Mjadala wa Bunge: Wanahabari, Edwin Soko na Moses Mathew warushiana maneno makali studio za Star TV

Kila siku hao hao! Wakibadili ni Martin nyoni, mansuri jumanne, hao kwa hao students wa st. Aug. au walimu wao basi! Hivi Mwanza hakuna watu wengine hodari ambao star tv inaweza kuwa tumia? Nahisi kuna tatizo hapo

Hata mimi nimejiuliza mara nyingi sana hili. Sijui hawa StarTV wana matatizo gani tu!

Mimi naona hata uwezo wa watangazaji (waliowengi) wa kituo hiki ni mdogo sana especially ktk kuendesha vipindi vya majadaliano (live talk)!

Wana udhaifu mkubwa ktk maeneo haya;

1. Kutokuwa na taarifa za kutosha juu ya jambo linalojadiliwa

2. Hawajiamini. Labda kwa sbb kituo hicho ni cha kada wa CCM na kwa hiyo wanakuwa na maelekezo maalumu juu ya uendeshaji wa baadhi ya vipindi na urushaji wa baadhi ya matangazo yao.

Nisieleweke vibaya tafadhali, baadhi ya watangazaji kwa mtazamo wangu bado ni wazuri tu pamoja na kubanwa na sera za mwenye kituo. Mfano Dotto Bulembo, Angalieni Mpendu na wengine kwa uchache, they are really good and professional oriented!
 
Moses mathew tangu jana akiwa hapahapa startv na kipindi hikihiki cha tuongee asubuhi nilimshusha hadhi pale anapotetea tbc1 kutokurusha vipindi vya bunge live nasapot kauli ya Edwin Soko, huyu mzee ni mp....zi
Yeyevni mwandishi wa Daily News..

Kuna tofauti gani kati ya daily news na tbc?.

Lazima mr.Moses aishi ktk misingi ya bosi wake(serikali)
 
CCM Tumejitoa Akili Sawa Ila Lakini Si Hata Nyie UKAWA Mnajulikana Kwa Kunya Hovyo au?
Uwa sielewi kwa nini moderators wa JF wanaruhusu maneno machafu kama haya na mengine mengi tu yasiyo na utu ambayo yamekuwa yakitolewa na kiumbe hiki mara kwa mara hapa JF. Kuna wakati anaweza kuja na hoja nzuri tu lakini lugha anayotumia siku zote imejaa dharau, majigambo ya kizamani sana, ushabiki egemezi katika itikadi ya kichama na uchafu mwingine mwingi tu. Hii kwa kiasi kikubwa inashusha sana credibility au trustworthiness ya JF.
 
Huyu edwin Soko ni kabila gani mkuu

Ninavyomjua Tokea Niwe Nae SAUT 2006 - 2009 Darasa Moja La BAMC Ni Mngoni Kwani Si Unajua Tena Majina Yao Huwa Wanayachukua Kutoka Kwa Wanyama Kama Nyani, Ngedere Na Nadhani Huyu Labda Atakuwa Sokwe Ila Pengine Kwakuwa Amesoma Basi Akaamua Kujiita Soko. TULIOSOMA NAE SAUT Hata HATUMSHANGAI Kwani Hata Na Sisi TULISHAMPA NAKOZ Za Kutosha Tu Pale Mwanza Kwa Hizi Hizi Tabia Zake Za Kiharakati Huku Akishirikiana Mno Na Mbunge Mtukutu Wa ASILI Ila Ni Poti Wangu JOHN HECHE Ambaye Tulikuwa Nae 2006 - 2009 Ila Yeye Akifanya EDUCATION au BAED. Ktk WABUNGE WOTE AMBAO CHADEMA WAMEPATA NAWAPONGEZA TU KUWA NA HUYU JOHN HECHE KWANI NI MCHAPA KAZI NA ANAIJUA SIASA KUNAKOTUKUKA NA CHADEMA KAMA WATAMTUMIA VIZURI JOHN HECHE NI MRITHI MZURI SANA WA ZITO KABWE. Natumai Leo Mbunge John Heche Atampigia Simu SWAHIBA Wake Wa KIHARAKATI Edwin Soko Ili Aweze Kumpa POLE Na Amwambie Kuwa ASIFANYE MZAHA Na Wana CCM Ataumia! (Angalizo Nimemtania Hapo Soko Kwakuwa Kwa Upande Mwingine Ni Mtani Wangu Kikabila Hivyo Msishtuke Sana Mkaanza Kumaindi).
 
kamanda kwani wewe unashabikia chama gani mpaka leo? ?? chadema chama ambacho kimekumbatia ufisadi na mafisadi? ? khaaa. wenzako tumekaa humo sasa hivi tunatafuta uelekeo wa kwenda. hatuwezi kaa chungu kimoja na mafisadi. Dr Slaa alikana na Prof Lipumba. viongozi mahiri na wenye misimamo thabiti. achaneni na waganga njaa na wapiga dili.zindukeni mnaliwa!
 
