Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Wikiliki

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
528
139
Kuna ndugu mmoja (Askofu mstaafu wa K.K.K.T) au maarufu kama Doctor anakaa wilaya ya Loliondo mkoa wa Arusha anatibu magonjwa yote sugu kama Ukimwi, kisukari, magojwa ya moyo, mifupa, ini, figo n.k kwa muda mfupi.

Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali za nchi,uarabuni,ulaya wanamimini. Binafsi kuna mzee wangu alikuwa na kisukari amepona kabisa.

Bei ya dawa ni shilingi mia tano tu.

=================
MISAFARA YA WAGONJWA KATIKA PICHA

PICHAMAGARI.jpg


magariwakinywadawa.jpg


GARILAMANISPAANDANIYAMCHUNGAJI.jpg
 
Maeneo anayoishi ni karibu kabisa na ziwa Natron. Namba ya simu sina na inakuwa ni vigumu kupata watu ni wengi nainachukua adi siku mbili mtu akiwa kwenye foleni ya kupata dawa.
 
Ila haichelewi kuchakachulika/kuchakachuliwa, Mola amsaidie.
 
Kuna ndugu mmoja( Askofu mstaafu wa K.K.K.T) au maarufu kama Doctor anakaa wilaya ya Loliondo mkoa wa Arusha anatibu magonjwa yote sugu kama Ukimwi,kisukari,magojwa ya moyo,mifupa,ini,figo n.k kwa muda mfupi. Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali za nchi,uarabuni,ulaya wanamimini. Binafsi kuna mzee wangu alikuwa na kisukari amepona kabisa. Bei ya dawa ni shilingi mia tano tu.
Ungeziongezea thamani habari hizi kwa kudisclose Jina na contacts za huyo Docta
 
Ni kweli hata mimi kuna ndugu yangu alikuwa na ugonjwa wa kisukari amepona kabisa lakini wakati ule alikuwa akitubu bure kama ameweka hiyo mia tano kaanza hivi karibuni anatumia mizizi na anasema kaonyeshwa na Mungu asaidie watu. Ni kweli watu ni wengi mno
 
Bado kuamini mie, kwani wengi wanatibu magonjwa nyemelezi na kufikiri wametibu ukimwi. Je wizara imethibitisha hilo ?
 
Huyo Askofu hiyo bei ilivyo ndefu, au anatoa hizo dawa/tiba mbinguni? Au hataki tibu watu wengi? Au kwa sababu ni biashara anataka tibu kundi fulani tu? Kweli mbinguni mbali sana............
 
Bado kuamini mie, kwani wengi wanatibu magonjwa nyemelezi na kufikiri wametibu ukimwi. Je wizara imethibitisha hilo ?

Naungana nawe. Sio vema watu kupewa matumaini ya bure hadi hiyo dawa hiyo ya ukimwi ithibitishwe.
.
 
Kuna ndugu mmoja( Askofu mstaafu wa K.K.K.T) au maarufu kama Doctor anakaa wilaya ya Loliondo mkoa wa Arusha anatibu magonjwa yote sugu kama Ukimwi,kisukari,magojwa ya moyo,mifupa,ini,figo n.k kwa muda mfupi. Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali za nchi,uarabuni,ulaya wanamimini. Binafsi kuna mzee wangu alikuwa na kisukari amepona kabisa. Bei ya dawa ni shilingi mia tano tu.

Kama maandiko hapo juu yana chembe ya ukweli basi itakuwa heri kwa wanaadamu. Tuombe Mola
 
Ni habari njema but it lacks authenticity! Hebu reporter jaribu kutafiti na kuleta habari iliyokamilika for wellbeing of the umma! Hizi si zama za kusadikika wala miujiza!
 
Jamani mimi nimefika hadi kwa huyo mzee. Sio askofu mstaafu kama mtoa mada anavyosema bali ni mchungaji mstaafu japokuwa bado anafanya kazi za uchungaji. Anatoa dawa aina moja tu (kikombe kimoja cha chai) kwa magonjwa yote iwe HIV, kisukari, pumu, vidonda vya tumbo na mengineyo. Sijathibitisha HIV lakini pumu na kisukari nimethibitisha watu wakipona. Naamini dawa anayotoa inaweza kuponya kwa sababu watu ni wengi sana wanaenda huko kwa siku (zaidi hata ya 100) na ni gharama kubwa kumfuata, zaidi ya km 300 kutokea Arusha mjini na barabara ni mbaya mno. Je ingekuwa watu hawaponi wangegaramika namna hiyo kumfuata huyo mchungaji ilihali hawana hata ushahidi wa mtu aliyemponya?
 
Ni ndugu zangu wawili wamekwenda huko, ila sijafahamu kama kweli wamepona au la...lakini ni ukweli kuwa watu wengi wanakwenda huko na ni mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiluteri huko Sonjo or something....na mimi nikisikia toka hao nitaweka response yao hapa, hao wote ni waathirika,,,,,,Mungu anaweza kutumia vitu vinyonge vya dunia na kuponya na sio tu sayansi...yote yawezekana kwake ila kwa aaminiye
 
Back
Top Bottom