Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
Leo siku ya jumanne tarehe 10.05.2022 Ndugu Januari Makamba, Waziri wa Nishati akiwa bungeni ametangaza uamuzi wa serikali kutoa ruzuku ya takribani bilioni 100 za kitanzania.
Nikirejea uamuzi wa Waziri Makamba miezi michache iliyopita wa kuondoa tozo ya shilingi 100 kwenye mafuta ulisababisha Serikali kukosa mapato zaidi ya bilioni 100 ikabidi Rais Samia abatilishe nafuu hio na kurudisha tozo hiyo.
Kwa hesabu za haraka haraka ni dhahiri ruzuku ya bilioni 100 huenda isiwe na unafuu wenye tija kwa lita ya mafuta ambayo kwa sasa yanauzwa angalau shilingi 3,200 kwa lita moja kwani wakati Makamba akitangaza nafuu hii itakayoanza tarehe 01.06.2022 pia amesema bei ya mafuta itaendelea kupaa.
Je,ruzuku hii ya bilioni 100 itaweza kumeza ongezeko la bei ya mafuta kiasi cha kuleta ahueni kwa mwananchi? Kimahesabu jibu ni hapana.
Bila Serikali kuwa kali na makini katika usimamizi wa "mnyororo" wa biashara ya mafuta ruzuku hii ni kazi bure.Mnyororo wa biashara ya mafuta unaanzia kwenye ununuzi wa mafuta kutoka ng'ambo hadi kumfikia mtumiaji wa mwisho.Hili ndilo jukumu la msingi kwani ruzuku sio "sustainable".
Serikali ikumbuke kuwa Rais kaahidi wafanyakazi nyongeza ya mshahara sasa kupunguza matumizi ya kawaida (recurrent expenditure) na kutumia kama ruzuku itasababisha kutokuwa na bajeti ya nyongeza ya mshahara.
Nawasilisha.