Mizengo Pinda declares assets in anti-graft drive

Nina imani na Pinda ...upande wa uadilifu...sio ajabu watu wa usalama ..walitaka tangu mwanzo mwaka 2005 awe waziri mkuu...ili kuondoa nguvu ya mtandao serikalini,kwani ni ukweli uliowazi kuwa Kikwete amelazimika kuchagua pinda baada ya things ku fall apart .....
deal la mwanzo la kikwete kuaminiwa kupewa urais lilikuwa kumbakisha SHEIN na kumpa Pinda uwaziri mkuu...
uhusiano wa kikwete ,na pinda na shein ni wa kikazi zaidi ....kwani hawa si marafiki zake wa kukaa vikao jioni...na ndio maana bado kuna malalamiko ndani ya circles kuwa JK hupata ushauri wa uendeshaji serikali kwa watu wengine wasiokuwa barazani kama Lowassa na kwa mawaziri ambao nimtandao kama sofia simba,shukuru,ghasia etc...its like baadhi ya ajenda za baraza la mawaziri hujadiliwa kwanza kweye kitchen cabinet ....kupata msimamo wa kuingilia barazani au hata kwenye vikao vya NEC na cc Mtindo ndio huo huo!!!

Upande wa pinda na shein tunakubali uadilifu wao lakini tunataka waongeze juhudi kuhakikisha serikali hayumbi!!!

Nitapenda kuona kama JK nae atatangaza mali ....katika siku za karibuni amejilimbikizia mali sana.....inawezekana kwenye campagne donations alibakiwa na pesa nyingi sana baada ya Pesa za EPA kutumika ni wazi ile michango ya marafiki zake na nje kama ule wa IRAN ...ilibakia kwenye personal account zake...ukizingatia hana wasi wasi na gharma za mwaka huu......inabidi sheria ya uchaguzi iweke hili wazi ....wagombea waweke wazi pesa zao za kampeni.......na baada ya kampeni wachapishe hesabu zao...na kwa aliyeshinda ...atakiwe kupeleka fedha zake za kampeni zilizobaki kwenye mashirika ya misaada...nadhani hata marekani wanafanya hivyo ...Obama alibakiwa na pesa nyingi na ali declare!!

Nakubaliana na mzungumzo yako. Pia Pinda ametangaza kutogombea tena ubunge, means hautaki tena Uwaziri Mkuu. WHY? Think Big.
 
How does he manage to pay tution fees for his two children who are studying at a foreign college which costs him more than U.S.$ 40,000 per annum? najua atasema allowances. Uzuri wa mkakasi......
 
1. Sina mashaka na ujamaa na kujivunia umaskini kwa PM wetu, surely kama hivyo ndivyo alivyo navyo tu hastahili kuwa PM wa Tanzania... Tunataka mtu anayechukia umaskini kwa vitendo, na mtu wa namna hiyo lazima angekuwa better than utajiri huo mdogo saana aliosema... kwangu ni maskitiko... yale yale kuona umaskini ni jambo la kujivunia.

2. Tanzania kweli tunamatatizo, account balance sio kigezo cha kumpima mtu ana kiasi gani, kwa kuwa ni record ambayo ni valid au invalid wakati wowote. Kwa taarifa kwa wadau hata fisadai mkubwa kabisa anaweza ku-withdraw hela zote na accounts ikabakiwa na TZS 10. au even overdraft, hivyo aidha kigezo ingekuwa kuona bank statement ya miaka mitano ya nyuma au kuangalia kiasi kikubwa kabisa kilichoingizwa kwenye account au kutolewa na sio balance.
 
- Vipi imeshafanyika facts finding kwamba maneno yake yote ni kweli? Kwani amekua mbunge kwa muda gani? Si kila mwisho wa miaka mitano ya ubunge kila mbunge hupewa gari jipya au lingine,

- I mean nina heshima sana na PM wa sasa as a person, sina uhakika sana na uongozi wake, lakini hii habari nina wasi wasi haijakaa sawa na ingawa pia siamini kwamba ni mwizi kama wale tuliowazoea.

Respect.

FMEs!

Wakuu, ninaijua nyumba yake ya Dodoma, Pia ya MPanda. nimebahatika kuijua familia ya huyu jamaa kwa hiyo mambo aliyosema nina uhakika nayo 90%

Labda hapo kibaoni kwa babu yake ndiyo sijafika. Ni Mkweli.
 
HAPA swala la msingi ni moja awe na ujasiri wakutuambia alicchochuma mara baada ya uwaziri mkuu wake kukoma, otherwise asante kwa ujasiri.
 
Mwanakijiji

Mkuu endelea kuota JK aseme mali zake? Hapo ndio utaona wanavyoruka viunzi, tunasubiri kama watajaza fomu. Hivi ni kwa nini hawajazi zile fomu wakati kuna sheria zinazowabana wafanye hivyo.

Hili fagio naona ingewaangukia hata wabunge wataje za kwao maana nao ni wawakirishi wa wananchi, kwa hiyo ni muhimu wananchi wajue viongozi wao wanamiliki mali gani na wamezipata lini na kipato kipi.
 
Tuseme kweli jamani,pinda si mla rushwa kama akina Lowassa na wenzake,maana kwa nafasi alizoshikiria tangu 1974 angekuwa ni mmoja wa matajiri hapa bongo. Maana makampuni mengi ya wawekezaji hapa nchini yana mikono ya wakubwa wa siasa.
 
Mr Pinda also explained that he was possessing three ‘simple' houses in Dodoma, Mpanda and Dar es Salaam.

"I've one in Dodoma which I built through loans, another one in Mpanda town which I built using my little savings and a small one in my farm. he elaborated.

According to the premier, he is planning to build another house at his home village (Kibaoni), to accommodate his delegation during his visits to the village.

"I've been staying in my grandfather's houses in all years while I'm at Kibaoni, but due to my current capacity and security concerns associated with it, I can no longer stay there. I'll build another one to accommodate us especially my delegation," said the Prime Minister.

Hapo penye Red, ina maana anajenga nyumba kwa ajili ya kukaa hadi mwisho wa mwaka huu au ameshajihakikishia kuendelea kuwa PM for the next term??

Kama ana mali hizo tu yeye na familia yake yote, na hakuna zingine zilizo kwa jina la mke, mtoto, au kampuni basi safi.
 
Hapo penye Red, ina maana anajenga nyumba kwa ajili ya kukaa hadi mwisho wa mwaka huu au ameshajihakikishia kuendelea kuwa PM for the next term??

Kama ana mali hizo tu yeye na familia yake yote, na hakuna zingine zilizo kwa jina la mke, mtoto, au kampuni basi safi.

Kama sikosei mawaziri wakuu wastaafu wanapewa ulinzi, dereva na mhudumu ata baada ya kustaafu. Kwa hiyo nadhani anamaanisha baada ya kustaafu, kwa sasa akienda uko kwao anafikia Ikulu ndogo.
 
He is not saying the thruth. Anasema ana akiba benki kati ya 20 - 25 million. Hana uhakika na akiba yake. inawezekana ni zaidi ya hiyo aliyotaja.
Tusubiri tuone mwisho wa haya yote.
 
NAJISIKIA FURAHA SANA KUONA WAZIRI MKUU ANAKUWA FREE KUSEMA MALI ZAKE, JAMAN NILAZIMA TUKUBALI WAZIR MKUU ANATISHA KTK KAZI ZAKE ANAFANYA MAMBO YAKE KIMYA KIMYA NA HII NIKWASABABU NCHI IMECHAFULIWA NA MDUDU RUSHWA. KAMA UNATAKA KUJUWA UKWELI TUMPE UWAZIR KWA MARA YA PILI NA IKIMPENDEZA MUNGU AWE RAIS HAKIKA TAIFA LITAKUWA NA MAENDELEO, JK KWA SASA KAMFUNGA SPËED GAVANA ILA WEWE NGOJA TEM YA PIL KILA MTU ATAFUNGUA MDOMO WAZI, PINDA ATALINYO OSHA HILI TAIFA NA KAMA SII PINDA TUNAYE MAGUFULI, SPIKA SITA, PINDA WEL NATARAJIA TAIFA JIPYA NA KWA BAHAT MBAYA MAFISAD WATAKUFA KWA PRESHA, FEDHA ZAO ZITAKUWA KAMA PAMBA NA KUPEPERUKA NAKURUD KTK MIKONO YA SERIKAL, NALIPENDA TAIFA LANGU NA NINA IMAN HILI NI TAIFA KUBWA KULIKO YOTE DUNIAN, LENYE WATU WENYE AKILI ZA AJABU. God bless Tanzania and God bless u Tanzanian. Thank u.
 
Hivi inawezekana waziri mkuu aamue kutangaza mali zake bila kui brief ikulu?Utakuta ana kabla hajamua kufanya hivyo alishamweleza Rais!Ili wengine wafuate na haswa na mawaziri waliopo sasa, tunaelekea uchaguzi mkuu janja imeshaanza!
 
Back
Top Bottom