MI Tokea Nimeanza Kutazama Kipindi Cha TUONGEE ASUBUHI Cha STARTV, Kwa Zamani, Not Now!! HUYO Mosses Mathew Sijawahi Kumuona Akipinga Jambo Lolote Ambalo Limefanywa Na SERIKALI, YEYE Kwake Ni MAZURI Tu!!!! MARA Nyingi Walikuwa Wanakwazana Na Wachambuzi /Waandishi Wenzake, Kutokana Na Kauli Zake Na Aina Ya Maneno Yake Yenye Dharau Na Kiburi!!! KUMBE Bado Yupo Tu!!!!? Ajitahididi Huenda MAGUFULI Akamuita Na Kumpa Walau Kanafasi Kaulaji, Kama Akina Mpanju!!!Kumetokea kurushiana maneno yasiyo na staha katika studio za Star TV baina ya wageni wawili waliolikwa wamealikwa studio za Star TV za jijini Mwanza ambao wote wawili ni waandishi wa habari. Wageni walikuwa mwandishi Edwin Soko na mwenzake Moses Mathew huku mtangazi akiwa ni Leonard Mapuli.
Chanzo ni kutofautiana kimtazamo ambapo bwana Edwin Soko(mchambuzi) alikuwa akipinga uamuzi wa serikali wa kusitisha matangazo ya TBC1 ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge huku bwana Moses Mathew(mwandishi mwandamizi) akionekana kutetea uamuzi huo. Maneno waliyoyatamka si vizuri kuyarudia hapa kwani haitapendeza.
Kwakweli wamerushiana maneno ambayo siyo mazuri kwa dakika kadhaa huku mtangazaji akiwasihi wawe watulivu lakini jazba ilitawala na baadae wakashutumiana kuwa wewe ni wa chama fulani huku mwenzake nae akijibu kuwa wewe ni wa chama fulani.
Binafsi licha ya yaliyotokea, nampongeza bwana Edwin Soko kwa msimamo wake wa kupinga uamuzi wa Serikali kwa kutoa hoja ambazo mimi binafsi naziunga mkono.
=======