Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 372,737
- 863,623
Hili ni jambo la kijamii la kimaadili zaidi kuliko kimtazamo... Uhalisia wake ukijikita kwenye mikanganyiko ya jinsia, imani, maadili, heshima, hekima, ustawi wa familia nknk
Ni jambo lenye ukakasi wa aina yake kiasi kwamba ukitoa rai lihalalishwe unaweza kuonekana kituko katika jamii na mtu usiye na maadili... Lakini lazima tubadilike na nyakati, hatuwezi kubaki palepale dunia inabadilika na kila kitu kinabadilika
Hili jambo halina madhara kama kutumia vilevi na madawa ama wizi nk... Ni jambo tu la kimaadili zaidi... Na hata tukilikataa na kulipinga leo bado watu wataendelea kufanya
Biashara ya kuuza ngono... Sio kuuza mwili, sio tafsiri sahihi, kinachouzwa mtu anaondoka nacho, akikitumia na kukiacha hapo hapo, huyo kakikodisha... Hii ni mojawapo ya biashara kongwe zaidi duniani inayowaingia watu kipato kikubwa na kuwapa maisha...
Ngono ni hitaji muhimu na la lazima la kiasili, ngono huleta furaha, afya na nafuu ya msongo wa mawazo... Afya ya akili hujengwa pia ufanyaji wa ngono.... Lakini si kila mmoja anaweza kupata hitaji hili kwa uhuru, kwa uwezo na kwa utashi
Kuna ambao hawawezi kutongoza
Kuna ambao hawana muda wa kutongoza
Kuna ambao hawana hisia kabisa za mapenzi (sio ngono)
Kuna ambao ni wa binafsi na hawawezi kuhudumia mwanamke kila siku
Kuna makundi katika jamii ambayo mazingira yao, muonekano, kipato na utashi huwanyima fursa ya kuwa na wapenzi
Wote hawa katika ujumla wao kimbilio lao ni kwa wale wanaofanya biashara ya ngono maarufu kama machangudoa ama madadapoa... Huko hakuna longolongo ni biashara tu
Lakini vilevile kuhalalisha biashara hii kunaweza kuwa na tija kubwa kwa jamii... Kama vile
. Kuwa na maeneo rasmi yanayotambulika
. Kuwa na vibali na leseni
. Kuwa na wahudumu... Ajira tayari
. Serikali kukusanya mapato
. Kuwa na ulinzi kwa watumiaji na watumiwaji
. Kupimwa afya na kufuata taratibu zote za kiafya...
Nknk
Kuendelea kuiharamisha hii biashara bila kuwa na sheria rasmi ni kuendelea kuinyanyasa jamii, kuikosesha uhuru, kuleta unyanyasaji na kufaidisha kundi fulani la watu kwa mapato haramu
Machangu wanapokamatwa huishia kushtakiwa kwa kosa la uzururaji.. Huwekwa mahabusu na kutakiwa kutoa pesa ili waachiwe... Wengine hutoa eneo la tukio, wengine hutoa wakifikishwa polisi, wengine hutoa baada ya kulala lupango na wale vigego hawatoi mpaka waachiwe huru
Tukiamua kwa dhati tunaweza sasa kuamua kuwa na mjadala huru kuhusu kuhalalisha hii biashara kongwe yenye wateja wengi wa kaliba zote