Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Haueleweki hata unachotaka kutuambia, mara unataka kumuombea baba yako mara aende akirudi ndio utoe ushuhuda, hivi ni lini babu wa Loliondo aliwahi kujitangaza kwamba yeye ni mungu? wewe huna cha ulokole wowote, ni mtu tu ambaye umeshakuwa brain washed na wajanja wachache wanaoishi kwa kutegemea fungu la kumi kwa gia ya ulokole, in short wewe ni mjinga tu kama wajinga wengine.

Mkuu mwambie huyu mungu ni mmoja,awe wa babaake ama wake yeye.Je anaweza kuelezea kwa nini wachungaji au mapdre hubariki kwa maji ya bararaka? Yana kemikali yale? Na kwa dua za waislamu je zinafanyaje kazi? Zinaweza kupimwa zile..ama anaona baba yake kujaribu tiba atapoteza nin? Anaweza kucompare nauli na mateso anayopata?
 
wapendwa wa nchi yetu kama angegundua mzungu zingalitolewa sifa kem kem kama jenerali anahitaji kupewa kikombe aje kwa babu kwani kila mtu anapewa na kikombe tofauti ila cha kuchoteaa babu anatumia hichohicho alichoshika yeye while vingine vinaoshwa na wasaidizi waliopo kipi cha ajabu? akumbuke alivyo kuwa mwkt ccm kili
 
Namuunga mkono jenerali pia wa2 hawakatai babu kutibu bt masharti anayotoa babu ni ya kitapeli na cyaki mungu ki ufupi
BABU + 500 = DECI MPYA
 
Huu ULIMWENGU nao umetoka wapi?

Huyu pia anahitaji tiba ya babu maana mawazo haya ni ya karne ya 10.

Lengo la huyu ULUMWENGU ni kuuza gazeti tu.
 
Hivi mtu aikipona ni lazima aanze kujitangaza kama mlivyozoea baadhi ya wanambembwe aka wanasiasa amabo wakitoa msaada ya pipi wanautangazia Umma?, hao wachache ni sample mimi binafsi nimesikia na nimeona watu watano tofauti ambao nilikuwa najua dhahiri wanasumbuliwa na maradhi sugu wameanza kurudisha afya na kwa vinywa vyao kwa nyakati tofauti wamethibitisha kupata nafuu sana. hao ni sample sasa ndugu yangu maggid unataka wakufuate na kukueleza kuwa Maggid sasa nimepona? Amini watu wamepona acha Mbwembwe, unmeshazoe kudanganywa na wanasiasa wewe na watawadanganywa sana!!!
 
Kibohehe unapotumia mobile epuka kureply with quote maana inajaza page na kuwapa wengine tabu kufuatilia hasa thread inapokuwa ndefu
 


Ndugu Zangu,


ABRAKADABRA ni neno lisilo na maana yoyote yenye kueleweka na kuleta mantiki. Mwenye kuongea na kujifanya anafanya vitu vya miujiza na vya kimazingaombwe kimsingi anachofanya ni abrakadabra, hata kama halitamki neno hilo. Ni mambo yasiyo na uthibitisho wa kisayansi na mara nyingi wenye kutenda hudai kuwa  wameoteshwa na kumhusisha Mungu, hivyo basi, huwezi kuthibitisha kisayansi.

Na Watanzania tunaumwa kweli. Tumekuwa wagonjwa wenye kutafuta chochote kile ili tupate nafuu ya maradhi yetu. Na  watalaamu wa tiba ya maradhi yetu wanatugombania. Ndio, ni wagonjwa tunaogombaniwa. Si tumemsikia Askofu fulani wa Kanisa la kule Mwenge, tayari amemshambulia  Babu hadharani. Anatishia kumchukulia  wagonjwa wake! Askofu nae ni  mgonjwa- maradhi yake ni pesa, hatosheki.

Na si tumemsikia  Babu wa Loliondo anavyojisifu na kujitangazia unabii? Anasema; Na kama nilivyokueleza, mimi ni Mchungaji mstaafu lakini pia ni Nabii ambaye naweza kuona maono au ndoto na kuzungumza na Mungu mara kwa mara . Na yote ninayoyatekeleza kama unavyoona ni maagizo ya Mwenyezi Mungu.
Nimefanya kazi za uchungaji tangu mwaka 1967 katika sehemu kadhaa nchini hadi mwaka 1989 nilipohamishiwa katika eneo hilo. Na nimefanya kazi za uchungaji hapa hadi nilipostaafu mwaka 2002

Nilianza kuota maono na kusikia sauti ya Mungu tangu mwaka 1991 ikinieleza kuwa nibaki kuishi eneo hili; kwani Mungu alikuwa anataka kunipa kazi maalumu ambayo kwa wakati huo sikuifahamu ( RAIA MWEMA NA: 176)

Sitatafuna maneno bali kuweka bayana, kuwa hayo ya  Babu wa Loliondo ni abrakadabra. Kwa wajanja neno hili Abrakadabra ni neno la ajabu, neno la miujiza. Kwa kawaida neno hulala, lakini abrakadabra laweza kusimama katika pembe tatu.

Zama hizi, ambapo watu wengi wamekumbwa na hali ya umasikini mkubwa, ujinga na maradhi, kumeibuka manabii wa siku za mwisho. Wenye kunufaika na hofu za wajinga, masikini na wenye maradhi kwa kutumia abrakadabra. Lakini abrakadabra inatumika pia kututoa kwenye kujadili mambo yetu ya msingi.


Manabii hawa wa kujitangaza hufika mahala wakawa na nguvu kiasi cha kuwa na ushawishi mkubwa. Mwandishi Danny Sofe katika kitabu chake; "His Exellency Head Of State" (Mheshimiwa Mkuu wa Nchi) anabainisha hili kwa kumchambua mmoja wa wahusika wakuu katika kitabu hicho. Moses Akaba,


Bwana huyu, Moses Akaba alikuwa Mwalimu na msomi wa uchumi na maarifa ya Biblia. Mwanafunzi mmoja wa shule yake alianguka ghafla na kuzimia. Alipelekwa hospitalini na kudhaniwa kuwa amekufa, mara alizinduka ghafla. Akaelezea kisa chake, kwamba alijikuta akiwa kwenye handaki jembamba na lenye giza. Mwisho wa handaki hilo kulikuwa na mwanga.



Alipoukaribia mwanga alimwona mtu aliyevalia joho jeupe. Mtu huyu alimwambia kuwa Mungu alimtaka arudi tena duniani kwa vile kazi aliyotakiwa kuifanya duniani alikuwa hajaimaliza. Kwamba wazazi wake masikini walimwihitaji.


Kijana huyu aliamini kuwa mtu yule mtakatifu aliyekutana naye kwenye mpaka wa mauti na uhai alikuwa Moses Akaba, mchumi na msomi wa maarifa ya Biblia na ambaye alikuwa mwalimu katika shule ya kijana yule. Baada ya kusikia kauli ya kijana yule, Moses Akaba akajitangaza kuwa nabii, akaanzisha kanisa la Life-After -Life (Maisha Baada ya Maisha.)


Nabii Akaba alikuwa hodari sana wa kulitawala jukwaa na kuzungumza katika hadhara. Akaba alikuwa na mbinu na uwezo mkubwa wa kushawishi. Watu wengi na hasa masikini walijiunga na kanisa lake. Walichanga pesa na vito vyao vya thamani.



Na Watanzania tunazidiwa na WaNigeria tu katika dunia hii katika mambo ya abrakadabra. Na foleni za kwa ' Babu' Loliondo zitapungua mara ile Watanzania watakapoamka kuwa abrakadabra ya ' Babu' ni miyeyusho. Lakini kwa vile bado tunaumwa, basi, tunabadilisha ' hospitali'.



Naam. Hakuna lililo bora kwa mwanadamu kama kuwa na hekima. Kwa mwanadamu, kuelewa jambo hutanguliwa na kutanabahi. Ina maana ya kufikiri kwa umakini na kugundua undani wa mambo. Ni bahati mbaya, kuwa wengi wetu tu wavivu sana wa kutanabahi.


Ndio, tumekuwa ni watu wa kufuata mkumbo wa fikra, hatujipi tabu ya kutanabahi. Jambo hili laweza kuwa na madhara makubwa. Zamani sana alipata kutokea mtabiri wa nyota katika mji mmoja mdogo kule Ulaya.



Huyu alitawatabiria watu wa mji huo , kuwa katika tarehe fulani kungetokea kimbunga kikubwa. Kimbunga hicho kingeangamiza majengo na kuna watu wangepoteza uhai. Salama yao? Ndio, pindi dalili za kuanza kwa kimbunga hicho zingeonekana, basi, wakazi wa mji huo waharakishe kuelekea Kaskazini ya mji huo kuliko na milima.


Jioni moja giza lilianza kuingia katika siku iliyotabiriwa. Ikafika saa tatu za usiku bila kuonekana kwa dalili za kimbunga. Ghafla, bwana mmoja kupitia dirisha lake aliona gari likitoka kwa kasi ya kutimua vumbi kutoka nyumba ya jirani. Bwana yule aliamini kuwa kimbunga hicho sasa kimeingia kwenye mji wao na kwamba jirani yake alikuwa akikimbia na familia yake kuokoa maisha yao.


Bwana yule naye akaamrisha familia yake kuingia ndani ya gari. Naye akaondosha gari lake kwa kasi ya kutimua vumbi kuelekea Kaskazini ya mji. Mwenye nyumba nyingine baada ya kuona gari mbili zikipita kwa kasi nje ya nyumba yake, naye akaamini kimbunga kilichotabiriwa kimewadia. Akabeba familia yake na kutimua vumbi na gari lake. Kuona hivyo, wakazi wa mji huo, mmoja baada ya mwingine, wakaanza kukimbia mji wao kuelekea Kaskazini wakihofia kimbunga. Kijiji kizima kikahama!


Huko walikokimbilia wakaanza kuulizana; Ilikuwaje? Ikabainika, kuwa yule bwana wa kwanza aliyevurumisha gari lake alikuwa amegombana na mkewe, na aliamua kuondoka nyumbani kwake akiendesha gari kwa kasi akiwa na hasira, basi. Na hasira zilipomwisha akajirudia nyumbani kwa mkewe!

Tuna cha kujifunza katika kisa hicho. Si tunaona, kuwa sasa kila mmoja anamzungumzia  Babu wa Loliondo. Wengi wanafunga safari kwenda Loliondo. Hatutumii muda mwingi kujiuliza; Ya kwa  Babu Loliondo yalianzaje? Na je, kama  Babu wa Loliondo ana dawa ya kutibu kansa, kisukari na hata UKIMWI kuna uthibitisho wa Kisayansi?


Na mengine ni rahisi kuyapima hata kwa masikio kujua kama kuna ukweli. Fikiria, maelfu haya ya watu waliopata  Kikombe Cha Babu, kama kungekuwa na watu mia tano tu waliopona, basi, tunashindwaje kuwapata watu ishirini miongoni mwao wa kututhibitishia kisayansi, kuwa walikuwa na maradhi hayo sugu kabla na sasa wamepimwa na hawana tena.


Ni mtazamo wangu, kuwa hii ya kwa  Babu Loliondo ni Abrakadabra nyingine. Serikali ilikuwa haina sababu ya kubabaika katika kulitolea msimamo hili la Loliondo. Msimamo wa awali ulikuwa sahihi kabisa; kusimamisha zoezi la utoaji wa tiba hiyo mpaka Serikali itakapojiridhisha juu ya dawa hiyo kupitia uchunguzi wa kisayansi.


Ndio, Serikali ilipaswa kuueleza umma, kuwa kwa sasa dawa hiyo haitambuliki kisayansi, haijafanyiwa uchunguzi, inahitaji kufanyiwa uchunguzi ili kuhakikisha, sio tu kama inatibu, bali kama ina madhara kwa mwanadamu. Hilo ni jukumu la Serikali katika kulinda usalama wa watu wake. Na huko hakutakuwa kuingilia masuala ya imani za watu.
Maggid
Dar es Salaam.
Jumatatu, Machi 14, 2011
http://mjengwa.blogspot.com
Good comments. Waamshe hao waliolala na kiini macho from Nigeria. Sasa hivi watakuona mpingaji ila badae watakaa kimya. Tutawakumbusha humuX2 JF. Yani hao wanaokubali danganya toto/mazingaombwe nao wanajiita GreatThinkers! kweli kuishi kwingi kuona mengi. Furaha ya kutibiwa HIV/kisukari ingesambaa kila mtaa na mifano hai,lkn sasa utasikia shangazi yake yule kapona,mtoto wa mzee flan kapona Fix fix fix. Halaf wavivu wakufikiria wanatetea wakidai Iman unaingilia. Watu wanajificha kupitia migongo ya dini Amkenii wabongo.
 
kwani hapa mnamzungumzia Maggid yupi? ni yule mwenyewe watoto wazungu wakati yeye ni mweusi kama mjaluo! au ni Maggid yupi huyo? kama ni yule ninaemjuwa mimi mbona akili zake alishazifungia stoo tangu kipindi cha kampeni? sitegemei jipya kutoka kwa mtu huyu.
 
Good comments. Waamshe hao waliolala na kiini macho from Nigeria. Sasa hivi watakuona mpingaji ila badae watakaa kimya. Tutawakumbusha humuX2 JF. Yani hao wanaokubali danganya toto/mazingaombwe nao wanajiita GreatThinkers! kweli kuishi kwingi kuona mengi. Furaha ya kutibiwa HIV/kisukari ingesambaa kila mtaa na mifano hai,lkn sasa utasikia shangazi yake yule kapona,mtoto wa mzee flan kapona Fix fix fix. Halaf wavivu wakufikiria wanatetea wakidai Iman unaingilia. Watu wanajificha kupitia migongo ya dini Amkenii wabongo.

wewe ulieamka mbona uko hapa hapa wakati nchi hii inaibiwa kila kukicha na akina Mkwere & co? akili zako ndogo ndio zinakusumbuwa, unao uhuru wa kutoamini, lakini usiladhimishe watu waamini kile unachoami wewe. mfano kama wewe unaona kuingiliwa kinyume na maumbile nisafi, unataka kutulazimisha na sisi tufate msimamo wako? mshamba kabisa wewe.
 
Jenerali as a thinker may enjoy the right to theoretical analyis. However, I think he should ponder a little more about characterising Babu as a probable exploiter of people's gullibility of the same kind like the DECI crooks. That appears to me to be a stretch. It's hard to imagine in the TZ of today for such a person to maintain himself at such a squalid location and ask for only 500/= and leave transporters and others to make a kill out of it! Collusion with the bloodsuckers? Highly improbable. And, you've never suffered that much as the so-called "victims", Jenerali.
 
Hakuna huu ni shida ya wenzetu mnaingiza mambo yenu ya Udini Hivi mnataka kusema muujiza ni kama ile yakina Shekh Yahya wa majini kila siku huyu ni mtu kaoteshwa na Mungu wetu TENA WATU WANAKUNYWA KWA JINA LA BWANA NA WAMEPONA!!!!!!!!

