Dkt Antony Mwandulami (58) mkazi wa kijiji cha Itunduma Wangama wilaya ya Njombe Mkoa wa Iringa, ameibuka na kuanza kutoa tiba kwa wagonjwa kwa mtindo wa babu wa Loliondo
Mjadala mkali kuhusu suala hili ulirindima kule kwaMjengwa na kwingineko; na inavyoonekana Watanzania wamegawanyika kuhusu suala hili: (1) Wapo wanaoziona tiba hizi kama neema kwa Watanzania wengi ambao ni masikini na wameteseka kwa
muda mrefu kutokana na huduma mbovu za kiafya kiasi kwamba wamekata tamaa. (2) Wapo wanaoona matukio haya kama dalili za mwisho wa dunia kama inavyorejelewa katika misahafu mbalimbali ya dini. (3)Wapo ambao hawajui
kinachoendelea; na ambao wanasubiri uthibitisho wa kisayansi ili wajue kama kweli tiba hizi zinatibu ama la (bila kujali kwamba mambo ya kiimani kama haya wakati mwingine yanaweza kukinzana na sayansi!). (4)Wapo wanaoona jambo hili kuwa ni
​njama za wanasiasaambao wanafurahia kuona kwamba mambo haya yanavutia sana vyombo vya habari kiasi kwamba mambo mengine ya muhimu hayapewi uzito wo wote. (5) Wengine wanaamini kwamba huu ni utapeli tu unaopoteza maisha ya watu bure!
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, akipata kikombe cha tiba ya babu, katika Kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro juzi. (Picha na Lilian Joel)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa bunge ), William Lukuvi (wa pili kulia) na Rosemary Nyerere wakipata kikombe cha babu Loliondo. Picha kutoka kwa Mjengwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Teresya Huvisa akipata kikombe cha Babu Loliondo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk Yohana Balelel wakipata tiba ya mchungaji Ambilikile Mwasapile wa kijiji cha Samunge, Loliondo.
Hahahaha! Hivi wakijiona sasa hivi wanajiskieje? Hahaha! Waafrika tuna matatizo sana. Na hawa viongozi ndio tunategemea walete maendeleo.
Hizo picha ndio kipimo halisi cha kuumwa kwetu na jinsi tulivowajinga na kuamini bila vithibitisho.
ngoja nicheke halafu nipite hahahahahahahahahaha hata WEWE upo?..................Kweli shule aisaidii wakati mwingine
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, akipata kikombe cha tiba ya babu, katika Kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro juzi. (Picha na Lilian Joel)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa bunge ), William Lukuvi (wa pili kulia) na Rosemary Nyerere wakipata kikombe cha babu Loliondo. Picha kutoka kwa Mjengwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Teresya Huvisa akipata kikombe cha Babu Loliondo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dk Yohana Balelel wakipata tiba ya mchungaji Ambilikile Mwasapile wa kijiji cha Samunge, Loliondo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.