Mizengo Pinda aenda kutibiwa UK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mizengo Pinda aenda kutibiwa UK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mayolela, May 19, 2010.

 1. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2010
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tumesikia kwamba mh. Pinda -Waziri mkuu wa Tz,kaondoka leo kwenda kutibiwa UK kwa wiki moja.
  Nadhani ziara ndefu na wingi wa kazi umemchosha sana,kwani hata mwendo miguu inaonekana sio sahihi kabisa,kwani asitibiwe Muhimbili tu.Wanadai kaenda na mkewe tu,kitu ambacho sio rahisi laziza wasaidizi wawepo.Anyway tunamtakia matibabu mazuri waziri mkuu wetu.
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huko UK si ajabu akajikuta anatibiwa na daktari mbongo/mtz aliyekimbia maisha magumu tz...hahaha, hapa kwetu hamna hospitali za kuwatibu hawa?, na je, kama wao wanaenda UK sisi tuliowapa kibarua/kura tuende wapi?, iyo ni sawa na baba anachinja jogoo anakula peke yake watoto wanakula mchicha....aibuuuu kwa viogonzi wetu. kwa stail hiyo hawatakuwa hata na mwamko au uchungu kuboresha hospitali zetu au hata kuboresha mishahara ya madaktari wetu ili wasikimbie nchi.
   
 3. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2010
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kweli kero ni nyingi sana,sidhani kama mtoto wa mkulima aliwahi kutibiwa Uk ,zaidi ya M2.Hakika cheo ni dhamana.Katoka kurenew kwao moja kwa moja Uk-maajabu sana.
   
 4. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,994
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Hii ni sababu moja tosha kati ya nyingine 1000 ya kuwanyima kura...ni lini watajua matatizo ya muhimbili kama wenyewe hawatibiwi hapo au wanafunzi kukaa chini kama watoo wao hawasomi kwenye hizo shule..lakini kwasababu atutumii kura yetu vizuri wacha waendelee kula bata
   
 5. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kweny blogu ya Michuzi,alipewa Ukamanda na Kingunge huko Mpanda.
  Naona vumbi limpepiga kiasi cha kwamba asafiri UK kula kuku na kutibiwa.
  Mkumbuke akiwa UK hatibiwa hospitali za serikali(NHS) ,ni binafsi ambazo ni ghali kubwa sana.Na London ndio imekuwa playground ya hawa Viongozi wetu,maana kuna wabongo wababaishaji wengi wanavaa shati za kijani !
  Je unajiuliza mtu anajiita Professor hapo Muhimbili,anatibu watu poor ambao hata kama kuna medical malpractice hawa watu hawawezi kusema
  kitu.


  PURE HYPOCRICY ya hawa watu,I am sick to death.
   
 6. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  inatia hasira!
   
 7. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hawa watu kweli hawana soni. Yaani hata hawaoni aibu kwenda kutibiwa kwenye nchi zinazoongozwa na viongozi kama walivyo wao? Sijui huwa wanajielezaje kujustify kwenda kutibiwa huku?
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  May 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Afadhali mtoto wa mkulima kaenda kutibiwa! Mzee wa 'vijisenti' huwa anapeleka suti zake majuu kufuliwa!
   
 9. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #9
  May 19, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ....kwa waziri mkuu that is a normal health check up ambayo hufanyika once a year.......

  ....sijui kwanini viongozi wa kiafrika hawaamini madaktari wa nyumbani....sijui wanagopa siri zao kuvuja..[simnajuwa wakienda ulaya wanaonekana watu wa kawaida na hakuna daktari anayekuwa interested ku share findings na mwenzake].....but pamoja na viapo ukweni nyumbani naona watu wengi hawapendi kufanyiwa vipimo sensitive hospitali za jirani na wanapoishi.....kuna watu wanatoka dar wanaenda hadi kcmc ...na wa moshi wanakuja muhimbili just for the sake of privacy!!!

  ulaya na hata afrika nchi kama south africa ,egypt etc marais wanatibiwa Millitary hospital...hapa kwetu wamejitahidi kuboresha Lugalo na e.mzena kwa kiwango kikubwa sana kiasi hata presidaa anaweza kutibiwa maradhi ya kawaida pale lakini ...no body goes!!...bora hizo pesa wangeboresha mikoani huko!...yaani imefikia mahali huduma pekee ambayo viongozi wetu wanaona fahari kuipata kwenye Millitary hospital yetu ni ile Ya Mortuary...ili apigiwe saluti za mwisho mwisho...hata afie wapi ...watampeleka mortuary ya jeshi lugalo....tungependa wahudumiwe pale wakiwa wazima na si wafu!!
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mtoto wa Mkulima haachi kunishangaza!
   
 11. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Nafikiri mkuu si kweli
  1.Anapokuja mgonjwa kutoka africa ambaye hana bima ya nchi husika madaktari wanamchangamkia vilivyo, maana hospitali inapata fedha za kutosha kutoka kwa mtu husika.

  2.Nafikiri viongozi wanawakimbia madaktari wetu kutokana na hofu ya kwamba wanaweza kuwa manipulated na wabaya wao na kuwa - theorodani, nafikiri hiki ndicho wanakiogopa zaidi.

  3. Viongozi wetu wote wana amini ktk ushirikina.
  Hawa jamaa nafikiri hawakimbii hospitali zetu kwa sababu hawaamini ma daktari, nafikiri wanachoogopa zaidi ni matatizo ya imani zetu za jadi kama vile kukolimba nk.
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wasu,
  Siyo hiyo tu. Nafikiri na kale ka mentality kuwa uzunguni ni bora zaidi ya kwetu pia kanasaidia kuchangia. Si uliwasikia wabunge nao wakililia dili la kupelekwa ulaya kwa matibabu?
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Du! mtoto wa mkulima ataipata mwaka huu. Maana alivyoshukiwa kama mwewe utadhani ni wa kwanza kumbe hilo limetokea kwa wakubwa wengi miaka nenda rudi maana hata baba wa taifa hakuwa akitibiwa hapa nchini pamoja na uzalendo wake usiotia mashaka. Na hivyo hivyo simba wa vita.

  Mimi nafikiri ni suala na kuwa na huduma za uhakika ambazo siyo siri hapa kwetu ni adimu hata kwenye hizo tuazoita first class private hospitals na mara zote watakuambia nenda nairobi, India au South Africa kwa watu wa kawaida. Hawa madaktari wetu si ndiyo wale waliompasua mtu kichwa kwa ugonjwa wa mguu? Mimi naikubali hoja ya kuimarisha hospitali zetu na hili liende sambamba na kubadilisha tabia na hulka za madaktari na manesi wetu wanaoshambulia wagonjwa kama vile ni wagoni zao.
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mmmhh mtoto wa mkulima anaenda kutibiwa UK? lol

  Wajinga ndio waliwao..

  BTW, wapunguze hiyo misafari yao ya kutalii na kujiongezea per diems wakati mafungu wanayotengewa wataalamu huko kwene halmashauri ni kisoda..too much of anything is harmful..Ujinga tuuuuu
   
 15. K

  Kagasheki Member

  #15
  May 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mtizamo wangu kwa kiongozi wa ngazi yake kwenda kutibiwa ughaibuni inaweza kuwa si hoja sana,maana wana stahiki za aina hiyo.Tatizo langu ni kwa nini waende mbali kote huko wakati hata Afrika ya Kusini wana matibabu ya kisasa kama wanayoyafuata huko na gharama zinaweza kuwa nafuu.Hivyo inaelekea gharama kwao si jambo la msingi sana kuzingatia
   
 16. m

  mapambano JF-Expert Member

  #16
  May 20, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pumbavu kabisa hawa!! Zamani viongozi wakitibiwa kwenye hospitali zetu!, sasa wenyewe hawana imani na hospitali zetu, watajua lini mwananchi wa kawaida anapata tabu gani? they make me sick!!
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  You are joking right?

  Yaani viongozi wana stahiki ya kutibiwa vizuri kuliko the rest of us.. si ndio unavotaka tukuelewe? Kwa gharama za wavuja jasho kwa lipi haswa?
   
 18. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Jamani ni matibabu pamoja na kupumzisha akili - ndiyo maana kaenda na mamsapu, nyie mnataka akae bongo kila siku matatizo hayaishi, la Tucta linafuka moshi linakuja lingine la Tendwa na CCJ na wengine nao wanadanganya miaka yao walioishi duniani - Mwee!! - Matatizo kila kukicha laa mwacheni akapumzike kidogo apige na shopingi na mama!! karibia anamalizia kipindi chake cha uongozi kama Waziri mkuu Miezi michache ijayo.
  Hapa bongo hukawii kurekebinswa Ini wakati kumbe unaumwa presha, bora nchi za wenzetu wanafuata utaratibu mzuri wa matibabu hata ningekuwa mimi na uwezo sitibiwi bongo hii.

  Nakutakia matibabu mema mzee pinda upone na usafishe macho siku mbili tatu. Sisi watanzania matatizo yetu hayataisha ni ya KURITHI.
   
 19. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  viongozi wetu hawana uzalendo, hawana uchungu na kodi zetu na hawataki hii nchi iendelee... ni mafisadi na mahasidi wakubwa
   
 20. a

  arasululu Senior Member

  #20
  May 20, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni uwezo tu sina but zingekuwepo faranga pet yangu nikkohoa tu nafly! hata kama ni flue! piriton nafuata ulaya meku...tuchukue tu mfano rahisi mtu anavunjika mguu hapa bongo ukienda hospital wanakuambia huu mguu ni wa kukata while kwa wenzetu unavunjika mguu unapewa week 3 au 4 mtu yupo road anadunda balaaa! cju elimu ya hawa madaktari hapa kwetu inakuwaje ama cc tuna vichwa maji? huduma za huko mbele mbele zingekuwa kama za hapa bc wachezaji wa soccer kama kiana roone na yule wa arsenal (simkumbuki kwa jina) wangekuwa viwete wote!!!
  PINDA MUNGU AKUTANGULIE MBELE URUDI UKIWA NA ARI MPYA NA KASI MPYA KAMA YULEA JAMAA WA MAISHA BORA
   
Loading...