Kama ningekuwa miongoni mwa wa viongozi waandamizi wa star tv ningeshauri moses Mathew asifike tena kwani yeye binafis ajitambui mpotoshaji amejaa kiburi majivuno kujifana kujua namjua kitambo lakini sijawai kujifunza kitu kwake kama mwana habari watu wengi tunawaamini wana habari lakini sio jamii ya moses.
 
kamanda kwani wewe unashabikia chama gani mpaka leo? ?? chadema chama ambacho kimekumbatia ufisadi na mafisadi? ? khaaa. wenzako tumekaa humo sasa hivi tunatafuta uelekeo wa kwenda. hatuwezi kaa chungu kimoja na mafisadi. Dr Slaa alikana na Prof Lipumba. viongozi mahiri na wenye misimamo thabiti. achaneni na waganga njaa na wapiga dili.zindukeni mnaliwa![/QUOTE!]
Hii sio mada yetu hapa!!
 
Uwe chadema au ccm au chama chochote kingine uamuzi wa kutorusha TBC live sio sahihi sababu zilizofanya TBC irushe live matangazo bado zipo kuturudisha miaka 10 iliyopita ni dhambi.
 
Star tv huwa hawana mtu makinitofauti na Moses?maana huwa yy tu wakati sio mtu makini kabisa huwaanaongea ongea tu..
 
Katika Hali Isiyokuwa Ya Kawaida Waandishi Wa Habari Mmoja Akiwa Ni Mwandamizi Moses Mathew Wa Gazeti La Serikali La Daily News Na Mwandishi Mwenzake Mmoja Ambaye Huwa Anajinasibu Kuwa Ni Mchambuzi Wa Habari Comrade Wangu Kabisa Edwin Soko.

Tatizo Lililopelekea Hadi WAANDISHI HAWA WAWILI MARAFIKI Na Ambao Ni WATANI PIA ( KIKABILA ) Ni Baada Ya Wote WAWILI Kuonyesha Dhahiri Kuwa Wanatoka Ktk HOJA ZA MSINGI Kuhusu Mada Ya TBC Kutoonyesha " Live " Matangazo Ya Bunge Ambapo Wawili Hao ILA HASA HASA Comrade Wangu Edwin Soko Kuonyesha Bila Aibu Kuwa ANAUTETEA MNO UPINZANI KWA HATUA ZAO ZA KIPUUZI ZA KUTOKA NJE YA BUNGE ILI KUSHINIKIZA BUNGE KUONYESHA LIVE MATANGAZO YA BUNGE.

Edwin Soko Hakuishia Tu Hapo Baadae Akaenda Mbele Na Kumchana Mwenzie Kuwa Yeye Ni KIBARAKA WA CCM Na Mganga Njaa Tu Hali Ambayo Ilipelekea Mwandishi Moses Mathew Kutaka Kumpa Mtu NGUMI ZA UHAKIKA Ila Mtangazaji Mwongozaji Boniface Mapuri ALIWEZA Kuwazuia Japo Kimtindo Nilimwona Kwa Mbali Kama Vile Edwin Soko AMESHAUMUKA USONI Nahisi Kuna Kangumi Alipigwa Ka Kiaina. Na Mwishoni Mwandishi ALIYENIVUTIA Leo Moses Mathew Akamtaka Mtangazaji Namnukuu "TAFADHALI SIKU NYINGINE UKINIALIKA STUDIO USINILETEE VICHAA KAMA HAWA ".

Ila Kiukweli Edwin Soko Ameyataka Mwenyewe Kwani Yeye Muda Wote Badala Tu Ya Kujenga HOJA Yeye Kazi Ni Kuitetea Tu UKAWA Na Hasa Hasa CHADEMA Na Bahati Mbaya Leo Kakutana Na MWANAMUME Moses Mathew Ambaye ALITAKA KUMWADABISHA.

Binafsi NAMLAUMU KUNAKOTUKUKA Mtangazaji Mwongozaji Kwa Kitendo Chake Cha KUZUIA TUSIONE MPAMBANO ULE MTAMU Na Kama Huyu Mwandishi Edwin Soko ASIPOBADILIKA Na Hii Tabia Yake Ya Kila Anapoalikwa Kufanya UCHAMBUZI Ktk Tv Kwa Kuonyesha MAPENZI YAKE DHAHIRI KWA CHADEMA Kuna Siku ATAKUTANA NA Mtu Mwingine ATAMUHARIBU USO WAKE KABISA Na Labda Nitoe RAI Kwa CHADEMA au UKAWA Kuwa Kama Mnaweza ANZISHENI REDIO Na TV Yenu ILI MTUONDOLEE HIZI SHIDA!

Big Up Sana Moses Mathew Huyo Dogo Hakika Ataenda KUSIMULIA Huko Kwa Akina Mbowe Na Lisu Kwa Discipline ULIYOMPA.
naona wametoka musoma
 
Kumetokea kurushiana maneno yasiyo na staha katika studio za Star TV baina ya wageni wawili waliolikwa wamealikwa studio za Star TV za jijini Mwanza ambao wote wawili ni waandishi wa habari. Wageni walikuwa mwandishi Edwin Soko na mwenzake Moses Mathew huku mtangazi akiwa ni Leonard Mapuli.

