Mjadala: Magari ya viongozi wetu na dhana ya kubana matumizi

Serikali za kiafrika ni extravagant.
Wanaingia unnecessary expenses.
Mleta mada nakuunga mkono asilimia mia.
Kuna gari comfortable na AWD ambazo zina pita popote pale.
Njia mbaya isiwe kisingizio kwa hawa mabwana kutumia magari ya gharama kiasi hiki.
Na kupita sehemu mbaya ni uwezo wa dereva.
Barabara yaweza kua mbaya lakini mtu mwenye vitz akapita na yule mwenye shangingi akakwama.
 
Hizi Mkuu zinaweza kukatwa kinyemela kisha Wabunge wa MACCM kupenyezewa pembeni ili waendelee kulifanya Bunge kama kitengo cha MACCM. Kumbuka rushwa ya milioni 10 kwa kila mbunge wa MACCM mwezi October 2016.
Aliyezoea vya kunyonga vyakuchinja hawaviwezi, hawa ndugu zetu wengi wao ni wafanya biashara, kwa hiyo hawakwenda pale kutetea masilahi ya wananchi walienda mjengoni ili kufanikisha mipango yao ya biashara haramu, mfano hivi mbunge wa morogoro mjini alifuata nini bungeni, mchungaji lwakatale anatafuta nini bungeni kama tu muumini maskini ambaye hajui atakula nini kesho aliyetoka mbagara charambe au bunju analazimishwa kutoa kiwango cha chini elfu kumi ili aombewe aende mbinguni huku mama wa watu anamiliki mashule tanzania nzima, ana mahekalu mbezi beach na vingine.
Angalau naona wabunge wa upinzani angalau wanawakumbuka wananchi wao angalau kwa kupiga kelele.
 

Haujaambiwa atumie pesa yake. ila asifuje pesa zisizo zake.
Upuuzi ni kutumia mali za umma kama hakuna kesho. wakati unaowatawala ni maskini wa kutupwa.
Mifano mliyopewa ya viongozi wanaotumia magari ya gharama nafuu relative to uchumi wao iwe chachu ya nyie kujitazama mlipo. sio mnataka kutimiza ndoto zenu za utotoni wakati mko vijijini kwa kutumia fedha za umma.

Kuhusu kutokutumia magari kwenda ofisini hilo sio tatizo, zipo nchi viongozi wanatumia baiskeli kwenda makazini, na uchumi wao uko juu kuliko wa kwetu.

Narudia tena, ni USHAMBA tu ndio unawageuza viongozi kuwa Pimps in the middle of poverty.
 
Kikubwa na kinachosikitisha ni kwamba haya Mahari ni kama vile wanajinunulia wao..sababu yanapoharibika vitu vidogo tu huwa hayatengenezwi na yakitengenezwa basi ni kwa gharama kubwa sana kupitia michakato mirefu na yenye utatanishi...kubwa zaidi magari haya huuzwa bei ya chini sana kwa wao kwa wao eti kwa kisingizio kuwa yamekufa!
 

Ulimbukeni uliopitiliza.
Unajua siku zote maskini akipata huwa ni patashika. Mtu anataka miaka 30-40 ya kupigika kwenye umasikini aimalizie hasira zote kwenye miaka 5-10 ya uongozi wa umma.

huwezi justify kununua gari la milioni 200 wakati nchi masikini ya kutupwa na kuna wajawazito wanalala chini. fix your problems first then start the grandiose.
 
Bado huzingatii Hali ya miundombinu ya TZ iliyopo. Wote tunatamani ingekua hivyo ila uhalisia unakataa. Nje wanatumia baiskeli kwenda kazini kama PM wa Netherlands sababu miundombinu inaruhusu wakati TZ bado. Matumizi ya haya magari haimaanishi jitihada za kuboresha miundombinu zimesimama, until then haya magari yataendelea kutumika.
 
Reactions: SDG
Kinachomshinda waziri kutoka masaki hadi posta kwa baiskeli ni kitu gani? acha kuandika pumba.
 

Nipe justification ya Spika kutumia S class 500 ku-commute kati ya Uzunguni-Bungeni-Uzunguni. Au PM kutumia S class 500 au LC 200 ku-commute kati ya home and office. Ama VP kutumia GL class ya mwaka 2015 ku-commute home and office.

Kwani wakitumia VW Passat kuna shida gani kwa hizi home and office commuting?
 
Reactions: SDG
Umeshawahi kutafakari,ukiwa na Suzuki grande au hiyo RAV 4 unayoizungumzia,unaweza kwenda vijiji vingapi ambavyo barabara zake asilimia 80 ni rough roads,na mara ngapi ili hiyo gari angalau iweze kuishi miaka 5?Hizo gari kama Landcruiser V8 kiuhalisia ni gari ngumu sana,kwa hali ya barabara za vijijini ukipeleka gari kama Rav4,Suzuki,Xtrail,Klugger na gari za mtindo huo maisha yake yatakuwa mafupi sana.
 
ni hivi hizi gari mazingira zinapita mfano kuna jamaa angu huwa anapeleka watu wa serikalini vijijin huko kigoma sehemu ina matope gar yenye four wheel peke yake haipiti kwa hiyo haya ma rav4 hayawezi kwenda huko litakufa siku moja imagine cruiser 200 mkonge inapigwa gia arusha kigoma siku moja kesho yake ni matope tu barabara mbovu hatar hapo ndani ina watu saba hata 109 ikakwama sembuse rav4?? acheni tu watumie hizo gari
 
Ni dhana nzima ya 'Ruling by Intimidation' Kwa dhana hii, kiongozi(soma mtawala kikwetu) lazima azungukwe na vitu vya ghali zaidi kuliko watawaliwa ndipo mtawala huyo aweze kuheshimiwa.
Kwa mfano, mkuu wa mkoa atawezaje kumtiisha raia kama gari ya ofisi yake ni Grand Vitara wakati ya huyo raia ni V 8?
Kwa hiyo magari ya gharama, makao ya kifahari, mavazi ya bei mbaya, wanawake warembo n.k ni nyenzo muhimu kwa watawala!
 

Kwahiyo hili suala linatakiwa kijadiliwa na upinzani?
 
Reactions: SDG
Mkuu hicho kichwa cha habari kimenikumbusha dereva wa mkurugenzi anayelala na gari la serikali tabata aamke nalo asubuhi kumchukua boss bunju ili ampeleke kazini posta.

Kwetu kuna mambo huwa sijui kwanini hayaingizwi kwenye vitabu vya Guiness.
Na mbaya zaidi wanatumia hayohayo magari yakuwabebea wakurugenzi au maafisa utumishi kuchukulia wake za watu au mademu za watu,inauma.
 
Reactions: SDG
Kwahiyo hili suala linatakiwa kijadiliwa na upinzani?
Wapinzani wanajukumu la kuonyesha vile watakavyoishi ikitokea wametawala leo.
Sasa umesimama kwenye vx unawaambia watu nikiwa madarakani nitauza haya mavx yote watoto wapate mikopo ya Shule. Hili ni kuwadharau na kuwaona hamnazo wanaokusikiliza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…