UZUSHI Hastings Kamuzu Banda alikuwa daktari binafsi wa Malkia Elizabeth na alihasiwa ili asitembee na Malkia

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Nimekuwa nikisikia kuwa Rais wa zamani wa Malawi, Dkt. Hastings Kamuzu Banda aliwahi kuwa Daktari wa Malkia wa Uingereza na alihasiwa asije akatembea na Malkia Elizabeth na kuzaa naye. Kuhasiwa kwake huko kulipelekea Dkt. Kamuzu Banda mpaka anafariki dunia mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 99 kutobahatika kupata mtoto yeyote.

Banda.png

Malkia Elizabeth ii akiwa na Dkt. Kamuzu Banda (Mwaka 1985)​
 
Tunachokijua
Hastings Kamuzu Banda (1898 au 1906 – 1997) alikuwa mwanasiasa na kiongozi Mmalawi ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika upatikanaji wa uhuru wa nchi hiyo. Alihudumu kama Rais wa kwanza wa Malawi kuanzia mwaka 1966 hadi 1994.

Banda alizaliwa katika eneo ambalo wakati huo lilikuwa Protektorate la Uingereza la Nyasaland (sasa Malawi). Alisomea Udaktari nchini Marekani na Uingereza, akawa daktari. Baada ya kurejea Nyasaland, alihusika katika siasa na hatimaye kuunda Malawi Congress Party (MCP), kilichotetea haki za Wamalawi Waafrika na uhuru wao kutoka utawala wa kikoloni wa Uingereza.

Uongozi wa Banda ulisababisha Malawi kupata uhuru kutoka utawala wa kikoloni wa Uingereza mwaka 1964. Baada ya uhuru, alikuwa Waziri Mkuu na baadaye Rais wa Malawi. Hata hivyo, utawala wake ulijulikana kwa utawala wa kiimla, ukandamizaji wa haki za binadamu, na kuzuwia upinzani wa kisiasa. Banda aliweka mfumo wa chama kimoja na upinzani ulikabiliwa na matokeo makubwa.

Je, Kamuzu Banda alikuwa daktari binafsi wa Malkia Elizabeth na alihasiwa ili asitembee na Malkia?
Licha ya kuwapo kwa uvumi kuhuhusu Kamuzu Banda kuwa Daktari binafsi wa Malkia Elizabeth, JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali vya kihistoria vinavyosimulia historia ya Kamuzu Banda na Malikia Elizabeth, lakini hakuna rekodi au ushahidi unaoeleza Banda kuwa daktari binafsi wa Malkia Elizabeth.

Kuna ukaribu wowote kati ya Kamuzu banda na Malkia Elizabeth?
Malkia Elizabeth II wa Uingereza alitembelea Malawi wakati wa utawala wa Kamuzu Banda. Ziara yake ilifanyika mnamo Julai 22 - 25, 1979. Wakati huo, Hastings Kamuzu Banda alikuwa Rais wa Malawi. Ziara hiyo ilikuwa sehemu ya ziara yake ya kifalme barani Afrika, na ilikuwa ni moja ya matukio muhimu katika historia ya Malawi.
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom