[TD="width: 5%, align: center"][/TD]
[TD="width: 20%"][/TD]
[TD="width: 5%, align: center"][/TD]
[TD="width: 14%"][/TD]
| |
| Salutation | Honourable |
| First Name: | Edward |
| Middle Name: | Ngoyai |
| Last Name: | Lowassa |
| |
| Constituent: | Monduli |
| Political Party: | CCM |
| Office Location: | P.O. Box 139, Monduli |
| Office Phone: | +255 754 800000 |
| Ext.: | |
| Office Fax: | +255 22 2452037 |
| Office E-mail: | elowassa@parliament.go.tz |
| Member Status: | Current Member |
| Date of Birth | 26 August 1953 |
[TH="colspan: 3, align: left"]
GENERAL
[/TH]
[TD="align: center"]
Member picture
[/TD]
[TD="width: 20%"]
Member Type:
[/TD]
[TD="width: 38%"]Constituency Member[/TD]
|
| School Name/Location |
|---|
| University of Bath, UK |
| University of Bath, UK |
| University of Dar Es Salaam |
| Milambo Secondary School |
| Arusha Secondary School |
| Monduli Primary School |
[TH="colspan: 5, align: left"]
EDUCATION
[/TH]
[TH="width: 27%"]
Course/Degree/Award
[/TH]
[TH="width: 15%, align: center"]
Start Date
[/TH]
[TH="width: 13%, align: center"]
End Date
[/TH]
[TH="width: 10%, align: center"]
Level
[/TH]
[TD="align: center"]MSc. (Development Studies)[/TD]
[TD="align: center"]-[/TD]
[TD="align: center"]-[/TD]
[TD="align: center"]MASTERS DEGREE[/TD]
[TD="align: center"]MSc.[/TD]
[TD="align: center"]1983[/TD]
[TD="align: center"]1984[/TD]
[TD="align: center"]MASTERS DEGREE[/TD]
[TD="align: center"]BA (Edu) Hons.[/TD]
[TD="align: center"]1974[/TD]
[TD="align: center"]1977[/TD]
[TD="align: center"]GRADUATE[/TD]
[TD="align: center"]A-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1972[/TD]
[TD="align: center"]1973[/TD]
[TD="align: center"]HIGH SCHOOL[/TD]
[TD="align: center"]O-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1968[/TD]
[TD="align: center"]1971[/TD]
[TD="align: center"]SECONDARY[/TD]
[TD="align: center"]Primary Education[/TD]
[TD="align: center"]1961[/TD]
[TD="align: center"]1967[/TD]
[TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
| |
| Company Name | |
|---|
| Tanzania Government | Prime Minister |
| Ministry of Water and Livestock Development | Minister |
| State, Vice President's Office | Minister for Environment & Poverty |
| The Parliament of Tanzania | Member - Monduli Constituency |
| Ministry of Lands, Human Settlement Development | Minister |
| State, Prime Minister's Office and First Vice President | Minister (Judiciary &Parliamentary Affairs) |
| Arusha International Conference Centre | Managing Director |
[TH="colspan: 4, align: left"]
EMPLOYMENT HISTORY
[/TH]
[TH="align: center"]
Position
[/TH]
[TH="align: center"]
From
[/TH]
[TH="align: center"]
To
[/TH]
[TD="align: center"]2005[/TD]
[TD="align: center"]2/8/2008[/TD]
[TD="align: center"]2000[/TD]
[TD="align: center"]2005[/TD]
[TD="align: center"]1997[/TD]
[TD="align: center"]2000[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]2015[/TD]
[TD="align: center"]1993[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]1990[/TD]
[TD="align: center"]1993[/TD]
[TD="align: center"]1989[/TD]
[TD="align: center"]1990[/TD]
| |
| |
| Chama Cha Mapinduzi, CCM | Member |
| Chama Cha Mapinduzi, CCM | Party Executive-District, Regional &Head Office |
[TH="colspan: 4, align: left"]
POLITICAL EXPERIENCE
[/TH]
[TH="class: text_menu"]Ministry/Political Party/Location[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 31%, align: center"]Position[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 12%, align: center"]From[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 10%, align: center"]To[/TH]
[TD="align: center"]1990[/TD]
[TD="align: center"]Todate[/TD]
[TD="align: center"]1977[/TD]
[TD="align: center"]1989[/TD]
Kutokana na CV hii kwa nini huyu kiongozi asiwe Rais wetu ajae wa taifa hili ukizingatia kwamba ana uwezo wa hali ya juu kwenye masuala ya kiutawala na uongozi. Nawasilisha
WAJUMBE WA MKUTANO MKUU
BAVICHA TAIFA 2014
Na;
Francis Boniface Marwa,
Mgombea wa nafasi ya
Mratibu wa Hamasa
BAVICHA Taifa
Awali ya yote, kwenu ninyi Waislam Asalaam Aleikum, hata pia kwenu ninyi Wakristo Bwana Yesu Asifiwe.
