Unakumbuka nini kipindi cha utotoni?

Unakumbuka nini kipindi cha utotoni?

Kimwakaleli

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2018
Posts
14,586
Reaction score
20,819
Nimekutana Leo na Rafiki yake mama, nimecheka sana!
Kanikumbusha mbali sana!

Nikiwa nimeandikishwa darasa la kwanza,Nilienda kuanzia shule, Sasa wakati wa kwenda,tulianza ofisini,Mimi na mjomba wangu.Ofisi ya walimu ilikuwa nzuri,Kuna ramani ya ulimwengu,ya Afrika nk. Nikaipenda.

Sasa Mwalimu, akasema twende nikupeleke darasani,kwenda darasani,nikagoma nikamwambia Mwalimu hili darasa sio zuri kama lile la kwenu!

Hapo shule ikawa ndio basi Tena!
 
Bi mkubwa alipika mboga nyingi tule mpaka usiku,akaniagiza nikaepue jikoni,Mimi na haraka zangu nawaza rede nikachukua shina la mgomba nikashikia Ile sufuria si ikatereza bhana😀😀😀😀😀😀 mboga yote mwaaaaa,nilichezea kichapo Sio cha nchi hii!!
 
Kweli, tunatoka mbali!
 
Mengi sana

Hadithi za Jioni:
Kusimuliwa hadithi za kale na babu au bibi karibu na moto.

Nyimbo za Shuleni: Nyimbo za mchakamchaka na gwaride la asubuhi kabla ya kuingia darasani.

Kula Pamoja: Kushiriki chakula sahani moja na marafiki au ndugu.
 
Na kukuomba mboga!
 
Nilikua napenda kucheza na kwenda kuzurura Bila ruhusa.Hapa kwenye kwenda kuzurura ndo nimepigwa Sana kwa ajili hiyo.Nna mwanangu mmoja kwenye hili alitaka kunirithi ila mazingira hayamruhusu.
 
Kuzurula Kila mtu limemkuta, labda wazubavu .
 
Back
Top Bottom