Tumesikia kwamba mh. Pinda -Waziri mkuu wa Tz,kaondoka leo kwenda kutibiwa UK kwa wiki moja.
Nadhani ziara ndefu na wingi wa kazi umemchosha sana,kwani hata mwendo miguu inaonekana sio sahihi kabisa,kwani asitibiwe Muhimbili tu.Wanadai kaenda na mkewe tu,kitu ambacho sio rahisi laziza wasaidizi wawepo.Anyway tunamtakia matibabu mazuri waziri mkuu wetu.
wanajamvi jana niliona katika taarifa ya habari TBC, Waziri Mkuu Pinda ameondoka jana kwenda London kwa ajili ya Uchunguzi wa Kiafya. nini kinamsumbua Mtoto wa Mkulima huyu kiafya mpaka aende London??.au ni issues nyingine!!!!! wenye news mwageni hapa
.Waziri Mkuu Pinda ameondoka jana kwenda London kwa ajili ya Uchunguzi wa Kiafya. nini kinamsumbua Mtoto wa Mkulima huyu kiafya mpaka aende London??.au ni issues nyingine!!!!! wenye news mwageni hapa
.
PM Pinda, ni mtoto wa mkulima kiukweli, haumwi chochote, ila anakwenda kutimiza tuu matakwa ya moja ya stahili zake.
Miongoni mwa stahili za wale viongozi watano wakuu pamoja na wasataafu wa nafasi hizo, ni pamoja na kuchekiwa afya zao nje ya nchi mara moja kila mwaka.
Huduma ambazo wakuu hawa wanapewa kama stahili zao, hawawezi kuzikwepa hata kama wako fit kabisa, lakini lazima wakachekiwe.
Miongoni mwa stahiki za waheshimiwa wabunge, ni pamoja na kupatiwa gari, dereva, ofisi, mwanhalizi wa ofisi na msaidizi. Fedha za huduma zote hizo, hulipwa kwa kila mbunge kwenye mshahara wake. Fanya utafiti utakuta wabunge wengi hawakai kwenye hizo ofisi zilizoandikwa Ofisi ya Mbunge, hivyo fungu la mwangalizi wa ofisi, wanatia ndani, wengi hawana wasaidizi, wanajisaidia wenyewe, fungu wanatia ndani, wengi hawana madereva, wanajiendesha wenyewe, fungu wanatia ndani, ila wabunge wao wakiugua, pia wanatibiwa nje ya nchi.
Mwachieni Pinda, mwana wa mkulima.
Stahili ni stahili na hivyo waliozibuni waliona inafaa, jee unajua kuwa kila rais akisafiri/akifanya ziara au kila alipo, yuko na timu ya watu 21?.kwa nini wasicheki pale muhimbili..au hilo sio kituo cha afya?
wewe ndiye mwenye news, sasa unaomba zipi tena? tujuze basi...wanajamvi jana niliona katika taarifa ya habari TBC, Waziri Mkuu Pinda ameondoka jana kwenda London kwa ajili ya Uchunguzi wa Kiafya. nini kinamsumbua Mtoto wa Mkulima huyu kiafya mpaka aende London??.au ni issues nyingine!!!!! wenye news mwageni hapa
Stahili ni stahili na hivyo waliozibuni waliona inafaa, jee unajua kuwa kila rais akisafiri/akifanya ziara au kila alipo, yuko na timu ya watu 21?.
Unajua kuna mtu kazi yake kubeba sanduku lake la nguo?. Mbona wabebaji wa hoteli wapo?.
Unajua kuna mtu kazi yake kumshauri avae nini au kumsaidia kuvaa?. Kwani mwenyewe hawezi?.
Unajua kuna mtu kazi yake kuonja tuu chakula kabla yeye hajala?
Kuna mbeba speech, siku hizi pia anabeba laptop?.
Unajua kuna mpiga picha?
Unajua kuna mpiga video?
Unajua kuna mwandishi wa habari?
Unajua pia mkurugenzi wake wa Mawasiliano yupo wakati wote? etc etc.
Hivi wote hawa ni rais anayewahitaji ama ni sehemu ya stahili zake?.
Hata kama Mtoto wa mkulima Pinda, angependa achekiwe Muhimbili, stahili inasema atachekiwa nje ya nchi mara moja kila mwaka atake asitake!
Mwacheni jamani mtoto wa Mkulima!.