Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?

Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
36,967
Reaction score
68,835
mjengwa_maggid.jpg

..naona Mjengwa ameanza kampeni za Uraisi za Kikwete 2010.

..tatizo ni kwamba hawezi hata kutaja achievement moja ya Kikwete tangu hajaingia madarakani, na mpaka sasa hivi 3 years as the President.

..Mjengwa ameishia kumsifa Kikwete kwa kuwa "karibu" na wananchi kwasababu hutembea kwa miguu kwenye viuchochoro vya Bagamoyo.

..Kikwete yuko karibu na wananchi kwa namna gani wakati aliitelekeza shule yake ya msingi aliposomea? shule hiyo ilionyeshwa ktk gazeti la Uhuru wakati wa kampeni za 2005 ikiwa na hali mbaya imechoka mithili ya zizi la ng'ombe.

..halafu kidogo kidogo Mjengwa anachombeza kuhusu hizi kesi mbuzi zilizofunguliwa majuzi na serikali. inavyoelekea zimempa imani kubwa sana na utawala wa Kikwete.

..Mjengwa anasahau kwamba Kikwete alimteua Chenge kuwa waziri wa afrika mashariki, baadaye akafanya mabadiliko na kumpeleka miundo mbinu. Kikwete huyo huyo alimteua Basili Mramba mara mbili ktk baraza lake la mawaziri. Baada ya Dr.Msabaha kuvuruga Nishati, Kikwete akajaribu kumficha wizara ya afrika mashariki. zaidi, kulifanyika mabadiliko mawili ya makatibu wakuu na yote hayakumgusa Gray Mgonja.

..sasa hii imani ya Majid Mjengwa kwa uongozi wa Raisi Kikwete inatoka wapi?

..Watanzania kwanini tunakumbukumbu fupi namna hii?

Majid Mjengwa said:

NAENDELEA na tathmini yangu binafsi ya miaka mitatu ya Uongozi wa Awamu ya Nne wa Rais Jakaya Kikwete.

Naam. Linapotokea jambo jema na zuri katika nchi, basi, ni vizuri jema hilo likaelezwa, vivyo hivyo kinyume chake. Kubwa kabisa linalotokea sasa ni ukweli kuwa Watanzania wameanza kurejewa na imani na uongozi wa juu pale wanaposhuhudia baadhi ya ‘vigogo' wakifikishwa mahakamani.

Hata kama ni chache kwa sasa, lakini hizi ni hatua za maana za uongozi wa Awamu ya Nne. Kwa Jakaya Kikwete, huu ni mtaji wa imani anaoanza kuuwekeza kwa umma. Kwa mwendo huu, mtaji huu unaweza kulipatia taifa mavuno makubwa, pengine si katika awamu yake, bali kwa awamu zijazo.

Katika kutathmini miaka mitatu ya Jakaya Kikwete madarakani bado nitarudi nyuma alikoanzia, maana huko nilipata pia kuandika fikra zangu kwa jinsi nilivyomwona akiianza awamu yake. Nilikuwa Bagamoyo siku tatu kabla ya Jakaya Kikwete kuhutubia Bunge la kwanza la Uongozi wa Awamu ya Nne, Desemba 30, 2005.

Nikiwa Bagamoyo nilipata wasaa wa kuzungumza na baadhi ya wananchi, kusikia maoni yao juu ya mtu huyu, Jakaya Kikwete. Nilitaka kupata maoni ya watu wa kawaida juu ya matarajio yao kwake.

Nakumbuka kuzungumza na kijana mwuza ‘chipsi' pale sokoni Bagamoyo. Huyu aliniambia; " Braza, Jakaya huwa anapita hapa kwa miguu akienda nyumbani kwake. Na kichochoro anachopita hiki hapa. Ukimaliza kichochoro hiki nyuma hapo utaukuta mti wa mkungu, mbele kidogo kuna kiwanja cha watoto, nyumba yake inaonekana kwa mbele".

