Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,190
- 128,239
Hata mimi katikati ya maelezo yake nikafikiri ni ni kisandu ikabidi nirudi juu kusoma jina lake vizuri
Huyu Mtanesco naona ana DNA ya mzee Kisandu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi katikati ya maelezo yake nikafikiri ni ni kisandu ikabidi nirudi juu kusoma jina lake vizuri
Huyu Mtanesco naona ana DNA ya mzee Kisandu.
Sasa kufyeka nyasi ndio udaktariAna maana kufanyakazi katika hospitali kama kufyeka nk casual labourer
Mimi nilivyofika tu hapo kwenye swala la udaktari nikagundua nimeingizwa mkenge ikabidi nirudi juu kusoma jina la mleta mada.
Sent using Jamii Forums mobile app


nadhani kaamua kutuchekesha


naomba ongea hata na rafiki yako anisaidie kazi hata udaktari tu kama atapata nafasi anipe ajira.
Hapa sijaelewa, kwani una taaluma hiyo?
Sent using Jamii Forums mobile app
anajua udaktari kama kuuza cd tunaomba ongea hata na rafiki yako anisaidie kazi hata udaktari tu kama atapata nafasi anipe ajira.
Hapa sijaelewa, kwani una taaluma hiyo?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kikwao mtu akiwa anafanya kazi katika Kituo cha Afya anaitwa Daktari hata mfagizi au karani. Akifanyakazi mahakamani anaitwa Hakimu hata kama ni mlugaluga. Akiwa Mlinzi wa shule ataitwa Mwalimu
Kwa hiyo Kilo ya ulezi unauzaje?Naomba leo nielezee kidogo kuhusu huyu mjomba wangu ambaye alikuwa tegemeo langu kipindi fulani ila alishindwa kunisaidia na nikajikuta nakuwa na maisha magumu sana huko jijini Dar es Salaam.
Mwaka 2004 niliondoka nyumbani kwenda Dar es Salaam kwa mjomba wangu nikiwa na miaka 22, nilikuwa kijana mwenye nguvu na nidhamu kwa watu wote. Ila sikuweza kuendelea na masomo kwa sababu nyumbani hali ilikuwa mbaya sana hivyo baada ya kuhitimu darasa la saba nikawa ni mtu wa kupambana kusaka riziki huku na kule ila sikuweza kufanikiwa kikubwa nilivyotegemea.
Mama yangu akampigia Mjomba simu na kuomba anichukue nikakae Dar es Salaam ili anisaidie kupata kazi. Kwa kweli mjomba alikuwa na uwezo na alifahamiana na watu wengi serikalini na katika sekta binafsi hivyo nilijua ataweza kunisaidia kupata kazi.
Mjomba yeye alikuwa ana duka kubwa la kuuza vifaa vya umeme pale Kariakoo na hakutaka kufanya kazi na mimi kwa kigezo kuwa ni mtu mzima sana hawezi kugombezana na mimi tena mbele za watu (mjomba ni mkali) basi tukazunguka huku na kule hakuna ajira na alipopata zaidi ni viwandani ila akataka nijitegemee nauli hivyo nikashindwa kuendelea.
Ila kinachouma ni kuwa Mjomba alikuwa na marafiki kila kona siku moja alikuja rafiki yake akajitambulisha alikuwa ni daktari hospitali moja maeneo ya Temeke basi wakaongea hapo muda mrefu wakati anaondoka nikawawahi na kuwaomba samahani na kumwambia mjomba tumehangaika sana kutafuta kazi naomba ongea hata na rafiki yako anisaidie kazi hata udaktari tu kama atapata nafasi anipe ajira. Mjomba akasema sawa nitaongea naye na yule daktari akasema akipata nafasi ataniambia.
Zikapita siku nyingi kimya hakuna jibu nikakutana na yule rafiki siku moja na kumkumbushia akadai alipata nafasi ila mjomba akakataa kuwa siwezi kuwa daktari atanitafutia kazi sehemu nyingine. Niliumia sana siku ile niliumia na kuona kama nimebeba dunia na mhimili wake mgongoni kwangu bila msaada wa mtu yeyote. Kweli kazi ya udaktari ilipatikana ila mjomba akakataa kweli? Nikamwambia mama na mama akalaani sana kile kitendo alichofanya mjomba ila tukasamehe.
Zikapita siku nikapata rafiki mmoja akaniambia kazi kwenye Shirika la Umeme na nikamwambia mjomba basi anisaidie nipate kata kazi ya utanesco akasema sawa nikajua ni zake zile ila kweli mjomba akanitafutia kazi na nikawa nafanya kazi ya utanesco. Siku moja isiyo na jina nilikutana na kisa kibaya zaidi niliporudi nyumbani usiku. Mjomba alikuwa anataka tufanye marekebisho ya umeme ndani na akasema wewe Mtanesco si utaweza au?
Nikasema nitaweza ila sikuwa najua chochote kuhusu umeme nilikuwa nachimba tu mashimo kazini na kubeba nguzo ila kufunga umeme walikuwa wanafunga wenzangu mimi nilikuwa sijawahi. Basi mjomba akasema chukua sijui huu waya ukate na uunge kwenye soketi ya nje. Nikasema sawa na nikaanza kazi ya kukata waya kumbe mjomba hakusema kuwa umeme ni hatari nakumbuka nilirushwa ukutani nikaanguka na kupoteza fahamu na siku napata fahamu niko hospitali na mama yupo kitandani sijui kuna nini wananishangaa na mimi nawashangaa tu. Nikatibiwa siku kadhaa nikapona.
Baada ya kupona mjomba akaninunulia nguo na viatu na kuniambia kesho utaondoka na mama kurudi kijijini. Nikamuuliza kuna nini na kwanini niondoke wakati niko kazini? Akasema tumeshauriana na mama yako urudi nyumbani kwa muda.
Sawa kwa shingo upande bila kujua sababu ya kurudi nyumbani nikarudi na mama. Nikafika kijijini watu wananiita fundi wengine daktari wengi Mtanesco mimi sielewi nani kawaambia kazi zangu hizo. Nikaanza kilimo taratibu na kuanza kupata tenda ya kupeleka ulezi Mwanza na hatimaye nikajenga na maisha yakawa yanategemea kilimo hadi sasa.
Mjomba nikawa nawasiliana naye na muda mwingine namtumia ulezi huku nikisema moyoni "Tenda wema nenda zako"
Siwezi kusahau kwa kweli..
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu Mtanesco naona ana DNA ya mzee Kisandu.
hivi aliishia wapi kisandu? Hahaha lohKikwao mtu akiwa anafanya kazi katika Kituo cha Afya anaitwa Daktari hata mfagizi au karani. Akifanyakazi mahakamani anaitwa Hakimu hata kama ni mlugaluga. Akiwa Mlinzi wa shule ataitwa Mwalimu
Mkuu, mjomba ni mama huwezi kumfanya lolote atakulaani.Dogo alikuwa mbumbumbu saba.Unajua kufunga umeme ? Ndio! Mjomba aliamini kuwa kijana kesha jiongeza huko na anajua.Kumrudisha kijiji ni msaada mkubwa kwa dogo maana ipo siku Kule saiti angeweza kushika umeme was kV na kubaki majivu.Mjomba ni mtu mwenye busara sana hana kosa lolote.Mnamcheka bure tu maskini, huyu alitakiwa apewe mwongozo na mjomba ili ajiweke sawa,
mjomba angemwelimisha tu si kumkomoa mpk kumpigisha shoti ili apate sababu kurudisha kwao.
Yes hawezi kuwa doctor wa meno but ilikua dream yake maybe, kuwa mtanesco that doesnt need too much power pale pale ana kibarua angesoma eve class veta kujiendeleza.
Kumrudisha kijijini mjomba kaonyesha pure miafrica tulivyo itasaidia nini?
Huyu dogo kakatishwa ndoto zake tukumbuke mamaake alikua anamtegemea na aliweka matumaini kwamba kijana kaenda mjini matunda yataonekana.
Then unarudishiwa mtu hospitali na tena najua alitoa diss kibao kabla jamaa hajazinduka.
I put down to 0.0000👎👎👎 kwa mjomba.
Dogo usiwe mnyonge tia nguvu hapo ulipo we bado kijana mjomba utakutana nae tu huko mbele kajichokea mpe ukweli, mmwagie hata pombe, mpigishe magoti akiri hila alizofanya, mnyanyapae nawewe mpaka ajute
Yes hamna kucheka na nyani.
Imeniuma sana,
halafu wapuuzi hapa mnaleta utani kwenye issue km hizi daah.