Poleni sana kwa maandalizi na hekaheka mlizonazo hivi sasa huko Mikoani zenye lengo la kuifanikisha Safari ya kwenda Dar Es Salaam kwa ajili ya kujumuika nasi pamoja katika tukio hili la kipekee na adimu sana linalotokea kila baada ya miaka mitano, tena miaka mitano ambayo ndani yake wanakuwemo washiriki wapya ama hata kwa kutegemea mapenzi yake mola, ni dhahiri wapo wanaoikosa fursa hii kutokana na kutangulia mbele ya haki ili kupumzika ahela, tukio ambalo ni la kuiandika historia ya Baraza letu na Chama kwa ujumla.
Kwa kuyasema hayo, nachukua fursa hii kwa niaba yenu nyote mliopo ndani ya Taasisi hii pendwa, ili kuwakumbuka mashujaa wetu wa Soweto Jijini Arusha, Mwandishi wetu Daudi Mwangosi kule Nyololo Iringa na wenzetu wote waliopoteza uhai wao kwa kuipigania, kuijenga, kuitetea na kuilinda CHADEMA kama Mboni ya Jicho.
Hata pia katika Siku hii ya kipekee tunayokwenda kujumuika pamoja, tunawiwa na roho ya huzuni na huruma kuu, kuwapeni pole na kuwatia moyo wa ushujaa ninyi nyote mliopata ulemavu wa maisha wakati wa harakati za kukipigania Chama hiki.
Baada ya maneno hayo machache yaliyogusa mioyo yetu, nipende kuzungumzia mambo mawili kama sio matatu kulingana na kadri nitakavyoweza,
Kwanza, kila mmoja wetu popote pale alipo, ambaye ni sehemu ya wapigakura ndani ya chaguzi hizi za Kitaifa ndani ya Chama, sio ndani ya Mabaraza ya Wazee, Bavicha na Bawacha au Chama kwa ujumla, unapaswa kutambua kuwa, tayari unayo dhamana kubwa ya kuifanya CHADEMA iwe Chama dola ndani ya Chaguzi zijazo, hata pia wewe unayo dhamana ya kuidhoofisha CHADEMA kutokana na Kura yako moja utakayoipiga Siku ya uchaguzi, pengine kwa kutofanya analysis nzuri kwa wagombea ama kwa kutoutambua umuhimu wako katika kuibadili CHADEMA ili iwe na Taswira ya utaifa na yenye nguvu.
Pili, tunapokwenda kupiga kura ili kuwapa ridhaa viongozi wa kuliongoza Baraza letu la Vijana, upo ulazima sana wa kutambua kuwa, tutalazimika kuwapa ridhaa watu mahili na wachapakazi watakaotuvusha katika kipindi hiki kigumu cha Chaguzi za Kitaifa ndani ya Serikali.
Watu hawa, upo ulazima wa kuijua historia yao katika utendaji kazi, tena utendaji kazi wenye u-serious ndani yake katika kukijenga, kukipigania, kukitangaza na kukilinda Chama hiki.
Hapa pia ni lazima tuwapime wagombea hawa, juu ya nini walichokifanya ndani ya maeneo wanayotokea, sio ngazi ya msingi, Tawi, Kata hata Jimbo pia.
