Mizengo Pinda: Serikali ibadilishe mfumo wa Elimu na Watoto wasiendelee kudanganywa kwamba kuna ajira

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,776
2,000
Waziri Mkuu mstaafu Mzee Mizengo Pinda ameishauri serikali kubadili mfumo wa elimu ili wanafunzi wajikite katika stadi za ufundi na ujasiriamali.

Mzee Pinda ametahadharisha kuwa siyo vema watoto wakaendelea kudanganywa kuwa kuna ajira wakati kiuhalisia ajira ni chache sana.

Pinda alikuwa anafunga kongamano la wawekezaji mkoani Songwe.

Chanzo: ITV habari

My take: Nimeupenda ukweli wa Pinda, msema kweli ni mpenzi wa Mungu!
 

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,275
2,000
Ataambiwa anawashwa lakini ndio ukweli! Uwezo wa kujiajiri uko zaidi kwenye stadi za ufundi na ujasiriamali.

Hatuna vyuo vya ufundi stadi vya kutosha na badala yake wameamua kufanya mambo kwa namna rahisi - shule za kata!!

Mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne na yule wa cha sita na hawakuendelea na masomo - wote sio wataalamu wa chochote!! Na ajira zao sio za kitaalamu kwa hiyo haziwezi kuwapa kipato kikubwa!
 

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
1,365
2,000
Ziko wapi mkuu? Tatizo wayanzania tunapenda kudanganywa huyu Mh kasema ukweli mchungu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani Waalimu, Wauguzi, Madaktari, Wataalamu wa Kilimo na Mahakimu wanatosha? Ajira zipo sema watu wameshindwa kuweka mikakati mizuri.

Mfano kama shule licha ya kuwa na waalimu tu inabidi iwe na watu wafuatao.
-mtaalam wa afya
-karani
-walinzi
-mtunza stoo
-wapishi
Je hawa wote ajira zao zikiwa rasmi kwa shule za serikali zote zilizopo uoni utakuwa umetengeneza fursa za ajira kwa mamia wa vijana Tanzania.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,711
2,000
Ziko wapi mkuu? Tatizo wayanzania tunapenda kudanganywa huyu Mh kasema ukweli mchungu

Sent using Jamii Forums mobile app
Pinda mwenyewe alikuwa Waziri Mkuu kwa miaka mingapi na kafanya nini kuweka hili sawa?

Hili jambo si jipya, tangu miaka ya sitini na sabini Mwalimu Nyerere aliliandika sana katika vitabu vyake.Nyerere alisisitiza sana elimu iwe practical, isiwe nadharia tu.Mfano, alisisitiza sana umuhimu wa elimu ya ufundi na elimu ya kilimo. Elimu ambayo ni rahisi kumpa mtu uwezo wa kujiajiri.

Sasa Pinda kafanya kipi katika Uwaziri Mkuu wake?
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,814
2,000
Mzee Pinda aka the Former prime minister of Tanzania and he served in different serious positions to this nation..

Mzee Pinda ajira haziji bahati mbaya bali hutengenezwa ndio maana ya kuwa na think tanks na Serikali, Tanzania bado ni Taifa masikini linalohitaji sana nguvu kazi litoke hapa, population ya watu zaidi ya 50milions na eneo lililobarikiwa rasirimali za kutosha ni silaha zinazohitaji kutumiwa kwa upana..

Ulaya na America wanatatizo la ajira kutokana na maendeleo ya teknolojia hivyo kazi nyingi za binadamu zimechukuliwa na robots na mifumo ni automations..sasa huku Africa tunashindwaje kutengeneza mamilioni ya ajira ilihali bado tuko kwenye mechanical world, viongozi wetu wanatakiwa wafikiri ndio maana ya kuwa viongozi na sio blah blah..
 

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
12,976
2,000
Tuweke uko kwenye nafasi za kisiasa,isizidi miaka kumi!Yaani kama ni ubunge basi ni miaka 10 mwisho,ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa hivyo hivyo!Nafasi za teuzi pia mtu asihudumu zaidi ya miaka 10,ili basi na wao wakishapata mitaji waende kujiajiri na wapishe wengine nao watafute!Ndio,siasani ni sehemu nzuri sana kutafuta mtaji!
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,814
2,000
Mwambieni Mzee Pinda atoe solution na sio kupiga blah blah, kama mtu aliyewahi kuwa kiongozi mkubwa anapaswa kufikiri mara 1000 ya hapo aje na solution anayoweza hata kushauri taasisi za maamuzi..Tanzania bado haijawa nchi yakuwa na tatizo la ajira watu wasikimbie majukumi wafikiri na kuzitengeneza hizo ajira..
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,814
2,000
Mapoli, Ardhi yenye rutuba, ardhi yenye madini chini, mito, maziwa, bahari, mbuga za wanyama nk hivi vyote vinahitaji fikra pana ili kutanua uwanja na mwisho kutoa mamilioni ya ajira..

Mifuko ya hifadhi ya jamii inunue meli za uvuvi bahari kuu, izikodishe kwa private companies, ijenge viwanda vya kuprocess samaki ivikodishe kwa private companies, samaki fresh and processed wauzwe worldwide as Tanzania product..

Serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara itafute wawekezaji wajenge viwanda vya juice vikubwa Tanga na Pwani, wananchi wawezeshwe walime kibepari kufeed hivyo viwanda through out the year..the same to mbogamboga, maua nk..

Vitu vingi sana aisee Serikali inaweza kuvipromote na kusimamia na uwanja ukawa mkubwa kiasi cha kutengeneza mamilioni ya ajira..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom