetu?

Au mwenzetu wewe U Mnyarwanda
Hata kama huipendi Kambi A ama Kambi B unapaswa unapaswa kujua kwa undani nini kinaendelea upande A angalau unaweza kuambua mbinu za kukusaidia kuuimarisha upande B.

Endapo unachoka na kuzikinai siasa mapema hivi basi utachelewa kila kitu.
 
Ukitaka ujue Lowasa anaungwa mkono kiasi gani kila ukikutana na mtu, iwe msomi, mfanyabiashara, askari n.k hebu muulize swali hili "Unadhani ni Mtu gani anafaa kuwa rais kwa Tanzania tuliyo nayo? mimi nimeanza ila sitaki kuongea hapa nisije kuwaumiza moyo wale wanaona Almasi wakasema "NIKOKOTO"
 
Ni wewe tu ndio umebaki na mawazo ya kupandikizwa,wengi tunasema NDIYO kwa LOWASSA.

Ni wewe tu na wenzako mnaotumiwa na Lowasa. Watanzania wenye akili tunajua team ya Lowasa imejaa Wezi, na tunawakataa kwa nguvu zetu zote na kwa akili zetu zote. Nguvu ya Mungu itatuepusha na kikombe hiki.
 
Ni wewe tu na wenzako mnaotumiwa na Lowasa. Watanzania wenye akili tunajua team ya Lowasa imejaa Wezi, na tunawakataa kwa nguvu zetu zote na kwa akili zetu zote. Nguvu ya Mungu itatuepusha na kikombe hiki.

Nina Ujasiri sana ninapoeleza ukweli juu ya LOWASSA kuliko Makada wengine woote walijitokeza kutaka urais ndani ya ccm.

Tuambie Lowassa aliiba nini na wapi
Acheni chuki zenu ni dhahiri WENGI HAMKUTEGEMEWA KAMA EDDO ATAKUWA NA NGUVU za kisiasa tena,
mlifanya makusudi kumtelekeza na kumchafua lakini ni Ajabu anafanya vizuri kwenye siasa,JINA LOWASSA KWA MIKAKATI ALIYONAYO NA TEAM YAKE MTAMPENDA TU NA KULAZIMIKA KUSEMA NDIYO KWA EDWARD N.LOWASSA MWAKA HUU.
 
ccm wanaogopa kumfukuza lowasa au mwizi yeyote kwa ccm ni ngumu mana 99.9%ni mafisadi

Walio ndani ya CCM yenye mamlaka na maamuzi,yawezekana wanasababu tofauti wala si ufisadi.Lakini hao CCM maamuzi wanataka sisi tulio nje tuamini kuwa Lowassa ni fisadi.Nasi kwa kutojua tunaitikia kwa jazba.Na ukienda mbele ukauliza au ukahoji kama ni mwizi kwa nini msimpeleke kwa Pilato?Hapo utasikia wakijikanyaga ohhh muda ukifika tutamvua gamba.Tunadanganywa kwa hila.
 
Hata kikwete mlimpamba hivohivo leo hii tunasaga meno kwa uongozi wake mbovu..
Hii ndo tanzania nchi inayoongoza kwa ujinga..
 
Kachukue posho yako

HAPO UMEPOTEZA DIRA KABISAAA!!!

Mmezoea siasa za kizushi,kinafiki,kiujanjaujanja, uongo na za kununuliwa.
Mimi sio miongoni mwa hao mliowazoea,Ni mwandishi huru asiye na mipaka ya vyama vyenu vya siasa.
 
HAPO UMEPOTEZA DIRA KABISAAA!!!

Mmezoea siasa za kizushi,kinafiki,kiujanjaujanja, uongo na za kununuliwa.
Mimi sio miongoni mwa hao mliowazoea,Ni mwandishi huru asiye na mipaka ya vyama vyenu vya siasa.

Wewe ni kipochi manyoyaa
 
kwa sasa team lowassa haisumbuliwi tena na watu aina ya membe walipofikia wanamudu kazi yao ya kuhakikisha mtu wao anashinda kwa kishindo cha sunammi ndani na nje ya chama

imebainika kutoka kwa wasiri wa ndani ya team lowassa kuwa hata hao akina mwigulu chemba na lazaro nyalandu hao vijana waaminifu kupita maelezo kwa mh.edward ngoyai lowassa.

Usishangae kuwaona vijana hao ni kama kila mtu yuko lwake na hana habari na eddo,kumbe ni damu damu na mzee wa maamuzi magumu.

Dakika,masaa,siku na miezi inayoyoma kuelekea uchaguzi wa ndani ccm utajaona wengi wakisema "kuanzia leo mimi namuunga mkono mh.saana edward n.lowassa.hio itafanyika dakika za mwisho kabla siku za uchaguzi huo kufanyika ndani ya chama tawala.

Mosi,
lengo ni kuvunja nguvu za mkuu wa kaya asiweze kupindisha maamuzi na kuteua mtu mwingine.

Mbili,
imekusudiwa kutokea wakati huo ili kama kuna masalio ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wajichokee na kukata tamaa zaidi hasa kwa kuona ushawishi,nguvu na uungwaji mkono wa laigwanan haviwezi kuzuiliwa na awaye yote iwe kwa uteuzi ama uchaguzi ndani nec ccm.

Sio hivyo tu hata baada ya uchaguzi mkuu ujao inaonyesha laigwanan amejipanga vizuri zaidi kuliko kada awaye yote wa ccm.nimedokezwa yuko tayari kufanya kaxi na watu makini,wachapa kazi wasiocheka na nyani huku shamba la mahindi linaisha na kubakiwa na mabua matupu.

Mipango ya inavuka mipaka ya vyama na kuweka mbele maslahi ya taifa letu.huyu mtu nijasiri sana, alisikika mmoja wa wana team lowassa akisema.

Msije mkashangaa hata hao watu wazuri walioko upinzani nao wakawekwa kwenye baadhi ya nafasi za uongozi ili kujenga taifa hili kwenye ustawi wa

kiuchumi
kiafya
kielimu
akilenga kila mwananchi lazima afaidi ama ale mema ya nchi yake mwenyewe.

Tumeshuhudia wabunge mia na hamsini (150)ccm, waliojitokeza wazi wazi bila kificho na kusema kwa rais ajaye lowassa ndiyo chaguo sahihi na halali ndani na nje ya ccm.

Hayo mliyoyaona kama ni mvua basi hio ni manyunyu/rasharasha tu,sunammi inakuja vigogo wengi kila wizara na idara wanamuunga mkono lowassa.

Hakuna siku hata moja laigwan e.n.lowassa atakwamishwa,amejipanga ipasavyo.

Hapo nimewapa kionjo tu.

Ngoma inogile.

akili ya njaa haishindwi kitu.
Njaa mbaya sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom