Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mjadala: Side Comments: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Majibu ya Zomba juu ya ahadi za Kikwete 2010 Uchaguzi mkuu:
"Ahadi zote za Rais zimetekelezwa sioni hata moja ambayo haijatekelezwa kwa hatua fulani au nyingine.

Kama kuna mtu ana ahadi ambayo haijatekelezwa aainisha hapa. naona Matola kaweka list ya vitu 69, ambayo ni kidogo sana kutokana na ahadi za Rais. Kikwete anatekeleza mengi sana zaidi ya ha yo 69.

Wengi hawaelewi kuwa ahadi ya Rais ni agizo kwa watendaji, sasa hesabu wilaya zote na kila wilaya imeahidiwa na zote zinatekelezwa.

Sioni hata moja amabyo haitekelezwi mpaka sasa, jee kuna anaeijuwa?

Kuna zingine zimekuwa ni World Record, mfano alipoahidi chuo Kikuu Dodoma, kilichukuwa exactly miaka miwili kuanza kuchukuwa wanafunzi toka kuahidiwa".
Inabidi unyang'anywe sehemu ya akili zako ili kutamka maneno kama haya!
 
gfsonwin kajikuta hana jibu anasema kuwa eti ahadi za kaka mkubwa zishatekelezwa so anataka tuamini kwa sasa nikienda Kigoma ni Dubai of Africa
Kwa kweli hili swali halina kudesa wala kuleta longo longo za data hapa unatakiwa useme katika ahadi zake karibu sabini amefikia wapi kuzitekeleza

i knew kwamba hawez kupata jibu na sasa naona anaanza kulalama kwamba matola katumia majibu ya kihuni kwenye post #30. kiukweli sitazamii kabsa kwamba zomba amnange kikwete lakini pia nilitegemea awe fair aonyeshe mazuri na mabaya.
 
Last edited by a moderator:
Jamani mnaona Zomba alivyojibu swali la pili, si ni dharau hizi sasa? basi aulizwe kwanini siku hizi Jakaya hasemi kwa nguvu zaidi, kasi zaidi ha hari zaidi, hata kwa utani tu kwa nini hasemi?
 
zomba tuambie ni jinsi gani basi hizo ahadi amezitekeleza au hata kama ameanza (yupo kwenye mchakato) tuambie
 
Last edited by a moderator:
Swali kwa Matola unafikri ni changamoto zipi alizokutana nazo JK ambazo zimekwamisha utekelezaji wa ahadi zake.

Swali kwa zomba ukitilia maanani mabadiliko ya katiba yanayokuja ambayo pengine yakaongeza au kuondoa kikomo cha kugombe urais ......unafikiri JK anastahili kuongezewa kipindi kingine cha miaka mitano? na kwa nini?
 
Last edited by a moderator:
zomba alitakiwa aongee from his perspectives na ku'compare' na 'international standards'..sasa kuorodhesha asilimia tu pamoja na maelezo mengi hakuleti tija ya mjadala!..

Swali langu..na naomba Mwali ulichukue..ni hivi:

Kwa kuwa tumeamua kuwa na Kauli Mbiu ya Kilimo Kwanza..na kwa kuwa karibu watu wetu 80% wanategemea kilimo..na kwa kuwa Ukiinua Kilimo obviously utakuwa umeinua Uchumi wa Mtanzania..Je? Kwa karibu miaka mitano tangu hii Kauli Mbiu ilipoanzishwa nini Mafaniko yake na nini kiwango cha Utekelezaji wake??
 
zomba haonekani kujibu kuhusu ahadi za kaka mkubwa

Naona mkku wangu Zomba anaona hiyo mambo haitekelezekei, kama unakumbuka kuna siku Mzee Yusuph Makamba alikiri kuwa alichoahidi Kikwete ni mchezo wa kiasiasa tu sio lazima atekeleze kila kitu, ile ni mbinu ya kupata kura.
 
mh diwani Kimbunga angalia muendelezo wa mtu wako hapo chini. Haahahaaa zomba ameganda kwenye web ya kikwete 2010:

SOURCE ni ile ile Http://www.Kikwete2010.Co.tz/mafanikio/uchumi/

UCHUMI
1. USIMAMIZI WA UCHUMI JUMLA: Ukuaji wa Uchumi Katika kipindi cha miaka minne (2005 – 2009). Uchumi umeendelea kuimarika na Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7.2 kwa mwaka katika kipindi hicho. Ukuaji huu wa uchumi ulichangiwa zaidi na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi katika sekta za: Bidhaa za viwanda; ujenzi; fedha; na mawasiliano na uchukuzi.

2. Pato la Mtanzania; Pato la Mtanzania limekuwa likiongezeka katika kipindi chote cha awamu ya nne kutoka Dola za Kimarekani 392.8 mwaka 2005 hadi dola 525.2 mwaka 2008.

3.Mwenendo wa Riba;
viwango vya riba vimeonesha mwelekeo mzuri hasa

kuanzia mwaka wa fedha 2006/07, ambapo riba kwenye amana za akiba zimekuwa zikiongezeka, wakati riba zinazotozwa kwenye mikopo zimekuwa zikipungua. Katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2009/10 wastani wa

viwango vya riba kwa amana za akiba za muda mfupi (hadi mwaka mmoja)ulikuwa asilimia 8.92 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 5.21 katika mwaka wa fedha 2003/04. Katika kipindi hicho, wastani wa viwango vya riba vilivyotozwa na benki za biashara kwa mikopo ya mwaka mmoja ulipungua hadi asilimia 13.93 kutoka asilimia 15.75. Kutokana na mwelekeo huo wa riba, tofauti kati ya viwango vya riba kwenye amana za mwaka mmoja na viwango vya riba kwenye mikopo ya mwaka mmoja ilishuka kutoka 10.54 mwaka 2003/04 hadi 5.01mwaka 2009/10, sawa na kushuka kwa asilimia 47.5.

