Mkakati mpya wa Marekani kuhusu Afrika haupaswi kutungwa kwa ajili ya kukabiliana na China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111358127335.jpg


Kwa muda usio mrefu sasa, serikali ya Marekani chini ya rais Joe Biden imeelekeza tena mkakati wake kwa Afrika. Alipofanya ziara yake ya kwanza barani Afrika mwezi Novemba mwaka jana, waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken aliahidi kuwa serikali yake "itachukua mtazamo tofauti" na kushiriki katika masuala ya Afrika kwa kile ilichokiita "masharti ya haki". Ni wazi kwamba kauli hii iliilenga China, ambayo inazidi kuwa na uhusiano wa karibu na Afrika. Lakini kama ni kweli alivyosema Biden hivi majuzi, kuwa hatua ya kukuza uhusiano kati ya Marekani na Afrika ni kuimarisha demokrasia na kujenga ushirikiano wa kudumu wa kiuchumi na kibiashara, basi kukabiliana na China barani Afrika sio njia ya kutimiza malengo hayo. Na serikali ya Marekani lazima ifikirie kwa makini na kuepuka kuijumuisha Afrika katika sera yake kuhusu China.

Mwishoni mwa mwaka jana, rais Biden alimteua Judd Devermont, mkurugenzi wa zamani wa mpango wa Afrika katika Kituo cha Utafiti wa Mkakati na Masuala ya Kimataifa CSIS nchini Marekani kusimamia utungaji wa mkakati wa Marekani kuhusu Afrika, huku akitangaza mpango wenye fedha kidogo unaohusiana na Afrika. Katika muongo mmoja uliopita, biashara kati ya Marekani na Afrika ilipungua kwa nusu kutokana na sababu za upande mmoja za Marekani. Kwa kuwa nchi nyingi za Afrika kwa sasa zinashuhudia ukuaji wa haraka wa uchumi na tabaka la watu wenye kipato cha kati linapanuka, ni jambo la busara kwa Marekani kurejesha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na kuunda fursa mpya kwa kuwa na mawasiliano na Afrika.

Hata hivyo, mpango mpya uliotolewa na rais Biden sio mpya wala wa dhati. Jarida la "Foreign Policy" la Marekani lilieleza kuwa mkakati wa serikali ya Marekani barani Afrika "unachanganya demokrasia na haki za binadamu na kukabiliana na ushawishi unaoongezeka wa nchi zenye nguvu kama vile China na Russia katika bara la Afrika", ambayo si tofauti na serikali za awamu zilizopita za Marekani. Aidha, kutoka serikali, wasomi hadi vyombo vya habari, kuanzia kile kinachoitwa mtego wa madeni, rasilimali za madini, maslahi ya usalama kati ya China na Marekani katika Pembe ya Afrika Mashariki, na ushawishi wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa watunga sera wa nchi za Afrika, serikali ya Marekani inayoongozwa na Biden inafanya kila iwezalo kuchafua jina la China kwa kile kinachoitwa "tishio la usalama" barani Afrika. Wakati Marekani inapotunga mkakati wake kuhusu Afrika, na mambo hayo yanayotajwa yanachukuliwa kama ni muhimu ya kuzingatiwa, lakini inapuuza tu maslahi ya maendeleo ya nchi na watu wa Afrika, basi ni dhahiri yanakwenda kinyume na mtazamo wa China.

Kwa hakika, badala ya kuendeleza ushindani na China barani Afrika, Marekani inapaswa kutambua na kuzoea maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika, na kisha kuwatafutia kwanza waafrika halafu wamarekani fursa za maendeleo kwa haki. Juhudi za China za kukuza uhusiano na nchi za Afrika ni sehemu ya sera iliyo wazi ya kuimarisha ushirikiano wa pande zote na nchi zinazoendelea. Kuanzia ujenzi wa miundombinu hadi kukabiliana na janga jipya laCOVID-19, China imetoa msaada kwa nchi za Afrika katika nyanja mbalimbali. Wakati huo huo, kama ilivyo kwa mataifa mengine, Afrika inaagiza bidhaa kutoka China na kusafirisha bidhaa zake za kilimo kwa China. Uhusiano huo wa kawaida umeifanya Marekani kuwa na wasiwasi, jambo ambalo bila shaka litaifanya serikali ya Biden ishindwe katika kutekeleza mpango wake kuhusu Afrika ambao umekuwa na hila tangu mwanzo.

Kuzingatia ushindani mkubwa bila shaka kutadhoofisha ufanisi wa juhudi za Biden na marais wajao wa Marekani kujenga uhusiano wenye usawa wa kibiashara na maendeleo ya demokrasia barani Afrika. Hatari itakuwa kubwa zaidi ikiwa ushindani na China barani Afrika utafanyika kwa kuwatumia mawakala, kama vile Somaliland, ambayo hivi karibuni imeahidi utii wake kwa Marekani. Bado tunakumbuka kuwa wakati wa Vita Baridi, kutoka Somalia ya Pembe ya Afrika hadi Angola Kusini mwa Afrika, waafrika, kama mawakala wenye silaha wa Shirikisho la Urusi na Marekani, waliathiriwa vibaya kutokana na ushindani wa nchi zenye nguvu. Uchungu mwingi hajapona hadi leo, na wahanga wakubwa zaidi ni waafrika wa kawaida.
 
Wawaache tu hawa macho mvimbo watujengee bara letu kwa amani kwanza wao ndio wangekuwa wanafanya haya wanayoyafanya hawa macho mvimbo wangetaka kila mahali walipo kuwe na kambi zao za kijeshi wanawaza vita tu. Mchina yeye hajali anachukua hadi zile sisi tunaona ni takataka kwake ni malighafi.
 
Shida ya marekani ni moja , ana
taka kuwapangia waafrika waiishi kama vile anavyotaka yeye , yani anaamini yeye anavyoishi ndiyo yupo sahihi hivyo waafrika wanapaswa waishi kama yeye .


Lakini ukija kwa mchina yeye yupo tofauti , mchina kashatuelewa sisi waafrika tulivyo , mchina haingilii kabisa mambo yetu kama vile sijui demokrasia , wala hatupaingii sijui tukubali ishu za ushogaa, yeye hana muda navyo hivyo vitu.

Mchina , kama atakuta nchi ya Afrika inajiendesha kwa mfumo wa kichifu , Mchina wala hana shida ya kutaka sijui kuwabadilisha ndipo afanye nao biashara kama anavyofanya Mmarekani na washirika wake . Mchina kama atakuta nchi ya Afrika haina mpango wa ushoga wala hana muda wakuaanza kuwahubilia umuhimu wa ushoga.

Mchina kashajua , licha ya kuwa nchi nyingi za Afrika ni masikini wa pesa lakini zina maliasili nyingi ambazo yeye anaziitaji , hivyo kashajua kuwa anaweza bado kufanya nazo biashara tofauti na mtazo wa marekani yeye hufikilia kuzetenga , rejea "alipotufungia ile rottery ya visa".

Tisa kumi , mchina kashajua soko la Afrika linataka nini ?. Kutu ambacho naoma kwa upande wa marekani kama bado hajakijua , au kama kakijua basi hajakipa uzito , na hapo ndipo anapopigwa force king na kuzidiwa kite na Mchina juu ya Afrika.
 
Back
Top Bottom