Mizengo Pinda declares assets in anti-graft drive

Habari wadau wenzangu……nimekua nikitafakari kwa makini sana mustakabali wa nchi hii, ilipotoka, ilipo na inapoelekea…mchanganyiko na mvurugiko wa mambo ulivyo sasa, bado hatujielewi kabisa..CCM kama chama kimetuangusha kwa kiasi kikubwa sana, however kuna watu ndani ya CCM ambao wanaweza….namuona Prime Minister Pinda kama mtu wa namna hiyo, ingawa kwa kiasi kikubwa anakosa support toka ndani, whether from His Excellency or the Cabinet…..kwa maoni yangu therefore, a man is the right Candidate for CCM in 2015 elections….he is mean, open, simple, humble………….and most important..Nyerererised much enough, both historically and ‘intelligenti-cally'-Tanzania anaijua in and out………he is the right person to save this country…NAWAKILISHA!!
 
Amechoka sana ukifika wakati huo, kiafya na kiakili

Besides uwezo wake ni mdogo kiakili na hata kiuchambuzi choka mbaya amesoma sheria hajui sheria, anabaki analia bungeni (anataka symphathy), swala makoti na matumizi ya serikali ..sentesi hizo tu zinaonyesha uwezo wake ni mdogo..therefore ni below standard

Hatuhitaji 2015 mtu ambaye computer hajawahi kutumia.
 
Tunahitaji kijana ambaye umri wake ni chini ya miaka 45 na zaidi... mwenye sifa kama za Mheshimiwa Pinda, anayechanganua maswala kama Mheshimiwa Zitto, asiyependa rushwa kama Mheshimiwa Sila, mwenye sera za kidiplomasia kama za Mheshimiwa Raisi wa jamhuri yetu Kikwete, mchapa kazi kama Mheshimiwa Magufuli, mwenye vision kama ya Mwalimu Nyerere na charismatic kama raisi Obama.

Kazi kweli kweli
 
Wakuu, ninaijua nyumba yake ya Dodoma, Pia ya MPanda. nimebahatika kuijua familia ya huyu jamaa kwa hiyo mambo aliyosema nina uhakika nayo 90%

Labda hapo kibaoni kwa babu yake ndiyo sijafika. Ni Mkweli.

inaonekana unamjua kidogo, unaweza ukatusaidia kujua matumizi yake makuu, hasa baada ya kuwa PM, maana hanunui hata maji, kila kitu tunamlipia...
 
Wabunge wa upinzani waoneshe mfano siyo kutangaza tu bali kuweka fomu hadharani labda wa CCM watafuata..
 
Baada ya vipindi viwili vya Uwaziri mkuu napo tutaomba atangaze ana ng'atuka akiwa amevuna nn? mwanzoni iwa wanakuwa maskini kama hivi mwishoni mmh
 
Hata hivyo kitendo alichofanya Pinda, kiwe ni cha hiyari au shinikizo ni cha busara na ujasiri mkubwa. Waliobaki Rais, Makamu wa Rais, mawaziri, Spika, Jaji mkuu, mwanasheria mkuu, makatibu wakuu, wakurugenzi wakuu wa kuteuliwa na rais hata kama hawalazimiki, basi wapime hili na watumie busara yao!

Sisi wananchi tutawajaji kwa hiyo busara.
 
Nawaomba "waliojipambanua" na kupinga ufisadi wafuate nyayo za WM wetu ili kutuongezea imani zaidi kwao.
 
Tunahitaji kijana ambaye umri wake ni chini ya miaka 45 na zaidi... mwenye sifa kama za Mheshimiwa Pinda, anayechanganua maswala kama Mheshimiwa Zitto, asiyependa rushwa kama Mheshimiwa Sila, mwenye sera za kidiplomasia kama za Mheshimiwa Raisi wa jamhuri yetu Kikwete, mchapa kazi kama Mheshimiwa Magufuli, mwenye vision kama ya Mwalimu Nyerere na charismatic kama raisi Obama.

Kazi kweli kweli

Na mwenye kujiheshimu kama........najaribu kumtafuta mfano wake..
 
EMPLOYMENT HISTORY Company Name Position From DateTo Date
United Republic of Tanzania Prime Minister 2/9/2008
Prime Minister's Office - Regional Admin.& Local Governments.Minister20062/8/2008
Prime Minister's Office - Regional Admin.& Local Governments.Deputy Minister2000/2005
State HouseClerk to the Cabinet1996/2000
State HouseAssistant Private Secretary to the President1982/1992State HouseSecurity Officer19781982

Ministry of JusticeState Attorney1974/1978

source:http://www.parliament.go.tz/bunge/mpcv.php?vpkey=39

inaonekana Mh. Waziri Mkuu ni muumini mkuu wa ideology ya ujamaa wa kiafrika kwa kutojitajirisha kwa mgongo wa ofisi ya umma au kufanya makeke ya kuwa na magari kibao binafsi wakati wananchi waliokupa dhamana ya uongozi wanaishi kwa kutumia chini ya dola mmoja ya kimarekani kwa siku.