Watu kadhaa walinipa simulizi zenye kufanana juu ya Jakaya Kikwete aliye karibu na watu. Jakaya waliyezoea kumwona akikatisha mitaa ya Bagamoyo kwa miguu na kuzungumza na wananchi. Kwa namna moja au nyingine, simulizi hizi zilionyesha ni kwa jinsi gani mtu huyu Jakaya Kikwete asivyo na makuu.

Na hakika, kiongozi wa watu hatakiwi awe mtu mwenye makuu, mbinafsi, mwenye tamaa ya mali na fisadi. Na katika hili la kuwa upande wa wananchi, Kikwete, kama mtu aliyekuwa na ndoto ya muda mrefu ya kushika nafasi ya ukuu wa nchi, naamini amesoma kwa kina maandiko ya wanafalsafa mbalimbali kama vile Niccolo Machiaveli na hata Plato.

Na kwa kupitia maandiko ya Machiavelli, " The Prince", yaani, "Mwana Mfalme", Kikwete ana mengi ya kujifunza . Machiaevelli anamtaka kiongozi kuwa makini na tabaka la waliomsaidia kuingia madarakani na hata wenye kumzunguka. Kwa mujibu wa Machiavelli, hutokea kwa Mwana Mfalme "kuwajeruhi" waliomsaidia kupata utawala. Hii ni kwa kutowatimizia yote yale waliodhani kuwa ni haki yao kutimiziwa.

Badala yake, Mwana Mfalme huwaingiza kundini wawe kama wengine. Katika manung'uniko yao, Mwana Mfalme hawezi kutumia dawa chungu dhidi yao kwa vile hujihisi ana deni kwao. Lakini, cha msingi kwa Mwana Mfamle ni kuzingatia ukweli, kuwa, hata kama atakuwa na maadui wachache, katika kuchukua nchi, muhimu ni kuwaridhisha walio wengi, na hapa ni wananchi.. Huwezi kutawala kwa amani bila upendo na utashi wa walio wengi. Ni kwa sababu hizi, Mfalme Louis XII wa Ufaransa aliweza kwa kasi ya ajabu kuitwaa Milan na kwa kasi ya ajabu kuipoteza Milan. Hakukidhi matakwa na matarajio ya wananchi walio wengi waliomfungulia milango.

Mtawala aliye mbali na asiyejali maslahi ya watu wake walio wengi ni mtawala mwenye hofu. Na mtawala mwenye hofu zaidi na watu wake kuliko adui wa nje, basi, hujijengea kasri ama ngome imara ya kujihifadhi ingawa hilo halitamsaidia kuzuia nguvu za umma za kumwondoa madarakani. Kwa mtawala, kasri ama ngome iliyo imara ni kuepuka kuchukiwa na wananchi, kuacha ubinafsi na kujali maslahi ya wengi.

Katika ubinafsi wa viongozi wetu, kiongozi wa Kiafrika, mara nyingi hapendi kukosolewa. Hana busara ya kutambua, kuwa, hakuna mwelevu wa kila jambo, kwamba sote hatujakamilika, tuna mapungufu yetu. Kwa kiongozi wa staili hii, akitamka jambo, basi hakuna wa kufikiri jingine. Fikra zake siku zote ni sahihi.

Plato, mwanafalsafa wa Uyunani ya kale anasema; katika nchi, kiongozi wa namna hii, hufikia kukoma kuwa kama wanadamu wengine, hugeuka mbweha. Atawaandama "wapinzani" wake. Wengine atawaua kwa kuwapachikia mashitaka batili, na wengine atawalazimisha kwenda kuishi uhamishoni.

Haya ni masuala ya kimaadili. Katika machapisho yake ya "Republic", yaani , "Jamhuri", Plato anazungumzia kwa kina juu ya ubinafsi na maadili. Je, kuna sababu gani nzuri na za kimsingi za kuwa mtenda haki na si kinyume chake, yaani mtenda maovu? Glaucon, ndugu wa Plato anajibu; "Binadamu wote kwa asili yetu tu wabinafsi, tunajijali sisi wenyewe kila tunapopata nafasi ya kufanya hivyo. Bila kujali kama jambo hilo si la haki kiasi gani kwa wengine. Lakini, kwa bahati mbaya, nasi pia hufikwa na hali kama hiyo kwa kufanyiwa yasiyo haki na wengine. Jambo hilo huwa si la kufurahia."

Maana. mlevi wa madaraka hupungukiwa haraka maadili ya uongozi. Basi, ghafla huwa mla rushwa mkubwa kwa kutumia ofisi aliyokabidhiwa . Na hatimaye, ghafla huwa tajiri mkubwa, bilionea! Vyote hivi huweza kumtokea kiongozi wa Kiafrika kwa kasi ya kutisha sana. Leo unapishana na Mwafrika mwenzako akiendesha baiskeli, kesho anaukwaa uongozi. Baada ya miaka 10 tu, anajenga "ikulu" yake mwenyewe ya kifahari, anaweza kuwa nazo mbili au tatu za namna hiyo na magari kadhaa ya kifahari. Je, yote haya ni kwa kipato halali cha "mteule" huyu kutokana na kazi yake?!

Mtu wa namna hii kamwe hawezi kukupa historia yenye kueleweka juu ya utajiri wake wa ghafla. Huyo si mhalifu kama walivyo wezi wa kuku au wenye kuvunja madirisha usiku. Huyo ni jambazi, ni mhalifu mkubwa anayetishia usalama wa taifa husika.

Hivyo basi, ili kuwapo na mazingira ya kuishi kwa amani na usalama ni vema, kwa mujibu wa mwanafalsafa Plato, kukawapo na taratibu za kuishi kistaarabu. Ndipo hapa dhana ya kuwapo kwa Mkataba wa Kijamii (Social Contract) ikaingia akilini kwa mwanadamu. Ndilo chimbuko la katiba za nchi. Chimbuko la misingi ya utawala bora.

Na hii ni changamoto kwa Rais Jakaya Kikwete na uongozi wake wa Awamu ya Nne. Ana nafasi ya kuwawekea Watanzania misingi na taratibu za kistaarabu za kuishi katika nchi yao. Aendelee na juhudi za kukirekebisha chama chake ili apate msingi wa kufanya marekebisho ya Katiba ya nchi. Ni kazi ngumu, lakini inawezekana, na hususan anapokuwa na umma nyuma yake.
 
..naona Mjengwa ameanza kampeni za Uraisi za Kikwete 2010.

..tatizo ni kwamba hawezi hata kutaja achievement moja ya Kikwete tangu hajaingia madarakani, na mpaka sasa hivi 3 years as the President.

..Mjengwa ameishia kumsifa Kikwete kwa kuwa "karibu" na wananchi kwasababu hutembea kwa miguu kwenye viuchochoro vya Bagamoyo.

..Kikwete yuko karibu na wananchi kwa namna gani wakati aliitelekeza shule yake ya msingi aliposomea? shule hiyo ilionyeshwa ktk gazeti la Uhuru wakati wa kampeni za 2005 ikiwa na hali mbaya imechoka mithili ya zizi la ng'ombe.

..halafu kidogo kidogo Mjengwa anachombeza kuhusu hizi kesi mbuzi zilizofunguliwa majuzi na serikali. inavyoelekea zimempa imani kubwa sana na utawala wa Kikwete.

..Mjengwa anasahau kwamba Kikwete alimteua Chenge kuwa waziri wa afrika mashariki, baadaye akafanya mabadiliko na kumpeleka miundo mbinu. Kikwete huyo huyo alimteua Basili Mramba mara mbili ktk baraza lake la mawaziri. Baada ya Dr.Msabaha kuvuruga Nishati, Kikwete akajaribu kumficha wizara ya afrika mashariki. zaidi, kulifanyika mabadiliko mawili ya makatibu wakuu na yote hayakumgusa Gray Mgonja.

..sasa hii imani ya Majid Mjengwa kwa uongozi wa Raisi Kikwete inatoka wapi?

..Watanzania kwanini tunakumbukumbu fupi namna hii?

Waandishi wengine uwezo wao wa kuchanganua mambo kwa kina ni finyu sana matokeo yake wanasifia watu wasiostahili kupewa sifa zozote. Kikwete hastahili kupewa tena awamu nyingine maana akiwa anaanza mwaka wa nne tangu aingie madarakani hakuna hata kimoja katika ahadi zake wakati wa kampeni 2005 alichofanikiwa kutimiza.
 
