Wandugu,
Kama kawaida yake, Bw. Mkinga ametamka waziwazi bila woga kwenye Kipindi cha Kipima Joto ITV kuwa wamiliki wa Dowans watakaofaidi mabilioni ni Rostam, Karamagi, Msabaha Chenge.
Nimempenda huyu Deus Kibamba. Ametumia kauli ya Nyerere kuhusu jeuri ya maskini kukataa kulipa madeni yasiyo ya haki. Kuna mwingine amesema serikali inataka malipo yatolewe kabla ya kikao cha bunge Februari ili hili swala lisiingie tena mikononi mwa wabunge.