Huyu bwana katika kutangaza mali zake katupiga dongo la macho kwani alipokuwa TAMISEMI, yeye na Ngwillizi pamoja na Ngombale kabla yao wote walitengeneza [read kuhongwa] fedha nyingi kutoka kwenye halmashauri; kama mnabisha waulizeni MADED wastaafu watawapasha!!
 
Habari wadau wenzangu……nimekua nikitafakari kwa makini sana mustakabali wa nchi hii, ilipotoka, ilipo na inapoelekea…mchanganyiko na mvurugiko wa mambo ulivyo sasa, bado hatujielewi kabisa..CCM kama chama kimetuangusha kwa kiasi kikubwa sana, however kuna watu ndani ya CCM ambao wanaweza….namuona Prime Minister Pinda kama mtu wa namna hiyo, ingawa kwa kiasi kikubwa anakosa support toka ndani, whether from His Excellency or the Cabinet…..kwa maoni yangu therefore, a man is the right Candidate for CCM in 2015 elections….he is mean, open, simple, humble………….and most important..Nyerererised much enough, both historically and ‘intelligenti-cally’-Tanzania anaijua in and out………he is the right person to save this country…NAWAKILISHA!!

Nitajie mambo makubwa aliyoyafanya tangu awe waziri mkuu yaliyokushawishi kumwona awe rais watu mwaka 2015, ondoa la jana kutangaza mali zake.
 
Tunahitaji rais anayeweza ku-dare making decisions openly, sio mtu asiye na maamuzi au asiyekamilisha kazi

daraja la kigamboni tu lina miaka 5, waziri mkuu wa ukweli angeshahakikisha linajengwa
utendaji wa wizara za serikali uko slow... nani kiongozi wake? Pinda
Ufuatiliaji wa haki za wanyonge (against ufisadi) ...nani incharge??
 
Mr Pinda wondered why high ranking government officials were amassing wealth, while their costs were borne by the government. The prime minister was optimistic that he would make good saving now as most, if not all, of his costs were borne by the government.

Hii fact ilipashwa kuzingatiwa na kufuatwa kwa ''dhati'' na kila kiongozi wa umma...hasa ngazi za juu.......! Costs zote zinabebwa na serikali aka Kodi za wananchi, kwanini kujilimbikizia mali? for what?
 
Wabunge wa upinzani waoneshe mfano siyo kutangaza tu bali kuweka fomu hadharani labda wa CCM watafuata..

I bet to differ,

Hao wabunge wa upinzani walikuwa wapi tangu miaka hiyo mbona hawakufanya?... in short yeyote atakayetangaza baada ya hapa simpi credit yoyote!

Hata kwa PM na-reserve credit by 95%... nani alimwambia kutangaza mali zako unatangaza katikati ya muhula...

Genuine ni kutangaza wakati wa kuingia na wakati wakutoka... mpaka sasa hakuna ambaye amefanya hivyo.

---------------------------->Uchaguuuuuuuuuuuuuuuuzzzzzziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Huyu bwana katika kutangaza mali zake katupiga dongo la macho kwani alipokuwa TAMISEMI, yeye na Ngwillizi pamoja na Ngombale kabla yao wote walitengeneza [read kuhongwa] fedha nyingi kutoka kwenye halmashauri; kama mnabisha waulizeni MADED wastaafu watawapasha!!
Haka kaugonjwa ni ka Cabinet nzima ya Tanzania tangu utawala wa Mzee Ruksa isipokuwa kwa mawaziri wachache sana kama Jackson Makweta. Wengine wote kuzitafuna taasisi zilizo chini ya wizara zao ni kama kawa!
 
Hii fact ilipashwa kuzingatiwa na kufuatwa kwa ''dhati'' na kila kiongozi wa umma...hasa ngazi za juu.......! Costs zote zinabebwa na serikali aka Kodi za wananchi, kwanini kujilimbikizia mali? for what?

Hapana mkuu;

Mr Pinda wondered why high ranking government officials were amassing wealth, while their costs were borne by the government. The prime minister was optimistic that he would make good saving now as most, if not all, of his costs were borne by the government.

This where our PM is wrong, watumishi wa umma wanaruhusiwa kufanya shughuli nyingine halali kujiingizia vipato zaidi... kinachokatazwa ni sema huna mradi wowote alafu ni tajiri wa kupindukia!!!

Tunataka viongozi wenye vision ya "UTAJIRISHO" sio "UONDOA UMASKINI".
 
PM hakutaja mali zake zote kwani alipokuja kuongea na wanabandari (wakati ni Waziri wa Local goverment) waliouziwa quoters za bandari akiwashawishi wakubali kupisha mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi, kwa kinywa chake alitamka kuwa hata yeye kauziwa nyumba ya serikali na amefanya renovation sasa ni gorofa. Mbona amekana hana nyumba Dsm ila kijibanda? au ndio banda lenyewe?
 
Back
Top Bottom