Huyu dogo si kwamba kaanza , bali anaendeleza mambo haya alianza way back kabla ya JK hajaukwaa .Mjengwa ni opportunist kama wengine ambao wako kwenye NGO ambazo hawawezi kwenda bila ya longo longo zao.Yeye ana asili ya kujipendekeza hata anaweza kuona mema lakini lazima akamilishe tabia yake.Ni kigeugeu sana lakini kwa JK naona ka stick kiasi fulani .Mjengwa ni wa kupuuzwa maana yeye kila siku analeta picha wananchi wakiwa choka mbaya ghafla JK amekuwa karibu na watu tena ?
 
Nawaita maripota wanafiki.....

Mjengwa kaingia mkenge siku nyingi......ule mkwara wake wa kuondoka RAI nilimuona ni mwanamtandao toka zamani.....mnakumbuka ile list of shame ilipotoka anony mmoja aliweka katika maoni akaifuta.....BTW Mjengwa hana jipya kwenye uandishi wake tumemzoea na simlaumu Njaa mbaya.....

Uzuri Mjengwa nui member hapa atakuja kuyaweka sawa.....

NAENDELEA na tathmini yangu binafsi ya miaka mitatu ya Uongozi wa Awamu ya Nne wa Rais Jakaya Kikwete.

Hiyo article ameanza kwa kuonyesha wazi analolifanya. Frankly speaking one is entitled to his own opinion.

That is his opinion - whats yours?
 
Yaani kuna watu wanataka huyu JK arudi tena madarakani 2010?? naanza kabisa kuamini kuwa asilimia kubwa ya watu wetu wanaulemavu wa ubongo!!
 
Mjengwa sijui ni msahaulifu yeye ametembea vijiji mbali mbali na anatundika picha kwenye blog yake akionyesha hali halisi ya WaTZ wanavyo ishi katika mazingira magumu hapo hapo anasahau kuwa waTZ walio wengi ni walalahoi wanashindwa kukidhi mahitaji yao msingi ambayo hayo mahitaji yamo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM hapo hapo tena anamsifia yule yule ambaye anatakiwa asimamie na kutekeleza ilani ya uchaguzi ambaye ni rais.
Huyu jamaa ana njaa ngoja tusubili labda mzee rais atampa kitengo naye akaimu.
 
Wakuu naona we are missing the point hapa.

Jamaa amedeclare katika opening statement kuwa ni "tathmini yake binafsi",... hajajumuisha watanzania wote kwenye huu mtazamo wake. Sasa huku kufoka povu kote kunatokea wapi?....

Ofcourse he is entitled to his opinion as an individual,...angekua ametujumuisha watz wote kwenye huo mtazamo wake,... tungekua na haki ya kumshambulia.

I dont necessarily share his opinion but still, nahisi we are missing the point kwa kumtolea personnal attacks as if watu mnataka kusettle nae scores za zamani hapa.

Kina Karl Rove wataendelea kuwepo tu, cha kufanya ni kujenga counter hoja za hiyo mitazamo yao instead of personal character assasinations.

Ni hayo tu wakuu.
 
Kwa hiyo mnamshauri Mjengwa angeandika Mbowe anafaa kuwa Rais 2010 anatakuwa ana uwezo wa kuchambua?
 
Yaani kuna watu wanataka huyu JK arudi tena madarakani 2010?? naanza kabisa kuamini kuwa asilimia kubwa ya watu wetu wanaulemavu wa ubongo!!

Kweli JF ina watu! Ulitaka nani apigiwe makofi ndio hao Watanzania waonekane wana akili kwenye ubongo?

Kwa siasa za Afrika JK atashinda 2010 tena kwa kura nyingi tu ingawaje sio kama alivyoshinda 2005.
 
Huyu dogo si kwamba kaanza , bali anaendeleza mambo haya alianza way back kabla ya JK hajaukwaa .Mjengwa ni opportunist kama wengine ambao wako kwenye NGO ambazo hawawezi kwenda bila ya longo longo zao.Yeye ana asili ya kujipendekeza hata anaweza kuona mema lakini lazima akamilishe tabia yake.Ni kigeugeu sana lakini kwa JK naona ka stick kiasi fulani .Mjengwa ni wa kupuuzwa maana yeye kila siku analeta picha wananchi wakiwa choka mbaya ghafla JK amekuwa karibu na watu tena ?

Lunyungu,

Mimi naona ungeamua kama alivyofanya Jokakuu kwa kuziweka wazi weaknesses za JK. Lakini inaelekea mwenzetu umeamua kumvaa messenger unafikiri ukimtwanga risasi Mjengwa hakutatokea waandishi wengine wa kumsifia JK?

Mwaga wazi wazi hapa mapungufu ya JK na pia kutuletea uwezo wa hao ambao wanaweza kumbadili JK.

JK ni reflection ya sisi Watanzania tulivyo. Ni ubabaishaji tu kuanzia matawi mpaka Ikulu.

JK atashinda mwaka 2010, atashinda sio kwasababu ka deliver sana, bali atashinda kwasababu labda yeye ni nafuu katika kundi la samaki waliooza.

Kwa siasa za Afrika ili kumshinda rais aliyeko madarakani inabidi wanaompinga wawe na uwezo zaidi ya mara mbili ya huyo rais. Mimi nimezoea kusema ni kama boxing, kama umewahi kuangalia ngumi, kumvua ubingwa boxer, inabidi umtwange knock-out au umburuze sana.

Kwa Tanzania sioni dalili ya JK kuburuzwa. Suala ambalo wanaompinga wamelivalia njuga ni la mafisadi tu, kwenye hilo suala JK ataenda kwa wananchi kwa mbwembwe zote na kusema I have delivered, si mnawaona akina Mramba, akina Yona, akina Mgonja, akina Jeetu nk.

Kama kuna mtu anafikiri atamshinda JK kwa agenda ya ufisadi pekee, anapoteza muda kwenye siasa. Kila JK akibanwa, atakuwa anamtema fisadi mmoja. Chukulia haya mapambano kama yule aliyekuwa rais wa Pakistan. KIla West wakitaka kumnyima misaada kwa kukumbatia terrorists, yeye alikuwa anamwibua terrorist mmoja kutoka kule milimani walikojificha. Busha na Blair wanafurahi, maisha yanasonga mbele na misaada inamwagwa.

JK anawajua mafisadi wote na ana nyenzo za kuwashughulikia akiona himaya yake inatishiwa. Kama kuna watu wanataka kumshinda JK lazima waingize na ajenda zingine kwa mfano maendeleo. Lazima walinganishe wilaya ambazo wanaongoza wao na zile ambazo aliongoza JK au wanaongoza CCM. Kama kuna tofauti kubwa, wananchi wataona na kuona kuna haja ya mabadiliko.

Change sio lelemama, watu wengi hupendelea stability kuliko change, heri zimwi ulijualo. Ili watu waone umuhimu wa kufanya change kama kule kwa Obama lazima kuwe na ushahidi wa wazi kuonyesha status quo imeshindwa au njia mpya za kufanya mambo zitakuwa bora zaidi.

Kutukana waandishi wa habari wenye misimamo tofauti haitawasaidia kitu, mageuzi yanafanywa na sera na sio vijembe.

Mjengwa ni messenger, unaweza usikubaliane naye lakini ni makosa kuanza kumjadili yeye badala ya kujadili alichoandika.
 
jamani mshaambiwa bahasha bahasha !!!jamani zitawaua hawa wana habari
 
Kwa hiyo mnamshauri Mjengwa angeandika Mbowe anafaa kuwa Rais 2010 anatakuwa ana uwezo wa kuchambua?

