Naisujaki Lekangai
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 1,340
- 1,378
Harry,Mjukuu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza ametangaza uchumba kwa rafiki yake wa kike aitwaye Megan Markle, na harusi inatarajiwa kufungwa rasmi mapema mwaka 2018.
Harry, mtoto wa pili wa mwanamfalme Charles alizaliwa mwaka 1984 na mchumba wake Megan mwaka 1982 kwa hiyo mdada kamzidi kijana kwa miaka 2.
Ni kweli kama wasemavyo, umri si kikwazo cha mapenzi, wawili hawa wanapendana kwelikweli na Harry anakiri waziwazi kwamba alipomwona Megan mara ya kwanza huko Toronto Canada alikokwenda kuzindua michezo mwaka 1996 aliona alichokuwa anakitafuta miaka yote kwenye haiba ya Megan."Maisha yangu yatakuwa ya raha sana," anasema Harry.
Megan si mzaliwa wa uingereza yeye ni mmarekani, na ni msanii maarufu anayeigiza mchezo uitwao Suits.Pia ni mwanaharakati wa kuwawezesha wanawake katika siasa, uanaharakati uliopata kumfikisha nchini Burundi kuzungumza na wanawake.Juu ya hayo yote huyu dada alishaolewa kisha wakatalikiana na mumewe kwa sababu za kuishi mbali. Mke akiishi Toronto na mume Los Ageles
Salamu nyingi za kuwapongeza hawa wawili zinamiminika kutoka sehemu na watu mbalimbali duniani kote uchumba ulipotangazwa rasmi jumatatu 27/11/2017.
Wachumba wakioneshana bashasha za mapenzi