Chanzo ni kutofautiana kimtazamo ambapo bwana Edwin Soko(mchambuzi) alikuwa akipinga uamuzi wa serikali wa kusitisha matangazo ya TBC1 ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge huku bwana Moses Mathew(mwandishi mwandamizi) akionekana kutetea uamuzi huo. Maneno waliyoyatamka si vizuri kuyarudia hapa kwani haitapendeza.

Kwakweli wamerushiana maneno ambayo siyo mazuri kwa dakika kadhaa huku mtangazaji akiwasihi wawe watulivu lakini jazba ilitawala na baadae wakashutumiana kuwa wewe ni wa chama fulani huku mwenzake nae akijibu kuwa wewe ni wa chama fulani.

Binafsi licha ya yaliyotokea, nampongeza bwana Edwin Soko kwa msimamo wake wa kupinga uamuzi wa Serikali kwa kutoa hoja ambazo mimi binafsi naziunga mkono.

=======



Asante sana na pongezi kwa moses Mathew kwa kumwadabisha huyu kunguru mfua chupi za Mwenyekiti wa ufipa.
 
CCM Tumejitoa Akili Sawa Ila Lakini Si Hata Nyie UKAWA Mnajulikana Kwa Kunya Hovyo au?
Utahila wa mtu unaonyeshwa na vitu anavyofinya. Haina shaka mnabishana tahila. Mtu mwenye akili timamu hawezi kuandika maneno machafu kiasi hicho. Hilo ni tahila achana kubishana nalo.
 
Star tv inamilikiwa na kada wa ccm lakin huwa wanajitahidi sana kubalance matangazo yao yasiegemee uchama. Kinachonishangaza ni kwa nini wanashindwa kuwatahadharisha wageni wao wasijikite ktk ukada na badala yake wajikite ktk hoja? Hilo ndo tatizo
 
hivi hiyo credibility au trustworthiness ya jf wewe unaipimaje mkuu? binafsi naona ni kama tu una chuki zako binafsi na huyo mleta uzi kwani kama ni maneno machafu humu tunayaona mengi sana kwa mfano ni jana tu kuna member humu humu tena ni maarufu tu kamtukania tusi kali la mama yake mbona hatukukoona ukijitokeza kukemea lile? au kosa humu jf ni mpaka lifanywe na mleta uzi tu? halafu wewe ni nani wa kuwaelekeza moderators nini cha kufanya? leo kwa mara ya kwanza najitokeza kumtetea mleta mada kuwa mnaojifanya kumlaumu huwa hamtendi haki na kama kweli hawa moderators wakiamua walivalie njuga suala zima hili la sijui lugha au dharau au kashfa nina uhakika kuwa tutakaobaki humu jf hatutazidi hata 500. tuache kuwa wanafiki humu na tukubali kuwa humu tupo changanyikeni. hivi mtu kuambiwa kuwa kanya ni tusi au neno baya? wewe hunyi? au labda nikuulize je una uhakika kuwa huyo aliyelengwa hakunya kweli? ni mara ngapi humu jf watu huja na hadi taarifa za siri za watu maarufu na mashuhuri na wanaziweka hadharani tena zingine zikiwa zinaaibisha lakini maisha yanaenda? peleka huko chuki zako binafsi na mleta mada ila sisi tunavyojua ktk siasa kupigana vijembe vya aina hii ni kitu cha kawaida mno tu.

Mkuu umeshauri nipeleke huko chuki zangu binafsi na mleta mada. Sawa nitazipeleka huko ulikosema. Lakini nifahamishe huyo MLETA MADA au UZI unaemzungumzia ni yupi?
 
Mwandishi Mosses Mathew ni Kibaraka wa CCM hata hoja zake asimamii ukweli bali ukada wake. Juzi pia hapo hapo StarTV alitetea sana Serikali ya CCM kuzima matangazo Bungeni ya moja kwa moja (Live) bila kuwa na hoja ya msingi. Sababu alizosema Waziri Nape ni 3 ambazo ni gharama kubwa, watu wafanye kazi nchana na jioni wakipumzika ndio waone Bunge Live kwa starehe. Gharama halina msingi kwani TBC inapata ruzuku serikalini, hailipi kodi wala pango wakati StarTV, AzamTV, EATV wanajitegemea na wanalipa kodi nk. la pili Habari za Bunge ni kazi kwa wengine kuna taasisi (Activists wanaharakati) zinafuatilia mwenendo wa Bunge kama kazi yao na kutoa report wakiwa wilayani hivyo wamefungiwa kazi, pili kazi za shamba zina msimu kwa mwaka zaidi ya miezi 4 wakulima hawaendi shamba na mwisho zaidi ya 60% ya wananchi hawana ajira rasmi na ajira zao zisizo rasmi wanafanya hata wakiangalia Bunge na la mwisho nani ana muda wa kuangalia TV saa 4 usiku? Vijijini wanalala saa 2-3 pia taarifa itakatwa (sensored) na kuchakachuliwa.
 
Back
Top Bottom