Mjadala wa katiba Zanzibar, Muungano haramu wanadai Startv Live | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala wa katiba Zanzibar, Muungano haramu wanadai Startv Live

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by bushman, Sep 24, 2011.

 1. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mjadala wa muungano ni mkali kweli,wazanzibar wanasema muungano huu ni haramu kwa sababu mikataba haionekani na wala serikali ya Zanzibar haina mikataba zaidi ya picha ya kuchanganya udongo kati ya Nyerere na arume!
   
 2. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wadau wazanzibari wanauchambua muungano,walio wengi wanaonekana kuupinga muungano wako tayari kujitoa,wao wanaitambua Tanganyika ambayo sisi ni uhaini kuitaja
  Hivi tunawabembeleza nini?
   
 3. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mdahalo unaorushwa moja kwa moja na star tv kutoka zanzibar wenye mada isemayo " mustakabali wa muungano katika katiba mpya" wazanzibari kwa kauli mmoja wanasema hawautaki muungano! Nawasilisha
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  huku tayari watu wa megawati wamefanya mambo yao tangu saa 3 na robo.

  ila naunga mkono hoja...hakuna haja ya Tanganyika kuendelea kuwa koloni la mamwinyi wa Zanzibar.

  waacheni waendelee na mambo yao ya OIC na Kadhia.
   
 5. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata huku kwetu mzee wa Megawat alishamaliza kazi yake, tunaishi kama tupo kwenye Old stone age! Ila la kuukataa Muungano hata mimi nipo pamoja nao. Sijaona faida ya Muungano. Kwanini tusipige kura tuone kama kuna Mtanganyika nje ya viongozi wa ccm ambaye anauhitaji Muungano?
   
 6. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,472
  Trophy Points: 280
  Tumeshasema sana,hawa jamaa tuachane nao mbona tunabembeleza mambo ya ajabu.wanavolalama utafikiri wanalisha Tanzania nzima.tuwapige chini tuendelee na Tanganyika yetu.
   
 7. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  kila kitu wanataka nusu kwa nusu, wanataka hata nafasi za viongozi wanaoiongoza tanzania wawe nusu kwa nusu hivi hapo kuna kutendeana haki kweli!! hapaa tunahitaji tanganyika yetu labda baadhi ya mikosi itapungua kwenye nchi yetu.
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Ki ukweli huu Muungano utakuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani badala ya kujenga amani....kuna tatizo la msingi katika muungano huu,na unapigiwa kelele sana na hata wanazuoni kama Tundu Lisu,Dr Sengondo Mvungi,Mabere Marando nk...lakini kwasababu serikali ya CCM ni kiziwi hawataki kusikia,nadhani wanataka mpaka watu wapigane ndio wasikie....
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama watoa mada wa Zanzibar wanasema kwa kauli moja kuwa hawataki muungano, wale wabunge watatu waliomshambulia Mh. Tindu Lissu hadi kufikia hatua ya kumdhalilisha yeye (Lissu) binafsi walitumwa na nani? Walikuwa wanawakilisha mawazo ya nani?
   
 10. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kila kitu kina wakati wake. wakati ule bara na visiwani watu waliukubali muungano na kuukaribisha. si kweli kuwa wawakilishi wa wananchi pande zote hawakupewa fursa ya kuujadili muungano. nakumbuka sana mchango wa Mama wa taifa la Tanganyika marehemu Bibi Titi Mohamed akionya katika bunge la Tanganyika wakati wa mjadala kabla ya kuridhia muungano. Titi alionya kuwa muungano unaotaka kufanywa usichukuliwe kuwa sasa Zanzibar inamezwa na Tanganyika - ikiwa hivyo hautadumu. na ndio hata matumizi ya hati za kusafiria zikaendelea kwa kipindi. Status ya Zanzibar katika muungano ndo changamoto kubwa kuliko status ya Tanganyika katika muungano. Na hii inaweza sababisha upande mmoja ukafunga masikio kama ule wa Egypt na wenzake (United Arab Republic) ambao ulivunjuka na Egypt ikabakia na jina la "UAR".
  Baada ya muda wote wa kuwa na huu muungano na kizazi hiki kutoziona sababu za kuwepo kwa muungano kama kizazi cha wakati ule kilivyoziona basi aidha itafutwe aina itakayofaa au meli ifike gatini na kuwaacha abiria wajiendee wanakotaka bila uhasama ila katika mwito ule ule wa UNDUGU kati ya bara na visiwani - mwito uliochukua nafasi kubwa kuzileta nchi hizi pamoja.
   
 11. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  jamaaa,wanadai kama tunataka kujadili katiba mpya na wao,tuitafute kwanza tanganyika bara,wao zanzibar wanayo tayari,lakini wamesema mkataba wa mungano ni haramu kwa sababu haupo ni sawa kuhararisha nguruwe kwa waislam,wanadai patachimbika!
   
