Mjengwa blog inavyochokonoa nini maandamano/matembezi ya mshikamano Chadema/CCM

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
IRINGA%2B1.jpg
IRINGA.JPG


Picha kushoto​
Umati wa wanaCHADEMA wakiwa kwenye maandamano yao mwaka jana (hapa ni Iringa)
Picha kulia
Umati mkubwa sana wa wana CCM wakitembea kwa mshikamano juzi wakati wa maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa chama chao (hapa ni Iringa)

Mwenyekiti nimeona niombe ufafanuzi wa mambo haya kwani naona kuna matumizi ya maneno tofauti kwa jambo lilelile kutokana na muhusika. Inapokuwa CCM wanatembea pamoja wanasema ni matembezi ya mshikamano, bali wanapotembea CHADEMA huitwa maandamano. Sasa ni nini tofauti kati ya matembezi ya mshikamano na maandamano na kwa nini maandamano hupigwa marufuku wakati matembezi ya mshikamano hayazuiwi wala kukemewa kama maandamano? Naamini uchambuzi na tafsiri zako mwenyekiti na nadhani utanipa tafsiri sahihi juu ya hili. Asante

Mchokonoaji ni mdau wa Mjengwa Blog​
Mpanduji Mpanduji​

 
hao wa kijani hapo wote wamelipwa hao bila shaka

Maandamano ya Chadema yamefurika mtaa mzima, lakini ya CCM inaonekana kama wanaoandamana wamekodiwa na hayaonyeshi uhai wa pekee bali ni kutekeleza wajibu tu.

Maandamano ya CCM yanaonekana msafara ulikoishia lakini ya Chadema ni kama msululu wa mabehewa ya train ya kusubiria kwa muda wa kutosha hadi uweze kukatisha barabara.
 
IRINGA.JPG
HPIM1099.jpg


Sidhani kama CCM wanafanya matembezi ya mshikamano vinginevyo ibadilishwe Chadema ndio picha inaonyesha wameshikamana na CCM wanaandamana tu.

CCM sasa wamebaki na rangi tu ya mavazi yao maana naona mshono ni wa kuiga ******** ya Chadema.
 
CDM wamebeba mabango na wametawanyika kila kona....na si CCM tungewavua sare basi tungesema wanaenda msibani au ni wapita njia mtaa wa kongo...hawaonyeshi kama wako kwenye safari ya madai yoyote zaidi ya matembezi. Nadhani CDM wanalenga kufikisha ujumbe wakati CCM wanaelekea sehemu fulani --- anaendamana hapo ni CHADEMA bila ubishi (kwa tafsiri ya maandamano).
 
hapa mkoa wa mara waliandamana watu thelathini katika maadhimisho ya miaka 35 yaliyofanyika Mugumu, Serengeti. Ikabidi walipofika uwanja wa mbuzi Lukuvi akahutubia dk 10 akakacha........ Makongoro alipohojiwa na wana habari akawaambia andikeni CCM mara Kwishney......... Hiyo taarifa haijaoneshwa mpaka leo........
 
Back
Top Bottom