4. Biashara ya Bidhaa Nje; Mauzo ya bidhaa nje yaliongezeka kwa asilimia 3.2 hadi kufikia dola za Kimarekani 2,697.6 milioni mwezi Novemba 2009. Ongezeko hilo lilichangiwa na mauzo ya dhahabu kwa asilimia 9.0 hadi kufikia dola 1,023.8 milioni, tumbaku kwa asilimia 35.3 hadi kufikia dola 151.4. Aidha, mauzo ya kahawa nje yaliongezeka hadi kufikia dola 117.2 milioni, sawa na asilimia 29.0.

5.MAPATO YA NDANI; Katika kipindi cha miaka minne, Wizara ya Fedha na Uchumi, kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanya marekebisho ya mifumo na viwango vya baadhi ya kodi. Hatua hii imesaidia kuweka mazingira mazuri zaidi ya uzalishaji kurahisisha ukusanyaji wa kodi. Aidha, wigo wa kodi umeongezeka katika kipindi hicho.

6.KUWEZESHA UPATIKANAJI WA MIKOPO; Mikopo iliyotolewa na mabenki kwa sekta binafsi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi iliongezeka kutoka shilingi bilioni 1,571.0 mwezi Desemba 2005 hadi shilingi bilioni 4,710.2 mwezi Juni 2009, sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 34.5 kwa mwaka. Mwezi Oktoba 2009 mikopo hiyo ilikuwa imefikia shilingi bilioni 4,836.0. Aidha, wastani wa riba kwa dhamana zote ilishuka kutoka asilimia 16.4,

7.KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI; Mifuko ya Dhamana ya Mikopo (Credit Guarantee Scheme): Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dhamana wa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME Credit Guarantee Scheme) ambao unaratibiwa na Benki Kuu kumeboresha mazingira ya wenye mitaji midogo na ya kati waweze kupata mikopo kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha. Tangu mfuko huu uanzishwe, jumla ya SMEs 48 zimepata udhamini wa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 3.054. Kati ya wajasiliamali hao, sekta ya uzalishiji inaongoza ikifuatiwa na sekta za ujenzi na kilimo. Ili kuleta ufanisi zaidi, mwaka huu Serikali imetenga jumla ya Shilingi bilioni 10 kuongeza mtaji wa mfuko wa wajasiliamali wadogo na wa kati. Kuongeza fedha katika Mfuko wa Uwezeshaji Kiuchumi wa wajasiriamali wadogo (Mfuko wa JK) kiasi cha Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB. ilitoa kiasi cha Shilingi bilioni 10.5 kupitia benki ya NMB (Shilingi bilioni 5.25) na CRDB (Shilingi bilioni 5.25). Kiasi hiki kiliwezesha kutolewa kwa mikopo ya Shilingi bilioni 37.17 ikiwa in asilimia 118 ya Shilingi 31.5 zilizotengwa kutolewa na benk hizo mbili.
 
Last edited by a moderator:
Zomba naona anaanza kulala mika yan kweli mtu kama zomba ana sema ahadi zote z kikwete zimetekelezwa, wakati hata Nape hawezi kusema hivyo.

Mungu msamehe zomba
 
Kwenye uchumi kuna hii ya micro na macro. Wachumi wote wanakubaliana kwamba Macro economics ya Tanzania inaenda vizuri lakini inachukua muda kuwa reflected kwenye micro economic.

Naona umeamua kujilipua sasa. ha ha ha ha, ati inachelewa kuwa reflected ha ha ha ha ha,
 
Mpenzi wangu Smile uko mjini kwa kuwa unajitahidi kufanya kazi ili upate kuishi
Hata hivyo ukichanganya kodi na makato unayokatwa ni balaa
kama sio hayo muda huu ungekuwa unaendesha na wewe liV8 lako mjini ututimulie vumbi
ivo ivo kaka nifanyeje nashukuru kwa yote
 
Ahadi zote za Rais zimetekelezwa sioni hata moja ambayo haijatekelezwa kwa hatua fulani au nyingine.

Kama kuna mtu ana ahadi ambayo haijatekelezwa aainisha hapa. naona Matola kaweka list ya vitu 69, ambayo ni kidogo sana kutokana na ahadi za Rais. Kikwete anatekeleza mengi sana zaidi ya ha yo 69.

Wengi hawaelewi kuwa ahadi ya Rais ni agizo kwa watendaji, sasa hesabu wilaya zote na kila wilaya imeahidiwa na zote zinatekelezwa.

Sioni hata moja amabyo haitekelezwi mpaka sasa, jee kuna anaeijuwa?

Kuna zingine zimekuwa ni World Record, mfano alipoahidi chuo Kikuu Dodoma, kilichukuwa exactly miaka miwili kuanza kuchukuwa wanafunzi toka kuahidiwa.
aiseeeeeeeee wakuu zomba atakuwa mgonjwa au hajui analoliandika......

Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera

Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora

sio mbali ahadi mbili tu hizo...wakuu nimpe jina gani mr dr jk? mlaghai? laa hasha halitoshi....

 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Back
Top Bottom