Mjumbe wa kamati kuu CHADEMA, Lazaro Nyalandu awakilisha chama mazishi ya Hayati Dkt. John Magufuli wilayani Chato

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,923
141,889
Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema mh Lazaro Nyalandu yuko wilayani Chato mkoani Geita akishiriki mazishi ya kitaifa ya Hayati Dkt. John Magufuli.

Nyalandu ameonekana muda mwingi akiwa na mbunge wa Ilemela Dkt. Mabula na mbunge wa Shinyanga mjini Patrobas Katambi wote wawili ni manaibu waziri.

Nyala.jpg
Nyalandu.jpg

RIP Magufuli
 
C mnasema wafu wazike wafu wenzao.? Naona mfu amekuja kwa mfu mwenzake.
 
safi sana ndugu zangu chadema hiyoo ndio siasa nilitamani mbowe awepo. wanachama wenu mtu wa ccm akifa huwa tunaenda na tunatoa michango wakati mwingine tunakuwa kwenye kamati maendeleo hayana chama. magu ni baba ni mjomba ni baba mdogo ni baba mkubwa ni mkwe ni shemeji ni kaka. tumpumzishe salama mpinzani wetu.
 
Wapi Chadema imetoa tamko kiwa Nyalandu ndio awakilishe Chama kwenye msiba?

Acheni kuandika mawazo yenu.

Huyo ameenda yeye kama yeye.
 
Nyalandu ni mtu wa msimamo. Alienda kumpa pole Lissu wakati wenzake hawakuenda. Na kwenye hili inawezekana amefanya kile ambacho nafsi yake imemtuma. Lakini inawezekana pia kuwa ana baraka za chama chake kama ilivyokuwa kwa wakina Mnyika. Hilo nalo halitakuwa la ajabu.

Amandla...
 
Vipi, yeye hakuporwa ushindi wa ubunge huko kwao kwenye uchafuzi wa 2020?

Nilitaka pia kuuliza kama Rev. Msigwa naye kaonekana huko; lakini najua anajiheshimu sana Revelend.
 
Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema mh Lazaro Nyalandu yuko wilayani Chato mkoani Geita akishiriki mazishi ya kitaifa ya hayati Magufuli.

Nyalandu ameonekana muda mwingi akiwa na mbunge wa Ilemela Dr Mabula na mbunge wa Shinyanga mjini Patrobas Katambi wote wawili ni manaibu waziri.

RIP Magufuli!
B9R8RY.jpg

Mazishi ya dikteta Jiseph Staoin yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu mwaka 1953 March 9
 
Back
Top Bottom