 12. A

  Albimany JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  aki muu

  Lusu hakupinwga kwa kua hautaki muungano bali alipingwa kwa kutaka wabunge wa zanzibar wasihudhurie vikao vinavyo husu mambo ya bara,na kuchukua posho za vikao ambavyo wao wahatachangia.
  Swali linakuja: Niyepi mambo yalioorodheshwa kua si ya muungano,katika katiba iitwayo ya Jamuhuri ya muungano?
  Tatizo hapa ni katiba ya Tanganyika iliorekebishwa kwa malengo ya kuwasahaulisha watu kua zilizoungana ni nchi mbili,nakama katiba Tanganyika haikuvaa koti la muungano basi hoja ya Lisu ingalikua na mashiko.

   
 13. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mh.A.Tundu Lissu was right
   
 14. B

  Buto JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sijaona umuhimu wa kuendelea kuwabembeleza watu wa Zanzibar kuendelea na muungano. Kwa kuwa wanahisi wananyonywa basi tutengane tubaki na Tanganyika yetu
   
 15. T

  Taso JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Naunga mkono hoja kwa dhati kuu.

  Sio Wazanzibari tu wanahisi wananyonywa, hata mimi Mtanzania bara najua ninanyonywa.

  Kwanza, la kwanza kubwa kuliko, kisheria Mtanzania bara haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar.

  Zanzibar wamejaza bunge la Tanzania wakati wako milioni moja tu, hivyo eneo dogo sana linakuwa na Mbunge. Ni upendeleo unaodhoofisha demokrasia kwa sababa kura ya Mzanzibar ina nguvu zaidi ya kwangu Mtanzania Bara.

  Wazanzibar hawana taasisi za elimu ya juu, wote waliosoma Tanzania wamesomea Bara.


  Wabunge wa Zanzibar wanaamua mambo ya Tanzania Bara ambayo hayawahusu, yasiyo ya Muungano, ndani ya Bunge.

  Tanzania Bara inagharamia huduma za Zanzibar bure, kama vile umeme. Waziri Shamhuna ametangaza kwa kujipiga kifua kwamba hawatalipa.

  Wazanzibari wanapata nafasi za uongozi kiurahisi na kiupendeleo kwa sababu wana "quota" yao kwenye serikali ya Muungano, kwa hiyo kwa sababu wako wachache ni rahisi zaidi kuwa Mzanzibar kuwa balozi, waziri, mbunge, jaji kutoka Zanzibar hata kama elimu, uzoefu, uadilifu, ustahili, upeo ni mdogo.

  Wazanzibar, japo wanatukana muungano na kutokuwa na shukrani, wananufaika na ukazi wa bara, yeyote anaepata nafasi, pamoja na viongozi wao wote wakistaafu, wanaenda kuishi Dar.

  Wazanzibar wanachoma maduka ya Watanzania Bara Unguja na Pemba wakati wao wamejazana wakifanya biashara Bara.

  Tanganyika ndio tunaoumia, tudai kuwatosa hawa wa Zanzibar, ni mzigo mkubwa, mkubwa mno.
   
 16. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  kimsingi nguruwe si haramu, sitaki kubishana na yeyote, kasomeni muktadha na aya inayotafsiriwa kuharamisha nguruwe.
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Muungano hautavunjika kwasababu ya wazanzibar wakuu..

  Muungano utavunjika siku wakigundua mafuta...

  Na atakayevunja muungano ni west power (americans) ili mfarakane..waibe mafuta..

  Zanzibar watapewa military support hamtawezi kupambana nao...

  Neema yetu ndio mwisho wa umoja ..watch out...
   
 18. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Muungano ni CCM kwa maslahi yao wanayoyajua hata mimi ni mtanganyika na sioni faida za muungano kama wazanzibar wanavyodai
   
 19. R

  RMA JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Raha sana! Tukiachana nao, yaani muungano ukivunjika itakuwa ni pigo kwa ccm kwa kuwa wakati wa uchaguzi kura nyingi feki za urais hutokea Zanzibar!
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kuna thread nilitaka kuianzisha kuwa Zanzibar ni kama Qatar na influence of western powers moderators wamechakachua kwasababu wanazojua wao. Inasemekana Qatar ilikuwa part of the United Arab Emirates. kutokana na utajiri wa mafuta na gesi wakashinikizwa na western powers kujitenga in 1971. Zanzibar pindi ikithibitishwa kuna mafuta basi Zanzibar ndio bye bye. Isitoshe kuna tetesi Zanzibar iko katika bonde la ufa na kama mafuta na gesi ipo wakianza uzalishaji sehemu za arabia uzalishaji utapungua.
   
Loading...