Kwa sababu unaweza unajikuta unamchagua mtu kisa anaonekana kwenye magazeti na runingani kila wakati, na ukipima utendaji wake kiundani zaidi, wazi unagundua kwamba ni kutafuta umaarufu bila utendaji wenye maslahi kwenye Taasisi yetu.
Tunahitaji kuwa makini
sana ili tusije tukafanya kosa la kuwapoteza watu muhimu ndani Chama, wanaoonekana kukipigania Chama usiku na mchana tena kwa nguvu Kazi na rasrimali zao, kisha tukazuzuliwa na mtu, eti kisa ana kitambi kikubwa, ana gari/magari ya kifahari, ana fedha nyingi, anaonekana magazetini na runingani n.k.
Hakika hakuna kosa baya ambalo tunaweza kulijutia, endapo tutasahau jukumu lililoko mbele yetu, na kuwapa watu ridhaa kwa kigezo cha ukwasi wa fedha na magari, au kuonekana magazetini na runingani, bila kumpima mtu kutokana na matendo yake ndani ya Chama.
Kiuhalisia, kuna watu mpaka hivi sasa ni wagombea ndani ya Chama, lakini ni dhahiri pasi na shaka kuwa wamekaa tenge, nadhani mnanielewa vizuri.
Wapambanaji, huu ni wakati muhimu sana kwetu, kuhakikisha kwamba tunaendelea ku-scan virus zote zenye chembe chembe za unafiki na usaliti ndani ya Chama, ili Chama kiendelee kukua, kuimaarika na kibakie salama na chenye nguvu.
Ndugu zangu,
nimeyasema haya kwa sababu natambua kuna mamillioni kwa mamillioni ya wazalendo wa Taifa hili, waliopanga foleni na misururu nyuma ya migongo yetu, wakiomba msaada wa kufunguliwa pingu na minyororo waliyofungwa kwa hila, uongo na unafiki wa CCM na vibaraka wao TLP, UDP na hao viroboto wanaojiita ACT.
Taifa letu kwa hatua lilipofikia
hivi sasa, wanahitajika watu wenye misimamo isiyoyumbishwa na watawala, watu wasio na chembe chembe za unafiki na usaliti kama tunavyoona kwa baadhi ya wenzetu tulionao ndani ya Taasisi, tena watu ambao tulijitoa mhanga kuwapigania ili wapate fursa za kuendelea kukijenga Chama hiki, lakini wamejisahau baada ya kupata fursa hizo, cha ajabu, baadhi yao tena wanaomba fursa ya kuchaguliwa tena katika nafasi zingine, licha ya kwamba wanatambua kuwa hawajafanya lolote ndani ya Taasisi hii, unafiki wa namna hii, huwa naufananisha na dharau iliyopita kiasi, na ifike mahala, tuseme hapana kidemokrasia.
Mwisho niwashukuru sana,
wale wote mliokilea na kukilinda Chama hiki kama mtoto mchanga, hususani pale tulipokumbana na upepo mkali wa dhoruba, hakika mlisimama kidete, na hakuna aliyedhubutu kutetereka, isipokuwa baada ya upepo ule mbaya uliokuwa na vumbi jingi kupita, naona mlijipangusa nyuso zenu uli kuondoa vumbi machoni, na tukaendelea na Safari ya kuitafuta Nchi yetu ya ahadi.
Niishukuru Kamati tendaji ya BAVICHA Taifa kwa nzuri na ya mfani wa kuigwa iliyofanya kwa kipindi hicho chote mpaka leo.
Tunaamini kwa wale tutakaobahatika kuwapokea mikoba yenu kwa ridhaa ya wajumbe wa Mkutano Mkuu, hakika tunaendeleza jahazi hili kwa kuanza na hapa mlipofia leo.
Tunawaahidi hatutawaangusha, bali tutaendelea kuwajaza matumaini ya ukombozi ulioko mbele yetu kwa vitendo bila kumung'unya maneno na wala hatutakuwa na muda wa kuwaonea haya wale wote watakaokuwa na malengo ya kutaka kukidhuru Chama hiki.
Francis Boniface Marwa,
Mgombea
Mratibu wa Hamasa
BAVICHA Taifa
0785881009/0767881009
04/09/2014.
*******************
Ahsanteni sana!