Hata kama ataandika Mbowe anafaa uraisi 2010 bila kutoa sababu zenye nguvu tutampuuza. Nionavyo huyu bw. Mjengwa hajachemsha kwenye hii issue tu ila makala zake nyingi anazotoa kwenye Raia Mwema zimepwaya. Naona tatizo anajaribu kuiga uandishi wa watu wengine... (au pengine hana kipaji cha uandishi?). Ningemshauri aandike mambo alio na upeo nao(afanye utafiti kwanza)...na sio kulazimisha
 
Demokrasia ni pamoja na kila mtu kuwa na uhuru wa kutoa maoni yake ili mradi havunji sheria Na kuyaheshimu mawazo ya mwingine hata kama huyapendi.
Hivi linapokuja suala la uchaguzi ni nani asiye na chaguo lake?Kila mtu hapa ana chaguo lake.Wengine mpaka sasa bado wanataka Malecela awe Rais Tanzania.Wapo pia ambao wangependa kuona Sumaye anakuwa Rais,Mbowe anakuwa Rais,Lipumba anakuwa Rais et al
Sasa kwanini tumshambulie Mjengwa?
 
Ni vigumu kumuelewa Mjengwa maana yeye huwa ni mtu wa kuuma na kupuliza, hana ile kitu inaitwa 'principles'!
 
Unajua kati ya sifa za uandishi nadhani hii ni mojawapo...
Kama tangazo (Ad) vile linavyotolewa. Kwa uabaya ama uvutio wake huonekana tu pale watu mnavyoumia vichwa na kulitazama, kusoma na kulizungumzia - ndivyo habari inazidi kunoga na tangazo kupanda chati..
Mjengwa kawaletea ya Kikwete, mishipa imewavimba na bahati nzuri imekuwa hoja nzito vichwani mwa watu, maandishi yake yanasomwa na wengi kwa mitazamo tofauti, ndio Uandishi wenyewe unapopata sifa!.

Binafsi hupenda sana hoja zinazonipa shida kutokubaliana na mara nyigi siwezi changia pale napokubaliana zaidi ya kutoa shukran kwa sababu nitakuwa narudia ama na mnukuu mwanzilishi..Hizi ambazo zinanipa chanzo cha kukubali kutokubaliana ndizo zina mvuto mkubwa kwangu..
Point kubwa hapa tupeni Ubovu wa Kikwete kama rais na sababu ambazo mnafikiria atashindwa uchaguzi ujao...Kumbukeni tu..
Kichwa cha nyoka huyu CCM ni Kikwete - in Tanzania winner takes all.. Hadi sasa hivi wandugu kusema kweli bila hata sifa hizo, mimi sioni sababu ya Kikwete kushindwa 2010!..
 
"JK atashinda mwaka 2010, atashinda sio kwasababu ka deliver sana, bali atashinda kwasababu labda yeye ni nafuu katika kundi la samaki waliooza."
-Mtanzania

...ama kwa hakika, hii naipa hadhi ya Quote of the day kama sio '...road to 2010'
...ukweli unauma, lakini heri yule anayekwambia ukweli!
 
Cha muhimu ni kuendelea kumbana JK, apunguze uozo kwenye serikali na CCM ikiwa ni pamoja na kutafuta practical method kutimiza ahadi zake....kuongelea JK kushindwa 2010 is just wastage of time wakati inajulikana wazi upinzani nako kwa uozo hawajambo, wanakula ruzuku tu, Tendwa kesha sema hakuna ukaguzi wa hesabu kwenye vyama, hii hatari sana....lazima vyama vyote vikaguliwe ili tujue nani msafi na mkweli....bongo yenyewe ni kama lumbesa ya kokoto, haibebeki kirahisi
 
...hivi humu kuna mtu na akili timamu anaamini JK atashindwa 2010? najua hata asipopiga kampeni atashinda ingawaje siipendi CCM,wenye akili wakapiganie ubunge ili mapambano yahamie bungeni ambako atleast kule unaweza ukasikilizwa,nawashauri wapinzani ili kuokoa zile karibu bilioni 100 za kampeni ili zitumike kwenye mambo mengine wasigombee uraisi wamwachie JK maana their winning chance ni ZERO na wasitupotezee muda wetu...hivi kwanini watu kama Lipumba,Mrema etc ambao wana probability nzuri ya kushinda ubunge wasihamishie battle zao bungeni ambako wanaweza wakaleta real change kuliko sasa na uwendawazimu wao wa kugombea uraisi kila mwaka!
 
Back
Top Bottom