Jaribuni kuwa mnakubali ukweli ndugu zetu. Mwenzetu kupitia jina la baba kaonyeshwa.:washing:
 
Duh! Kwanini watu mnashindwa kuwagundua walaghai ? Hawa jamaa wanaona babu kawaharibia maslahi yao. . .may be wanafanya kazi angaza na kama angaza hivyo kupoteza ajira.
Hivi umeshaskia m2 kaenda kwa babu na hajapona! Eeh.
 
Namuunga Mkono Ulimwengu 100% .. Kisukari na magonjwa mengine yanatibika na herbs za kawaida pia.. hapo babu si mpingi lakini linapokuja swala zima la HI5 "HIV" .. ni utapeli "nukta"
 
Hivi kweli serikali au respectable medical Drs/group wameshindwa kufanya simple investigation ya hii dawa ili kutoa opinion zao ambazo zitakuwa more based in science /lab? kwanini wasitafute sample ya wagonjwa 50 or any number wawapime in the lab na kuweka records zao then wawapeleke kwa babu kupata kikombe bila kumwambia mtu na wahakikishe wanakuwa chini ya uangalizi,then warudi baada ya muda wawapime tena...may be majibu yanaweza kutupa idea kama kweli hi dawa inaponya au laa,idea ni kuangalia kama kweli hii dawa inaponya na kama kweli kuna mtu amepona hata kama ni 10% itabidi kukaa chini na babu kumwomba kibali ili dawa yake iangaliwe zaidi inavyofanya kazi in scientific ways.....personally siamini mambo ya imani/mungu ndio anaponya hii,kama inaponya ni huo mti anaotumia,dawa zote tunazotumia nyingi zimetengenezwa kutokana na hii miti/plants au chemicals ambazo zinachimbwa ardhini
 
Mbona tutasikia mengi mwaka huu!!. Kama cancer inapona wazungu watajenga airport Loliondo
 
Jenerali anataka kuanzisha mjadala ambao majibu anaweza kuyapata yeye mwenyewe.
Loliondo sio mbali, kwa nini asiende kujionea mwenyewe akiwa kama mtafiti?
What testimony do you want if thousands and thousands of people are scrambleling for KIKOMBE every day!!!
Anaongea kuhusu kutumia kikombe kimoja!! ana uhakika na hayo au ni maneno matupu?
I call upon Jeneraly once again that No research, no right to say
Yaani watu kama nyie ndio tatizo. Jenerali anataka ushahidi wagonjwa wenye proven medical record waliokunywa dawa wakapima wakaonekana wamepona. Sio kutuambia tutizame idadi ya watu wanao miminika kule! Kumbuka mulitoa hoja hii hii kwenye DECI kuwa watu wengi wanavuna! Mwisho mkaumbuka ilipogundulika ni ushetani mtupu! Kuweni makini mnamdhalilisha Mungu
 
Jenerali Ulimwengu ur nt correct .pastor Ambilikile Masapila was nt proud himself in any media bt still visitors are visiting him for his cure. science can nt interfere God will.
 
Good comments. Waamshe hao waliolala na kiini macho from Nigeria. Sasa hivi watakuona mpingaji ila badae watakaa kimya. Tutawakumbusha humuX2 JF. Yani hao wanaokubali danganya toto/mazingaombwe nao wanajiita GreatThinkers! kweli kuishi kwingi kuona mengi. Furaha ya kutibiwa HIV/kisukari ingesambaa kila mtaa na mifano hai,lkn sasa utasikia shangazi yake yule kapona,mtoto wa mzee flan kapona Fix fix fix. Halaf wavivu wakufikiria wanatetea wakidai Iman unaingilia. Watu wanajificha kupitia migongo ya dini Amkenii wabongo.

Mimi binafsi nimepona kisukari baada ya kunywa hii dawa last week. Nilikuwa natumia insulin kabla ya mlo lakini baada ya kunwa hii dawa sijatumia insulin na ninakula vyakula ambavyo hapo mwanzo nilikuwa sigusi kabisa.
 
Back
Top Bottom