Miguel255
Member
- May 13, 2020
- 35
- 111
Ama kweli tembea uone tulia usimuliwe, hii dunia haiishiwi mambo. Kuna msemo waswahili husema kuna watu na viatu sasa leo nataka nikusilumie story ya kiatu kimoja hivi.
Katika jiji la Mumbai nchini India kuna jamaa mmoja anaitwa Bharat Jain. Huyu jamaa ni omba omba maarufu jijini na shughuli zake hufanyia kwenye jua katikati ya jiji, yaani jua lake mvua yake.
Huonekana mtaani akiwa amechoka, mavazi machafu sura haina nuru lakini cha kushangaza Bharat ni mmoja kati ya omba omba matajiri zaidi duniani. Pengine hata ndio omba omba mwenye pesa ndefu kuliko wote pale Dodoma.
Jamaa anamiliki maghorofa mawili hapo hapo Mumbai. ana maduka ya nguo na viatu, ana sheli moja pembezoni mwa jiji ana frame kapangishia watu kama uchafu. Unaambiwa utajiri anaomiliki huyu matonya ni zaidi ya dolla milioni 1 za kimarekani. Yaani kwa pesa za bongo ni kama bilioni 2 hivi na upuku upuku.
Familia yake ilimuomba sana aachane na maisha ya kuomba omba kwani walihisi kudharirishwa lakini Bharat aliwaambia hizi pesa ninazomiliki, hizi pesa zilizofanya nyie familia yangu kuwa moja ya familia tajiri hapa India nimezitoa kwenye hii kazi. Chezea mshahara usichezee kazi, siwezi kuacha kuomba labda mmoja wetu atoweke kwenye uso wa dunia yaani yeye afe au kazi ya kuomba omba isiwepo kabisa duniani🤣🤣
Unaambiwa jamaa hanaga utani awapo kazini, ukikutana nae hata uwe na roho ngumu vipi utampa tu hela. Yeye mwenyewe anadai kuomba omba ni sehemu ya nafsi yake. Yqani mapigo yake ya moyo tu hayalii "tum tum tum" yanalia "omba omba omba" Kwahiyo aache kuomba bora afe🤣🤣
Unajua mnaweza kudhani natunga ila hii ni ukweli mtupu kama una mwenyeji wa India hasa mumbai muulize atakwambia kwasababu hakuna kiumbe kisichomjua Bharat. Unaambiwa kila kati ya watu kumi basi kuna mtu mmoja alishawahi kumpa hela mwamba.
Kwenye moja kati ya mahojiano yake alisikika akisema kwa alipofikia sasa yeye haombi kwaajili ya njaa. Anaomba kwasababu kwanza ana enjoy kufanya hivyo pili anafurahia kuona sura mpya mpya mbazo asingeweza kuziona kama angebaki kwenye jumba lake la kifahari.
Huyo ndo Bharat omba omba tajiri kuliko wote Duniani