Lizarazu
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 6,331
- 7,885
Hapa nadhani haujanielewa yaani kwa kifupi iko hivi ninyi mnajiona ni haki yenu kukosea ila sisi tukikosea mnasema tunawalipizia au tunataka usawa na ushindani na ninyi na mnasema tunafanya makusudi yaani ninyi wanaume ndo mnatuona sisi malaika kwamba hatutakiwi kukosea
Mnasahau kwamba na sisi ni binadamu tuna madhaifu ila ninyi hamtaki kabisa tuwe na madhaifu lakini wanaume ndo mnajiona binadamu tena msio na hatia kabisa kwamba hata mkifanya makosa tuwachukulie tu hivyo hivyo na tuwavumilie kwamba mna madhaifu na ndo hulka yenu kufanya makosa hivyo hamtakiwi kubadilika
Basi sasa nimekuelewa ila hapo unaposema eti mwanaume anajiona ni haki yake kukosea ondoa, hakuna mtu mwenye utimamu wake wa akili anayekosea kwa makusudi halafu anajiona yuko kwenye haki, kama yupo basi huyo mgonjwa.
Unachoshindwa kuelewa wewe ni kwamba sisi wanaume hatuko tayari kufanyiwa malipizi kwa mistakes ambazo tumezifanya halafu tukakaa kimya. Kumbuka ubaya haulipwi kwa ubaya kwani kufanya hivyo ndio kuubariki ubaya wenyewe uendelee kuwepo, imagine umenikamata nacheat kwa hasira et na wewe unaenda kutafuta bwana wa kucheat nae kama malipizi. Halafu useme eti huko kwenye haki? ni haki gani hiyo? kuna njia sahihi ya kuweza kudeal na situation kama hii tofauti na hiyo.
Pia kitendo cha mimi kukataa kufanyiwa malipizi haimanishii kwamba najiona ni malaika au mwenye kustahili kukosea, kukataa kufanyiwa malipizi ni njia moja wapo ya kuzuia muendelezo wa tatizo! sasa mimi nikikuruhusu unitende kama nikivyokutenda mimi, hivi siku nyingine nikifanya kosa hilo hilo unaweza kunizuia kweli? si ukijaribu kunizuia nitakwambia nenda kafanye tu na wewe hili utulize moyo wako.? kisha cycle itaendelea hivyo hivyo!